Sina rafiki ninayeweza kumwambia siri yangu yoyote

Vyeria

Member
Feb 26, 2018
57
75
Habari wadau

Mimi ni mdada wa miaka 27 kuna hiki kitu nashindwa kukielewa ni kawaida ama nina mapungufu.

Nimepita kwingi kwa maana ya kukutana na watu tofauti tofauti kuanzia primary, olevo, advance, diploma chuo kikuu na sasa kazini, majirani, kanisani na kijijini nilikozaliwa kuna wengi ambao tumekutana huko wa jinsia yangu na hata jinsia nyingine tukapendana sana na kushirikiana but linapokuja swala la jambo linanisumbua akili huwa sinaga rafiki naeweza kushare nae.

Ni kama kila mtu kwa tabia zao navyowafahamu nikimshirikisha jambo langu najua ndo utakuwa kwanzo wa kila mtu kufahamu. Mpaka umri huu sina mtu naemwamini 100% hasa mdada mwenzangu wa kuweza kusaidiana kimawazo.


Unanishauri nini?
Ni kawaida ?
 
Mie naona si jambo baya mwaya. Sababu kikawaida jambo lolote mkishakuwa wawili wenye kulifahamu basi hilo sio siri tena mwaya. Yaani ipo siku tu litakuwa dhahiri.

Maana kuna zile "nakwambia ila usimwambie mwingine" basi lugha hiyo inaendelea mpaka mtaa mzima utajua siri yako.

Usimuamini mtu mwaya. Ukiamua kumuamini mtu muamini tu ila kaa ukijua dunia haijawahi kuwa na siri.
 
Habari wadau

Mimi ni mdada wa miaka 27 kuna hiki kitu nashindwa kukielewa ni kawaida ama nina mapungufu

Nimepita kwingi kwa maana ya kukutana na watu tofauti tofauti kuanzia primary,olevo,advance,diploma chuo kikuu na sasa kazini,majirani,kanisani na kijijini nilikozaliwa kuna wengi ambao tumekutana huko wa jinsia yangu na hata jinsia nyingine tukapendana sana na kushirikiana but linapokuja swala la jambo linanisumbua akili huwa sinaga rafiki naeweza kushare nae.

Ni kama kila mtu kwa tabia zao navyowafahamu nikimshirikisha jambo langu najua ndo utakuwa kwanzo wa kila mtu kufahamu ,mpaka umri huu sina mtu naemwamini 100% hasa mdada mwenzangu wa kuweza kusaidiana kimawazo.


Unanishauri nini?
Ni kawaida ?
Okey !! Inategemeana na makuzi yako na inawezekana ulishawahi kumwambia rafikiyo,nduguyo Jambo ambalo lilikuwa la Siri lakini hakuweza kulitunza na kuliongea kwa watu wengine na likakuathiri hivyo inawezekana ukawa uliweka nadhiri kuwa hutoweza mwamini mtu tena
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom