Sindumuja - Ukweli kuhusu burundi 2

Sindumuja - Ukweli kuhusu burundi 2

Ninakuhakikishia kile kinachoendelea Burundi huwezi kukitenga na kagame. Kagame hasa ndio yupo nyuma ya mkakati huu ili kuhakikisha nkurunziza ambae ni muhutu atolewe madarakani. Kwa watu waishio Burundi wanalijua hili. Hoja ya kuwa mapinduzi ya Burundi yaliongozwa na godifroid niyombare ambae ni muhutu ni ya kipuuzi.Kwa anayekumbuka mapinduzi ya mwaka 2003 alipouawa rais Melchior ndadaye aliyekuwa kiongozi wa mapinduzi yale alikuwa muhutu tena ambae alikuwa waziri wa mambo ya ndani lakini kilichotokea ni kwamba buyoya Pierre ndie alikuwa rais.Siasa za Burundi na Rwanda huwezi kizizungumzia kwa ufasaha kama unategemea story tells.Hakuna ubishi kuwa kagame na RPA yake ndio walioitungua ndege ya rais habyarimana na ntaryamira wa Burundi.

hahahaha....naona foot soldiers wa hii JF interahamwe wanaongezeka. karibu sana. alianza na akina rushasha lakini sijui jamaa alitokomea wapi. unajua uongo una short life span. walianza na "facts" nyingi lakini kadiri siku zinavyoendelea wanaishiwa.
 
Last edited by a moderator:

Ndio tatizo lenu ninyi banyamulenge/m23,MTU yeyote anaesema ukweli anakuwa ni FD RL kwenu.Refer kikwete alipomshauri kagame kuzungumza na wapinzani wake aliropoka majina mbalimbali ya kimtukana kikwete.The same to you, mwisho wa propaganda zenu umefika, I am telling you!
 
Last edited by a moderator:
Asante for your comment.

1. Ni kweli kabisa, you smelled well. Ingawa sikutaka kubase sana huko kwa sababu tayari nilishapost thread kuelezea hilo. Rwanda's involvement in Burundi ni ile kitu wazungu wanaita 'open-secret', yani siri ya wazi. Kama ambavyo kila mtu alikuwa anajua Rwanda ndio M23 kabla hata ripoti ya UN haijathibitisha hilo. Kwa sasa kuna sababu zifuatazo za hiyo 'smell'.

  1. Baadhi ya viongozi wakuu wa mapinduzi yaliyofeli wamejificha Rwanda. Na Burundi imeshaomba wawe extradited kurudishwa Burundi kujibu mashtaka, Rwanda haitaki. Na hii sio ajabu, Rwanda huwa inalinda sana vibaraka wake. Hata M23 ambao Rwanda inakataa kuwa sio wanyarwanda, haitaki kuwarudisha DRC, Laurent Nkunda mahakama ya ICC lakini Rwanda inamhifadhi haitaki kumtoa, je kuna sababu gani za Rwanda kulinda watu waliojaribu kufanya mapinduzi nchi za wengine?
  2. Mwanzo kabisa wa maandamano, Burundi ilikamata na kuwa deport raia wa Rwanda waliobainika kufanya kazi ya ushushushu katika makampuni ya telecom pamoja na media, vile vile baada ya kugundua kuwa wao ndio coordinators wa maandamano. Swali ni kwa nini wanyarwanda wawe involved kwenye maandamano katika nchi isiyowahusu?
  3. Viongozi wote wakubwa 'wanaharakati', 'journalists' wanao cordinate media/publicity ya hawa 'sindumuja' wa Burundi, wako Rwanda.
  4. Kagame na serikali yake ndio pekee hapa EAC wanao support wapinzani wa Nkurunzinza. Quote: "?If your own citizens tell you we don?t want you to lead us, how do you say I am staying whether you want me or not,? Kagame said May 8, 2015, at the 45th St Gallen Symposium in Switzerland."
    Lakini cha ajabu Kagame hazungumzii mkataba wa makubaliano ya Arusha wala katiba ya Burundi, labda kwa sababu yeye mwenyewe ALIVUNJA makubaliano ya Arusha kuhusu Rwanda alipoipindua serikali ya Habyarimana! Mahakama zote zilizopelekewa mkataba zimethibitisha kuwa Nkurunziza ana haki, sasa hao wanaompinga wana uhalali gani? Yeye anasema warundi hawamtaki Nkurunziza, je haoni kuwa warundi hao ni wachache sana? Maandamano yangefanyika nchi nzima hapo sawa, inakuwaje maandamano yafanyike kisutu na upanga, halafu atokee rais wa kabila la kihindi wa nchi jirani, adai watanzania wooote mpaka wale wa mpanda hawamtaki Magufuli kwa sababu ya maandamano hayo? Huyo rais mhindi wewe utamuonaje?

  5. Wakimbizi wanaokimbilia Rwanda mainly ni wa kabila moja na wale wanaokuja TZ ni wa kabila lingine. Tayari serikali ya Burundi imeshatoa malalamiko kwenye jumuiya za kimataifa kuwa kwenye makambi ya wakimbizi kule Rwanda, inafanyika recruitment, training na arming. Na hao ndio wanaorudi na kufanya mashambulizi Burundi. Kuna incidents nyingi tu ambazo jeshi la Burundi limepambana na the so called 'waasi' mpakani mwa Burundi na Rwanda. Hapa unaweza kuangalia mwenyewe ripoti ya Aljazeera inayothibitisha hilo. Burundi refugees lured to join rebel group - Al Jazeera English
  6. Uzushi wa serikali ya Rwanda nayo ni sababu kubwa. Vurugu zilipoanza, Rwanda haraka ikaanza kueneza uongo kuwa kundi la FDLR limehamia Burundi, and that Rwanda is 'ready to defend itself against FDLR in Burundi'. Huo ni uongo ambao uko designed kujustify askari wa Rwanda kuingia Burundi and nothing else. Wamefanya hivyo DRC kwa miaka mingi. Rwanda toka 1994 inaingia na kutoka huko DRC kwa kisingizio cha kupambana na FDLR, mpaka ikafikia DRC wakapigana vita na Rwanda! Hao FDLR hawaishi? Cha kushangaza FDLR walishasambaratishwa zamani sana na majeshi ya FARDC hapa majuzi, na kila siku Rwanda kupitia watu kama Mushikiwabo huwa wanasema kuwa FDLR "is not a threat militarily". Sasa hii concern ya FDLR leo hii imetokea wapi? Na how come ni Rwanda tu peke yake ndio wanaowaona hao FDLR huko Burundi? Not EAC community, not UN, not DRC, nobody else!
  7. Tukimalizia kimataifa, Burundi kumegundulika madini, na kampuni za kirusi na kichina tayari ziko huko. Wanaofahamu wanajua kuwa Kagame ni kibaraka wa marekani linapokuja suala la kuvuruga nchi za hapa kati ili makampuni ya marekani yapate access. Hivyo ukichanganya na hizo sababu zilizopita pamoja na role ya 'international media' ya kunyamazia mashambulizi dhidi ya raia ambayo yako coordinated, na badala yake ku amplify mauaji ya wapinzani ya kulipiza kisasi, unaona wazi kuwa yanatengenezwa mazingira hapa. Utawala unaotakiwa hapa ni ule ambao utaipa marekani foothold kwenye rasilimali za Burundi na kuwatoa wachina na warusi. Kama ambavyo makampuni ya ufaransa yaliyoondoka na utawala wa Mobutu na makampuni ya kimarekani kuja na Kabila....
2. Kuhusu RPF kutungua ndege, naomba tusidhani, mahakama TATU zina mashitaka ya kagame na RPF kutungua ndege. Mahakama ya ufaransa, mahakama ya spain pamoja na iliyokuwa ya ICTR. Sababu pekee kagame na RPF hawajashitakiwa ni kutokana na geo politics. Ufaransa na spain bado zina arrest warrant dhidi ya kagame na maofisa wake. Kagame hawezi kukamatwa kwa sababu ya presidential immunity. Ndio maana anajiongezea miaka afie madarakani. Kwa upande wa arrest warrant ya ICTR, imekaliwa mpaka mahakama imeisha kutokana na influence ya marekani. Tafuta taarifa kuhusu mwendesha mashtaka Carl del ponte wa ICTR alivyoshurutishwa kukalia file la Kagame kwa sababu Kagame alikuwa 'ally' wa marekani kwenye region hii.
Hio theory unayosema (kuwa Hutu extremists ndio wahusika) ni standard propaganda ambayo serikali ya kagame huitumia kila siku. Nisamehe lakini ni theory ya kipuuzi sana kwa sababu zifuatazo:

