Sio kuumbwa tu, wanawake wanatengenezwa pia

Sio kuumbwa tu, wanawake wanatengenezwa pia

Umeegemea upande mmoja tu mkuu. Hata wanaume pia wanahitaji kutengenezwa. Suala la mapenzi linahitaji kila mmoja kumfanya mwenzake vile anataka aonekane, na si swala la mwanaume pekee. Vinginevyo utakuwa unamfanya mwanamke awe tegemezi siku zote. Lakini pia juhudi binafsi zinatakiwa ili umpendezeshe mwenzi wako na si kusubiri mwenzako anakufanyia nini katika muonekano wako.
 
^^
Ujumbe mzuri, ni vema pia kutazama akili ya unaemjenga. Hawakawii kukugeuka
^^
 
^^
Ujumbe mzuri, ni vema pia kutazama akili ya unaemjenga. Hawakawii kukugeuka
^^

Hilo nalo kweli mkuu, unamgharamia mwanamke akipendeza anachukuliwa na mwingine. Cha msingi ni kuaminiana na kupendana kwa dhati, kama si wa maisha chunga mizigo yako!
 
Watu wanataka ready made, mteremko tuuu kama wamekanyaga ganda la ndizi
avalishiwe, akarabatiwe ye agegede tu....
 
Hilo nalo kweli mkuu, unamgharamia mwanamke akipendeza anachukuliwa na mwingine. Cha msingi ni kuaminiana na kupendana kwa dhati, kama si wa maisha chunga mizigo yako!

^^
Na zaidi siku hizi sio kupendana, ni kupenda. Hujui mwenzako ana plan nini !!
^^
 
Salaaam wanaMMU wenzangu! Hakuna kitu wanaume tunapenda kama kumpata mwanamke mwenye uzuri wa umbo na tabia, naamini na hata kwa wanawake ipo hivyo pia.

Awe na sura nzuri, mguu mzuri, macho mazuri, ngozi nyororo, nywele, na lile eneo la kati awe nalo zuri haswa; kwa kifupi namba 8. Mchangamfu, mstaarabu, lugha nzuri, mwenye upendo, akili za maisha, heshima na kadhalika. Ila sio mara zote kuweza kumpata mwenye sifa zote, nyingine sasa tuwatengenezee! Unamwacha mpenzi wako na kwenda nje kisa nywele na ngozi, saloon zote hizi? Mimi mwanzo sikumpenda saana mpenzi wangu, because alikuwa na kama 81% ya sifa za mwanamke bomba na u busy ikawa tatizo.

Likizo hii nilimgharamia make up, mavazi na tukajengana ki tabia.

Sasa ni kama angel, hata miss gani haniumizi kichwa.

A call upon my fellow men, kama hujaridhika saana na mwenza wako ila unampenda basi usimbwage wala usichepuke.

Anatengenezeka, mtengeneze tu awe mwanamke umtakaye. Vinginevyo hakuna mwanamke atakayekukidhi hapa duniani!

mkuu umeongea point sana......... Lakin sisi wengne ni kunguru hatufugiki tunaamini kuwa kibaya ulicho nacho ila kizuri usichokuwa nacho......... Uzur na mvuto wa mke wangu sio kigezo cha kunizuia kutaman wengne. Kunguru kamwe hafugiki porin ndo makaz yake
 
Wanaume wengi siku hizi wanapenda waandaliwe wao wale tu. Mbaya zaidi haya yapo hadi ndani ya ndoa wanawake wengi hawatengenezwi na waume zao. Ila wanaume wanapenda vizuri.

Wanaume watulie waangalie kwanza wapenzi wao wao ndiyo wakuwabadilisha watakavyo.

Umenena muanzisha mada hongera kwa kujitambua na kuwajibika kama mwanaume.
 
Bora ww umesema labda watakuelewa,,, maana kuna vilizi hapa kugharamika kwao ni kosa kubwa.
 
Back
Top Bottom