SIO KWELI WANANIZUSHIA..NAOMBA MUWAPUUZE

mbagokizega

Senior Member
Oct 22, 2016
111
297
Nawasalimia.

Kwa mlio tanga mtakuwa mmesikia habari inayovumishwa na mashilawadu wa mtaani kuhusu tukio lililotokea huko korogwe ktk kijiji cha mashewa mitaa ya kwa mzee shed.........

Kuna wajinga wanazusha tena huku wakisambaza na picha ya tukio,nikiri kwamba picha ya tukio ni ya kweli lkn sio kama wanavyosema Leo ntawaambia ukweli ili kuweka sawa tofauti na uzushi wao.

Mimi sio mwenyeji kabisa wa kijiji hiko lkn nilikuwa huko kumsindikiza rafiki yangu ktk msiba wa babaake,basi hapa msibani nikakutana na msichana mwenyeji nikajaribu kupiga ndogo ndogo akawa kanielewa sasa tatizo lilikuwa kutimiza miadi hivyo ilinibidi nibaki hapo kijijini kwa Siku tatu baada ya msiba ili nipate mazingira mazuri ya kumla ndege wangu kwakuwa alikuwa anaishi nyumba ya jirani kutokea kwenye msiba.

Basi hiyo Siku tulipanga tuonane usiku mnene tufanye yetu na kweli mi nkazuga naenda chooni usiku na kipens i tukakutana na msichana kichochoroni kinapotenganisha nyumba niliyofikia na nyumba yao naye akaja na kanga moko tu basi akatandika kanga yake chini mi nkavua kibukta changu tuanze yetu Mara ghafla wakatokea watu wanne wakatukulupua msichana ye mwenyeji akapita njia nyingine mi nikakamatwa.

Nikashangaa wale jamaa wanaamshana kwamba wamekamata mchawi sababu nilikuwa uchi wakaanza kunijazia watu huku wakinilisha madawa gani sijui huku wakinishurutisha nitaje watu niliowahi kuwala nyama ktk shughuli zangu za uchawi.

Hivyo ieleweke mimi nilifumaniwa tu wala sio mchawi na sijui kuhusu uchawi ila mijitu ijayoendekeza mambo hayo ndo ilinikamata ikinizushia hivyo na kwa mtindo wenu huu wa kuendekeza ushirikina watu wa tanga mtachelewa kimaendeleo.

Mmeniaibisha saana watu wa kijijini mnajidai na nyie mnajuuuua kupiga picha kwa kutumia smartphone,mpaka mwenyeji wangu amesononeshwa saaana.

Mlichonifanyia mtalipiwa malipo ni hapahapa duniani
 
Kama Pole pole tumempuuza, hata hao watu wa Tanga wanaokuzushia tu wameshapuuzwa! Pole kwa maswahibu... Ajali kazini.
 
Mh! Kulikuwa na tangazo moja la soda ya Pepsi linasema "THUBUTU KUKUTWA NA BWANA PEPSI". Mtu kakutwa na bwana Pepsi kakiri uzinzi kakana ushirikina. Lakini kusingekuwa na kipengele cha uchawi angekiri ugoni?
 
mshahara wavkuzini ndo huo

na wao walipweje sasa

umeenda kwa msiba na kuzini juu ulikuwa na machungu kweli wew
 
Sasa wewe ulienda msibani au ulienda kutafuta mademu huko? :p :cool: !! acha tu wakusingizie uchawi na ingekua huku kwetu TARIME / RORYA tungeku "RAFI" kabisa.
 
Unatafuta kiki habari yako sijaiona popote Kwenye social networks lete picha
 
Kwenda msibani af unaanza kuendekeza nye.ge huo nao tunaweza kusema ni uchawi kwa hiyo hawajakuonea saana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom