Sio dada yake ila mdogo wake ndiye chaguo langu

Sio dada yake ila mdogo wake ndiye chaguo langu

ALU255

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
2,089
Reaction score
2,125
Upendo wangu na haupo kwake kiukweli upo kwa mdogo wake, lakini nilishindwa kuwa wake kabla ya dada yake kufanya mambo yake kweli nimeamini chelewa chelewa utakuta mwana si wako'.

Kwa jinsi nilivyompenda mdogo wake sijui ni nini kilichonifanya nisimwambie.Nahisi ule usemi wa 'subira huvuta heri' ulinipumbaza, ona sasa kaniwahi dada yake na mdgo wake katambua.

Jamani nilimpenda na bado nampenda mdogo wake ila mazoea ya dada yake kwangu yamechukua sura nyingine.Niliona njia rahisi ya kumpata mdogo wake ni kuzoeana na dada yake, lakini sasa dada yake kanizoea vibaya .

Hadi kufikia kuniomba namba yangu ya simu haikutosha akaamua kunitamkia kabisa eti anataka kuwa nami bila kujua kama mimi nina malengo na mdogo wake.

Nahisi ndoto zangu kupotea, nipo katika wakati mgumu sana sijui nimjibu vipi dada yake na sijui nitampata vipi nimpendae na wote wanakaa nyumba moja.

JAMANI EEH!

Nimetongozwa na dada yake msichana ninaempenda, bado sijamjibu chochote nimekata mawasiliano kwa muda ili kutafakari.

Tafadhali anayeweza kunishauri
 
Last edited:
Wew jamaa kwani ukitongozwa kama hutaki si unakataa,tena ndio wakati wa kumjibu aka mi sikutaki nampenda sana mdogo wako...
 
Kuwa muwazi kwake kuwa mapenzi yako yapo kwa mdogowe
Tena itakusaidia na kukurahisishia kazi ya kumpata
 
Nitumie namba ya huyovdada yake nikuondolee kuwingu ili wewe uendelee na mdogo wake.
 
Yaan huyu dada yake mbona anafanya ivo lakini? Hivi hajui kuwa dada yake hapindwi na mdogo wake na dada yake kaaamua kutaka kabisa dada.

(Maelezo mengine taabu tupu)
 
Mwambie ukweli wewe,au unamtaka na huyo dada?? Maana kama hujisomi vilee
 
ndo marako ya kwanza kutongozwa na mwanamke? tulia basi mkuu hyo ni proposal tu waweza ipiga chinu
 
Wew jamaa kwani ukitongozwa kama hutaki si unakataa,tena ndio wakati wa kumjibu aka mi sikutaki nampenda sana mdogo wako...

kumkataa sio kazi tatizo kamwambia mdogo ake kuwa sisi ni couple wakati hata sijampa jibu na mdogo wake anajua hivyo so naona dalili kama za kukosa wote hivi
 
Kuwa muwazi kwake kuwa mapenzi yako yapo kwa mdogowe
Tena itakusaidia na kukurahisishia kazi ya kumpata

kashamwambia mdogowe kuwa sisi ni wapenzi so nikimwambia nampenda mdogowe lazima ataniharibia tu...!
 
Yaan huyu dada yake mbona anafanya ivo lakini? Hivi hajui kuwa dada yake hapindwi na mdogo wake na dada yake kaaamua kutaka kabisa dada.

(Maelezo mengine taabu tupu)

sijakuelewa mkuu
 
Mwambie ukweli wewe,au unamtaka na huyo dada?? Maana kama hujisomi vilee

napenda kumwambia ukweli ila tatizo mdogo wake anajua sisi wapenzi sasa nikimkataa huyu akiamua kuniharibia kwa mdogo ake anaweza
 
ndo marako ya kwanza kutongozwa na mwanamke? tulia basi mkuu hyo ni proposal tu waweza ipiga chinu

tatizo sio kutongozwa tatizo aliyenitongoza ananiwekea mimi ugumu kumpata mdogowe
 
Sikiliza kk wewe usiwe na waswas coz utpo kuwa unamnyenyekea ataona haun msmamo na mapenz ya kwel kwake we mkatae tu akikutosa dadaye achan nao
 
There is a lot of girls are hanging over the street.
Piga chini Dada MTU, mdogo MTU akichomoa na yeye piga chini pia ingawa roho itakuuma Mwisho wa siku roho itapoa.
 
Back
Top Bottom