Sindumuja - Ukweli kuhusu burundi 2

Sindumuja - Ukweli kuhusu burundi 2

Probably burudi na rwanda mnahitaji kuzichapa tena tu ili mbabe awe madarakani. Maana ideology za uhutu/utusi zimewakaa sana akilini na kibaya zaidi hamjapata kiongozi wa kuwaunganisha kama sisi tunavyounganishwa na Dr. Magufuli.
 
1. Rwanda's involvement in Burundi. The way you put it ni kuwalaumu Watutsi bila kuangalia vyema root course.

Kwa nini Watutsi wakimbilie Rwanda au coordinators kuwa watutsi? Mkimbizi hukimbilia ambapo atakuwa safe. Hata Tanzania bara pakitokea shida ni very simple Maasai kukimnilia Kenya na Mpemba Pemba. Hii ni kwa sababu upande utakaokimbilia unayohakika na usalama wa maisha yako.

Pili Rwanda kuweka vikosi mpakani ni hatua ambayo kwa mtazamo wangu ni sahihi since uwepo wa vita au FDRL Burundi kunastabilize amani ya Rwanda kwenyewe. Wala hili sio geni kidunia.

Pili la kutungua ndege, unakubali ilitunguliwa na askari halali wa serikali ila unahoji mbona hawakuwa na plan ya whatafter. Hili si sahihi, kwa mujibu wa statements ya baadhi ya waliokuwa Peacekeeping mission walikiri after ile bombing vikosi vya serikali vilianza kumove into action. Pia swala la kuwa RPF walikuja instantly kwa kuwa walijua tukio prior to its happening nadhani ni kuignore kuwa since 1990 RPF walikuwa stationed kijeshi na walikuwa wanafanya raids kwenye mpaka wa Rwanda na Uganda.

Suala la warrants za kumkata Kagame by French and Spain nadhani ni unafiki wa kisiasa. Madai ya Nyamwasa hayo nadhani yapo fully biased. Baada ya kuasi nchi ndio anatoa ushahidi, intentions zake ni malicious towards Kagame. Maake ukiangalia vizuri utagundua hata yeye mwenyewe hujifanya hajahusika na RPF bali ni Kagame pekee. Seriously Kagame pekee bila hao majenerali wenzie??

Tatu, kuhusu Niyombare na wengineo ni kielelezo cha failure ya utawala Nkurunzinzah. Ukiona watu wapo ready kukutoa madarakani na unapingwa jitathmini kama unafaa.

Pia nimeona issue ya location ya maandamano. Maandamano ni contagious yanaweza kuanzia ndani ya nyumba yasipodhibitiwa yaweza kusambaa nchi nzima. I think Burundu millitia iliyadhibiti and this is obvious kwani wote tuliona. So you cant expect it to have spread nchi nzima.

Sorry natumia simu sikuweza kujadili points zote kwa pamoja.

Japo nadhani tukubaliane Burundi kuna tatizo Nkurunzinzah wants to be Kagame lakini hana strength wala influence ya kuwa Kagame. Hata Kagame aweza kuwa ana matatizo yake kama issue ya Congo na madini au sakata la Fred Rwigyema but as a leader he is pretty outstanding.

Mwisho help me with this book kama unacho Mimi natafuta kitabu cha Stephen Kinzer: a thousand hills: rwandas rebirth and the man who dreamed it

1. Sijawalaumu watutsi wala wahutu kwa kuchagua wapi wanakimbilia, ninachofanya ni analysis. matokeo ya analysis ni bahati sio deliberate. Facts remain facts. Lakini kama wewe ume observe kuwa suala ni safety issue, je unataka kusema watutsi hawajisikii safe wakiwa Tanzania? Mbona tuliwahifadhi walipopinduliwa mwaka 1958 na baadae kuwapa uraia? Mfalme wao kakaa hapa miaka miwili nadhani. Issue haiwezi kuwa safety pekee.
Pili, kumbuka kuwa mwaka 1993 kwenye machafuko ya burundi ambapo jeshi la kitutsi lilifanya massacres dhidi ya wahutu, wahutu walikimbilia Rwanda. Sasa kama issue ni safety, jiulize je, ni nini kifanye wahutu wengi safari hii wakimbilie TZ na watutsi wengi wakimbilie Rwanda? What makes Rwanda not safe for hutus this time around? Si eitheir wote wangeenda Rwanda au wote wangekuja TZ?
kumbuka i'm not saying kwamba 100% waliokimbilia Rwanda ni watutsi na 100% waliokimbilia bongo ni wahutu, tunaongelea majority.

2. Sheria za kimataifa zinakataza kuweka majeshi mpakani ila kwa masharti maalum. Kuweka majeshi mpakani bila kutaarifu jumuiya ya kimataifa ni 'act of war' dhidi ya yule ambaye umepakana naye. Ndio maana huwezi kukuta kambi za kijeshi mipakani. Kuna umbali fulani wa kimataifa ambapo hakutakiwi kuwa na jeshi from the border. Rwanda haijaweka vikosi vyake mpakani na haiwezi kufanya hivyo officially. Vikosi vilivyopo ni vya hawa waasi.
Na hii ni sababu nyingine kwa nini Rwanda ituhumiwe. Kama kuna vita Uganda na jeshi la Uganda linapambana na vikundi vyenye silaha mpakani mwa Uganda na TZ, Tanzania lazima tungetoa taarifa UN na kuweka jeshi letu mpakani ili kujilinda na kikundi hiki as well. Lakini Rwanda imetulia tuli! Kama yenyewe haihusiki na vikosi hivi, basi na yenyewe ingeogopa na kuweka vikosi vyake mpakani kwa kufuata sheria za kimataifa. Lakini haijafanya hivyo. why? Ni kwa sababu inawajua!

3. Naona na wewe unaongelea kuwa kuna uwapo wa FDLR Burundi. Je una taarifa zozote independent from zile za Rwanda kuhusu jambo hilo. Je unaweza kuthibitisha hata existance ya FDLR anywhere toka wapigwe na FARDC?

4. Tuje kwenye ishu ya ndege. Sijakubali kuwa wanajeshi wa serikali ndio waliotungua, read my comment carefully. Nimesema "ikiwa". kwa maana ya 'for the sake of argument lets assume...' Pili, mimi na wewe hatuna haja ya kutegemea statements za yule na yule, mahakama TATU tofauti zimesha mu implicate Kagame na RPA kwenye hiyo ishu ya ndege. Sasa kwa nini tutegemee statements za watu wengine tena? Mahakama hizi ushahidi wake ni mzito kiasi cha kufikia kutoa arrest warrants, unazipingaje kwa kutumia hearsay statements mkuu? Kusingekuwa na siasa za kimataifa kwenye hii ishu, leo hii kagame na kundi lake wangekuwa ndani kwa mashtaka ya ICTR, ufaransa na spain.
Tatu, historia yako iko flawed kidogo. RPA mpaka siku ndege inatunguliwa walikuwa tayari wameshikilia sehemu kubwa ya Rwanda, soma kwa mfano jinsi walivyoua watu zaidi ya 40,000 na kuteka Ruhengeri for example, na vile vile kutokana na mazungumzo ya Arusha, moja ya masharti ilikuwa ni kuruhusu RPA kuweka vikosi vyake katikati ya Kigali wakati mazungumzo yanaendelea. FACT ambayo haipingiki ni kwamba RPA kwa siri, kinyume na sheria, walizidisha kiwango cha silaha na wanajeshi walioruhusiwa na mkataba ule. Sio kweli kwamba RPA walikuwa Uganda mpaka ndege inatunguliwa. They were already there in Rwanda. Kwa hiyo mpaka tukio linatokea wao walikuwa wameshapanga strategies za nini cha kufanya next. Vikosi hivi ndivyo vilivyoanza immediately kushambulia baada ya ndege kutunguliwa.


5. Mahakama za France na Spain hazijatumia ushahidi wa Nyamwasa, hakuna siasa hapo. Nyamwasa ushahidi wake bado anao mwenyewe. Na narudia tena Nyamwasa of course alihusika ndio maana anasema yuko tayari kutoa ushahidi kamilifu ikiwa mahakama yoyote itampa immunity. Hilo hatushindani. Na je vipi kuhusu mashtaka ya ICTR dhidi ya Kagame ambayo yalikuwa yameandaliwa na Carla del ponte? Mahakama tatu haziwezi kufanya vitu kisiasa my friend.

6. Nkurunzinza anaweza kuwa kiongozi wa hovyo. Lakini anakubalika na waburundi walio wengi. Lete ushahidi kuwa majority ya waburundi hawamtaki Nkurunzinza. Niyombere kajaribu na kashindwa na wenzake wa jeshi hilo hilo, are you sure Nkurunzinza hatakiwi kama unavyodai? Kushindwa kwa coup ni kielelezo tosha kuwa Nkurunzinza anakubalika na kwamba wale ambao hawamtaki ni wachache. Sijui kama unajua kuwa Julius Nyerere aliponea kupinduliwa mara 3! Je huo ni ushahidi kuwa watanzania tulikuwa hatumtaki kwa vile kaponea kupinduliwa mara nyingi kuliko Nkurunzinza?

7. Kuhusu location za maandamano kuwa contagious na militia kuzuia sio kweli. Maandamano yanaendelea hadi leo hii, kwenye sehemu za "sindumuja". Sehemu zingine kuko shwari tu.

8. Mtazamo wako juu ya Kagame nauheshimu ila sikubaliani nao, nobody that know Kagame for what he really is angetaka kuwa Kagame. The only people wanaomuona Kagame kuwa ni kiongozi mzuri ni wale ambao either are ignorant of the facts about the man, au wale ambao kula yao inamtegemea Kagame.
Kagame alivamia Rwanda kwa miaka minne akiua wananchi wasio na hatia, Kagame katungua ndege na kusababisha genocide, Kagame kafanya mauaji ya wahutu ndani ya Rwanda (kibeho massacre), kafanya mauaji ya wahutu nchini DRC (mapping report), mauaji ambayo UN yenyewe imeyaita "genocide" kwenye ripoti yake iliyokaliwa kisiasa, Kagame katengeneza vikundi vya kigaidi vya M23, CNDP,...vilivyofanya atrocities za kutisha pale DRC, ushahidi huu umethibitishwa na ripoti za UN, sanctions za US pamoja na UK, Kagame kashiriki mapinduzi ya Uganda, mapinduzi ya Rwanda, mapinduzi ya DRC. Kabla ya Kagame Rwanda ilikuwa ina uhusiano mzuri na mataifa yote. Baada ya Kagame kuingia, kagombana na Kenya, Africa kusini, Ubelgiji, Ufaransa, Tanzania, Uingereza, na nyinginezo nyingi; South Africa, Kenya, Sweden na nchi zingine zilifikia kufukuza diplomats wa Rwanda na kuvunja uhusiano wa kibalozi at some point in time!
Yeye alikuja Rwanda akidai kaja kumaliza mgogoro wa wakimbizi wa Uganda, na kuleta inclusive goverment. Well, leo hii wakimbizi wa Rwanda ni wengi maradufu kuliko wakimbizi wa Habyarimana! Leo raia wa Rwanda kupotea nchini kwao ni jambo la kawaida tu, miili kukutwa inaelea ziwani ni jambo la kawaida tu. Hiyo demokrasia aliyoleta ndio hii ya kujiongezea miaka ya utawala mpaka 2034? Au ile ya kufunga wapinzani wote kwa mashtaka ambayo hata mashahidi wa serikali wakifika mahakamani wanaigeuka serikali (victoire ingabire)?
Tukubaliane kutokukubaliana mkuu. kuhusu hicho kitabu mimi sina, asante.
 
Hatimaye balaa la BURUNDI linatuwa ktk mgongo wa TANZANIA !!

Mwisho wa siku Taifa la waungwana (TZ) lina beba wakimbizi wakiwemo na majambazi/majangili kuzagaa nchini humu!! (ktk kila msafara wa mamba, kenge hujipenyeza!!)

Wakati hapohapo Tanzania inamkumbatia Dictator Nkurunziza....... "THINK"
jMali dushe lowestein

Tanzania haimkumbatii Nkurunzinza. Nkurunzinza ndio mwenye haki kwenye hili suala. Hao wanaompinga Nkurunzinza ndio wanaoua watu hovyo tena kwa kulenga makabila yao. Hao ndio wanatakiwa wakemewe.
 
Kwa wale ambao wanataka kujua kwa undani historia na events leading up to the 1994 Genocide against tutsi please take time to read :

Conspiracy to Murder

vitabu viko vingi vya pande nyingi, wewe ungesoma halafu utoe hoja zako uki refer to books including that one, kama great thinkers wanavyofanya, ili hoja zijibiwe kwa hoja.
 
Umemetetea sana Nkurunzinza na kujaribu kuonyesha yeye hana kosa...suala la msingi hapa ni kwamba mtu amekaa madarakani miaka 10 hiyo tayari inatosha...hajafanya kitu cha maaana ukuiangalia Burundi iko hoi taabani kiuchumi...mshauri aachw madaraka mtu mwingine aingie amani itawale

Inachekesha unazungumzia muda wa Nkurunziza wakati unatumia avatar ya Muammar Gaddafi! Nkurunzinza amekaa Kikatiba, huyo Gaddafi yeye alikuwa HANA UKOMO!

1. Nchi inaendeshwa kwa katiba. Kama kuna mtu anatatizo na katiba anaweza kwenda mahakamani kudai haki yake. Wapinzani wameshindwa mahakama ya ndani, wameshindwa mahakama ya nje, na bado wako huru kwenda mahakama zingine lakini hawafanyi hivyo kwani zote tafsiri yake ni kuwa Nkurunzinza anaweza kugombea tena na amefanya hivyo.
Kwa nini wameamua kuunda vikundi vya watu wenye silaha na kufanya machafuko? Je unajua kuwa hawapigani na jeshi bali wanarusha mabomu hovyo sokoni? wanapiga risasi hovyo kwa raia wasio na silaha? Hivi ndio unavyotaka wewe?
Tafadhali jikite kwenye sababu hasa ya kwa nini Nkurunzinza ana makosa, hili ndio suala la msingi. Hebu wewe tuambie jambo moja rahisi tu. Hao 'sindumuja' hoja yao ni nini? Msingi wa hoja yao ni nini? Tuanzie hapo.

2. Pili, hao wapinzani sio majority ya wananchi wa Burundi. Ni kikundi cha watu wachache, majority ya waburundi wanakubaliana na Nkurunzinza wao, na ubovu wake wa uchumi. Hata mimi nadhani Nkurunzinza angemuachia mtu mwingine lakini hilo ni kwa warundi wenyewe kuamua. Kama walio wengi wameamua basi ndio hivyo. Hao 'sindumuja' wanaandamana kwa sababu uchumi mbovu?
 
Hapana shaka mleta mada ni mhutu.

Tufanye mimi ni mhutu, hoja yako? Wahutu hawatakiwi kuleta mada JF? au umekasirika kwa kuwa wewe 'sindumuja' hutakiwi kushare jukwaa na mimi 'mhutu' ? 🙂
 
jMali
Ki msingi una hoja za kiuchunguzi na zenye kushawishi. Wajumbe wanaokupinga sijaona hoja hata moja toka kwako zaidi ya kukunasibisha na uhutu. Kiukweli Tutsi na Kagame ni waa kulaumiwa ktk mgogoro wa burundi maana wanatafuta sana symphathy kupitia media ili kuharamisha utawala wa Nkurunzinza. Nina imani raisi w awamu ya tano wa TZ ataendelea kuwa upande wa Nkurunzinza maana TZ tuna maslahi na utulivu wa kisiasa nchini Burundi as tumechoka kupoka wakimbizi.
 