  1. Habyarimana alishatia saini ule mkataba wa kugawana madaraka. Sasa hao Hutu extremists wamtungue ili iweje? Kama walikuwa hawataki kugawana madaraka basi ndege wangetungua wakati anakwenda sio wakati anarudi! Kwani mkataba ule ulikuwa suprise? Actually Habyarimana alikuwa tayari kusaini muda mrefu sana, ni upande wa RPA ndio uliokuwa unajivuta vuta kwa sababu hii na ile, sio Habyarimana. Hii theory sio valid.
  2. Pili, tunaweza kubishana upande gani umetungua ndege, lakini hatuwezi kubishana kuwa ni wanajeshi ndio waliofanya hivyo. Kuitungua ndege kunahitaji utaalamu wa juu, na silaha maalum, hivyo tunakubaliana at least kuwa, kama waliotungua walikuwa ni upande wa serikali, basi waliotungua walikuwa ni jeshi la Rwanda chini ya Habyarimana. Lakini ukiangalia kilichotokea baada ya kutunguliwa ndege, wanajeshi wa RPA walimove haraka sana kuanza mashambulizi, wakati jeshi la Rwanda likiwa limezubaa. Hii inashangaza, kwa sababu kama jeshi ndilo lililopanga kutungua ndege, basi ni lazima wawe wamepanga the next step. Hakuna jeshi la kipuuzi linalopanga tukio zito la kutungua ndege, halafu lisijue what do to next. Jeshi la Rwanda lilipigwa kama limesimama, kwa sababu the truth ni kuwa hawakuwa hata na habari ya kutunguliwa ndege, wao na nchi nzima walikuwa wame relax wakijua vita imeisha na amani imekuwa secured kupitia mkataba. Ndege ilipotunguliwa jeshi la Habyarimana lilikuwa limepigwa butwaa, lilikuwa suprised, haikujulikana kamanda ni nani, na nani yuko in control. Upande pekee ambao reaction yao ilikuwa swift as if walikuwa wanajua ndege itatunguliwa ni RPA!
  3. Waliokuwa washirika wa kagame wa karibu kama Gen Nyamwasa na Dr Theogene Rudasingwa na wengineo tayari wameshakiri kuwa Kagame ndio aliyehusika. Kila siku wanatoa ushahidi kwenye tume mbalimbali kuhusu hilo. Ingawa kwa sasa hawa ni wapinzani lakini ushahidi wao ni muhimu kwa sababu umejaa details. By the way Gen Nyamwasa ameshasema yuko tayari kushirikiana na mahakama yoyote ile ku provide details of what happened as long as kuna deal in place for him (immunity maybe), kwa sababu shida ni kuwa akishashusha mambo na yeye mwenyewe atakuwa ameji -implicate. Ndio maana kagame watu kama hawa anawawinda popote pale.
  4. Kagame and co wakiwa wanaelezea hii theory huwa wanawatuhumu watu wanaowaita Akazu. Hawa Akazu ni watu wa karibu na Habyarimana ambao wao wanasema ndio waliokasirika na kutungua ndege. Cha ajabu ni kuwa miongoni mwao ni mke na watoto wa Habyarimana mwenyewe. Idea ya kuwa eti mke wa Habyarimana , wanae, wajomba zake, mashangazi, washikaji zake n.k wameshiriki kwenye njama za kutungua ndege ya ndugu yao kwa sababu tu hawataki kugawana madaraka na watutsi, mimi hainiingii akilini kabisa. Mkataba uliweka wazi kuwa baada ya kipindi cha mpito ungefanyika uchaguzi huru na haki. there is no way kagame na kundi lake waliokuwa wanaua watu kwa miaka minne wangechaguliwa. The hutus did not down that plane. they had nothing to gain from it.
3. Niyombere na wengine: Nilishasema mwanzo kuwa ishu ilianza kama siasa. Lakini siasa zimemalizwa kisiasa mahakamani. Niyombere mwenyewe ameshasema hataki vita na amesurrender. Jeshi zima la Burundi liko intact, hakuna wanajeshi wowote walioasi isipokuwa viongozi wachache sasa haya majeshi ya waasi yenye silaha ambayo yanadai yanapigania sababu zile zile za Niyombere wanapokea amri toka kwa nani? Obviously kuna mtu amechukua advantage hapa na kugeuza mgogoro uwe kitu kingine.

Mwisho, kuhusu mechanism ya kujuana makabila. Ni kweli kuna mchanganyiko mkubwa na kwa sisi nje ya mataifa haya hatuwezi kuwajua, lakini wenyewe kwa wenyewe wanajuana. Hakuna IDs hiyo mambo ilishafutwa. Lakini socially watu wanajuana. Ndio maana ukitembelea #sindumuja kwenye twitter utaona kuwa hawa 'sindumujas' wanatangazia dunia kuhusu genocide ambayo Nkurunzinza anataka kuwafanyia, sasa wewe jiulize kama haijulikani nani mhutu na nani mtutsi hiyo genocide wanayozungumzia itatokeaje? How will those killers know which one is Tutsi and which one is Hutu? ili hali hakuna IDs?
Kuhusu makazi sio kweli kwamba serikali imeruhusu makazi ya watu fulani na fulani. Hii imetokea naturally. Historically watutsi walikuwa ni priviledged class hivyo mpaka sasa vizazi vyao viko concentrated sana kimakazi maeneo ya mijini. Sio kitu cha makusudi. Ni kama vile hapa bongo, wazungu, wahindi na waarabu kuwa concentrated kwenye baadhi ya makazi sio jambo la makusudi ni jambo la kihistoria.

Thank you.

Jmali, hawa kina murutongole kwa asili yao huwezi kuwatifaitisha na kagame au karake. Wamekuwa wakikuita majina mbalimbali labda ni mabaya kwatazamo wao, usikate tamaa, endelea kuwaumbua na kuweka wazi mipango yao. Nimekuwa nikisoma mada zako mbalimbali, kwa hakika hakuna unapodanganya. Kagame na museveni wamekuwa mstari wa mbele kuvuruga amani ya DRC na Burundi kwa kusaidiwa na marekani. Ukiwaambia tu ukweli huu, hawachelewi kukuunganisha na mauaji ya kimbari au kukuita majina ya hovyohovyo.Kuhusu siasa za maziwa makuu hujawahi kudanganya!
 
we fdlr roho yako mbaya ya kihutu itakuua, katika uzi huu huna lolote ni ushuzi mtupu lengo lako ni kuspark chuki zako za kikabila ili uwapate wasio na akili kama wewe, kama shida yako ni kutetea uhalali wa bwana wako nkurunzia sasa issue ya uhutu na utusi imetokea wapi?
mlishindwa na mtaendelea kushindwa maisha yenu yote, na vizazi vyenu vitatawaliwa milele, mtabaki kupiga kelele nyuma ya keybord.

