OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 437
Harakati za wagombea urais kutafuta wadhamini zinazidi kushika kasi na kuchukua sura mpya ya kuvuna idadi kubwa ya wanachama.
Wapo wagombea wanavuna zaidi ya wadhamini makumi maelfu hadi wengineo kufikia wadhamini zaidi ya elfu hamsini.
Watu wanahoji juu ya hiyo idadi kubwa ya wanachama lakini wanasahau ya kuwa CCM ina zaidi ya wanachama milioni sita (6,000,000) ambayo ni wastani ya wanachama laki mbili (200,000) kwa kila mkoani.
Hiyo ni takwimu ya mwaka jana, mwaka huu kuna kundi kubwa la vijana ambao wametimiza vigezo vya kupewa kadi za uanachama wa CCM.
Endapo tu kila mkoa una wastani ya wanachama laki mbili, leo hii utashangaa vipi katika mkoa mmoja mgombea akipata wadhamini elfu hamsini?
Mathalani katika mkoa wa Mbeya nikisikia kuna mgombea kavuna zaidi ya wadhamini 50,000 sintashangaa.
Mkoa wa Mbeya una wilaya tisa na kila wilaya una wastani wa wanachama wasiopungua 10,000.
Mathalani wilaya ya Mbeya mjini pekee ina wanachama wasiopungua 30,000 hapo bado haujaweka idadi ya wanachama katika wilaya zingine 8 za mkoa wa Mbeya. Leo hii utashangaaje kupatikana kwa wadhamini 50,000 kwa mkoa mzima?