Imeripotiwa kuwa Singasinga wa IPTL ametoweka kwa kuogopa mkono wa dola(Raia Mwema,leo 10.09.2014).
Je,unafikiri kuna uhusiano wowote kati ya kusuasua kutekelezwa kwa maazimio ya bunge na kutoweka kwa bwana Seth Singh?
Na baada ya kutoweka anaweza kurudi tena nchini au atafuata nyayo za homeboy wake Daudi Balali?
==============================
Haya yote ndio majibu halisi ya Uchochoro wa KATIBA PENDEKEZWA (YA CCM), iliyoandikwa na CHENGE na CCM wameapa kuilinda kwa mitutu ya Bunduki na kumwaga damu, ili wezi kama hawa na waliojaa ndani ya CCM waendelee kuachiwa watokomee kumbe tu ni kutokana na 'uzito na ubovu' wa mihimili ya dola isiyokuwa na watekelezaji wenye uzalendo. Haya yote yalionyeshwa madhaifu yake ktk RASIMU YA 2 YA JAJI WARIOBA! Ila vipofu na walafi wakayang'oa ili waendelee kuidhoofisha nchi kwa kutumia 'matobo' yaliyojaa ktk hii KARIBA iliyopo na ILIYOPENDEKEZA NA CCM!! No way! JK ameonyesha wazi kuwa hawawezi au ni sehemu yao wanaoangamiza urithi wetu.
Maneno bila Matendo ni dalili za kuelekea kifo...ndio maana matendo yanahitajika haraka ili kuondoa tabaka hili lililojaa uovu na kionyesha wazi kuwa maovu yao hayavumiliki tena!!
mkono upi wa dola? hata akikamatwa, mahakamani alishatanguliza zaidi ya milioni 400.....unadhani zile milioni 400 ni za jaji mmoja tu? ule ni mgao wa systems yote.....hujiulizi kwa nini JK anagugumia kuchukua hatua? mfumo wote ni hovyo, anavuta pumzi tu muda ufike amtwishe mwingine msala.
Kama CCM ingekuwa makini ingewavua uanachama watuhumiwa wote kuanzia Chenge, Ngeleja, Tibaijuka etc. Hii ingethibitisha uadilifu ndani ya chama. Lakini kuwaambia wajiuzulu tu halafu kuendelea kuwaambia wajivue ghamba si kusimamia maafili ndani ya chama. Ni kuwapeleka watuhumiwa honey moon wakatumbue walizoiba
Jambo la msingi kwa sasa kufanya ni kukubali matokeo na hili suala na mengine yote kuachana nayo kwa sasa na kuwatangaza Watawala kuwa ni washindi dhidi ya wananchi. Tukubali tuu kuwa wao ni wajanja kwa sasa na sisi wananchi ni mbumbumbu tusio na uwezo wa kufanya chochote hata kama kwa katiba iliyoko sasa inasema mamlaka yote yatatoka kwa wananchi.
Lakufanya kwa sasa ni wale watendaji wazalendo watutunzie ushahidi kwa kadri watakavyo weza na sisi wananchi October 2015 tuitendee haki nchi yetu kwa kuweka viongozi watakaoweza kuja kuliendeleza hili tuliloshindwa sasa hivi. Kesi za jinai huwa hazichachi na hayo tumeyaona Zambia,Malawi,Nigeria na kwingineko.
Ila najiuliza sana mkulu na timu yake hawapendi kuja kupumzika kwa furaha na amani pamoja na familia yake kama mzee Mwinyi? Kama kuna wazee wenye mapenzi mema naye hebu wamshauri kuwa hao "washauri" wake wa sasa wanampotosha kabisa.
Ana washauri basi mpwa? Washauri wote wamehusika katika kupokea mgao wa pesa za wizi kuanzia milioni 400 hadi bilioni 5. Watendaji wote wa Ikulu ni wa kufukuza kisha na yeye ajiuzulu.
Ndio maana Mkulu anasema eti tusomewe kwanza report ya CAG.....hivi sijui washauri wake ni akina anani huko, haya leteni na mikataba ya Gesi nayo tusome
Ahhhhhhhhhhhhhhhh Wapi ,kwani kwao si kule Kagilonga?Au amehama siku hizi?Jamani mbona mnamsingizia huyu Mnyalukolo mwenzetu,mtanzania mwenzetu,mwema kabisa,muwezkezaji mwenye uwezo wa kununua hata serikali yetu akaiweka mfukoni,kweli kaka!!!!!!!!!!!!!Sasa ana uraia wa nchi ngapi huyu Mnyalukolo?
