Sioni haja ya kwenda chuo

Lengo lako ni nini?? Waulize ambao walikua na maoni km yako wakayatimiza kisha waulize walioendelea kusoma,
Hakikisha umewauliza usiwaone tu ukajiongeza .
 
Mapenzi yanakutesa sana mkuu😂😂 jus kidding.
 
Usipoenda chuo utafikisha miaka 40 ukiwa mtupu na ukienda utafikisha miaka 40 ukiwa na elimu, you choose, Waone wasanii wa zamani wengi wamekula kitabu ndio wakaanza uhuni, japo katika jamii wengi walionekana masela, kina Master J wamekula engineering zao, mtu kama S2kizz kala kitabu we muone vile uchukulie poa, jux ni computer scientist mzuri tu ana degree yake, waone wanagonga beats lakini ikitokea hamna mziki wanatoa vyeti wanaendelea na maisha.
 
Lengo la kwanza la kwenda chuo ni kujifunza elimu na kuongeza maarifa...hatuendi chuo kwaajili ya kupata ajira .Ajira ni bonus tu...maarifa utakayoyapata yatadumu hadi unakufa
 
So unataka kwenda Wapi?Kila Uamuzi huwa na Pros and Cons.Tafakari UPYA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…