sina raha na ndoa yangu......

polee...pili huyo mwanamke hajaelimika bado maana hajui kuwa kuwa na elimu pekee sio suala toshelevu, muache amange-mange ataja-juta mapemaa...anaringia elimu, akija pata pesa ndio itakuwa balaa zaidi...take action
 
heshima kwenu wote,................wana jamvi,ni takribani mwaka wa tatu sasa tangu niingie ktk ndoa na mwanamke ambaye niliamini tunapendana sana,lakin mambo yamenibadilikia hasa baada ya wife kuhitimu masomo yake ambayo pia nilimgaramia kama njia ya kumkwamua kielimu na kwa maisha ya baadae kwani amebadilika na kufikia hatua ya kunitamkia kuwa ni kheli tuachane na kila mtu aishi maisha yake kwa kua kama kazi anayo na anaweza kujitegemea.na sababu kubwa iliyopelekea yote hayo ni baada ya kugundua kua anamahusiano ya kimapenzi na bwana mmoja na nilipomuuliza likanusha na kudai nisimfatilie na nimwache na maisha yake,

tuna mtoto 1,naombeni busara zenu

Kusema ukweli wanaume wengi wakifunguka, utagundua kuwa kwenye ndoa wanaume wengi wamepata very raw deal. Wengine hukaa kimya ila huishia kuwa "violent" na kuonekana wanyanyasaji! Wanaume wanaokuwa fair sana kwenye marriege hii ndo malipo yao!

All you hear is the same story always! Nadhani marriege consellors wana kazi nyepesi sana sababu cases nyingi zinafanana!
 
Dah! inauma ila ndio maisha ya ndoa hayo...halafu mi nashangaa kuona harusi zinazidi kuwepo siku hizi wakati sisi tulio ndani ya ndoa tunataka kuchomoka huko na walio nje wanatamani sana kuingia "why"?....tulia na washirikishe wazee utapata maamuzi mazuri japo kweli mkeo kama kaishakwambia hivyo basi ujue wamefika mbali na huyo jamaa yake
 
Ivi kumbe kuna wanawake pia ni pasua kichwa kwenye ndoa,mi nlijua ni wanaume tuu,Pole Bro Ushauri ni Fuata moyo wako unataka nini,We dont knw the details of ur relationship.
 
Achana naye, we ni mwanaume Chukua mtoto lea, maisha yenyewe yako wapi kwani? akuletee ukimwi uje ujute, hana akili...kweli mwanamke mpumbavu huvunja nyumba kwa mikono yake hata biblia imethibitisha hilo...
ILA MALIPO NI HAPA HAPA DUNIANI....ATAKUKUMBUKA SIKU MOJA
 
Only time will tell how the clock tics....mpe muda...ila kama anazidi kujifaragua kuwa aachwe..mpe ruksa aende kwa huyo mwanaume aliyempenda baada ya wewe kumtoa ujinga...ila mkumbushe kuwa "mtalaka huwa haolewi na mwanaume mwenye akili zake".
 
Pole sana kaka.kwa mifano niliyopata kusikia na kushuhudia wallah sitamsomesha mwanamke,nikimuoa na form4 yake ndo hiyohiyo!
 
Katika maisha kuna mitihani mingi sana na huu ni mmoja wapo busara zako zinahitaji sana ktk hili kuwa na muda wa kutulia na kutafakali pia usisahau kumshilikisha mungu pole sana.
 
wakati nipo chuo nilikuwa na mpenzi wangu akawa anataka sana tuoane, nikamwambia ukimaliza chuo tu ntakuoa, kamaliza mwaka huu na habari za ndoa hana na tumekwisha achana. unajua kwanini nilimwambia akimaliza ndio ntamuoa, kwasababu mimi mwenyewe nilikuwa chuo na nilikuwa naona jinsi mahusiano ya watu yanavyoharibika hivyo nilijua miaka mitatu ya chuo kwake itakuwa ni kipimo kikubwa cha uaminifu, lakini alilshia kupata bwana mwingine na kunisahau. usimwamini mtoto wa chuo hata sikumoja.

ushauri: muweke chini muyaongee kama hataweza kujirekebisha bora umuache songa mbele na maisha yako, wala usipeleke suala kwa wazazi, kwani akikubali kwa shinikizo la wazazi huko mbele atakusumbua tu.
 
ungekuwa na moyo kama wangu ningekwambia hivi mdharau kwa namna ya ajabu na ndoa kama ni ya kanisan ama mskitin usimpe talaka ila mwonyehe as huoni kama kuna mtu humo ndani yaani mfanye kuwa fenicha. ukirudi pita na 50 zako, ukienda chumban kulala lala kimya wala usimguse. usimulize jambo lolote la heri wala la shari wala usimpige. ufanyapo haya jitoe akili kabisa ona kama ni binti wa kazi tu humo ndani. kama anaakili lazima nanga itapaa.

Ndugu yangu gfsonwin ikifika kwenye haya mambo huwa naheshimu sana maoni yako. Hakika huwa najifunza mengi na kuchanganya za zangu. God bless you.
 
Last edited by a moderator:
Kweli kua uyaone...lakini ndio waja wa Mwenyezi Mungu tulivyo. Ni wepesi sana kusahau.
 
pole mkuu ameona elimu aliyopata ndio kamaliza kila kitu......mkataa pema pabaya panamwita mwache aende zake maana kwa sasa hana mapenzi/upendo nawe tena
 
wakati nipo chuo nilikuwa na mpenzi wangu akawa anataka sana tuoane, nikamwambia ukimaliza chuo tu ntakuoa, kamaliza mwaka huu na habari za ndoa hana na tumekwisha achana. unajua kwanini nilimwambia akimaliza ndio ntamuoa, kwasababu mimi mwenyewe nilikuwa chuo na nilikuwa naona jinsi mahusiano ya watu yanavyoharibika hivyo nilijua miaka mitatu ya chuo kwake itakuwa ni kipimo kikubwa cha uaminifu, lakini alilshia kupata bwana mwingine na kunisahau. usimwamini mtoto wa chuo hata sikumoja.

ushauri: muweke chini muyaongee kama hataweza kujirekebisha bora umuache songa mbele na maisha yako, wala usipeleke suala kwa wazazi, kwani akikubali kwa shinikizo la wazazi huko mbele atakusumbua tu.

Kaka yangu alishawahi kuniambia, mume utampatia kazini; kumbe wengi mna mitazamo kama hiyo. Ukiwa independent unakuwa kwenye uwezo mzuri wa kuchagua mtu wa kuishi naye na unapunguza possibility za kuolewa kwa ajili ya kujikimu, inabaki mapenzi au kuanzisha familia. Pia unakuwa mature tayari!
 
...Unaishi na mke maisha ya namna hii halafu unasema umeoa? Utaishi hivi kwa muda gani? miezi miwili miezi sita mwaka? Halafu mke akiamua kuanza kulala nje ndiyo inakuwaje? Hakuna ndoa hapa kupunguza maumivu ya roho na labda kupata magonjwa ya pressure na kushindwa kufanya kazi zako za kila siku ni kupiga chini tu na kuanza upya katika idara ya mahusiano kuliko kuendelea kujiumiza roho kiasi hiki.

ungekuwa na moyo kama wangu ningekwambia hivi mdharau kwa namna ya ajabu na ndoa kama ni ya kanisan ama mskitin usimpe talaka ila mwonyehe as huoni kama kuna mtu humo ndani yaani mfanye kuwa fenicha. ukirudi pita na 50 zako, ukienda chumban kulala lala kimya wala usimguse. usimulize jambo lolote la heri wala la shari wala usimpige. ufanyapo haya jitoe akili kabisa ona kama ni binti wa kazi tu humo ndani. kama anaakili lazima nanga itapaa.
 
heshima kwenu wote,................wana jamvi,ni takribani mwaka wa tatu sasa tangu niingie ktk ndoa na mwanamke ambaye niliamini tunapendana sana,lakin mambo yamenibadilikia hasa baada ya wife kuhitimu masomo yake ambayo pia nilimgaramia kama njia ya kumkwamua kielimu na kwa maisha ya baadae kwani amebadilika na kufikia hatua ya kunitamkia kuwa ni kheli tuachane na kila mtu aishi maisha yake kwa kua kama kazi anayo na anaweza kujitegemea.na sababu kubwa iliyopelekea yote hayo ni baada ya kugundua kua anamahusiano ya kimapenzi na bwana mmoja na nilipomuuliza likanusha na kudai nisimfatilie na nimwache na maisha yake,

tuna mtoto 1,naombeni busara zenu

Pole sana. Ila mimi nashauri kama una ushahidi wa mkeo na huyo bwana, mtafute huyo bwana na umpe ultimatum aachane na mkeo nina Imani ukienda serious ataogopa labda mkeo alimwambia hajaolewa. Na huyo mkeo ana hulka tu ya kazi akizoea ataacha. Ndoa yenu bado ni changa, Simama imara we ndio baba usikubali kuyumbishwa nina Imani ukumuoa kwa bahati mbaya ulimpenda and you need to fight for your love.
Akiendelea kukujibu mtie vibao atakuheshimu sometimes ukiendekeza mapenzi ya tamthilia utaumia sana.
Swala la kuachana NO.
 
...Pole sana...sasa umeshatamkiwa hivyo na mkeo unasubiri nini tena kufanya maamuzi mazito? au unataka akuletee mtoto wa nje ya ndoa?
Face the truth, go for the hardest decision and move on. Don't fool yourself that shez gonna come and tell you that all that i did was wrong!You are dead wrong giving her the benefit of doubt. I know u kind of avoiding the tough decision, but thatz the reality, you are no longer wanted dude!
 
i've learned..
I came alone and i've to go alone
i've learned
people r with u only when they need u, not otherwise
i've learned.
Extra care of anyone by you will ultimately bring a blame for you, not appreciation
i've learnd..
A simple lie of ur close one can break you more than anything
i've learnd

i've learnd..
Help people but not upto the point beyond ur dignity.

dont let someone become a priority in your life
when you are an option for them............

pole sana, mwache aende kama ndicho anachotaka, kisicho riziki hakiliki wangu

hapo kwenye red ndio fimbo yangu yakuchapia binadamu sina muda kabisaaa na hawa binadamu
hivi ni vitu important kwangu
1.mungu wangu aliyeniumba nakunitetea sana uhai wangu
2.familia yangu
3.kazi na mali zangu basi.
Vyoote vilivyobakia ni optional
 
Back
Top Bottom