Sinema ya Ngono za Mashoga Yaonyeshwa Kanisani


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,975
Likes
5,344
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,975 5,344 280
4113390.jpg

Mchungaji Martin Ssempa
Mchungaji wa nchini Uganda anayepigania sheria kali zipitishwe dhidi ya mashoga nchini humo, amewaonyesha waumini wake kanisani sinema ya ngono wanaume wakiwaingilia kinyume cha maumbile wanaume wenzao. Waumini zaidi ya 300 waliojazana kwenye kanisa la mchungaji Martin Ssempa la mjini Kampala nchini Uganda, walishuhudia sinema ya ngono kanisani wanaume wakiwainamisha na kuwaingilia kinyume cha maumbile wanaume wenzao.

"Angalia mwanaume huyu anakula uume wa mwanaume mwenzake", alisema mchungaji Ssempa akitoa maelezo juu ya kipengele kimoja cha video hiyo.

"Je ni haya kweli Obama anataka kutuletea barani Afrika?", alisema mchungaji huyo kufuatia kauli ya Obama kupinga sheria kali dhidi ya mashoga nchini Uganda na kutaka mashoga nao wapewe haki zao.

Mchungaji huyo aliamua kuionyesha sinema hiyo kanisani katika kutafuta kuungwa mkono juhudi zake za kutaka sheria kali dhidi ya mashoga nchini Uganda.

Sinema hiyo ilionyeshwa siku ya jumatano na kuangaliwa na waumini wengi baada ya polisi nchini Uganda kuyafuta maandamano ya watu milioni moja yaliyokuwa yafanyike kuuunga mkono muswada wa kuwahukumu kifungo cha maisha mashoga.

"Tulikuwa tumepanga wanaume na wanawake milioni moja tuandamane kwenye jiji la Kampala lakini tuliambiwa kuwa hatuwezi kuandamana kutokana na sababu za kiusalama", mchungaji Ssempa aliwaambia waumini wake.

"Hivi mnajua ni vitu gani wanavyofanya mashoga wanapokuwa kwenye vyumba vyao?", alisema mchungaji huyo na kuanza kuwaonyesha waumini wake picha za ngono za mashoga.

Mchungaji huyo aliweka video ya picha zinazoonyesha wazi wazi jinsi wanaume wanavyowaingilia wanaume wenzao.

Serikali ya Uganda imekuwa ikipata upinzani mkubwa toka nchi wafadhili ambazo baadhi zimetishia kusitisha misaada yake iwapo Uganda itapitisha muswada wake wa kuwabana mashoga na wasagaji.

Katika mojawapo ya vipengele vya muswada huo, watu wanaowakodisha nyumba mashoga na wasagaji nao pia watakumbana na sheria na watafikishwa mahakamani.

Baadhi ya mashoga watahukumiwa adhabu ya kifungo cha maisha cha maisha na wengine adhabu ya kifo kama muswada huo utapitishwa.
 
T

Tall

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2010
Messages
1,429
Likes
17
Points
0
T

Tall

JF-Expert Member
Joined Feb 27, 2010
1,429 17 0
Sijui kama mchungaji huyu alikuwa anahamasisha au anaonya. Sina shaka juma lililofuata mashoga walijaa kanisani kuona staili mpya hasa kama aliahidi kuuonyesha tena.
 
Bill

Bill

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
4,847
Likes
2,063
Points
280
Bill

Bill

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
4,847 2,063 280
Hii ni staili mpya ya mahubiri, nataraji siku wanandoa watarajiwa watakapokuwa wanapokea semina kwa mchungaji huyu atawawekea mkanda wa namna ya kulishirki tendo la ndoa. Sasa sielewi pale atakapoikosa hiyo mikanda atatumia mbinu gani kutoa mafunzo.

Dunia imekwisha.
 
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
16,231
Likes
346
Points
180
PakaJimmy

PakaJimmy

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
16,231 346 180
repeatition of threads...!
Jamaa aliitoa juzi hadi na mapicha!
Iam afraid you are too late!
 

Forum statistics

Threads 1,235,422
Members 474,534
Posts 29,221,465