Sinaga Swaga inairudisha Hip Hop ya Bongo kwenye mstari wake – Young Killer

Me kama dozi mkuu... asubuhi mchana na jioni bila kusahau usiku

Nimeukubali sana
Hahah mkuu mimi sasaivi nikibadilisha mziki mwingine nauona hauna ladha na gafla nashikwa na arosto ya Sinaga swaga
 
wimbo wa kawaida sana, sina swaga ya kuusikia mara nyingi nyingi aisee na kichupa hakiko vizuri sana ila kajitahidi
Wewe wimbo unaouskiza mara nyinginyingi kwa kipindi hiki ni upi???
 
young killer. .karudi katika ubora wake tunaoujua ..kupitia hii hii ngoma..yaani kuanzia beat mpaka mistari.huchoki kuisikiliza.
Haswaaa.... Real definition ya ubora wa zamani... Sasa ajitahidi kukaza
 
Ni wimbo mzuri ila bado haujafikia ubora wa Young Killer yule wa Dear Game,Jana na Leo au August 13.

Kikubwa nilichokiona humu Ni kaamua kuja name style ya Ney wa Mitego kaamua kuwaponda watu Kwa kuwataja majina labda anatafuta Attention ya watu.

Wimbo wa kawaida afate ushauri wa wanaomkubali arudi Kwa Mona Gangster kuanza upya si utumwa.
Kurudi kwa mona hatukatai ila awe anachanganya ladha za beat manake beat za mona zinafanana kiasi flani...
 
Rapper Young Killer anadai kuwa wimbo wake
mpya, Sinaga Swaga umekuja kuirudisha ‘real hip
hop’ kwenye mstari. Amedai kuwa kipindi cha hivi karibuni rappers
wengi wa Bongo wamekuwa wakilegeza ngoma
zao ili kuvutia biashara, lakini yeye ameamua
kukaza.

“Dhumuni la kufanya hii ngoma, nimetaka
kuwaonesha kwamba hip hop yetu bado ipo na
ina nguvu kubwa na ina uwezo wa kufika mbali
zaidi ya hapo ambapo ipo endapo tutaendelea
kuisupport na kuipa nafasi,” rapper huyo
amemuambia mtangazaji wa Pride FM, Eddy Msafi.

Rapper huyo amesisitiza kuwa masikio ya
mashabiki wa muziki Tanzania yanahitaji ngoma za
aina ya Sinaga Swaga na si kupewa nyimbo za
kuimba na kuchezeka tu.
Ila ukweli hii nyimb ní ya kawaidà nyimbó yake ya mwisho nzur ni ile aliyemshirikishà maua sama tumsaport tu ila ajipime dear gambe,superstar mpaka hapa vp
 
Japokuwa kwa mbaali nimeiona flow ya Songa, lakini kwakweli hii ladha ilikuwa inapotea mpaka mashabiki tukapatwa na arosto...
palla kaitendea haki hiyo biti in short hajawahi niangusha toka kwenye ngoma ya tunaizindua mitaa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom