Sio kila rafiki ni mkweli

NIMPENDENANI

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2014
Posts
6,114
Reaction score
5,398
Habari zenu waungwana,

Tuwe makini sana na mashoga hasa sisi baadhi wanawake tunaowapa siri zetu shoga zetu, siri zako mpe mzazi wako na kama mzazi hayupo hai kama wangu basi bora jifunze kunyamaza.

Nina rafiki yangu anapenda sana mashoga zake yani mara sijui Zahra mara Fahima, mara Mirfatt, na kuwapa siri zake juu mume wangu kanipa hiki mume wangu anapenda kile mume wangu ananiomba hiki.

Huyu ni muhenga mwenzangu ila yeye anapenda sana mambo ya mjini na kua na ma shosti wa mjini, wenzie wamemzidi kete, mume amezaa na rafiki yake kipenzi na zawadi kapeleka bila kujua kama mke mwenzie.

Sasa siri imevuja baada ya mwanamke aliozaa na mumewe kugombana na mtu ndio akampigia simu na kumpa shosti ubuyu kamili.

Mume kuulizwa kasema bahati mbaya imetokea na hatofanya tena, shosti kaondoka kwake amekuja kwangu ila anataka kurudi kwao kwa wazazi wake, wanawake wenzangu angalieni sana.

Hawa mashoga wengine wanaojifanya vipenzi kuweni makini nao sana, na angalieni sana malezi unayompa mumeo sio most of the time mume apite akachukue chakula hotel au mkale nje 3times a week wakati wewe mke upo.
 
Nina girlfriend lakini kanitambulisha kwa rafiki yake mmoja tena jujuu tu ingawa najua ana marafiki
zaidi ya mmoja.

Msifanye hivyo sio wote mabazazi!!!
 
Mie ndomana sinaga urafiki mbele ya mume wangu na wala hajui kama ninamarafiki, habari ya urafiki unaishia nje ya get la ofisi na mitaani sihitaji kuingiliana na mashoga story hadi sebuleni nooo
 
Kuna baadhi ya wanawake wanasikia basiii,.sijui ndio kutaka sifa na majigambo kwa wenzake ndio hayo yanawatokea puani,.mtu unajimaliiiizaa nani dunia hii hataki raha!??we kila siku kumsifia mumeo anakupenda sana,Mara outing Mara 4 kwa wiki mara lunch quality center looh utaacha kuonjewa,..tuwe na vifua jamanii sio kila MTU anafurahia MEMA yako...na sijui kwann adui hatokagi mbali.
 
Maneno yako kweli tupu,na mimi naona hua ni ulimbukeni tuu na kujitia mikosi sifa nyengine hazifai sasa ivi anabakia kulia ooh nimemsaidia alikua hana hata hela ya kodi sijui mpaka pochi alikua anaomba kwangu ila hasemi kua kosa ni lake..
 
Mie ndomana sinaga urafiki mbele ya mume wangu na wala hajui kama ninamarafiki, habari ya urafiki unaishia nje ya get la ofisi na mitaani sihitaji kuingiliana na mashoga story hadi sebuleni nooo
Tunaendana,mie kwa tangu zamanai shogangu alikua Marehemu Mama na Dada zangu na pia Dada zangu wanapata yale mepesi anaepata yote ni Mama peke yake,ila sasaivi nimejifunza sana kumeza shoga no..
 
Bora umetukumbusha japokuwa mpaka leo huwa sijajua shida iko wapi sababu tunaubiriwa kila siku haya mambo ila baadhi yetu wanawake huwa hatujui kujiongeza.

Mie sijawahi muamini rafiki kiasi hicho mie urafiki wangu tuwe kwenye kuelekezana mbinu za kuyatusua maisha na sio vinginevyo.
 
Nina girlfriend lakini kanitambulisha kwa rafiki yake mmoja tena jujuu tu ingawa najua ana marafiki
zaidi ya mmoja.

Msifanye hivyo sio wote mabazazi!!!
Mie Wallah nawaogopa sanaaaaaaaaaaaa..
 
Shosti wengine wana tabia ya ajabu sana eti shosti anakuja nyumbani wewe mwenyewe haupo na mume mara karudi wako wao na watoto wanacheza nje,mie no way wacha waseme nna wivu au vyovyote vile ila tfaran staki..
 

Hapo kwenye sifa napakubali na ndo ugonjwa wa walio wengi.

Na hilo la kuwa na kifua ndio wengi panawashindwa sababu wanataka waonyeshe wenzao utofauti ambao mara nyingi unaleta madhara na kubaki majuto.

Sa sijui waambiwe kwa lugha gani ili hili somo kuwa wasiri wa mambo yao lipate kueleweka.
 
Dawa yao ni hivyo wanavyo fanyiwa,huyu shosti wangu nilimuliza ivi unajua wapi ilipo kosea? anasema kosa langu nikumsaidia ahahaha,nikamwambia apana kosa lako nikumpa siri zako nakujifanya wewe unapendwa sana unachotaka ndio unachopata,na mume hawezi kumfata mwengine manake wewe unajifusha Udi wa ghali,sasa kamfata mtu wala hafanani nae ila ndio amesha zaa nae, amekua mdogo mara kidogo analia..
 
Shosti wengine wana tabia ya ajabu sana eti shosti anakuja nyumbani wewe mwenyewe haupo na mume mara karudi wako wao na watoto wanacheza nje,mie no way wacha waseme nna wivu au vyovyote vile ila tfaran staki..
Dada kwa hilo nina mfano nalo hayo mambo ya kuamini marafiki na kuwapa siri za ndani na madhaifu ya mume.

Kuna Mama alikuwa mfanya biashara sasa ikawa kila akisafiri ana mtoto wa shoga ake tena ni mwari tu ndio anakuja nyumbani kumpikia mume wake na kufanya shughuli zote za humo ndani ikiwemo kuhudumia watoto sasa kilichotokea safari moja mke karudi mume anamwambia nataka kuoa mke wa pili kuja kushtuka ni mtoto wa shoga ake.

Mbona alichanganyikiwa. Tangu hapo mambo ya kumuamini mtu hasa rafiki huwa siyaafiki kabisa.
 

Hahahaaa. Pole yake ila atakuwa kajifunza jambo japokuwa ameshachelewa.
 
Una upeo mkuu barikiwa...
Hakuna anaependa kuona mtu anafanikiwa hasa maadui zako...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…