Sio mabasi yaendayo kasi bali litafutwe jina lingine

Niambieni

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
625
170
Kwa jina la mabasi yaendayo kasi haliendani ni ukweli unaoonekana. Sababu:

  1. Barabara ni nyembamba kuruhusu vyombo vya moto kukumbia zaidi ya 50 km/hr
  2. Vituo vimekaribiana sana- toka kituo kimoja, kabla ya kubadili gear ya pili umeshafika cha pili
  3. Basi likiharibika njiani hakuna pa kuliruhusu lingine lipite.
  4. Watembea kwa miguu na pikipiki hawana vizuizi vya utumiaji barabara.

Hivyo hayataenda kasi bali ni vema kutumia jina lingine.

Nawasilisha na kusubiri nihamishwe na kuunganishwa na topics zingine.
 
Kama haujaelewa uliza kwanza! Haiwezekani Wizara nzima pmj na Serikali yote yenye Wahandishi wa ndani na nje ya nje wakawa wajinga kiasi hicho!

Kinachomaanishwa hapa ni kwamba haya mabasi yana njia yake na hivyo hayatakuwa na haja ya kufwata foleni kama magari mengine na ndiyo maana yakaitwa ya kasi, kasi maana yake ni haraka, ina maana wakati magari mengine yakiwa kwenye foleni haya mabasi yatakuwa yanapita tu na kusimama kwenye vituo kuchukuwa abiria na labda taa tu ndiyo maana yakaitwa mabasi ya kasi au unaweza kusema haraka kama ukipenda!
 
Nadhani umekurupuka. Yale Mabasi hayaitwi Mabasi yaendayo Kasi bali yanaitwa Mabasi yaendayo kwa Haraka. Kuna tofauti baina ya Kasi na Haraka. Mabasi yaendayo kwa Haraka yanapewa muda maalum wa kukaa na kuondoka kituoni. Ni kama Treli ya Mwakyembe. Ndo maana wamekadiria kuwa kutoka Kilara hadi Ferry Basi litatumia dakika 45.
 
Haswa hilo la gari moja kuharibika barabarani sijui wale designers walikuwa wanafikiri kwa kutumia MASABURI?maana hata sielewi itakuwaje kuweza kuliondoa hilo gari bovu kupisha mengine yaendelee na safari
 
Halafu Kingine, hv mabasi ya mwendo kasi yakifika ubungo mataa yanapaa juu? au itakuwaje pale ili kasi iendelee?
 
Kama haujaelewa uliza kwanza! Haiwezekani Wizara nzima pmj na Serikali yote yenye Wahandishi wa ndani na nje ya nje wakawa wajinga kiasi hicho!

Kinachomaanishwa hapa ni kwamba haya mabasi yana njia yake na hivyo hayatakuwa na haja ya kufwata foleni kama magari mengine na ndiyo maana yakaitwa ya kasi, kasi maana yake ni haraka, ina maana wakati magari mengine yakiwa kwenye foleni haya mabasi yatakuwa yanapita tu na kusimama kwenye vituo kuchukuwa abiria na labda taa tu ndiyo maana yakaitwa mabasi ya kasi au unaweza kusema haraka kama ukipenda!
Pia kwenye maelezo yake kipengele cha tatu, anasema eti basi likiharibika hakuna sehemu ya kupita gari jingine. Yaani inashangaza sana. Sijui ameona hizo barabara zilivyo ama yupo nje ya nch na anaona kwenye mitandao tu. namshauri afanye ziara kuanzia Kimara hadi Akiba ama kuanzia Magomeni hadi Morocco.
 
Haswa hilo la gari moja kuharibika barabarani sijui wale designers walikuwa wanafikiri kwa kutumia MASABURI?maana hata sielewi itakuwaje kuweza kuliondoa hilo gari bovu kupisha mengine yaendelee na safari
Mkuu, na wewe unaungana na huyu jamaa? Subiri mradi uanze ndo mtajiona mlivyo wajinga
 
Nadhani umekurupuka. Yale Mabasi hayaitwi Mabasi yaendayo Kasi bali yanaitwa Mabasi yaendayo kwa Haraka. Kuna tofauti baina ya Kasi na Haraka. Mabasi yaendayo kwa Haraka yanapewa muda maalum wa kukaa na kuondoka kituoni. Ni kama Treli ya Mwakyembe. Ndo maana wamekadiria kuwa kutoka Kilara hadi Ferry Basi litatumia dakika 45.

