Sio kila kitu kinazuilika hata kama hupendi

Sio kila kitu kinazuilika hata kama hupendi

Mafwi Munda

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2017
Posts
1,749
Reaction score
1,605
Inaaminika Yesu ni mwana wa Mungu, au ni Mungu mwana, au ni mtume wa Mungu. Wapo waliompenda Yesu na waliapa kumlinda na kutamka wangepigania uhai wake. Lakini wapo ambao hawakumpenda na hawakujali awe hai au auawe.

Inaaminika wale wasiompenda waliandamana kwenda kumkamata na walimpeleka kwa Pilato kwa maandamano wakitaka wapewe ruhusa kumsulubu hadi wamuue. Hawakutaka kingine na waliwasamehe, majambazi sugu wakimtaka Yesu tu.

Maandamano yao yalifanikiwa na Yesu aliuawa siku ile. Wapo waliouzunika na wapo walioona ule aliofanyiwa Yesu ni ukatili na unyama.

Lakini kifo chake kilikuwa ni cha lazima sana. Maandiko ilibidi yatimie kwa Yesu kuuwawa. Na ilibidi afe ili tuone ukuu wa Mungu.

Maandamano yaachwe yafanyike labda kuna kitu tunapaswa kukiona, hata akiondolewa madarakani aondolewe tu, kama imepangwa itokee hivyo kwanini mtake kuzuia?!

Hata akiuwawa kama imepangwa auwawe ili tujutie acheni iwe hivyo! Tunajifunza kutokana na makosa yetu, kama ni funzo acha liwe funzo.

Eti kwasababu wewe hupendi basi hutaki itokee, wapo ambao hawakupenda Yesu afe, lakini ililazimu afe, na ikawa hivyo.Sio kilakitu kinahitaji kuzuilika, hata kama wewe hupendi.

Acheni waandamane!
 
Maswala ya Yesu yaache kama yalivyo usilinganishe na siasa zingine,jadili harakati za kumng'oa madarakani kama zilivyo.
 
Siasa Na Dini ni Sawa kujaribu kuchanganya Mafuta Na maji havichanganyikani.
Mafuta hukaa juu maji chini, Ya Kalisari Mwachie Kalisari Na Ya Mungu Mwachie Mungu.
 
Siasa Na Dini ni Sawa kujaribu kuchanganya Mafuta Na maji havichanganyikani.
Mafuta hukaa juu maji chini, Ya Kalisari Mwachie Kalisari Na Ya Mungu Mwachie Mungu.
Na huwezi tenganisha dini na siasa maana vyote vinagusa maisha ya kila siku ya watu.Ndo maana wanasiasa utumia Vitabu vya dini na si katiba kuapa.
 
Na huwezi tenganisha dini na siasa maana vyote vinagusa maisha ya kila siku ya watu.Ndo maana wanasiasa utumia Vitabu vya dini na si katiba kuapa.
Hahaha kuna watu humu, utadhani wana patent ya hizi dini. Yani Yesu wao, Mungu wao, Biblia yao.
Ukigusa tu haoooo!
 
Hata Yesu aliomba kikombe kimuepuke, lakini maji yalizidi unga



Mkuu kumbe thread zenyewe za kukufanya uleft 4ever ndio hizii.!

Nakutakia safari njema

BTW: au unatingishia Mods kiberiti??
 
Rasilimali nyingi zitatumika kuzuia maandamano kuliko yakifanyika. Hicho kipengele kifutwe kwenye katiba
 
Hivi walipoimba WAACHE WAANDAMANE WAJINGA WALE.... hawakumaanisha maana ya WIMBO WAO?
au Maandamano ni kitisho kikubwa zaidi kuliko vyote wa utawala wao?
 
Back
Top Bottom