Sio tu Wabongo, hadi Wanaijeria ni COPYCATS

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
145
335
Wiki hii kule Twitter kumekuwa na mjadala mkubwa sana, Moja ya Page ya Twitter ya Kinaijeria imemshutumu Msanii Mkubwa kuwa Nigeria ndio imempa umaarufu kupitia namna anavyokopi Sound ya Miziki yao na baadhi ya vipande vya nyimbo zao. Jambo ambalo limezua Gumzo kidogo mitandaoni, na baadhi wa wabongo wakafunga safari mpaka kwenye page hiyo ya Twitter inayofahamika kwa jina la Unorthodox Reviews, na wakaanza kuipigania nchi yao. Watu wengine wakaingia chimbo na kutafuta baadhi ya nyimbo za kina Burna Boy na Wizkid ambao nao inasemekana wamekopi kutoka kwa wasanii wengine. Mtu anayekopi kazi za ubunifu za wengine anaitwa Copycat kwa lugha ya kiingereza. Kwenye pitapita zangu nikakutana na hii video inayoelezea baadhi ya nyimbo alizokopi Diamond na Walizokopi kina Burna Boy.



Wengi wanamtetea Burna Boy kuwa anapokuwa anakopi au kufanyia Sampling Nyimbo za watu wengine uwa anawalipa, Je Vipi kuhusu Diamond Platnumz je uwa hawalipi watu hawa pale anapotaka kuwafanya kopi au sampling ya Nyimbo zao. Maana Diamond Platnumz hayuko juu ya sheria tulitegemea angeshitakiwa na kulipishwa faini au nyimbo kufungiwa, ila tunaona nyimbo zake zinapeta tu bila kuzuiwa. Hii inaweza kumaanisha Diamond Platnumz nae analipia na kuomba kibali nyimbo za hawa wasanii kabla ya kuzikopi. Na katika Mziki au Sanaa watu wanakopiana sana tu. Je mtu aliyegundua Smartphone angesema makampuni mengine yasitengeneze simu ila ni yeye tu atengeneze unahisi tungefika hapa. Inasemekana Diamond Platnumz kitendo cha wimbo wake wa "My Baby" kuingia Trending YouTube nchini Nigeria, kimeshtua Wanaijeria wengi sana, maana ni nadra kwa Watanzania kuingia Trending ya Nchini Nigeria. Hivyo wakaamua kumlipua na kadhia ya Kukopi Nyimbo zao. Kwenu Wadau wa Jamiiforum
 
SASA wewe umeleta taarifa tayari ukiwa na upande yaani ni shabiki wa diamond . ungeleta taarifa bila kuonesha upendeleo, Wizi ni wizi tu hata akiiba Mwanzo bado uta mwita mwizi.
 
Back
Top Bottom