Mara SA,mara KQ duhhhMnyalukolo wangu unatuacha tuendeleaa kugombana wenzio maana miradhi ya bibi inaelekea umibeba na kugawa kwa wajukuu wachache wa Marehemu bibi!:A S-frusty::A S-frusty::sad::sad:
MMILIKI wa kampuni ya IPTL, Harbinder Sethi Singh, ametoweka na vyombo vya usalama vimejiandaa kumkamata endapo atarejea nchini, Raia Mwema limeelezwa.
Singh ambaye kampuni yake ya Pan African Power Solutions (PAP) inadaiwa kununua umiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL katika mazingira yaliyozua utata, anadaiwa kuwa yupo nchini Kenya au Afrika ya Kusini.
Gazeti hili lilielezwa kwamba Singh aliondoka nchini siku chache kabla ya Bunge la Tanzania kutoa maazimio yaliyotaka wahusika wote wa makosa ya kijinai katika suala hilo wakamatwe na hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe.
Azimio namba moja la Bunge lilisema;….. "Takukuru, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya Ulinzi na Usalama viwachukulie hatua stahiki za kisheria, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, watu wote waliotajwa na Taarifa Maalumu ya Kamati kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya Escrow, na watu wengine watakaogundulika kuhusika katika vitendo hivyo vya jinai kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea".
Raia Mwema limeelezwa kwamba Singh ambaye katika siku za nyuma alikuwa akipenda kufikia katika hoteli tofauti ikiwamo Sea Cliff ya jijini Dar es Salaam, sasa hayupo Dar es Salaam lakini anafuatilia kwa karibu yanayoendelea.
"Naweza kukuthibitishia kwamba Sethi hayupo nchini hivi sasa. Kwenye hili suala sitaki kuwa mzungumzaji wake lakini nafahamu kwamba aliondoka kabla ya Bunge kuazimia wahusike wakamatwe.
"Sasa kama alifanya hivyo kwa kujua hayo yanaweza kutokea mimi sijui. Siwezi pia kujibu swali lako la atakuja lini kwa sababu sijaambiwa. Hata hili la kukwambia kwamba hayupo nimekwambia kwa sababu tunafahamiana na sitaki kukudanganya," alisema mmoja wa watu wafanyakazi wa Seth ambaye hata hivyo gazeti hili haliwezi kumtaka jina.
Mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege, ambaye pia ndiye msemaji wa kampuni hiyo, hakupokea simu wala kujibu ujumbe mfupi wa maneno kupitia njia ya simu aliyoandikiwa na gazeti hili tangu juzi.
Hata hivyo, gazeti hili limeambiwa kwamba vyombo vya usalama vinafahamu Seth hayupo na vimejipanga kumkamata endapo atarejea nchini ili ajibu tuhuma zinazomkabili.
Msemaji wa Takukuru, Doreen Kapwani, hakutaka kuthibitisha wala kukana kuhusu mpango wa taasisi hiyo kumkamata Singh, kwa maelezo kwamba kwa sasa yuko likizo na hana taarifa rasmi. "Ningeshauri umtafute Mkurugenzi Mkuu, Dk. Edward Hoseah, ili akupe taarifa rasmi. Mimi niko likizo na hivyo sina taarifa zozote. Mkurugenzi anaweza kuwa na taarifa mpya zaidi," alisema Kapwani.
Ingawa Seth ni mzaliwa wa Iringa, Tanzania, anaishi nchini Afrika Kusini ambako inaelezwa anafanya biashara; akitajwa kuwa mshirika muhimu wa kibiashara wa mtoto wa Rais mstaafu wa Kenya, Daniel Moi, aitwaye Gideon Moi.
"Hatuwezi kutangaza kwamba tutamkamata Singh. Hii itamfanya ajifiche huko aliko na asije. Wewe subiri arudi uone. Wengine waliopo hapa nchini ambao tutahitaji kuwakama tutawakamata tu. Ngoja kwanza tuanze naye huyo," alisema mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina.
Nchini Kenya, Singh anafahamika kama mmoja wa wahusika katika ufisadi wa Goldenberg ambako yeye na baadhi ya wafanyabiashara kama Kamlesh Pattni na familia ya Moi walihusishwa nayo.