Hadi sasa, nkurunziza ni rais halali wa Burundi, hao unaodhani watatawala milele wameshashindwa!
 
Wewe "mtanzania". Usiingize rwanda kwenye masuala ya burundi. Nenda kamsaidie Nkurunziza manake naona the Hague inamuandalia one way ticket.
aah acha kunivunja mbavu! Mtanzania? hata kama keshanunua uraia, ideology haijabadilika... they say, if you see a bird that walks like a duck, swims like a duck and quacks like a duck then it's what? na kwa kasi aliyo nayo, hata huko Bongo wakimkenulia tu, basi we juwa hata radio kama RTLM iko njiani kufunguliwa.
 
Baada ya Nkurunzinza kuamua kugombea tena, upinzani wa mwanzoni ulikuwa ni wa kisiasa zaidi, na ulijumuisha waburundi wa makabila yote ya wahutu na watutsi, ingawa watutsi walikuwa ndio wengi katika kupinga hatua hii ya Nkurunzinza. Mgogoro huu wa kisiasa ulimalizwa kisheria baada ya mahakama mbili tofauti kuamua kuwa tafsiri ya katiba ya Burundi inamruhusu Nkurunzinza kugombea.

Uchaguzi ukafanyika ingawa wapinzani walisusia uchaguzi.kwa sababu wanazozijua wao. Sababu ya wao kutokwenda mahakamani kupinga tafsiri ya katiba haijulikani. Ni wazi kuwa wanajua hawana hoja! Ingawa haipendezi lakini ukweli ni kuwa kwa makubaliano ya Arusha, kisheria Nkurunzinza anaruhusiwa kugombea.

Baada ya kushindwa kesi za mahakamani ndani na nje ya nchi. Wapinzani wakasusia uchaguzi..Hivyo waliopiga kura ni wanachama na wafuasi wa Nkurunzinza tu. Lakini cha ajabu pamoja na kuwa wapinzani walisusia uchaguzi, uchaguzi uliandamwa na mashambulizi mbalimbali. Vituo vya kupigia kura vilichomwa moto, vikapigwa mabomu, watu walipigwa risasi, vifaa vilichomwa n.k. Ni wazi nani alikuwa nyuma ya machafuko haya. Nkurunzinza hawezi kuvamia vituo na kuua wapiga kura wakati yeye peke yake ndio anagombea! Cha ajabu the so called "international community" (read: the western countries and their media) haikulaani vitendo hivyo. Kwa nini wapinzani wafanye vitendo vya kigaidi dhidi ya raia wasiokuwa na hatia waliotaka kushiriki uchaguzi?

Uchaguzi ukampa Nkurunzinza ushindi. Waangalizi wakakubali matokeo na mpaka sasa hakuna nchi HATA MOJA DUNIA NZIMA ambayo haimtambui Nkurunziza kama rais halali wa Burundi kwa sababu yoyote ile.

Baada ya kuona hivyo maandamano sasa yamechukua sura mpya.. Sasa wapinzani waandamana kwa slogan ya "sindumuja" movement. They can't be serious. Hiki ndicho kiwango cha upumbavu wao. Wameweka wazi malengo yao hadharani kwa yoyote yule ambae alikuwa na wasiwasi na hayuko biased. Hili neno kwa tafsiri rahisi ni "mimi sitakiwi kuwa mtumwa", au "I am not a slave", "not meant to be a slave" na tafsiri za karibu ya hapo.

Kwa mtu anayefahamu siasa za Burundi/Rwanda huu ni uchochezi. Of course ukiwauliza watakuambia inatafsiriwa vibaya, wao wanamlenga Nkurunzinza tu. .Lakini nani hajui kuwa historically, wahutu walikuwa watumwa wa watutsi kwa miaka zaidi ya 400? Nani hajui kuwa mapinduzi yoyote ya wahutu yaliyofanyika yalisababisha wale watutsi wa "matawi ya juu" kuhamia uhamishoni kwa sababu tu ya kutotaka kuwa chini ya uongozi wa wahutu (original sindumuja) ambao wao wanawachukulia kuwa watumwa wao? Sasa wahutu ambao ndio wengi wachukuliaje hii slogan ya sindumuja ambayo inatumiwa na wapinzani ambao "coincidentally" majority ni watutsi, ambapo "coincidentally" wanayemlenga ni raisi mhutu wa chama cha kihutu kilicho madarakani baada ya kufanya vita vya miaka mingi dhidi ya serikali za kijeshi za kitutsi toka uhuru?

Hii imefanya hata wale wahutu wachache waliokuwa hawamtaki Nkurunziza kushitukia kuwa kumbe suala hapa sio kupigania demokrasia bali suala ni kabila la Nkurunziza, hivyo hata wahutu wachache ambao walikuwa wanampinga Nkurunzinza nao wamejitenga na hawa kina "sindumuja". Hii imesababisha kuanza kuonekana waziwazi kuwa wapinzani ni watutsi peke yao exclusively.

Mashambulizi na Mauaji:

Upande wa wapinzani ulishatangaza kuingia msituni na kufanya vita dhidi ya Nkurunzinza, .cha ajabu wanaua raia wasio na hatia kwa kurusha mabomu hovyo, kuvamia mitaani na kumwaga risasi pasipo sababu. Kwa mtu asiyejua unaweza kuona hawa ni wendawazimu lakini angalia, kitakwimu wahutu ni asilimia zaidi ya 80 ya warundi wote, watutsi ni chini ya 20. Kimakazi watutsi wengi wako mjini Bujumbura tena wamejaa kwenye baadhi ya maeneo tu. Maeneo hayo hayashambuliwi na "waasi" ila ndio yanayoongoza kwa maandamano na vurugu dhidi ya Nkurunzinza. Mashambulizi haya ya "watu wasiojulikana" yanayoonekana ni ya hovyo hovyo, ya kupiga risasi masokoni yanamlenga nani? Niliwahi kusema, huwezi kuwa na vita kati ya wadosi na wabongo halafu useme hujui upande wa nani unarusha mabomu hovyo hovyo Tandale, na upi unarusha mabomu hovyo hovyo kisutu.

Mipango ya genocide:

Kwa anayejua siasa za watutsi na wahutu, kinachofanyika ni. utengenezaji wa genocide kwa makusudi. Hatua zote zinazoendelea sasa zimeshawahi kufanya kazi Rwanda.

Sababu za vita:
Rwanda: Kagame alikataa mazungumzo na kufanya vita na serikali halali ya Rwanda chini ya raisi Habyarimana kwa miaka minne. Muda wote huo, Habyarimana alikuwa ni rais halali na anayetambulika dunia nzima na jumuiya zote za kimataifa except kwa watutsi wa RPA peke yao! Habyarimana akaamua kugawana nao madaraka kupitia mazungumzo, walipoona bado watakuwa chini ya wahutu ili hali wao ni "sindumuja", ndege itatunguliwa na wahutu wakalipa kisasi (genocide) na sasa hoja ikabadilika kuwa inabidi waingie kijeshi ili kuzuia genocide.

