Huo ni mtazamo wangu tu, kwani nadhani katika mazingira ya sasa, CCM inajaribu kuepuka mchakato wa kura za maoni katika chaguzi ndogo kwani kura za maoni kwa kawaida zinaambatana na gharama na vurugu nyingi zisizo za lazima.
hoja mfu ni ipi kiongozi,
ninani asiyejua kuwa SOLOMONI SUMARI ni mkwe wa LOWASA?tunakumbuka uchaguzi mkuu JEREMIA SUMARI ambae ni baba wa SOLOMONI,alikua hoi anaumwa na aliye simamia na kufanya kampeni ni lowasa,kama aliweza kumfanyia kampeni mtu aliye hoi kitandani na kwamsaada wa kichakacha akashinda,atashindwa kuchakachua kwenye kura za maoni ilimradi mkwe apate??
Kwenye uchaguzi mdogo, huwa hakuna ule utaratibu wa kwenda kupiga kura za maoni kila kata kwa sababu ya ufinyu wa muda na pia gharama za uchaguzi.
Wanaopiga kura za maoni ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo [sawa na jinsi Mchambuzi alivyosema vikao husika vitateua/pendekeza jina la mgombea]. Then litakwenda kwenye vikao vya wilaya na mkoa, finally mwenye mamlaka ya mwisho ya uteuzi ni CC ambayo hupitia madokezo/maelezo ya vikao vya chini ili kufanya maamuzi.