Katika kipindi cha wiki iliyopita, Singh amezungumza na baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini ambapo katika mahojiano yake yote, amekataa kueleza alipo.
Baadhi ya tuhuma ambazo zinamkabili Singh moja kwa moja kutokana na maazimio ya Bunge ni madai ya kukwepa kulipa kodi, kughushi nyaraka na kutakatisha fedha haramu. Chanzo cha habari cha gazeti hili kimeeleza kwamba Singh hana pa kukimbilia zaidi ya Kenya au Afrika Kusini ambako kimsingi ndiko kwenye biashara zake na makazi yake.
Singh alikwenda nchini Kenya kwenye miaka ya 1980 ambako alifanikiwa kujiingiza kwenye familia ya Moi na kutengeneza urafiki na baadhi ya wanasiasa wenye nguvu na ushawishi nchini humo kama Nicholas Biwott.
Mbali na IPTL, Singh tayari ameingia katika biashara ya kutafuta mafuta katika Visiwa vya Songosongo, eneo la Mnazi Bay, ambako yeye ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Hydrotanz ambayo inaendeshwa kwa ubia na kampuni ya Adhunik.
Suala la Singh limefika hapa kutokana na kazi ya uchunguzi iliyofanywa na Takukuru pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo iliwasilishwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo ilichambua taarifa hizo na kisha kuzipeleka bungeni. PAC ilipendekeza Sethi akamatwe na kuhojiwa kutokana na tuhuma mbalimbali kama vile utakatishaji wa fedha, kukwepa kulipa kodi na udanganyifu lakini maazimio ya Bunge ndiyo yaliyojumuisha na wahusika wengine katika suala hilo.
Katika gazeti hili wiki iliyopita, iliripotiwa kwamba mtu wa karibu zaidi na Sethi hapa Tanzania kwa sasa anafahamika kwa jina la Rajiv Bhesania, ambaye jina lake limeonekana katika miamala iliyofanywa kupitia akaunti ya PAP ya Benki ya Stanbic ya hapa nchini ambayo inafanyiwa uchunguzi kwa sasa.
"Kama Serikali inataka kupata chochote kutoka kwa Sethi inabidi wambane huyuhuyu Rajiv Bhesania. Yeye ndiye kila kitu kwa Sethi hapa Tanzania. Hata akitaka mambo yake yanyooke mahali huwa anamtumia huyu.
"Nafahamu si rahisi kusema kila kitu lakini nafahamu kwamba kama vyombo vya ulinzi vitambana kisawasawa, anaweza kutoa siri zote za Sethi na hatimaye Watanzania wakapata wanachokitaka," alisema mfanyakazi huyo wa IPTL.
Ni katika benki hiyo ndiko ambako muamala wenye thamani ya shilingi bilioni 73.5 ulifanyika siku ya Januari 23 mwaka huu; muamala ambao sasa ndio unachunguzwa na vyombo vya ulinzi. Ripoti za CAG na Takukuru zilieleza kwamba kuna watu waliondoka katika ofisi za benki hiyo wakiwa na magunia yaliyojaa fedha.
"Kwa mujibu wa Takukuru baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa (Stanbic) wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa," ilisema sehemu ya ripoti iliyowasilishwa bungeni na PAC.
Muamala huo unachunguzwa vikali na Takukuru pamoja na ule wa Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi jijini Dar es Salaam ambapo kiasi cha shilingi bilioni 3.3 zinadaiwa pia kuchukuliwa kwa siku moja.
Habari hizi za Stanbic kuhusishwa na fedha za Escrow zimesababisha benki hiyo kumpa uhamisho aliyekuwa Meneja wake, Paul Omara, ambaye sasa anadaiwa kurejeshwa nchini Uganda.
Omara anaelezwa kuitumikia benki hiyo kwa muda wa miaka zaidi ya 11 na Raia Mwema limeelezwa kwamba ofisa huyo tayari amehojiwa na Takukuru kuhusu suala hilo kabla hajaondoka.
Mmoja wa maofisa wa Takukuru aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina kwa maelezo kwamba uchunguzi unaendelea, alisema wamepata ushirikiano mzuri kutoka Stanbic na kuna uwezekano kwamba " watu watakula Krismasi wakati tayari Takukuru ikiwa imemaliza kazi".
