Singida: Mwalimu Mkuu na Msaidizi wake wavuliwa vyeo na kukamatwa kwa wizi wa vifaa vya Ujenzi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
MKUU wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amemwagiza Mkurugenzi wa Halmshauri ya Singida Dc Ndugu Rashid Mwandoa kumvua cheo Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mwachambia, Edward Ighonde pamoja na Mwalimu Mkuu Msaidizi Charles Mtiko Kwa tuhuma ya wizi wa vifaa vya ujenzi wa nyumba ya walimu (Two in one).

Vifaa vinavyodaiwa kuibiwa ni mbao za kupauliwa, Saruji na nondo ambayo thamani yake bado haijafahamika.

Dkt. Nchimbi ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kwa lengo la kukagua miradi ya maendeleo ya ujenzi ambapo watuhumiwa wote wako Polisi.

Aidha ametoa maagizo kwa viongozi kuacha tabia ya kuwatetea watumishi wanao tuhumiwa kwa ubadhilifu na atakaye bainika atashughulikiwa vilivyo.

Nchimbi amewataka viongozi wa Serikali kusimamia miradi na kuwa waminifu katika fedha zinazoletwa na Serikali ya Rais Magufuli pia wananchi wa hakikishe wanalinda mali hizo kwani miradi hiyo ni kwa ajili ya maendeleo yao.
 
Aidha ametoa maagizo kwa viongozi kuacha tabia ya kuwatetea watumishi wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu, na atakayebainika atashughulikiwa vilivyo.

Nadhani Mr Mzungu huko Ubelgiji akipata hiyo!
 
walimu ndio wakuonewa...
huenda angemuuliza vizuri huenda mwalimu alienda kuweka sehemu salama!
 
Aidha ametoa maagizo kwa viongozi kuacha tabia ya kuwatetea watumishi wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu, na atakayebainika atashughulikiwa vilivyo.

Huyo Dr. Wa mifugo au?

Hajui kwamba hata majambazi na wauaji wanatetewa na mawakili...

Hawa ndio wakuu wanao tembea na bakora kucharaza watuhumiwa kabla ya maamuzi ya mahakama..
 
Mwalimu badala ya kupewa kazi za kufundisha anapewa majukumu ya kusimamia ujenzi!
Mwalimu atolewe haraka sana lock up akafundishe.Wanasiasa achaneni na kujipendekeza na ushambua wa kijinga.
Nhvgyuimxg
 
Back
Top Bottom