Sindano Iliyomuua Michael Jackson Kupigwa Mnada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sindano Iliyomuua Michael Jackson Kupigwa Mnada

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 25, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Michael Jackson
  Sindano ambayo iliripotiwa kuwa Michael Jackson aliitumia kujidunga dozi kubwa ya madawa yaliyopelekea kufariki kwake, itapigwa mnada na inategemewa kununuliwa kwa dola milioni 5. Kwa mujibu wa gazeti la The Telegraph la Uingereza, sindano hiyo inapigwa mnada mjni Las Vegas ikichukuliwa kama mojawapo ya kumbukumbu muhimu za Michael Jackson.

  Vyanzo vya habari vilisema kuwa sindano hiyo inatarajiwa kununuliwa kwa dola milioni tano na huenda ikapata mnunuzi wakati wa mnada mkubwa utakaofanyika juni 25 wakati wa kuadhimisha mwaka mmoja tangia alipofariki mfalme huyo wa muziki wa Pop.

  Familia ya Michael Jackson inasemekana kuwa inazo taarifa za mnada wa sindano hiyo na imekasirishwa sana na mawazo ya watu wanaotaka kunufaika na kifo cha Michael Jackson.

  "Hili ni mojawapo ya matukio kadhaa ya kusikitisha", alisema mdau mmoja wa familia ya Jackson.

  "Sindano hiyo haihitajiki kwenye kesi ya mauaji aliyofunguliwa daktari wa Michael Jackson, Dr Murray, lakini inasikitisha kuona kuna watu wasio na utu hata kidogo", alisema mdau huyo wa familia ya Jackson ambaye hakutajwa jina lake.

  Mwanaume aliyeitia mikononi sindano hiyo amekuwa akiwasiliana na wanasheria wake kuhakikisha kuwa hakuna mtu atakayejitokeza kumnyang'anya sindano hiyo wala hatakaliwa kuipiga mnada sindano hiyo.

  Michael Jackson alifariki mwezi juni mwaka jana kutokana na matatizo ya moyo kufuatia tabia yake ya kutumia dozi kubwa za madawa ya kupunguza maumivu.

  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=4236782&&Cat=2
   
 2. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Dunia ina mambo ya ajabu loh
   
 3. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,458
  Likes Received: 1,331
  Trophy Points: 280
  hayo ni mambo ya ajabu sana na huku ni kumkufuru mungu
   
 4. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kweli duniani kuna mengi
   
Loading...