Suala la fedha za Escrow lililiteka Taifa wiki iliyopita na sasa wananchi wanasubiri kwa hamu hatua itakayochukuliwa na serikali kuhusu vigogo wanaotajwa kusaidia kutokea kwa kashfa hii.
Nchini Kenya, Singh anafahamika kama mmoja wa wahusika katika ufisadi wa Goldenberg ambako yeye na baadhi ya wafanyabiashara kama Kamlesh Pattni na familia ya Moi walihusishwa nayo. .....
.... Katika gazeti hili wiki iliyopita, iliripotiwa kwamba mtu wa karibu zaidi na Sethi hapa Tanzania kwa sasa anafahamika kwa jina la Rajiv Bhesania, ambaye jina lake limeonekana katika miamala iliyofanywa kupitia akaunti ya PAP ya Benki ya Stanbic ya hapa nchini ambayo inafanyiwa uchunguzi kwa sasa. "Kama Serikali inataka kupata chochote kutoka kwa Sethi inabidi wambane huyuhuyu Rajiv Bhesania. Yeye ndiye kila kitu kwa Sethi hapa Tanzania. Hata akitaka mambo yake yanyooke mahali huwa anamtumia huyu.
Eh, yameshakuwa hayo wakati huyu ni Mhehe wa Ipogolo!
Uzuri wa nchi hii kesi nyingi zinafanana hivyo kuwapa watafiti kazi rahisi ya kufuatilia mambo. Sasa hii inaelekea kufanana na ile ya Mpakistani aliyetorosha twiga ambaye bila hata chembe ya soni imetolewa hukumu kwa jina ambalo hakuna uhakika kama ndilo lenyewe, hakuna picha yake na kuna rekodi kuwa alikamatwa lakini wadhamini hawajulikani!!!!!!!!
Swala la Goldnberg baada ya kumtight Kamnelshi Patni (mwenye asili ya Asia) mwishowe jamaa akaokoka ndio akaweza kuweka wazi kuwa yeye alikuwa architecture tu na waliokuwa wakimuelekeza ni kutoka ofisi kuu. Mpaka leo halijatolewa maamuzi lakini ukweli ni kuwa halijafa na ni wazi halitakufa na haki huenda ikatendeka kwa wahusika japo wengi ni 'tembo'.
Nakuwa na wasi wasi kama na hapa hii timu ya wabeba viroba, masandarusi nk ambao wanataka kutolewa kafara huenda akatokea mmojawapo akatutajia kuwa Seth kama architecture alikuwa anapokea maelezo kutoka kwa mwenye 'mali na kiwanja' na huenda huyo huyo ndio kamuelekeza 'asepe' zake.
Muda ni rafiki wa ukweli!
Ahofia kukamatwa akirejea Vyombo vya Dola vyamwinda
MMILIKI wa kampuni ya IPTL, Harbinder Sethi Singh, ametoweka na vyombo vya usalama vimejiandaa kumkamata endapo atarejea nchini, Raia Mwema limeelezwa.
Singh ambaye kampuni yake ya Pan African Power Solutions (PAP) inadaiwa kununua umiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL katika mazingira yaliyozua utata, anadaiwa kuwa yupo nchini Kenya au Afrika ya Kusini.
Gazeti hili lilielezwa kwamba Singh aliondoka nchini siku chache kabla ya Bunge la Tanzania kutoa maazimio yaliyotaka wahusika wote wa makosa ya kijinai katika suala hilo wakamatwe na hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe.
Azimio namba moja la Bunge lilisema; .. Takukuru, Jeshi la Polisi na vyombo vingine husika vya Ulinzi na Usalama viwachukulie hatua stahiki za kisheria, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, watu wote waliotajwa na Taarifa Maalumu ya Kamati kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya Akaunti ya Escrow, na watu wengine watakaogundulika kuhusika katika vitendo hivyo vya jinai kufuatia uchunguzi mbalimbali unaoendelea.
Raia Mwema limeelezwa kwamba Singh ambaye katika siku za nyuma alikuwa akipenda kufikia katika hoteli tofauti ikiwamo Sea Cliff ya jijini Dar es Salaam, sasa hayupo Dar es Salaam lakini anafuatilia kwa karibu yanayoendelea.
Naweza kukuthibitishia kwamba Sethi hayupo nchini hivi sasa. Kwenye hili suala sitaki kuwa mzungumzaji wake lakini nafahamu kwamba aliondoka kabla ya Bunge kuazimia wahusike wakamatwe.
