"Sioni hata ndoa moja ya mfano itakayonishawishi kuolewa........!"

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
Geri-Halliwell-im-BBC-Interview-%C2%A9-Screenshot-YouTube.jpg

Geri Halliwell akihojiwa.....................

Hivi karibuni nilibahatika kusoma mahojiano ya Mwanamuziki wa kundi la zamani la muziki, maarufu kama Spice Girls la nchini Uingereza Geri Halliwell. Nilisoma mahojiano yake mtandaoni aliyoyafanya na Gazeti la Woman's Day la nchini humo.

Labda niwakumbushe wale wasiolifahamu kundi hili la Spice Girls.Kundi Hili liliwahi kuvuma sana miaka ya 90 nchini uingereza likijumuisha wanamuziki wanne, Victoria, aliyeolewa na Mchezaji maarufu wa soka nchini Uingereza David Beckgham, Emma, Melanie na Geri Halliwell.

Katika Mahojiano hayo, mojawapo ya maswali aliyoulizwa na mwandishi, ni hili la yeye kutoolewa pamoja na kwamba ana mtoto.

Akijibu swali hilo, Geri alisema kwamba hana imani kabisa na maisha ya ndoa, na ndoa kwake sio mojawapo ya agenda zake katika maisha. Alisema katika kizazi hiki familia nyingi zimeshuhudia kuvunjika kwingi kwa ndoa kama ilivyotokea kwa wazazi wake. "Katika makuzi yangu nimeshuhudia ndoa nyingi zikivunjika mpaka nimefikia kuona kwamba ndoa hazina maana kabisa" alisema Geri. ……… Aliendelea kusema kwamba haoni ndoa hata moja ya mfano ambayo anaweza kuitumia kama Dira yake inayoweza kumshawishi kuolewa, ingawa anapenda sana kuwa na watoto wengi.

Hebu wana JF fungukeni, Je anayosema huyu bibie yana ukweli?
 
kwa nini kina dada?comment kutolewa na mdada sio hoja kwamba kinadada ndo wahanga.ndoa manake 2 people.wote wachangie coz it is a two way traffic
Haya nimerekebisha swali langu..................
Changia sasa.
 
Mimi sijaolewa lakini naamini ndoa nitakayoingia mimi itakuwa ya Amani na Upendo.... Sikatishwi tamaa na sikubaliani na maneno ya watu!
 
Kwangu mimi naegemea zaidi swala la kiimani kwamba shetani ameona kuivuriga dunia atumie kiungo kikuu cha muungano wa binadamu ambapo ni kuisambaratisha familia,anajua familia ikishavurugika everyth will end up ovyo ovyo however successfull you are.
Kingine tunatumia zaidi mifumo ya kimwili katika kutaka kuoana, zaidi ya kiroho hi inabeba mengi mfano getting married for the sake of so many many.Na ukisaget married for the sake of what nxt,hutaheshimu ndoa yako katika nyanja zote then of it goes
 
Hio ya hakuna ndoa za mifano ni uzushi tu. watu wanajiendekeza tu.

na wanatumia kigezo hicho kuvunja ndoa zao au kueleza why hawajaolewa,

papito Mtambuzi hio dhana ikiwa kweli fikiria watoto watakuwa katika makuzi gani?

familia ni msingi wa makuzi ya watoto, ndio maana mm Ero nipo kuhangaika kutafuta baba

kwa ajili ya mapacha wangu. not that siwezi walea peke yangu, ila tu nataka what is best for them

na what is best for them wanapozaliwa na kukuwa ni mother na father figure. Hata kama atakuwa Kaunga.
 
Last edited by a moderator:
Lakini kuna ukweli kuwa ndoa zetu nyingi zimeshindwa kumshawishi m-Dada aolewe,huenda yeye toka utotoni aliamini kuwa na maisha mazuri ni mpaka aolewe.Mwache amini hivyo huenda atakuja kugundua ndoa ni mchakato wa kuvumiliana kwa tabu na raha ktk maisha,bila kujali una watoto au la.
 

