Singida yauzwa rasmi kwa mafisadi

Singida yauzwa rasmi kwa mafisadi

MADORO

Senior Member
Joined
Nov 12, 2011
Posts
198
Reaction score
117
Wanaharakati wa Tanzani, Wanasheria, Wanasiasa. Kesho ni siku rasmi ya kuanza kudanganywa wananchi wa vijiji vya Kisaki, Ughaugha A, Ughaugha B, Unyamikumbi A, Unyamikumbi na Kisasida kuanza kuombwa watoe ardhi kwa kampuni inayoitwa WIND EAST AFRICA inayotarajia kuhamisha vijiji sita.

Kampuni hiyo ikiwa bado haina eneo Singida, imebebwa na Mkuu wa Mkoa wa Singida mpaka akatoa matusi kwa wananchi, Serikali yetu kupitia TIC ilitoa Certificate of Insentive kabla kampuni haijapewa eneo, Ewura walitoa leseni ya kuikubalia kampuni hiyo kuanza uzalishaji, na Tanesco walianza Power Purchasing Agreement bila kampuni kuwa na eneo. Ramani ilichorwa na kampuni hiyo licha ya Mkurugenzi wa Manispaa kusema kuwa haina eneo kauli inayopingana na Mkuu wa Mkoa huo.

Pamoja na juhudi za Vilio hivyo hakuna Mwanaharakati aliyeingilia kuwasaidia wanavijiji hawa, wala Mwanasiasa aliyewasaidia hawa wasiojua hata sheria zilizokiukwa
 
Mradi huo nimrusikia lakini naamini Tundu Lissu yupo atawatetea watu wa Singida.
 
Hapo kwa wanaSingida hakuna lenu mwekezaji ananguvu kuliko ninyi waulizeni watu Wa Nyamongo.
 
Singida imelala sana labda wananchi wataanza kuamka maana wanawapigia kura magamba.
 
Mkiletewa umeme shida msipoletewa umeme shida.

Kuhamishwa watu kwa ajili ya kuleta maendeleo ni kitu cha kawaida duniani. Unafikiri maendeleo yanakuja kwa kuota kama miti?

Wacheni kulala, amkeni. Mnaletewa umeme, mnaanza ooh Singiga imeuzwa, imeuzwa imepelekwa wapi? kuwa na fikra japo kidogo.
 
Hivi Sheria gani inavunjwa hapa?

Huoni hapo watu hawana eneo la kuwekeza kibali wamepata, jiulize una kibali cha kuchimba madini lakini hujui ukachimbe wapi huoni ni vichekecho? Kuna kila dalili ya rushwa hapo.
 
Tatizo siyo umeme unaousemea wewe, tatizo ni ukiukwaji wa sheria ambao kama hujauona basi tena!!!!!
Hakuna mtu anayepinga uwekezaji.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mnyampaa Ifaghaa mie pia niko Singida! ninavyofahamu mie ni kuwa watu watalipwa fidia kama ulivyosema mwenyewe..!! kama kutakuwa na mwenendo tofaut na huu then activists have to do something.!
 
Du komaeni mlipwe fidia nzuri,swala la maendeleo ni jambo zuri sema mwambieni mb(mp) wenu awasimamie vizuri mpate mafao
 
Ni vigumu sana kuamini kuwa mwekezaji huyo ameletwa kwa namna hii ambayo mleta mada anasimulia. lakini kwa mambo ya Tanzania, hakuna kisichowezekana... ama kwa hakika tumerogwa na aliyeturoga alishafariki, sijui nani atatuagua
 
KAFUMU mwizi tu huyo wala hatoweza kuwasaidia chochote.kama alikula rushwa na jairo kwanini hapo pia asiwapige changa la macho???????chagueni CHADEMA ndio wanaosimamia haki sawa kwa kila mtu tena kwa watu wa hali ya chini kama hao wa singida.anywayTUNDU LISU yupo atawapigania msijali.hakuna asiependa maendeleo alakini haki itendeke sio kuwaburuza watu kwa ujira usio lingana na mnachotaka kutoka kwao.
 
Jamani shida iko wapi? kama wanalipwa fidia mi naona its okay. Kama hawalipwi hiyo siungi mkono. Acha hawa jamaa wajenge mitambo yao, watu wapate sehemu ya kujifunzia technolojia wa umeme wa upepo. Nchi yenyewe tuko nyuma, tuna upepo kibao lakini hatuutumii ipasavyo!! Wind is free, ni mitambo tu unaanza kuwasha.
 
Tatizo siyo umeme unaousemea wewe, tatizo ni ukiukwaji wa sheria ambao kama hujauona basi tena!!!!!
Hakuna mtu anayepinga uwekezaji.

Hakuna ukiukwaji wa sheria hapo, hao watu wanahamisha na wanakuwa "compensated", wanahamishwa bila kulipwa?