Burundi:
Hawa nao hawataki mazungumzo ya aina yoyote bila sababu za msingi ila wanataka vita bila sababu. Nkurunzinza hajawapiga, wala hapambani (ila anajilinda) ni rais halali na anayetambulika na nchi zote duniani. There is no legal basis ya kumpinga Nkurunzinza kwa kutumia vita. Mauaji yanayofanywa sasa na hawa ?sindumuja? hayana sababu yoyote ile. 10: Lengo ni kughadhabisha wahutu ambao ndio majority (8/10) ya waburundi kufikia hasira za kuanza kulipa kisasi kwa kuua raia wenzao wa kitutsi, ili isemekane kuwa kuna genocide, na hivyo jumuiya ya kimataifa ipokonye utawala Nkurunzinza. Fikiria leo kutokee bomu sokoni likaua mkeo, kesho risasi shuleni, wafe wanao, hivi unadhani utaendelea kuwa mzima kichwani? Hawa wachochezi wanacholenga kuchochea ndio hicho. Kuwa ifikie wahutu wawehuke kama walivyowehuka Rwanda ili kutokee genocide.

Maandalizi ya keywords kwa matumizi ya baadae:
:Rwanda: Wakati wanavamia Rwanda, waasi wa kitutsi RPA chini ya kina kagame walikuwa wanajiita "inyenzi", au "Mende", wakijisifia kuwa wanashambulia usiku na mchana hawaonekani. Neno hili halikuanzia hapo bali lilianzia kwenye miaka ya 60 kwa waasi wa kitutsi wakiongozwa na Aloyce Ngurumbe. Hivyo kina Kagame kutumia neno hili lenye historia hii ililenga tu kukasirisha wahutu kwa kuwafahamisha nini hasa wanamaanisha. Baada ya genocide, zikatengenezwa sinema nyingi na vitabu lukuki na wengi wasiojua wanaamini mpaka leo kuwa "inyenzi" ni tusi liliotungwa na wahutu dhidi ya watutsi. Kumbe it was not that simple. Ukisoma tu historia unajionea mwenyewe.
Pia karne za zamani kulikuwa na mtemi wa kitutsi (Rwabugiri) aliyekuwa na jeshi lake maalum lililoitwa "inkotanyi", hili jeshi lilitumika toka zama hizo kuzima majaribio ya mapinduzi ya wahutu. Wakati anavamia Rwanda, kagame alianza tena kulitumia kwa jeshi lake akijiita RPA inkotanyi. Deliberately provoking the hutus.

Burundi:
Sasa hivi hawa waasi watutsi wanaofanya mashambulizi dhidi ya wahutu wanajiita "sindumuja". Kila mtu anaona kuwa hawa ni watutsi. Lakini ikitokea wahutu wakaanza kulipa kisasi dhidi ya hawa sindumuja, kesi za genocide zitakazotokea zitadai sindumuja ni tusi dhidi ya WATUTSI WOTE na sio hawa waasi wanaofanya mashambulizi dhidi ya raia wasio na silaha. Hivi kama suala ni Nkurunzinza kugombea tena, imekosekana slogan nyingine yoyote isipokuwa "sindumuja" yenye kugawa watu kimakabila?

Foreign media biaseness:

:Rwanda:
Mauaji ya waasi wa RPA mpaka leo hayaongelewi, hata baadhi ya watoto humu JF hawajui wala hawaoni uzito wa mauaji yaliyofanywa na wanajeshi wa kitutsi, RPA, kwa MIAKA MINNE dhidi ya wananchi wa Rwanda (majority wahutu), kwa bunduki na mabomu kwa sababu media zote zinatoa uzito kwa mauaji ya siku 100 tu yaliyofanywa na wananchi wa kawaida kabisa wa kihutu dhidi ya wananchi wenzao kwa kutumia mapanga na visu. Media za kimataifa hazitoi uzito wowote ule kwa mauaji aliyofanya kagame dhidi ya mamilioni ya wahutu ndani ya Rwanda (kibeho massacre), na nje ya Rwanda (DRC). Matokeo yake Kagame anaheshimiwa kama "mkombozi" wa Rwanda wakati wapinzani wake anaowaua kila siku ndio wanaitwa magaidi.

Burundi:
The same trend inaonekana sasa Burundi. Yakitokea mauaji ambayo jeshi la Burundi limepambana na watu wenye silaha, media za nje zinaonyesha mauaji. Wakiuawa wanaharakati wa sindumuja na watu WASIOJULIKANA, media za nje zinaonyesha. Lakini kila siku wanakufa makumi ya waburundi katika yale maeneo yasiyo ya kitutsi, media hazionyeshi, wanakufa wanachama vigogo wa CNDD-FDD kwa kuchinjwa lakini media za nje hazionyeshi, wala13: "international community" hailaani. Hii inalenga kumfanya Nkurunzinza aonekane ndie gaidi. Hata hapa kwetu majuzi tuliona b.we.ge mmoja anaitwa JoeTrippi akianza kututengeneza ila tukambwekea twitter kule akasepa?.Kinachoendelea kule Burundi sasa hivi kwa upande wa media ni exactly what people like JoeTrippi are paid to do.

Wengi wanaotumia mitandao kumuongelea Nkurunzinza vibaya ni jamii ya sindumuja ambao hata hawako Burundi, waburundi wa kweli wanapatikana kupitia hashtag hizi:

https://twitter.com/hashtag/TheSilentMajority?src=hash
Ukweli inaelekea unafuatilia kweli yanayotokea nchi ya Burundi, na kwenu Rwanda:
1:Unasema mgogoro wa kisiasa ulimalizwa kisheria baada ya mahakama mbili kuamua kuwa Nkurunziza anaruhusiwa kuongoza:
Kwa hili you are very WRONG,japo kweli mahakama iliamua hivyo lakini what about the coup attempt?? unaongeleaje mgawanyiko jeshini baada ya failed coup serikali ilianza kuwinda wale wote waliokuwa wanasapoti coup d`etat.
Kwahiyo kusema uamuzi wa mahakama ulimaliza mgogoro hapo unatudanganya.
Leo hii nina uhakika Maalim Seif akienda mahakamani akidai uchaguzi usirudiwe atashindwa tu..lakini hii haitakuwa mwisho wa mgogoro uliopo Zanzibar.
2:Unasema Wapinzani walisusia uchaguzi kwasababu wanazozijua wao...hapa tayari unaonesha upande wako, wapinzani walikuwa hawakubaliani na kitendo cha Nkurunziza kutaka kuendelea kuongoza.
3.Mwenyewe unakubali kwamba Nkurunziza alipigiwa kura na wanachama wa chama chake tuu.. mpaka hapa unakubali kwamba issue sio kabila kwani kuna zaidi ya vyama kumi ambavyo viko active kati ya hivyo very few are owned by Tutsi, as such Wahutu wengi pia hawakumpigia Nkurunziza kura.
4:Hivi unaweza kutujuza ni kwanini International Media/Community imefumbia macho mauaji yanayo fanywa na waasi?? international media inachuki gani na Nkurunziza na kwa sababu gani.. kumbuka all was well kwa mda wote aliokuwa madarakani kabla ya kutangaza kugombea tena.
5. Sindumuja movement... hii umeifanya title ya post yako, nimejaribu kuisearch kumbe ni twitter hashtag ambayo ina tweets 124 kati ya hizo mwenye account kapost more than 80 posts, hashtag yenye 80 followers na 4 likes!!!
Is this a big deal for a country?? hastag with last tweet done in May?? Cmon!
6:Issue ya history ya Ufalme huwa unapenda kuileta sana, yes it happened lakini kumbuka this was everywhere in Africa,Tanzania inclusive: Ufalme ulikuwa hereditary na Familia za kifalme lived as dictators...issue ni current leaders.
Nyerere angekuwa na idelogies kama zako Tanzania ya sasa isingekuwepo kungekuwepo na ukabila..angeanza kukumbusha wananchi jinsi walivyonyanyaswa na wafalme.
7:Reference uliyotoa juu ya Rwanda is irrelevant to the topic you started though wengi tunakujua huwezi kumalizia bila ya kuongelea Kagama au kabila la Kitutsi in a negative way lakini please, Rwanda ni Rwanda na Burundi ni Burundi:
8:Unasema Watutsi wanataka kuwachokoza wa Hutu ili in turn wahutu waue wa Tutsi, so that Nkurunziza can be removed by International community??? really??? hivi watu wanachukua mda wa kuanalyse statements zako??
Sasa nani atachukua madaraka kama watakuwa tayari wameuawa, kwa msemo wako nikama vile wanajitoa mhanga..
Hapo sikuelewi eti UTENGENEZAJI WA GENOCIDE DHIDI YAKO KWA KUKUSUDIA is it ???????
Ukweli ni kwamba mauaji yanayoendelea Burundi yanafanywa na pande zote it is tit for tat... in this case as long as Nkurunziza ndiye Rais wa nchi he is answerable.
Yeye hajitofautishi na waasi wa serikali yake, wakiua na yeye anaua, huo sio uongozi kashindwa.
 
