Sioi kuibukia Arusha Mjini

Nabii Mke Flora Peter alitabiri kuwa miungu yake imemuonyesha kuwa Sioi Summari ataibuka mshindi jimbo la Arumeru!!!



Nabii Flora akiwa kanisani kwake

[h=2]Wiki mbili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa jimbo la Arumeru Mashariki Nabii Mke aitwaye Flora peter wa Kituo cha maombezi Mbezi Beach mtaa wa Maguruwe aliibuka na kutoa utabiri wa ndoto kuwa ameoteshwa na miungu yake kuwa Mgombea wa CCM Bw SION SUMARI mkwe wa Edward Lowasa ataibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho. Utabiri huu uliandikwa kwa uzito mkubwa kwenye gazeti la Uhuru katika ukurasa wa Mbele huku tahiri ya gazeti la Jambo leo ikishabikia unabii huo.[/h] [h=2]Katika gazeti la Uhuru linalo milikiwa na CCM la siku ya jumatatu Machi 26,2012 toleo namba 21148 ,lilikuwa na kichwa cha habari ,..SIONI aahadi neema,. Nabii aoteshwa Ushindi wake.[/h] [h=2]Mwaandishi alikuwa ananukuu kauli ya nabii Flora peter iliyotolewa siku ya jumapili machi 25,2012 kanisani kwake kama ifuatavyo; ‘Sijui Sioni ni nani ila wakati naombea uchaguzi wa Arumeru nilionyeshwa watu wawili, mmoja Sioni na Joshua waliokuwa wakuchuana vikali, Sioni aliokota karatasi huku mwenge ukiwa umeinuliwa juu na watu wakaanza kushangilia', Huyu Sioi sijui ni wa chama gain na ni motto wa nani ila ataibuka mshindi kutokana na ndoto niliyo oteshwa.' ‘Najua kuna baadhi ya watu watashangaa Nabii kuzungumzia masuala ya siasa lakini mimi ni kiongozi anayehudumia wananchi,hivyo kama kuna jambo nimeoteshwa na lina maslahi kwa Taifa sina budi kuliweka wazi kama hili"[/h] [h=2][/h] [h=2]Hata hivyo uta biri huo umeonyesha kuwa wa uongo na upotoshaji baada ya Joshua Nassari wa Chama cha Demoksrasia na maendeleo (CHADEMA) kuibuka mshindi kwa kupata kula 32,972 huku akimtupa kwa mbali mkwe wa Lowassa , ambaye aliambulia kura 26,577.[/h]
 
Asijaribu kujitosa ili alinde heshima aliyobakiwa nayo katika jamii...Sioi kama unapitia huku tafaaaaadhali usiende kugombea Arusha wallahi utaadhirika vibaya kaka yangu....bora ubaki Stanbic uendelee na mishe mishe yako kama kawaida
 
Back
Top Bottom