Mkoroshokigoli
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 14,593
- 5,583
Ni kweli kabisa unayoyasema mkuu si vyema kumhukumu mtu ambae hujui amepitia maswahibu gani mpaka kufikia hapo alipo na umetaja mifano mingi tu mizuri!Kundi kubwa linalonyanyapaliwa ni la jinsia ya kike na sielewi kwanini wawe wanawake tu ambao ni wakosaji mbona wanaume wengi wanazaa tu hovyo na hawatekelezi majukumu yao na wengine ndo wanasimamia dede wanawake zao wauwe viumbe visivyo na hatia nani atawahukumu wao?Hii mada ni nzuri sana sana sana....na ni ya kujenga haswaaa. Lakini humu MMU kuna pepo la kudharau na kukashifu single mums,walioachika na wale waliozaa kabla ya ndoa. Mtu anaweza akaelezea challengez na masahibu yanayompata litakuja jitu linamwambia 'ndo mkome kuvuavua ovyo'. Imagine mtu umepitia mateso na challenge kibao katika kuzaa hadi kulea mtoto na pengine hiyo mimba ulipata kwa mtu ambaye wewe ulimheshimu,ulimpenda, ukajiachia kwake ukidhani ndiye baba watoto wako af mtu anakuja na kauli kama hiyo utajisikiaje? Na huenda hata ulilazimishwa sex na mtu uliyekuwa unamwamini au ulibakwa na bahati mbaya ukashika mimba....kauli za kijinga kama hizi utazivumilia? Huwa naumia sana ninapoona mwanamke mwenzangu anadharaulika kwa kosa ambalo mwanaume pia amechangia.....naumia kwa sababu najua challenge za mahusiano, najua situations ambazo wadada wanakutana nazo katika mahusiano yao, na mbaya zaidi wanaotoa lugha za kashfa kama hizo utaona ndo mabingwa huko mtaani kwa kulazimisha ngono zisizo salama kwa wapenzi wao.
Ni kweli kabisa unayoyasema mkuu si vyema kumhukumu mtu ambae hujui amepitia maswahibu gani mpaka kufikia hapo alipo na umetaja mifano mingi tu mizuri!Kundi kubwa linalonyanyapaliwa ni la jinsia ya kike na sielewi kwanini wawe wanawake tu ambao ni wakosaji mbona wanaume wengu wanazaa tu hovyo na hawatekelezi majukumu yao na wengine ndo wanasimamia dede wanawake zao wauwe viumbe visivyo na hatia nani atawahukumu wao?
Kwa uelewa wangu mimi:mtu single na mwenye mtoto awe wa jinsia yoyote si lazima awe amezaa nje ya ndoa,!anaweza kuwa amezaa ndani ya ndoa akatengana na mwenzi wake bado ana wadhifa uleule wa kuitwa single mum/dad!
Ngoja niwe msomaji
Kwangu Mimi ilikuwa bahati mbaya na nilipomtaarifu mhusika alikana. Baadaye alikubali lakini kila nilipotaka kujua jinsi tutakavyojipanga kumlea mwanetu mtarajiwa akawa anakwepa. It really broke my heart since sikuwa nafahamu chochote kuhusu yeye na hata home walikuja kujua nikiwa nimetimiza miez 6. Aisee I went through a lot mpaka najifungua. Hakuwa mtu wa kupiga simu kujua tunaendeleaje na hela ya matumizi mpaka atakapojisikia yeye. Mtoto alikuja kumuona akiwa na mwaka na miezi 6 tena baada ya kusogea karibu....changamoto ni nyingi lakini kubwa kwangu ni pale napoulizwa " mama baba yuko wapi? " au anapochukua simu na kujifanya kama vile anaongea na baba yake akiomba aletewe soseji, pipi, matunda n.k. Huwa naumia sana natamani he was there for her. Sijui kama niko sahihi but nimepanga kwenda nyumbani kwao (baba) at least mtoto awatambue ndugu zake pia kufight 4 the last time mwanangu apate mapenzi ya baba na mama, na kama itashindikana will move on with my life
Ngoja niwe msomaji
umerudia id yako?
Nmerudia mwayaa
anhaaa Good mzima lakini