Last edited by a moderator:
vitabu viko vingi vya pande nyingi, wewe ungesoma halafu utoe hoja zako uki refer to books including that one, kama great thinkers wanavyofanya, ili hoja zijibiwe kwa hoja.

This was not meant for you...najua umeshakisoma lakini kutokana na hatred yako kwa Rwanda you decided to bury your head in the sand. Hii nimewawekea watanzania wengine wanaopenda kujisomea, wakisome hiki kitabu then they can form their own opinion.
 
Mkuu kiasi fulani umechambua vizuri ila nachelea kuna jambo either unaficha au unatafuta mtu wa kulink kisicho sahihi.

1. I can smell unataka kutuambia kuwa kuna force behind inasponsor hao sindumuja ambaye ni Kagame???

2. Pili kusema RPF ndio waliotungua ile Ndege kule Rwanda nadhani si kweli na undermine influence ya Hutu extrimists ambao hawakutaka kushare power na mtu.

3. Mtu kama Niyombare (mhutu) aliyeongoza mapinduzi dhidi ya Nkurunzinzah unamuweka wapi?? Mi nadhani its not about maandalizi ya genocide ni tatizo la kimfumo wa utawala na kikatiba la Burundi.

Mwisho I thought mechanism za kujua huyu ni mtutsi au muhutu zilishaisha. Au mpaka leo bado kuna ID za mtutsi na mhutu?? Na pia nilidhani muungano wa taifa umesababisha intermingle baina ya hawa watu wawili. How comes serikali imeshindwa na kuruhusu makazi ya wahutu au watutsi??

hata iweje, mhutu ataendelea kuwa mhutu na mtutsi pia. hawafanani hata kidogo halafu mila na desturi za kitutsi one can judge ni mbovu maana popote walipo hutaka kuwa super tu
 
we fdlr roho yako mbaya ya kihutu itakuua, katika uzi huu huna lolote ni ushuzi mtupu lengo lako ni kuspark chuki zako za kikabila ili uwapate wasio na akili kama wewe, kama shida yako ni kutetea uhalali wa bwana wako nkurunzia sasa issue ya uhutu na utusi imetokea wapi?
mlishindwa na mtaendelea kushindwa maisha yenu yote, na vizazi vyenu vitatawaliwa milele, mtabaki kupiga kelele nyuma ya keybord.
 
jMali
Ki msingi una hoja za kiuchunguzi na zenye kushawishi. Wajumbe wanaokupinga sijaona hoja hata moja toka kwako zaidi ya kukunasibisha na uhutu. Kiukweli Tutsi na Kagame ni waa kulaumiwa ktk mgogoro wa burundi maana wanatafuta sana symphathy kupitia media ili kuharamisha utawala wa Nkurunzinza. Nina imani raisi w awamu ya tano wa TZ ataendelea kuwa upande wa Nkurunzinza maana TZ tuna maslahi na utulivu wa kisiasa nchini Burundi as tumechoka kupoka wakimbizi.

Asante sana mkuu. Hawa wenzetu wameshazoea huko kwao kulazimisha hoja za nguvu badala ya nguvu ya hoja. Bahati nzuri serikali zote za Tanzania huwa ni za watu makini linapokuja suala la siasa za maziwa makuu.
 
we fdlr roho yako mbaya ya kihutu itakuua, katika uzi huu huna lolote ni ushuzi mtupu lengo lako ni kuspark chuki zako za kikabila ili uwapate wasio na akili kama wewe, kama shida yako ni kutetea uhalali wa bwana wako nkurunzia sasa issue ya uhutu na utusi imetokea wapi?
mlishindwa na mtaendelea kushindwa maisha yenu yote, na vizazi vyenu vitatawaliwa milele, mtabaki kupiga kelele nyuma ya keybord.

hahahaha, thread inazungumzia 'sindumuja' ilivyo kampeni ya kikabila ya watu wanaojiona ni wafalme wa wenzao. Hujibu hata hoja moja nilizotoa kwenye thread, hupingi fact yoyote ile, nothing. Badala yake unanitukana na kusema "vizazi vyenu vitatawaliwa milele", hapo tayari umeshaniita FDLR... basi sawa wana JF wanaona wewe ni nani
 
jmail, hivi ni RPA au RPF-Rwanda Patriotic Front? Naona kama unachanganya mambo hapo
 
This was not meant for you...najua umeshakisoma lakini kutokana na hatred yako kwa Rwanda you decided to bury your head in the sand. Hii nimewawekea watanzania wengine wanaopenda kujisomea, wakisome hiki kitabu then they can form their own opinion.

Msomi wa vitabu anajulikana. Wewe husomi vitabu kwa sababu kama ungekuwa unasoma ungejadili kwa hoja halafu ukawa unafanya reference. Huwezi kufanya hivyo kwa sababu kila hoja utakayotoa itajibiwa kwa counter reference vile vile. Ndio maana una prefer kuwaonyesha watu vitabu badala ya kujadili na kuwaonyesha vitabu kama msingi wa hoja zako.
 
hahahaha, thread inazungumzia 'sindumuja' ilivyo kampeni ya kikabila ya watu wanaojiona ni wafalme wa wenzao. Hujibu hata hoja moja nilizotoa kwenye thread, hupingi fact yoyote ile, nothing. Badala yake unanitukana na kusema "vizazi vyenu vitatawaliwa milele", hapo tayari umeshaniita FDLR... basi sawa wana JF wanaona wewe ni nani
wewe fdlr hata maandishi yako yanaonesha sio mtanzania unajinasibisha ili kuficha uhutu wako, mlikimbia nchi yenu kwa chuki zenu na akili ndogo, na sasa mnajaribu kutafuta sympath ili ionekane mnaonewa!
 
jmail, hivi ni RPA au RPF-Rwanda Patriotic Front? Naona kama unachanganya mambo hapo

Unayechanganya ni wewe, uliza uambiwe.

RPF ni chama cha Rwandan Patriotic Front, au ukipenda, Rwandese Patriotic Front au kwa kifaransa kinajulikana kama FPR yani Front patriotique rwandais, yote hayo ni majina ya Chama.
RPA ilikuwa ni Rwandan Patriotic Army, Rwandan patriotic army ilikuwa ni armed wing ya RPF. Kwenye siasa za africa, ni kawaida kwa chama kuwa na armed wing
Hivyo kabla Kagame hajapindua Rwanda, RPF ndio ilikuwa inashughulika na siasa lakini kwenye mashambulizi ya kivita walikuwa wanashughulika RPA. Baada ya kuchukua nchi ya Rwanda, jeshi la RPA likageuka hili jeshi la sasa la Rwanda, yaani RDF (rwanda defense force). Hivyo katika kuzungumzia historia ya Rwanda kwenye vita kabla ya 1994, sio makosa kuchanganya RPF na RPA. Maneno yote yanaweza kutumika sawa kabisa. Ukisema jeshi la RPF, maana yake umemaanisha RPA, ila ukisema RPA unakuwa umekuwa specific zaidi. RPA wote ni RPF. Mfano Red brigade wote ni Chadema, na green guard wote ni CCM. Green guard wakifanya fujo unaweza kusema green guard wamefanya fujo au CCM wamefanya fujo, yote sawa tu.