Ndugu Talkandtalk , nafurahi leo unazungumza kiungwana. Baadhi ya majibu kwa maswali yako:

1. Unasema mgogoro wa kisiasa ulimalizwa kisheria baada ya mahakama mbili kuamua kuwa Nkurunziza anaruhusiwa kuongoza:
Kwa hili you are very WRONG,japo kweli mahakama iliamua hivyo lakini what about the coup attempt?? unaongeleaje mgawanyiko jeshini baada ya failed coup serikali ilianza kuwinda wale wote waliokuwa wanasapoti coup d`etat.

JIBU: Hapa ni wewe ndie unayekosea, mgogoro ulikuwa tafsiri sahihi ya mkataba wa Arusha kisheria. Sasa kama mahakama zimeamua kuwa hakuna tatizo, hao wenye matatizo na Nkurunzinza msingi wa hoja zao ni nini? Maana kama kungekuwa na any ruling inayokubaliana na tafsiri yao halafu Nkurunzinza akakataa hapo sawa, otherwise ni magaidi tu.

Kama wangekuwa wanapinga uchaguzi uliompa Nkurunzinza madaraka, maybe wangeeleweka, but they chose to boycott the elections AFTER mahakama ya EAC allowed it! Kama wana msingi wowote ule please tuelezee sisi tusiojua.

Kuhusu the coup, naona wewe umegeuza maneno. Wanaowindwa sio walio support coup, actually wanaowindwa ni wale waliomrejesha Nkurunziza madarakani! Aliyepambana na Niyombere na kumrudisha Nkurunziza madarakani Lt. Gen. Adolphe Nshimirimana amepigwa roketi na kuuawa, MKUU WA MAJESHI Gen Prime Niyongabo naye kaponea chupu chupu kuuwawa last month katika tukio ambalo walinzi wake 7 waliuawa! What are you talking about kuhusu walio support coup kulengwa. Jeshi lote sasa hivi liko chini ya Nkurunziza, maafisa wote wanamtii Nkurunzinza. Niyombere na wenzie walisha surrender na wako chini ya Nkurunziza. Hao wanajeshi wanaompinga Nkurunzinza wanaolengwa ni kina nani? You should be asking who is behind these targeted assassinations against government officials ikiwa Niyombere is no longer in the picture.

Mfano wako kuhusu Zanzibar ni irrelevant. Maalim Seif hawezi kuchukua silaha na kuanza kuua maafisa polisi na jeshi wa serikali ya Zanzibar, hawezi kuchukua mabomu na kurusha hovyo mashuleni na masokoni ili kuleta vita vya kikabila. Na hata akiandamana, ataandamana kwa sababu za msingi na zinazoeleweka, hataandamana kwa kutumia slogans alizokuwa anatumia anatumia sultani aliyepinduliwa na karume zisizo na kichwa wala miguu!

2. Unasema Wapinzani walisusia uchaguzi kwasababu wanazozijua wao...hapa tayari unaonesha upande wako, wapinzani walikuwa hawakubaliani na kitendo cha Nkurunziza kutaka kuendelea kuongoza.
3.Mwenyewe unakubali kwamba Nkurunziza alipigiwa kura na wanachama wa chama chake tuu.. mpaka hapa unakubali kwamba issue sio kabila kwani kuna zaidi ya vyama kumi ambavyo viko active kati ya hivyo very few are owned by Tutsi, as such Wahutu wengi pia hawakumpigia Nkurunziza kura.

JIBU: Sababu zao zilishapingwa na mahakama, kwa hiyo tendo la kufanya uchaguzi lilikuwa halali. Vinginevyo toa sababu zingine tofauti na zile ambazo wapinzani walikuwa nazo zilizowafanya kususia uchaguzi. Na zaidi ya hapo tafadhali tupe hypothesis yako juu ya nani aliyekuwa anaua raia wasio na hatia kwa kutupa mabomu vituo vya kura, kwa kupiga risasi wapiga kura etc, ikiwa wapinzani walisusa uchaguzi.

Sindumuja movement... hii umeifanya title ya post yako, nimejaribu kuisearch kumbe ni twitter hashtag ambayo ina tweets 124 kati ya hizo mwenye account kapost more than 80 posts, hashtag yenye 80 followers na 4 likes!!!
Is this a big deal for a country?? hastag with last tweet done in May?? Cmon!

JIBU: Mimi nazungumzia sindumuja yenye link hii: https://twitter.com/hashtag/sindumuja hiyo ya mwezi mei ni ya kwako mkuu.

Issue ya history ya Ufalme huwa unapenda kuileta sana, yes it happened lakini kumbuka this was everywhere in Africa,Tanzania inclusive: Ufalme ulikuwa hereditary na Familia za kifalme lived as dictators...issue ni current leaders.
Nyerere angekuwa na idelogies kama zako Tanzania ya sasa isingekuwepo kungekuwepo na

ukabila..angeanza kukumbusha wananchi jinsi walivyonyanyaswa na wafalme.

JIBU: Usemayo ni kweli kabisa. Naona umekubaliana na mimi kuwa hata Nyerere ?angeanza kukumbusha?? tungekuwa na matatizo. Sasa je kuna haja gani ya wapinzani ambao ni watutsi kuanzisha slogan ya #sindumuja fully knowing its implications kwa wahutu regardless of how ?positive? YOU tutsis define it? Huu sio uchokozi wa wazi wazi kukumbushia historia kama ulivyosema? Burundi was more advanced in tribal reconciliantion than Rwanda, look at what this #sindumuja is doing now. How would a Tutsi feel if a political party, majority composed of Hutus use #SinduInyenzi? Halafu wadai wanamlenga Kagame because he has extended his rule? Where is the relationship here?
Zingatia kuwa wahutu wa Burundi wamekandamizwa na watutsi toka uhuru, kila rais aliyechaguliwa toka uhuru aliuawa na jeshi la watutsi kuchukua madaraka kwa mtutu. Nkurunzinza ana uhalali unaothibitishwa na mahakama halafu watutsi wanatumia #sindumuja kutaka atoke bila sababu za kisheria?

JIBU: Watutsi wa kawaida sio wanaojitoa mhanga, wao ndio wahanga, wanaowatoa mhanga ni the elite behind #sindumuja. Kama ambavyo when the dust settled ndio ikajulikana kumbe Interahamwe iliyokuwa inafanya genocide against the Tutsis, ilikuwa inaongozwa na MTUTSI afterall! Kwa hiyo sio ajabu kabisa kuwa when its all over ukagundua kumbe ?Imbonerakure? wanaofanya unyanyasaji wa watutsi kiongozi wake ni mtutsi! Right now ripoti zote zinadai wanaofanya mauaji wamevaa nguo za polisi. Lakini polisi wenyewe hawana rekodi zozote za hao watu, na hata mauaji yenyewe ni senseless. Why would a police officer atumwe na Nkurunzinza kwenda kurusha mabomu kwenye neighbourhood ambayo ni stronghold ya CNDD??? Huu ndio ule uongo wa Kagame enzi zile za kudai miili inayoelea mto Kagera ni watutsi waliouawa na interahamwe, mpaka pale watu wetu walipomtolea uvivu na kumkumbusha kuwa jeshi lake la RPA lilikuwa limeshikilia hayo maeneo for a whole year!

JIBU: Yes majeshi ya Nkurunziza kill, lakini why do they kill? Hilo ndio swali. What reason do these sindumuja have for killing innoncent civilians? Why don?t they target the army only kama vikundi halali vya uasi vinavyofanya? Did ANC kill innoncent white people during the struggle? Here you have tutsi opposition thugs, killing hutu innocent civilians while shouting #sindumuja, what do you expect if not revenge killings? Do they have to burn buildings and destroy properties? Sasa hapo kuna kosa gani kwa polisi wa Nkurunzinza kutumia risasi kupambana na hawa watu?

Mwisho kabisa labda nikuulize wewe, given the situation, what would you have done if you were Nkurunzinza? Na kwa sababu ipi?
 
nilishakuambia ideology yenu itaharibu sana, iwapo watu wataendelea kuwakenulia... mlianza kwa Mobutu mkatia kimavi, hivi sasa mshatia kimavi mshikaji wenu Nkurunziza... nafikiri huu ndio unaenda kuwa mwisho wenu wa kuwaponza viongozi wa nchi za watu,anyway yetu macho...
 
I will not go into the detail nadhani jibu langu kwa swali lako, includes everything:
Ningekuwa Nkurunziza 1:Nisingegombea , hii ni kwasababu tayari wananchi wake walikuwa wamemuonyesha kuwa hawamtaki..rejea maandamo yaliyokuwa yakifanyika kabla hata ya coup attempt:
Maandamo yalikuwa yamakabila yote, hii issue ya ukabila Nkurunziza ndiye aliingiza ili kupata support ya upande mmoja.Kwanza kugombea kwenyewe kulikuwa na utata, kama anaipenda nchi yake kwanini asingemwachia mwingine kutoka chama chake agombee?:
2:Ningekuwa Nkurunziza wale wanaonipinga ningetumia vyombo vyangu vya dola, kuwasaka, niwakamate, niwafungulie mashtaka...sio kuuwa mtaa kwa mtaa, kila unaye msasuspect unatuma polisi kuuwa, then unatofauti gani nahao unao waita waasi?
Umeongelea watu wa upande wa Nkurunziza waliouawa, lakini nani alimuua kiongozi wa upinzani..Zedi Feruzi?nani kamuua Charlotte Umugwaneza kiongozi wa chama cha MSD? who burned down RPA Radio? list is endless na hii yote imefanywa na utawala wa Nkurunziza, sasa Raisi akianza ku act kama waasi, then he has lost control of the state.
 
Watu wanakufa kwa sababu gani? Yeye ndie anayewaua ili atawale? Nani anawaua na kwa nini? tuanzie hapo.

Watu wanakufa kwa sababu hataki kuachia madaraka , askari watiifu kwake ndio wanauwa wapinzani na . Kwani ni lazima awe raisi? Acheni upumbavu mnaivuruga nchi kwa tamaa za kishenzi mnaniudhi sana nyie warundi basi tu hamjuwi.
 
we fdlr roho yako mbaya ya kihutu itakuua, katika uzi huu huna lolote ni ushuzi mtupu lengo lako ni kuspark chuki zako za kikabila ili uwapate wasio na akili kama wewe, kama shida yako ni kutetea uhalali wa bwana wako nkurunzia sasa issue ya uhutu na utusi imetokea wapi?
mlishindwa na mtaendelea kushindwa maisha yenu yote, na vizazi vyenu vitatawaliwa milele, mtabaki kupiga kelele nyuma ya keybord.
Aisee na wewe ni mtusi nini? Dunia kuna kazi ya kufanya hapa hili tatizo ni zaidi ya nijuavyo.
 
Post nzuri umegusia maeneo yote na sababu za chokochoko za Kagame na vibaraka wake.Ni vyema tukajadili hoja za msingi.

Asante for your comment.

1. Ni kweli kabisa, you smelled well. Ingawa sikutaka kubase sana huko kwa sababu tayari nilishapost thread kuelezea hilo. Rwanda's involvement in Burundi ni ile kitu wazungu wanaita 'open-secret', yani siri ya wazi. Kama ambavyo kila mtu alikuwa anajua Rwanda ndio M23 kabla hata ripoti ya UN haijathibitisha hilo. Kwa sasa kuna sababu zifuatazo za hiyo 'smell'.