Typing error nyingi kaka, rudia kutuma hujaeleweka
 
Nadhani umekurupuka. Yale Mabasi hayaitwi Mabasi yaendayo Kasi bali yanaitwa Mabasi yaendayo kwa Haraka. Kuna tofauti baina ya Kasi na Haraka. Mabasi yaendayo kwa Haraka yanapewa muda maalum wa kukaa na kuondoka kituoni. Ni kama Treli ya Mwakyembe. Ndo maana wamekadiria kuwa kutoka Kilara hadi Ferry Basi litatumia dakika 45.

Asante mkuu kwa hilo jina jipya la mabasi yaendayo kwa haraka. Haraka, mbio, kasi, upesi, ....Je mazingira yaliyopo yanaruhusu kuwa na haraka? au tusubiri utekelezaji ndio tu evaluate.
 
Pia kwenye maelezo yake kipengele cha tatu, anasema eti basi likiharibika hakuna sehemu ya kupita gari jingine. Yaani inashangaza sana. Sijui ameona hizo barabara zilivyo ama yupo nje ya nch na anaona kwenye mitandao tu. namshauri afanye ziara kuanzia Kimara hadi Akiba ama kuanzia Magomeni hadi Morocco.

Huyo Jamaa ni typical mbongo, sisi Wabogno tuna tabia moja kila kitu huwa tunajikita sana kwenye kutafuta makosa badala ya kuangalia manufaa kwanza!
Kwangu mimi huu mradi ni kitu kizuri sana kwanza kama ukiniuliza mimi ni bora wasitishe hata miradi yote ya kujenga fylovers na hizo fedha waziingize kwenye huu mradi ili ujengwe Dar yote kuanzia kama br. Madela, Nyerere/Pugu, n.k
 
Ni kweli mradi ni mzuri sana, hapa sio vema kuubeza mradi wetu. Mada ya hapa ni kuupa mradi wetu jina zuri. Nawasilisha
 
kama haujaelewa uliza kwanza! haiwezekani wizara nzima pmj na serikali yote yenye wahandishi wa ndani na nje ya nje wakawa wajinga kiasi hicho!

Kinachomaanishwa hapa ni kwamba haya mabasi yana njia yake na hivyo hayatakuwa na haja ya kufwata foleni kama magari mengine na ndiyo maana yakaitwa ya kasi, kasi maana yake ni haraka, ina maana wakati magari mengine yakiwa kwenye foleni haya mabasi yatakuwa yanapita tu na kusimama kwenye vituo kuchukuwa abiria na labda taa tu ndiyo maana yakaitwa mabasi ya kasi au unaweza kusema haraka kama ukipenda!
express!
 
Huu mradi ni mzuri iwapo tu utaenda sambamba na ujenzi wa barabara za juu ila kama utaendeshwa kwa mazingira haya ya sasa ile mantiki ya kasi,haraka, upesi,mbio, spidi na a.k.a zoooote munazozijua nyinyi muupanjike huu mradi bado lengo kuu la kupunguza foleni halitafanikiwa litabaki palepale kwa sababu na yenyewe yakifika trafic light yanasimama hayapai wala kuruka.
 
Haya ni Rapid transit sio speed bus! Gharama zilizotumika kwa mawazo yangu naamini ingetosha kusambaza Trein za mjini kwny njia kuu zote i.e Kilwa road, nyerere road, morogoro road na Ally Hassan Mwinyi Road!! Treni ndio usafiri wa gharama ya chini dunia nzima lakin hata ile tren ya Mwakyembe inasuasua japo watu wanalipa Nauli ya soko ( Marketing price), Mawazo ya Mkapa kubinafsisha baadhi ya huduma yako sahihi, leo ATC ime park ndege zote watu wapo kimya ikiuzwa ili lijiendeshe wanakuja wazawa kupiga kelele!! Magufuli ana kazi nzito sana ila naamini Allah atampa hekima na ujasiri wa kutuvusha hapa tulipoachwa na Manyang'au ya Mtandao!
 
Mimi hilo la kasi nakataa ila nasema ule ni mradi wa mabasi yapitayo katika njia maalum na vituo maalum bhaaas
 
mradi wa hovyo kuwahi kutokea
We yaseme ikibidi uyamalize, wenzako walikuwa wanaangalia vipaumbele. Na hapa kipaumbele ilikuwa ni 10% (kama sio 50%) na walishajichukulia kitambo nadhani imeshaingizwa mpaka kwenye urithi wa vitukuu vyao!
 
Back
Top Bottom