Sasa kama alifanya hivyo kwa kujua hayo yanaweza kutokea mimi sijui. Siwezi pia kujibu swali lako la atakuja lini kwa sababu sijaambiwa. Hata hili la kukwambia kwamba hayupo nimekwambia kwa sababu tunafahamiana na sitaki kukudanganya, alisema mmoja wa watu wafanyakazi wa Seth ambaye hata hivyo gazeti hili haliwezi kumtaka jina.
Mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege, ambaye pia ndiye msemaji wa kampuni hiyo, hakupokea simu wala kujibu ujumbe mfupi wa maneno kupitia njia ya simu aliyoandikiwa na gazeti hili tangu juzi.
Hata hivyo, gazeti hili limeambiwa kwamba vyombo vya usalama vinafahamu Seth hayupo na vimejipanga kumkamata endapo atarejea nchini ili ajibu tuhuma zinazomkabili.
Msemaji wa Takukuru, Doreen Kapwani, hakutaka kuthibitisha wala kukana kuhusu mpango wa taasisi hiyo kumkamata Singh, kwa maelezo kwamba kwa sasa yuko likizo na hana taarifa rasmi.
Ningeshauri umtafute Mkurugenzi Mkuu, Dk. Edward Hoseah, ili akupe taarifa rasmi. Mimi niko likizo na hivyo sina taarifa zozote. Mkurugenzi anaweza kuwa na taarifa mpya zaidi, alisema Kapwani.
Ingawa Seth ni mzaliwa wa Iringa, Tanzania, anaishi nchini Afrika Kusini ambako inaelezwa anafanya biashara; akitajwa kuwa mshirika muhimu wa kibiashara wa mtoto wa Rais mstaafu wa Kenya, Daniel Moi, aitwaye Gideon Moi.
Hatuwezi kutangaza kwamba tutamkamata Singh. Hii itamfanya ajifiche huko aliko na asije. Wewe subiri arudi uone.
Wengine waliopo hapa nchini ambao tutahitaji kuwakama tutawakamata tu. Ngoja kwanza tuanze naye huyo, alisema mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina.
Nchini Kenya, Singh anafahamika kama mmoja wa wahusika katika ufisadi wa Goldenberg ambako yeye na baadhi ya wafanyabiashara kama Kamlesh Pattni na familia ya Moi walihusishwa nayo.
Katika kipindi cha wiki iliyopita, Singh amezungumza na baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini ambapo katika mahojiano yake yote, amekataa kueleza alipo.
Baadhi ya tuhuma ambazo zinamkabili Singh moja kwa moja kutokana na maazimio ya Bunge ni madai ya kukwepa kulipa kodi, kughushi nyaraka na kutakatisha fedha haramu.
Chanzo cha habari cha gazeti hili kimeeleza kwamba Singh hana pa kukimbilia zaidi ya Kenya au Afrika Kusini ambako kimsingi ndiko kwenye biashara zake na makazi yake.
Singh alikwenda nchini Kenya kwenye miaka ya 1980 ambako alifanikiwa kujiingiza kwenye familia ya Moi na kutengeneza urafiki na baadhi ya wanasiasa wenye nguvu na ushawishi nchini humo kama Nicholas Biwott.
Mbali na IPTL, Singh tayari ameingia katika biashara ya kutafuta mafuta katika Visiwa vya Songosongo, eneo la Mnazi Bay, ambako yeye ni mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Hydrotanz ambayo inaendeshwa kwa ubia na kampuni ya Adhunik.
Suala la Singh limefika hapa kutokana na kazi ya uchunguzi iliyofanywa na Takukuru pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ambayo iliwasilishwa kwa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ambayo ilichambua taarifa hizo na kisha kuzipeleka bungeni.
PAC ilipendekeza Sethi akamatwe na kuhojiwa kutokana na tuhuma mbalimbali kama vile utakatishaji wa fedha, kukwepa kulipa kodi na udanganyifu lakini maazimio ya Bunge ndiyo yaliyojumuisha na wahusika wengine katika suala hilo.
Katika gazeti hili wiki iliyopita, iliripotiwa kwamba mtu wa karibu zaidi na Sethi hapa Tanzania kwa sasa anafahamika kwa jina la Rajiv Bhesania, ambaye jina lake limeonekana katika miamala iliyofanywa kupitia akaunti ya PAP ya Benki ya Stanbic ya hapa nchini ambayo inafanyiwa uchunguzi kwa sasa.