Wacheni kulala katafuteni kazi kwenye hizo kampuni, zinalipa vizuri. Mnaletewa maendeleo mnalalamika, hata siwaelewi mu watu wa aina ipi? Sheria za Tanzania hazizuwii maendeleo, yanahamishwa makaburi kwa kufuatwa sheria itakuwa watu walio hai? wacheni chokochoko na ufataani.

Huyo anaeleta ufataani humu mbona hajasema kuhusu barabara ya Dodoma - Singida - Shinyanga na Singida - Dareda - Arusha, wamehamishwa watu wengi sana kupisha barabara mbona alikaa kimya?

Umeme wa upepo unahitaji utafiti wa kina wa kujuwa upepo unapopatikana kwa kasi fulani kwa mwaka mzima unapatikana wapi na hapo sehemu iliyochagiliwa ndio pameonekana panafaa zaidi, mnachotaka ni nini?

Ngojeni na hivi karibuni kuna kampuni zinakuja, moja ya dhahabu, nayo inahitaji eneo kubwa tu na moja ya uranium pale karibu na Manyoni, ndio mseme vizuri.
 
Hakuna ukiukwaji wa sheria hapo, hao watu wanahamisha na wanakuwa "compensated", wanahamishwa bila kulipwa?

Wacheni kulala katafuteni kazi kwenye hizo kampuni, zinalipa vizuri. Mnaletewa maendeleo mnalalamika, hata siwaelewi mu watu wa aina ipi? Sheria za Tanzania hazizuwii maendeleo, yanahamishwa makaburi kwa kufuatwa sheria itakuwa watu walio hai? wacheni chokochoko na ufataani.

Huyo anaeleta ufataani humu mbona hajasema kuhusu barabara ya Dodoma - Singida - Shinyanga na Singida - Dareda - Arusha, wamehamishwa watu wengi sana kupisha barabara mbona alikaa kimya?

Umeme wa upepo ubahitaji utafiti wa kina wa kujuwa upepo unapopatikana kwa kasi fulani kwa mwaka mzima unapatikana wapi na hapo sehemu iliyochagiliwa ndio paeonekana panafaa zaidi, mnachotaka ni nini?

Ngojeni na hivi karibuni kuna kampuni zinakuja, moja ya dhahabu, nayo inahitaji eneo kubwa tu na moja ya uranim pale karibu na Manyoni, ndio mseme vizuri.

Wanakuwa compensated wapi banaaa!!!...Wacha hizo FF hujayasikia malalamiko ya Watanzania waliondolewa mkuku ili kuipisha Barrick na hadi hii hawajalipwa mafao yao ya kunyang'anywa ardhi? Malalamiko kama hayo yako sehemu chungu nzima nchini ambazo hawa wageni wameingia nchini kwa kivuli cha uwekezaji.

Nguvu ya Hoja:Wawekezaji kwenye ardhi wadhibitiwe

Mkiletewa umeme shida msipoletewa umeme shida.
Kuhamishwa watu kwa ajili ya kuleta maendeleo ni kitu cha kawaida duniani. Unafikiri maendeleo yanakuja kwa kuota kama miti
Wacheni kulala, amkeni. Mnaletewa umeme, mnaanza ooh Singiga imeuzwa, imeuzwa imepelekwa wapi? kuwa na fikra japo kidogo.

Singida kuna upepo lakini hakuna sio mkubwa wa kufanya nchi hii iuze vijiji! Huu umeme utakuwa very unreliable and it is only a matter of time kabla watu hawajaanza kulaumiana. Jingine ambalo watu wanakaa kimya ni capital & maintance cost. Huu mradi ni sawa na CASH COW.

Kama ni mambo ya renewable energy Tanzania ingeangalia zaidi kwenye Solar. Jua lipo January to January lakini upepo una-flactuate vibaya sana. Lakini ndio hivyo wabunge wengi wa ccm toka huo Mkoa wameshaingiza mikono na miguu yao na Tanesco wame-sign!
 
Mkiletewa umeme shida msipoletewa umeme shida.

Kuhamishwa watu kwa ajili ya kuleta maendeleo ni kitu cha kawaida duniani. Unafikiri maendeleo yanakuja kwa kuota kama miti?

Wacheni kulala, amkeni. Mnaletewa umeme, mnaanza ooh Singiga imeuzwa, imeuzwa imepelekwa wapi? kuwa na fikra japo kidogo.

Ni kweli FF tunahitaji umeme. Ila sheria zote za nchi ni vema zikazingatiwa na anayewekeza. Maana yale tunayoyaona Nyamongo si mambo mema hata kidogo. Kule vurugu imekuwa sehemu rasmi ya maisha yao
 
Ni vigumu sana kuamini kuwa mwekezaji huyo ameletwa kwa namna hii ambayo mleta mada anasimulia. lakini kwa mambo ya Tanzania, hakuna kisichowezekana... ama kwa hakika tumerogwa na aliyeturoga alishafariki, sijui nani atatuagua
Mpita Njia,
Sio tumejiroga wenyewe kwa kuamua kuwaachia matapeli wachache wafikiri na kuamua kwa niaba yetu?
 
Back
Top Bottom