Singida: Watu 14 wafariki na watatu kujeruhiwa ajali ya Lori na hiace

Emmanuel Robinson

JF-Expert Member
May 29, 2013
1,503
1,139
Haya maisha haya tuendelee kumuomba Mungu anatulinda sana hapa nimetoka kushuhudia ajali mbaya hapa Singida, Hiace na semi trailler. Hiace hautamani kuitazama mara mbili. Yaani polisi ndiyo wanawapanga barabarani mimi nimeshuhudia miili sita dah huzuni maisha ya watu🙆🏿‍♂️😭😭😭. Mimi napita tu basi so msiniombe picha.

======

Ajali ya Lori aina ya Scania na Hiace imeacha watu 14 wakifariki dunia na watatu majeruhi. Ajali hiyo imetokea Kijiji cha Mkiwa wilaya ya Ikungi majira ya saa 9:30 Alasiri.

Dereva wa Hiace alitaka kulipita 'overtake' gari la mbele yake bila mafanikio na kukumbana na lori uso kwa uso.

Majeruhi watatu wanatibiwa hospitali ya wilaya ya Manyoni.
 
HAKUNA AJALI NZURI, kwahiyo huu msemo AJALI MBAYA UONDOENI.
Bora umefanya hivyo kutoweka picha,
 
Mungu awatangulie….
 
Dah mwisho wa mwaka huu😥😥
Mungu awape imani, uvumilivu na utulivu wafiwa
Pole kwa majeruhi
Marehemu walale salama
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…