  1. Baadhi ya viongozi wakuu wa mapinduzi yaliyofeli wamejificha Rwanda. Na Burundi imeshaomba wawe extradited kurudishwa Burundi kujibu mashtaka, Rwanda haitaki. Na hii sio ajabu, Rwanda huwa inalinda sana vibaraka wake. Hata M23 ambao Rwanda inakataa kuwa sio wanyarwanda, haitaki kuwarudisha DRC, Laurent Nkunda mahakama ya ICC lakini Rwanda inamhifadhi haitaki kumtoa, je kuna sababu gani za Rwanda kulinda watu waliojaribu kufanya mapinduzi nchi za wengine?
  2. Mwanzo kabisa wa maandamano, Burundi ilikamata na kuwa deport raia wa Rwanda waliobainika kufanya kazi ya ushushushu katika makampuni ya telecom pamoja na media, vile vile baada ya kugundua kuwa wao ndio coordinators wa maandamano. Swali ni kwa nini wanyarwanda wawe involved kwenye maandamano katika nchi isiyowahusu?
  3. Viongozi wote wakubwa 'wanaharakati', 'journalists' wanao cordinate media/publicity ya hawa 'sindumuja' wa Burundi, wako Rwanda.
  4. Kagame na serikali yake ndio pekee hapa EAC wanao support wapinzani wa Nkurunzinza. Quote: " ?If your own citizens tell you we don?t want you to lead us, how do you say I am staying whether you want me or not,? Kagame said May 8, 2015, at the 45th St Gallen Symposium in Switzerland."
    Lakini cha ajabu Kagame hazungumzii mkataba wa makubaliano ya Arusha wala katiba ya Burundi, labda kwa sababu yeye mwenyewe ALIVUNJA makubaliano ya Arusha kuhusu Rwanda alipoipindua serikali ya Habyarimana! Mahakama zote zilizopelekewa mkataba zimethibitisha kuwa Nkurunziza ana haki, sasa hao wanaompinga wana uhalali gani? Yeye anasema warundi hawamtaki Nkurunziza, je haoni kuwa warundi hao ni wachache sana? Maandamano yangefanyika nchi nzima hapo sawa, inakuwaje maandamano yafanyike kisutu na upanga, halafu atokee rais wa kabila la kihindi wa nchi jirani, adai watanzania wooote mpaka wale wa mpanda hawamtaki Magufuli kwa sababu ya maandamano hayo? Huyo rais mhindi wewe utamuonaje?
  5. Wakimbizi wanaokimbilia Rwanda mainly ni wa kabila moja na wale wanaokuja TZ ni wa kabila lingine. Tayari serikali ya Burundi imeshatoa malalamiko kwenye jumuiya za kimataifa kuwa kwenye makambi ya wakimbizi kule Rwanda, inafanyika recruitment, training na arming. Na hao ndio wanaorudi na kufanya mashambulizi Burundi. Kuna incidents nyingi tu ambazo jeshi la Burundi limepambana na the so called 'waasi' mpakani mwa Burundi na Rwanda. Hapa unaweza kuangalia mwenyewe ripoti ya Aljazeera inayothibitisha hilo. Burundi refugees lured to join rebel group - Al Jazeera English
  6. Uzushi wa serikali ya Rwanda nayo ni sababu kubwa. Vurugu zilipoanza, Rwanda haraka ikaanza kueneza uongo kuwa kundi la FDLR limehamia Burundi, and that Rwanda is 'ready to defend itself against FDLR in Burundi'. Huo ni uongo ambao uko designed kujustify askari wa Rwanda kuingia Burundi and nothing else. Wamefanya hivyo DRC kwa miaka mingi. Rwanda toka 1994 inaingia na kutoka huko DRC kwa kisingizio cha kupambana na FDLR, mpaka ikafikia DRC wakapigana vita na Rwanda! Hao FDLR hawaishi? Cha kushangaza FDLR walishasambaratishwa zamani sana na majeshi ya FARDC hapa majuzi, na kila siku Rwanda kupitia watu kama Mushikiwabo huwa wanasema kuwa FDLR "is not a threat militarily". Sasa hii concern ya FDLR leo hii imetokea wapi? Na how come ni Rwanda tu peke yake ndio wanaowaona hao FDLR huko Burundi? Not EAC community, not UN, not DRC, nobody else!
  7. Tukimalizia kimataifa, Burundi kumegundulika madini, na kampuni za kirusi na kichina tayari ziko huko. Wanaofahamu wanajua kuwa Kagame ni kibaraka wa marekani linapokuja suala la kuvuruga nchi za hapa kati ili makampuni ya marekani yapate access. Hivyo ukichanganya na hizo sababu zilizopita pamoja na role ya 'international media' ya kunyamazia mashambulizi dhidi ya raia ambayo yako coordinated, na badala yake ku amplify mauaji ya wapinzani ya kulipiza kisasi, unaona wazi kuwa yanatengenezwa mazingira hapa. Utawala unaotakiwa hapa ni ule ambao utaipa marekani foothold kwenye rasilimali za Burundi na kuwatoa wachina na warusi. Kama ambavyo makampuni ya ufaransa yaliyoondoka na utawala wa Mobutu na makampuni ya kimarekani kuja na Kabila....
2. Kuhusu RPF kutungua ndege, naomba tusidhani, mahakama TATU zina mashitaka ya kagame na RPF kutungua ndege. Mahakama ya ufaransa, mahakama ya spain pamoja na iliyokuwa ya ICTR. Sababu pekee kagame na RPF hawajashitakiwa ni kutokana na geo politics. Ufaransa na spain bado zina arrest warrant dhidi ya kagame na maofisa wake. Kagame hawezi kukamatwa kwa sababu ya presidential immunity. Ndio maana anajiongezea miaka afie madarakani. Kwa upande wa arrest warrant ya ICTR, imekaliwa mpaka mahakama imeisha kutokana na influence ya marekani. Tafuta taarifa kuhusu mwendesha mashtaka Carl del ponte wa ICTR alivyoshurutishwa kukalia file la Kagame kwa sababu Kagame alikuwa 'ally' wa marekani kwenye region hii.
Hio theory unayosema (kuwa Hutu extremists ndio wahusika) ni standard propaganda ambayo serikali ya kagame huitumia kila siku. Nisamehe lakini ni theory ya kipuuzi sana kwa sababu zifuatazo:

  1. Habyarimana alishatia saini ule mkataba wa kugawana madaraka. Sasa hao Hutu extremists wamtungue ili iweje? Kama walikuwa hawataki kugawana madaraka basi ndege wangetungua wakati anakwenda sio wakati anarudi! Kwani mkataba ule ulikuwa suprise? Actually Habyarimana alikuwa tayari kusaini muda mrefu sana, ni upande wa RPA ndio uliokuwa unajivuta vuta kwa sababu hii na ile, sio Habyarimana. Hii theory sio valid.
  2. Pili, tunaweza kubishana upande gani umetungua ndege, lakini hatuwezi kubishana kuwa ni wanajeshi ndio waliofanya hivyo. Kuitungua ndege kunahitaji utaalamu wa juu, na silaha maalum, hivyo tunakubaliana at least kuwa, kama waliotungua walikuwa ni upande wa serikali, basi waliotungua walikuwa ni jeshi la Rwanda chini ya Habyarimana. Lakini ukiangalia kilichotokea baada ya kutunguliwa ndege, wanajeshi wa RPA walimove haraka sana kuanza mashambulizi, wakati jeshi la Rwanda likiwa limezubaa. Hii inashangaza, kwa sababu kama jeshi ndilo lililopanga kutungua ndege, basi ni lazima wawe wamepanga the next step. Hakuna jeshi la kipuuzi linalopanga tukio zito la kutungua ndege, halafu lisijue what do to next. Jeshi la Rwanda lilipigwa kama limesimama, kwa sababu the truth ni kuwa hawakuwa hata na habari ya kutunguliwa ndege, wao na nchi nzima walikuwa wame relax wakijua vita imeisha na amani imekuwa secured kupitia mkataba. Ndege ilipotunguliwa jeshi la Habyarimana lilikuwa limepigwa butwaa, lilikuwa suprised, haikujulikana kamanda ni nani, na nani yuko in control. Upande pekee ambao reaction yao ilikuwa swift as if walikuwa wanajua ndege itatunguliwa ni RPA!
  3. Waliokuwa washirika wa kagame wa karibu kama Gen Nyamwasa na Dr Theogene Rudasingwa na wengineo tayari wameshakiri kuwa Kagame ndio aliyehusika. Kila siku wanatoa ushahidi kwenye tume mbalimbali kuhusu hilo. Ingawa kwa sasa hawa ni wapinzani lakini ushahidi wao ni muhimu kwa sababu umejaa details. By the way Gen Nyamwasa ameshasema yuko tayari kushirikiana na mahakama yoyote ile ku provide details of what happened as long as kuna deal in place for him (immunity maybe), kwa sababu shida ni kuwa akishashusha mambo na yeye mwenyewe atakuwa ameji -implicate. Ndio maana kagame watu kama hawa anawawinda popote pale.
  4. Kagame and co wakiwa wanaelezea hii theory huwa wanawatuhumu watu wanaowaita Akazu. Hawa Akazu ni watu wa karibu na Habyarimana ambao wao wanasema ndio waliokasirika na kutungua ndege. Cha ajabu ni kuwa miongoni mwao ni mke na watoto wa Habyarimana mwenyewe. Idea ya kuwa eti mke wa Habyarimana , wanae, wajomba zake, mashangazi, washikaji zake n.k wameshiriki kwenye njama za kutungua ndege ya ndugu yao kwa sababu tu hawataki kugawana madaraka na watutsi, mimi hainiingii akilini kabisa. Mkataba uliweka wazi kuwa baada ya kipindi cha mpito ungefanyika uchaguzi huru na haki. there is no way kagame na kundi lake waliokuwa wanaua watu kwa miaka minne wangechaguliwa. The hutus did not down that plane. they had nothing to gain from it.
3. Niyombere na wengine: Nilishasema mwanzo kuwa ishu ilianza kama siasa. Lakini siasa zimemalizwa kisiasa mahakamani. Niyombere mwenyewe ameshasema hataki vita na amesurrender. Jeshi zima la Burundi liko intact, hakuna wanajeshi wowote walioasi isipokuwa viongozi wachache sasa haya majeshi ya waasi yenye silaha ambayo yanadai yanapigania sababu zile zile za Niyombere wanapokea amri toka kwa nani? Obviously kuna mtu amechukua advantage hapa na kugeuza mgogoro uwe kitu kingine.

