Singasinga wa IPTL, Harbinder Singh Sethi atoweka

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,651
Imeripotiwa kuwa Singasinga wa IPTL ametoweka kwa kuogopa mkono wa dola(Raia Mwema,leo 10.09.2014).
Je,unafikiri kuna uhusiano wowote kati ya kusuasua kutekelezwa kwa maazimio ya bunge na kutoweka kwa bwana Seth Singh?
Na baada ya kutoweka anaweza kurudi tena nchini au atafuata nyayo za homeboy wake Daudi Balali?
==============================

Mmiliki wa kampuni ya IPTL,Harbinder Seth, ametoweka na vyombo vya usalama vimejiandaa kumkamata ndapo atarejea nchini, Raia mwema limeelezwa.Singh ambayekampuni yake ya Pan african Power solution (PAP) inadaiwa kununua umiliki wa kampuni ya kufua umeme ya IPTL katika mazingira yaliyozua utata, anadaiwa kuwa yupo nchini Kenya au Africa ya Kusini.

Gazeti hili limeelezwa kwamba Singh aliondoka nchini siku chache kabla ya bunge la Tanzania ya wahusika wote wa makosa ya kijinai katika suala hilo wakamatwe na hatua za kisheria dhidi yao zichukuliwe.

Azimio namba moja la Bunge lilisema;....Takukuru, Jeshi la polisi na vyombo vingine husika vya Ulinzi na usalama viwachukule hatua stahiki za kisheria, kwa mujibu wa sheria za nchi yetu,watu wote waliotajwa na Taarifa maalumu ya kamati kuhusika na vitendo vyote vya kijinai kuhusiana na miamala ya akaunti ya Escrow, kuhusika katika vitendo hivyo vya jinai kufuatia uchunguzi mbalmbali unavyoendelea.

Raiamwema limeelezwa kwamba, singh ambaye katka siku za nyuma alikua akipenda kufika katika hotel mbalimbali ikiwemo Sea cliff ya Jijini dar es salaam, Sasa hayupo Dar es salaam lakini anafuatilia kea karibu yanayo endelea.

Naweza kukuthibitishia kwamba sethi hayupo nchini hivi sasa. Kwenye hili swala sitaki kuwa mzungumzaji wake lakini nafahamu kwamba aliondoka kabla ya Bunge kuazimia kwamba wahusika wakamatwe.

"Sasa kama alifanya akijua kwamba hayo hayo yanaweza kutokea mimi sijui. Siwezi pia kujibu swali lako la atakuja lini sabau sijaambiwa. Hata hili la kukuambia kwamba hayupo nimekwambia kwa sababu tunafahamiana na sitaki kukudanganya, Alisema mmoja wa watu wafanyakazi wa Sethi ambaye hata hivyo gazeti hili haliwezi kumtaja jina
 
JK alikuwa anamfanyia mbinu za kusepa ndiyo maana hajatoa maamuzi yoyote.
Singasinga hatabalaliwa ila atabadilisha jina tu
 
Imeripotiwa kuwa Singasinga wa IPTL ametoweka kwa kuogopa mkono wa dola(Raia Mwema,leo 10.09.2014).
Je,unafikiri kuna uhusiano wowote kati ya kusuasua kutekelezwa kwa maazimio ya bunge na kutoweka kwa bwana Seth Singh?
Na baada ya kutoweka anaweza kurudi tena nchini au atafuata nyayo za homeboy wake Daudi Balali?
Inadaiwa kutoroka kwake kumefanikishwa na kidogo mmoja bila kupepesa masikio huyo ni Pinda aka Mzee wa nyuki
 
Ndo maana walikuwa wanapinga asikamatwe ili atoroke kwanza
Mimi nakubaliana kabisa na wewe mkuu. Walikuwa wanamtafutia mazingira ya kuishi kabla ya kuanza kutajataja mambo yake ili asiwepo akitakiwa kukamatwa.

Hata hivyo bado naona giza kwa kauli kinzani toka Ikulu. Katibu Mkuu kiongozi anasema lazima uchunguzi kwanza ufanyike; Mkuu anasema atatoa majibu ndani ya wiki...bado kuna kusigisishana kwa hali ya juu kwa taarifa mbili tofauti toka ofisi moja. Naona jambo hili itabidi libebwe kichama zaidi kuokoa images za wakubwa. Hii inaweza kumaanisha kuwa waliokwapua walikwapua kwa niaba ya chama ndiyo maana ukiwa gamba hata bila kufikiria mara mbili unawatetea hawa jamaa na wizi wao.
 