Akijibu swali hilo, Geri alisema kwamba hana imani kabisa na maisha ya ndoa, na ndoa kwake sio mojawapo ya agenda zake katika maisha. Alisema katika kizazi hiki familia nyingi zimeshuhudia kuvunjika kwingi kwa ndoa kama ilivyotokea kwa wazazi wake. "Katika makuzi yangu nimeshuhudia ndoa nyingi zikivunjika mpaka nimefikia kuona kwamba ndoa hazina maana kabisa" alisema Geri. ……… Aliendelea kusema kwamba haoni ndoa hata moja ya mfano ambayo anaweza kuitumia kama Dira yake inayoweza kumshawishi kuolewa, ingawa anapenda sana kuwa na watoto wengi.

Hebu wana JF fungukeni, Je anayosema huyu bibie yana ukweli?

Mtambuzi ukweli ni kuwa watu wenye matatizo ya ndoa ni wachache sana ukifananisha na watu wasio na matatizo ya ndoa. Lakini kwa bahati mbaya, walio na matatizo ya ndoa ndio hufunguka zaidi ili kuhangaikia kupata suluhu za ndoa zao na hivyo kujikuta wakitangaza matatizo yao kwa watu pasipo kikomo, na bila kujijua, wanajikuta wakichafua na upande wa pili!

Mtu asiye na matatizo ya ndoa hawezi kuzungumza na ndiyo maana group hili hutulia huwa likiendelea kula mema ya nchi kimya kimya.
Swali la sasa ni kujiuliza ndoa ngapi zinamigogoro maeneo unayoishi na ngapi hazina? Hapo utaweza kupata jibu la nini namaanisha.

Tukirudi kwenye mada yako, huyo Geri ni kuwa hakupata mtu wa type yake wa kuweza kumfikisha anapostahili. Ubaya wa kuwa Star* ni kuwa watu wanakosa mapenzi ya dhati kwa mhusika, na hutafuta ndoa au urafiki ili na wao wajipatie umaarufu. Hiyo ndiyo hofu yangu na ndiyo sababu kubwa ya mastaa wengi kuwa na migogoro ya kindoa au kimahusiano; hakuna mapenzi ya kweli.
 
Leo kikweli sina mood kabisaaaa! sijui kwanin kukawaga na hali ii. yaani Mtambuzi ngoja kwanza i'll be back.............
 
Last edited by a moderator:
ameshasema yawazazi wake ilivunjika alipata psychological effect huyo

Mfano wa ndoa mbaya ya wazazi wake imempelekea huko?
Nadhani angejaribu kuona kwake yeye mwenyewe kuliko kuhisi hisia ambazo ana deep source ya mahusiano mabaya ya wazazi wake.
 
Kama alivyosema Erotica siyo kweli kwamba hakuna ndoa za mifano, labda aseme kwamba hajaziona within peer group yake - this way I can understand.
Ila kama alivyosema HorsePower tusisahau kuwa ustaa nao sometimes ni mzigo ktk relationship.

Lakini yote tisa, kumi ni kwamba binadamu ye yote hujengwa au huaribiwa na kile anachokiona, anachosikia anachofanya au anaocho-experience ktk maisha yake. Kwahiyo binafsi simshangai huyu dada kwani mtizamo wake inawezekana umetokana na hivyo nilivyovitaja.
 
Pole gfsonwin, siku hazifanani my sister, ndo binadamu tulivyoumbwa! If things are not okay with you, just be an 'international observer' for a while!

thank you ma bro mito. note taken
 
Last edited by a moderator:
huyo mdada maisha alokulia hajawahi ona watu wakiishi kwa upendo na uvumilivu,kwani ndoa inahitaji uvumilivu na uwejabari wakuweza kukabiliana na majaribu ya kila aina....
 
Back
Top Bottom