Mwisho, kuhusu mechanism ya kujuana makabila. Ni kweli kuna mchanganyiko mkubwa na kwa sisi nje ya mataifa haya hatuwezi kuwajua, lakini wenyewe kwa wenyewe wanajuana. Hakuna IDs hiyo mambo ilishafutwa. Lakini socially watu wanajuana. Ndio maana ukitembelea #sindumuja kwenye twitter utaona kuwa hawa 'sindumujas' wanatangazia dunia kuhusu genocide ambayo Nkurunzinza anataka kuwafanyia, sasa wewe jiulize kama haijulikani nani mhutu na nani mtutsi hiyo genocide wanayozungumzia itatokeaje? How will those killers know which one is Tutsi and which one is Hutu? ili hali hakuna IDs?
Kuhusu makazi sio kweli kwamba serikali imeruhusu makazi ya watu fulani na fulani. Hii imetokea naturally. Historically watutsi walikuwa ni priviledged class hivyo mpaka sasa vizazi vyao viko concentrated sana kimakazi maeneo ya mijini. Sio kitu cha makusudi. Ni kama vile hapa bongo, wazungu, wahindi na waarabu kuwa concentrated kwenye baadhi ya makazi sio jambo la makusudi ni jambo la kihistoria.

Thank you.
 
I will not go into the detail nadhani jibu langu kwa swali lako, includes everything:
Ningekuwa Nkurunziza 1:Nisingegombea , hii ni kwasababu tayari wananchi wake walikuwa wamemuonyesha kuwa hawamtaki..rejea maandamo yaliyokuwa yakifanyika kabla hata ya coup attempt:
Maandamo yalikuwa yamakabila yote, hii issue ya ukabila Nkurunziza ndiye aliingiza ili kupata support ya upande mmoja.Kwanza kugombea kwenyewe kulikuwa na utata, kama anaipenda nchi yake kwanini asingemwachia mwingine kutoka chama chake agombee?:
2:Ningekuwa Nkurunziza wale wanaonipinga ningetumia vyombo vyangu vya dola, kuwasaka, niwakamate, niwafungulie mashtaka...sio kuuwa mtaa kwa mtaa, kila unaye msasuspect unatuma polisi kuuwa, then unatofauti gani nahao unao waita waasi?
Umeongelea watu wa upande wa Nkurunziza waliouawa, lakini nani alimuua kiongozi wa upinzani..Zedi Feruzi?nani kamuua Charlotte Umugwaneza kiongozi wa chama cha MSD? who burned down RPA Radio? list is endless na hii yote imefanywa na utawala wa Nkurunziza, sasa Raisi akianza ku act kama waasi, then he has lost control of the state.

1. Nkurunzinza hatakiwi na watu wachache sana kwenye baadhi ya wilaya za Bujumbura. With the exception of hizo wilaya (ambazo hutaki kukubali sababu zake), the rest of Bujumbura and the rest of Burundi is calm and peaceful. Hivyo sio kweli kwamba 'WATU' hawamtaki, hatakiwi na 'watu' kwa herufi ndogo. Nini maandamano? Hakujawahi kuwa na maandamano dhidi ya Nyerere lakini Nyerere amenusurika coup attempts zaidi ya tatu kama sikosei! Je maana yake WATANZANIA tulikuwa hamtutaki?
Lakini personally nakubaliana kuwa Nkurunzinza hakutumia busara kugombea tena even though kisheria yuko sahihi. Just like Kagame na Museveni hawatakiwi kugombea tena no matter how legally feasible it is.

2. Ni kweli mwanzoni maandamano hayakuwa na ukabila. Msingi wake ulikuwa wa tafsiri ya kisheria. Baada ya mahakama kukubali, walio wengi wakaachana nayo. Waliobaki hivi sasa wanaandamana kwa nini? Na kwanini watumie "sindumuja"? Hiyo "sindumuja" ina wahutu wangapi?
Vile vile kama hakuna ukabila, mbona hao "sindumuja" wanalia kwamba kunataka kufanyike genocide? Je hiyo genocide itakuwa against nani? Unachoongea kinapishana na hata hao sindumuja wenyewe unaowatetea.

3. Kupambana na magaidi ni vigumu. Waasi wa Burundi wanavamia vituo vya polisi na kijeshi na kufanya ambush, wanaua raia kwa mabomu, wanavamia kwa risasi na kuua indiscriminately. Hivyo huwezi kutumia mbinu za kawaida za kijeshi kwa sababu hupambani na jeshi la kawaida. That being said, mauaji mengi yanayofanywa na upande wa serikali yanafanywa dhidi ya watu walio na silaha na wanauawa katika mapambano. Hayo mauaji dhidi ya watu wa upinzani hayafanywi na serikali ya Nkurunziza kama serikali, kwa sababu politically haina sababu. Nkurunzinza hata akijiuzulu leo atakayeshinda ni mtu wake tu. There is no threat politically upande wa upinzani kiasi cha serikali kuwaua. It doesn't make any sense. Hata hivyo nakubali kuwa wanaoua wapinzani ni watu wanao support serikali ya Nkurunziza.
 
J mali you seem to know mach about RwandaURUNDI history! I believe on you!
 
wewe ni muhutu na ni mwanachama wa fdlr nachochote kile utakacho kijadili hapa jukwaani ni lazima utaje mabaya ya kagame na watutsi,
hivi nikuulize kitu kwani huwezi kuandika bila kutaja watusti na kagame? wenzio wako wanajenga nchi wewe unapiga kelele mitandaoni mwisho unaonekana chizi tu!
 
Hahahaha. Wewe ungekuwa mtanzania mwenzangu ungeandika "mhutu" sio "muhutu". Hapo umejianika maana hivyo ndivyo mnavyoongea. Wewe ndio uache propaganda za FDLR na uungane na wahutu wenzio mjenge nchi yenu ikiwa na umoja.
 
hivi unaona raha gani kujipakazia utanzania na kuficha nationality yako?
 
Back
Top Bottom