Ndio maana Mkulu anasema eti tusomewe kwanza report ya CAG.....hivi sijui washauri wake ni akina anani huko, haya leteni na mikataba ya Gesi nayo tusome

Wajua Mkulu anatafuta moto zaidi.Akumbuke huku TANZANIA hatupo wajinga kiasi hiki,ningewaomba WAKAGUZI wawe wazalendo waieleze jamii ya watanzania kwa uelewa wa LAYMAN maana ya ripoti yenyewe bila kumung'nya maneno,maana mwisho wa siku tutajigawa mara nyingine tena baada ya ile Katiba ya Mafisadi kupitishwa kwa kutoshelezwa KURA leo RAIS wetu mpendwa anarudia tena kutugonganisha wananchi wake.

Tunachotakiwa kuwa ni WAMOJA zaidi na ziadi.Wahasibu na Wakaguzi tuwepamoja kuielimisha jamii ili tusitenganishwe tena,Huu ni wakati wetu kulitendea haki TAIFA letu.
 
Vipi Katiba Mpya imeishia wapi?

Katiba mpya unamaanisha PENDEKEZWA aka ya MAFISADI?Kwa sasa sidhani kama kuna MCCM mwenye ubavu wa kuipigia chapuo,unless amepata KIPUPWE cha ESCROW..................
 
Ni kweli kabisa Mpwa wangu, anajua kuwa kitakachosomwa na wachache wetu kitaishia kutuchonganisha zaidi, na kama kweli ana nia ya dhati juu ya hili basi augawe na urais wake tumsaidie kufanya maamuzi. Kweli JK anatuvuruga tu hakuna lolote la maana.
Wajua Mkulu anatafuta moto zaidi.Akumbuke huku TANZANIA hatupo wajinga kiasi hiki,ningewaomba WAKAGUZI wawe wazalendo waieleze jamii ya watanzania kwa uelewa wa LAYMAN maana ya ripoti yenyewe bila kumung'nya maneno,maana mwisho wa siku tutajigawa mara nyingine tena baada ya ile Katiba ya Mafisadi kupitishwa kwa kutoshelezwa KURA leo RAIS wetu mpendwa anarudia tena kutugonganisha wananchi wake.

Tunachotakiwa kuwa ni WAMOJA zaidi na ziadi.Wahasibu na Wakaguzi tuwepamoja kuielimisha jamii ili tusitenganishwe tena,Huu ni wakati wetu kulitendea haki TAIFA letu.
 
Huyu wala tusijisumbue kumtafuta ilimradi mitambo yake ipo hapa, dawa ni kuitaifisha ilikufidia hasara aliyotupa.
 
Singa singa Sethi yuko kwao Iringa. Jana nimemuona hapa Iringa maeneo ya Kihesa
 
Ni kweli kabisa Mpwa wangu, anajua kuwa kitakachosomwa na wachache wetu kitaishia kutuchonganisha zaidi, na kama kweli ana nia ya dhati juu ya hili basi augawe na urais wake tumsaidie kufanya maamuzi. Kweli JK anatuvuruga tu hakuna lolote la maana.

URAIS kaisha ugawa kwa FAMILIA na RAFIKI zake,na sasa hizi group mbili ndizo zinatufanyia maamuzi.Kuumbuka IKULU ndiyo wahusika wakuu,sasa wategemea kipi chemakitoke kwenye JUMBA bovu?Wajua JUMBA bovu lakaa akina nani...kuna vibaka,misheni town,wezi,majangili,madawa ya kulevya na majambazi,hivyo usitegemee MALAIKA atatoka huko.

Na kumbuka SERIKALI pia imebinafsihwa kwa Singasinga ,siumesikia akisimama na kuongea?Miti yote hutikisika na ndege wakakimbia kuepusha balaa...

Uliona wapi MUWEKEZAJI akafika MAHAKAMANI akasema NATAKA SUPIKA,AG na PM wote wakamatwe wawekwe ndani?Nguvu hii kaipata wapi kama hajabinafsishwa IKULU?:shock:
 
Thubutttuuuuuuuuuuu hakuna aisee tena hapo Magogoni Chenge ndio kwanza atapokewa kwa nderemo na vifijo

Na kwenye zile kura zetu za kuwateua wagombea ubunge,lazima atapita tena kwa kasi na nguvu zaidi.Chezea pesa,hivi Mjomba haujui huku kwenye chama chetu bila TAKRIMA haiwezekani?
 
Back
Top Bottom