DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,129
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa amekasirishwa na kitendo cha wafugaji Wilaya ya Iramba mkoani Singida kuijeruhi vibaya kwa panga familia ya watu wawili wanaofanya shughuli za
kilimo Wilayani humo.
Amebaini hayo kwenye ziara zake za kusikiliza na kutatua changamoto za wafugaji na wavuvi nchini ambapo mmoja wa wakulima wa Wilaya hiyo Bw. Mkoma Mustapha alielezea namna wafugaji walivyomshambulia yeye na mtoto wa kaka yake, ambapo Dkt. Bashiru ameielekeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Iramba igharamie matibabu yote ya Mkulima hiyo ikiwa ni pamoja na kurejesha gharama alizotumia mpaka sasa.