Sioni kosa la mtu huyu

Sioni kosa la mtu huyu

doppla2

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2014
Posts
1,393
Reaction score
1,462
Katika hali isiyo yakawaida, nimeshangaa na nitazidi kushangaa ni kwa nini haya yanakua ajabu na taharuki kwenye jamii ya kitanzania.

Toka kumalizika kwa ibada za krismas , tumesikia mengi na kujionea taharuki kufuatia kauli za watumishi wa Mungu juu ya hali ya kisiasa nchini kwenye vyombo vya habari na social media.

Taharuki kubwa ni kufuatia tamko la Askofu zacharia Kakobe , lilioenda mbali na kuwataka watawala kujitathimini na kuchukua hatua ya Kutubu, kwa kile alichodai mwenendo mbaya wa kuendesha nchi pasina kufuata haki, sheria na katiba ya nchi na hivyo kuhatarisha usalama wa nchi na maendeleo pia.( Nime paraphrase)


Ukipitia mitandao ya jamii, utashangaa kuona taharuki juu ya msimamo huu wa mtumishi wa Mungu huyu, wengine wakisema hawaoni shida na matamko hayo, huku kundi lingine likidai ametumia uhuru wake vibaya, kutumia nafasi yake ya kidini kuingilia na kuchochea chuki baina ya serikali na wananchi.

Leo naombeni mnijuze , hii tafsiri ya uchochezi hasa maana yake nini?

Kutoa maoni yako public ambayo si lazima yakubaliwe na kila mtu siku hizi ni kosa la jinai?

Neno kutubu - kweli ni nonga?

Kwa tafsiri isiyo lasmi ya kithiolojia, kutubu ni kuungama/ kukiri kuwa hujatenda kwa haki (umekosa) na kudhamilia kugeuka njia hiyo na kuacha kurudia matendo hayo yanayozaniwa agharabu ni maovu na machukizo kwa Mungu au kwa watu.

Kiimani fursa, ya kutubu ni hali ya juu kabisa ya kupendwa na Mungu na kupewa second chance ya kujisahiisha.

Kama ukweli ndo huo, naumia kuona jamii yangu sasa inataharuki kwa neno hili, je ni kweli neno kutubu ndo limetupa taharuki au kunalingine nyuma ya pazia?

Acheni kujificha kwenye kauli za watu, tuelezeni bayana hapa tatizo ni nini? La sivyo tutahoji mbona mna hofu kiasi hiki?

Ni vizuri kutambua ; kuwa hofu zenu hazisaidii kulijenga taifa hili, nachokiona ni mpasuko mkubwa na kujenga chuki katika jamii hii ya kitanzania.

Mnaweza kujificha katika matukio kama haya mkishadidia kuwa mtu anachochea ,lakini ukweli ni kuwa jambo hili linatuonyesha hatuko sawa kama Taifa, ni kweli lazima tujitathimini na tuchukue hatua ya kutubu.


Ikumbukwe: " Na kazi ya haki itakuwa amani,na mazao ya haki yatakuwa ni utulivu na matumaini daima. Isy 32:17


Nimalize kwa msemo wa pilato....

[HASHTAG]#Hata[/HASHTAG] sasa sioni kosa la mtu huyu#
 
Back
Top Bottom