Mfano wa pili kwa vile tunazungumzia Burundi, chama cha Nkurunzinza upande wa siasa kilikuwa kinaitwa CNDD, hii ni political wing, lakini upande wa jeshi lake wa chama hicho unaitwa FDD. Hivyo kwa ujumla ndio unapata CNDD-FDD. Kwa hiyo ukizungumzia historia ukasema CNDD walivamia eneo fulani, maana yake umemaanisha FDD. Mwingine akisema hivyo hivyo lakini akatumia FDD anakuwa amekuwa specific zaidi, na sio kwamba mmoja wapo amekosea. FDD wote ni CNDD.

Natumaini umenielewa.
 
wewe fdlr hata maandishi yako yanaonesha sio mtanzania unajinasibisha ili kuficha uhutu wako, mlikimbia nchi yenu kwa chuki zenu na akili ndogo, na sasa mnajaribu kutafuta sympath ili ionekane mnaonewa!

Ndugu hebu wasaidie wanachama wengine wa JF kujua jinsi wewe unavyomtambua mhutu, tena wa mhutu wa FDLR! Maana mimi nashangaa thread inahusu burundi, ila wewe unanipachika uhutu wa Rwanda, umejuaje mimi ni mhutu, na tena sio mhutu wa Burundi bali wa Rwanda? Au kuna FDLR ya burundi siku hizi?
Halafu unadai kuwa "naficha uhutu wangu" , hebu nisaidie katika hili, kuwa mhutu ni dhambi mpaka mtu ajifiche? Kwa nini unadhani endapo mimi ni mhutu basi lazima najificha? Mbona tumewapa uraia wahutu wengi tu miaka ya karibuni, unadhani wakija JF watajificha kuwa wao sio watanzania wenye asili ya kihutu? Why would they need to do that?
Halafu unaunganisha FDLR/uhutu na akili ndogo really? Kwa hiyo wahutu wana akili ndogo eti ee? Sasa unakataa nini na unafanya nini? Maneno yako kwa kila mtu anayekusoma yanathibitisha kuwa wewe ni miongoni mwa hawa 'sindumuja' ndio maana unaniambia sisi 'wahutu' tutatawaliwa milele.
Chuki haijengi ndugu, jifunzeni kutoka kwetu mjenge nchi zenu. Kila mnapopigana ni ndugu zenu huwa wanakufa sio sisi.
 
Msomi wa vitabu anajulikana. Wewe husomi vitabu kwa sababu kama ungekuwa unasoma ungejadili kwa hoja halafu ukawa unafanya reference. Huwezi kufanya hivyo kwa sababu kila hoja utakayotoa itajibiwa kwa counter reference vile vile. Ndio maana una prefer kuwaonyesha watu vitabu badala ya kujadili na kuwaonyesha vitabu kama msingi wa hoja zako.

Unfortunately sina muda wa kukaa na kuandika riwaya na kuishupalia Tanzania kwa maovu yote inayoyafanya na sio kwamba haina maovu ila kwa sababu its not my business. Lakini wewe hata mtu yoyote akisoma comments zako on Rwanda, automatically ana conclude kuwa you have an interest in the country. Until you agree that you do, sina muda wa kupoteza kubishana na wewe.
 
Mkuu kiasi fulani umechambua vizuri ila nachelea kuna jambo either unaficha au unatafuta mtu wa kulink kisicho sahihi.

1. I can smell unataka kutuambia kuwa kuna force behind inasponsor hao sindumuja ambaye ni Kagame???

2. Pili kusema RPF ndio waliotungua ile Ndege kule Rwanda nadhani si kweli na undermine influence ya Hutu extrimists ambao hawakutaka kushare power na mtu.

3. Mtu kama Niyombare (mhutu) aliyeongoza mapinduzi dhidi ya Nkurunzinzah unamuweka wapi?? Mi nadhani its not about maandalizi ya genocide ni tatizo la kimfumo wa utawala na kikatiba la Burundi.