Kama Serikali inataka kupata chochote kutoka kwa Sethi inabidi wambane huyuhuyu Rajiv Bhesania. Yeye ndiye kila kitu kwa Sethi hapa Tanzania. Hata akitaka mambo yake yanyooke mahali huwa anamtumia huyu.
Nafahamu si rahisi kusema kila kitu lakini nafahamu kwamba kama vyombo vya ulinzi vitambana kisawasawa, anaweza kutoa siri zote za Sethi na hatimaye Watanzania wakapata wanachokitaka, alisema mfanyakazi huyo wa IPTL.
Ni katika benki hiyo ndiko ambako muamala wenye thamani ya shilingi bilioni 73.5 ulifanyika siku ya Januari 23 mwaka huu; muamala ambao sasa ndio unachunguzwa na vyombo vya ulinzi.
Ripoti za CAG na Takukuru zilieleza kwamba kuna watu waliondoka katika ofisi za benki hiyo wakiwa na magunia yaliyojaa fedha.
Kwa mujibu wa Takukuru baadhi ya watu walienda kugawana fedha kwenye Benki tajwa (Stanbic) wakiwa na mifuko ya rambo, sandarusi, maboksi, magunia na lumbesa, ilisema sehemu ya ripoti iliyowasilishwa bungeni na PAC.
Muamala huo unachunguzwa vikali na Takukuru pamoja na ule wa Februari, 2014 katika Benki ya Mkombozi jijini Dar es Salaam ambapo kiasi cha shilingi bilioni 3.3 zinadaiwa pia kuchukuliwa kwa siku moja.
Habari hizi za Stanbic kuhusishwa na fedha za Escrow zimesababisha benki hiyo kumpa uhamisho aliyekuwa Meneja wake, Paul Omara, ambaye sasa anadaiwa kurejeshwa nchini Uganda.
Omara anaelezwa kuitumikia benki hiyo kwa muda wa miaka zaidi ya 11 na Raia Mwema limeelezwa kwamba ofisa huyo tayari amehojiwa na Takukuru kuhusu suala hilo kabla hajaondoka.
Mmoja wa maofisa wa Takukuru aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina kwa maelezo kwamba uchunguzi unaendelea, alisema wamepata ushirikiano mzuri kutoka Stanbic na kuna uwezekano kwamba watu watakula Krismasi wakati tayari Takukuru ikiwa imemaliza kazi.
Suala la fedha za Escrow lililiteka Taifa wiki iliyopita na sasa wananchi wanasubiri kwa hamu hatua itakayochukuliwa na serikali kuhusu vigogo wanaotajwa kusaidia kutokea kwa kashfa hii.
Yaani nashangaa sana vyombo vya usalama na polisi ,wezi wametajwa bungeni ,tena wezi walioiba serikalini ushahidi umejaa na mashahidi wapo sasa mnasuasua nini ,mboni hamuwakamati ,mpaka lini >Mnamuogopa nani ?
Singasinga kishatingisha masharubu hayupo zamani ,masharubu yalimcheza na mapema na kuona kishanuka ,leo hii imebaki kubahatisha yupo Kenya ,yupo SouthAfrica ,longolongo tupu ,mmeshamuachia akimbie nina wasiwasi na hawa wengine mnawahimiza wakimbie na bila ya shaka mnakereka sana kuwepo mitaani ,wanawaharibia kazi au vipi ?
Hivi siku mtakayoamua kuwakamata (Najua hamfundishwi kazi ila sijui kwanini mkawahitaji polisi jamii) mkaambiwa walishapanda mapipa kila mmoja na directiona yake mtawambiaje wananchi au mnasubiri Mheshimiwa KIkwete awambie haya basi wakamateni ??
hapo ndio ujue kuwa kuna ushirikiano na wausika, kama mnakumbuka RADAR yule muhindi sijui alikuwa Upanga wakati bomu la Radar linafumuka, watu kibao wakashauri wamkamate mhusika kwani atakimbia, serikali ikaonyesha kigugumizi kikubwa na kweli baada ya muda akakimbia. wewe leo ukisingiziwa wizi unajua wazi utalala jela lakini ukishirikiana na wanasiasa watakwambia hakuna ushahidi, ohoo huwezi kumkata mtu kwa kusikia tu kwahiyo nchi hii kuna standard mbili ya wanyonge na wezi vigogo
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.