Singida tumesahaulika

Singida tumesahaulika

Mmesahaulika vipi wakati mna mawaziri wanne ktk mkoa mmoja ambao wana uwezo wa kuwasemea kwa mawaziri wenzao kuhusiana na changamoto ulizozitaja

1. Mwigulu Nchemba - Waziri Wa sheria na katiba mbunge Iramba Magharibi

2. Kitila Mkumbo- Waziri wa uwekezaji, mbunge wa Ubungo ila ni mzaliwa kata ya Mtoa Iramba Magharibi

3. Doroth Gwagima- Waziri Afya mzaliwa Shelui Iramba Magharibi

4. Palamagamba Kabudi- Waziri Mambo Nje - Mzaliwa Manyoni mgogo upande wa Baba.

Sasa Mungu awape nini
Loudspeaker haina uwezo wa kuiamrisha mic.
 
Ndugu wanajukwaa wote mnajua kabisa katikati ya nchi yetu ni wilayani Manyoni mkoani Singida na tena Singida ni njiapanda ya majiji Kama Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma hivyo ilipaswa itengenezwe kisasa lakini kiukweli hali sio nzuri sana kuanzia miundominu mpaka huduma Kama za afya. Mfano katika barabara ya kushusha sokoni pale wanapouza kuku mkabala na maduka ya Mo Dewji barabara libovu lipo mjini Katikati.

Kitu kingine ni jengo la makao ya CCM mkoa aibu tupu kwa viongozi Bila kusahau jengo la TRA halivutii halijawahi kupigwa rangi lipendeze huduma ya umeme nayo sio nzuri kwa maeneo ya Singida Kaskazini mpaka Mkalama maeneo mengi bado giza.

Nakuomba mheshimiwa Rais wajina wangu John Pombe ukimaliza Chato mkoa wa kuangalia uwe Singida tuzingatie sana kwenye barabara za mitaani maana naona viongozi wetu wa ngazi za mtaa wameshindwa.

La mwisho ni ajira kwa vijana. Sisi wanasingida ni wachapakazi na tuna uwezo mkubwa sana tutengenezee mazingira ya ajira tuache kuzurura mitaani.
Rais wa chato huyo tutafute sasa rais wa Tz tumechoka.
 
Back
Top Bottom