Mwisho I thought mechanism za kujua huyu ni mtutsi au muhutu zilishaisha. Au mpaka leo bado kuna ID za mtutsi na mhutu?? Na pia nilidhani muungano wa taifa umesababisha intermingle baina ya hawa watu wawili. How comes serikali imeshindwa na kuruhusu makazi ya wahutu au watutsi??

Ninakuhakikishia kile kinachoendelea Burundi huwezi kukitenga na kagame. Kagame hasa ndio yupo nyuma ya mkakati huu ili kuhakikisha nkurunziza ambae ni muhutu atolewe madarakani. Kwa watu waishio Burundi wanalijua hili. Hoja ya kuwa mapinduzi ya Burundi yaliongozwa na godifroid niyombare ambae ni muhutu ni ya kipuuzi.Kwa anayekumbuka mapinduzi ya mwaka 2003 alipouawa rais Melchior ndadaye aliyekuwa kiongozi wa mapinduzi yale alikuwa muhutu tena ambae alikuwa waziri wa mambo ya ndani lakini kilichotokea ni kwamba buyoya Pierre ndie alikuwa rais.Siasa za Burundi na Rwanda huwezi kizizungumzia kwa ufasaha kama unategemea story tells.Hakuna ubishi kuwa kagame na RPA yake ndio walioitungua ndege ya rais habyarimana na ntaryamira wa Burundi.
 
Mkuu kama ulikuwepo... huyu FDLR jMali ni majanga kwenye jamii yoyote ile! tatizo lake kila siku anarudia yaleyale... ukitaka kujuwa jinsi matatizo ya Burundi walivyo yavalia njuga basi we tazama jinsi wanavyoyaunganisha na ukabila... ndugu yangu ugomvi unao endelea Burundi haufanani na ulio wahi tokea hata siku moja... Rwanda, watutsi walioukimbizini waliambiwa eti nchi imejaa... na waliokuwa ndani ya Rwanda walijuta kuzaliwa... huyu mwehu Interahamwe atakupotezea wakati, kwani ukimbananisha sana na kumuuliza maswali mazito atakuambia eti basi tuache, tufanye umeshinda, you see? tatizo la Burundi sio ukabila hata kidogo! tatizo la Burundi ni la madaraka, kama hauamini basi waulize kina Nyangoma, Radjabu, Rwasa, Mbonimpa, Ngendakumana, ntavyohanyuma na wengine na wengine... kina jMali ndio wamemtia kimavi Nkurunziza na hivi kaamuwa kuanzisha ukabila kusudi azuge... hawa Interahamwe sio watu, kitu ambacho hakimuingii jMali kichwani ni kwamba hata iwe vipi haiwezekani kuuwa raia wasio na hatia... hata ndege ikitunguliwa au ufanyiwe coup d?tat! mbona Raisi wa Burkinafaso karudishiwa ofisi yake na hivi anaendelea kupeta bila mauwaji? huyu jamaa jMali atakupotezea wakati bure, hana la maana zaidi ya Hutu power ideology...

Mkuu nina uhakika wewe una chuki binafsi na jmal. Kwa uchambuzi huu alioufanya hakukosea hata kidogo. Historia ya Rwanda inajulikana hata kama wewe na kagame mnapindisha ukweli.Mauaji ya Rwanda ya siku mia moja(genocide ) ni cha mtoto kwa mauaji wanayoyafanya hadi leo kagame na wenzake (Watusi ). Kwa kile kinachoendelea Burundi ni vigumu sana huwezi kukitenga na kagame na ndio maana wale kina Hussein Rajab na wengineo waliompindua nkurunziza 90% walikimbilia Rwanda na kagame anawapa msaada wa hali na mali. Hata yale mapinduzi engineer mkubwa ni kagame niyombare aliwekwa mbele kuzuga mataifa tu. Waliokuwa wanaandaliwa kuwa viongozi baada ya mapinduzi ni Rajab au buyoya ama sinduhije.
 
Back
Top Bottom