Sina muda wa kupoteza, all in one!

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
I. Jamaa waliona raha sana kunipiga ban mwana wa mwenzao, ila poa uzuri nimelelewa na mama wa kambo, wageni walikuwa wanaita manyanyaso ila kwangu mimi yalikuwa mazoezi. Nimerudi salama wa salmini. Kama ulinimiss here I am, kama gauge inasoma vinginevyo barida. Chuki tumeumbiwa binadamu bwana, alipingwa Yesu mtoto wa Mungu, sembuse mimi Bin Letsholonyane?
II. Nina muda mrefu sana sijapokea PM, mara ya mwisho ilikuwa 17 Julai mwaka huu, tena meseji yenyewe ilikuwa ya mkwara kutoka kwa modereta, umeeona nilivyokuwa na bahati mbaya eh? Najua nyie watu wazima, sio mpaka muambiwe kila kitu. Messages from men will be highly discouraged, this is for sure!
III. Moyo mpweke jamani, tangu binti fulani atemane na mimi hali si hali huku. Show zangu zote hazina manager. Jitihada za kumpata Cantalisia ziligonga mwamba, nadhani Rejao alihusika hapa kutia ndumba kidogo. No sweat, tangazo ndo hilo hapo! Ofa ni mpaka kuisha kwa bidhaa…
IV. Nimerudi rasmi, kama unadhani hoja hii ina uhusiano na ile no. 1, you are deadly wrong. Hii ni maalum kwa wale JF-Fasta, ambao wanakuja kwa msimu, aidha kutongoza au kutimiza ajenda za kisiasa walizotumwa na wanasiasa uchwara wao. Naitwa Mphamvu (jina langu halisi), avatar yangu ndo hiyo unayoiona hapo juu ya post. Nadhani ni member mwenye zengwe kuliko yeyote humu, sio kwamba nakutisha, huo ndio ukweli wenyewe. Usije ukalikoroga halafu ukasema sikukuambia, maisha ya kuviziana mimi siyawezi.
V. Nikiwa kama shabiki wa soka kupitiliza (mpira kunoga), sasa hivi nafanya kazi ya kuitambulisha klabu ya Coastal Union yenye maskani yake Barabara ya 11 Ngamiani Street, hukoooo, Tanga yalikozaliwa mapenzi. Hii ni maalum kwa wale washabiki mdananda wa soka la Ulaya, wanaojifanya wanaijua EPL sijui na La Liga kuliko hata kina Thomas Mlambo na Jamie Roux wenyewe. Wakati huo huo wanalalamika soka la Bongo halikui wakati yeye kwao Mwanjelwa, jirani tu na Uwanja wa Sokoine, afu Simba ikifungwa analia machozi.
VI. Timu yetu bado inajikongoja kimapato na kila kitu, hatuna wabunge wa kucheza mechi kwa majina yetu kama zile timu za Kariakoo. Hatuna website kwa sasa (though tuko kwenye mchakato), lakini kwa kuanzia tunao ukurasa wa Facebook ambao tunautumia kuyoa taarifa za klabu kwa haraka.
VII. Tembelea huu ukurasa halafu mengine yatafuatia; Coastal Union | Facebook
VIII. Chagua hoja yoyote hapo juu ambayo unaona unaweza kuichangia, halafu tutaenda sawa. Usiogope!
IX. Kwaherini kwa sasa, na samahani kwa ambao nimewachosha kwa kachumbari hii ya hoja. Taratibu taratibu tu tutaelewana, hata babangu alimwagiwa maji ya ukoko na mama siku ya kwanza alipomtongoza...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mphamvu naona ujio wako sio wa verse moja,mengi yamejiri when you were out, welcome back!
 
Last edited by a moderator:
Welcome back Arifu, kumbe ulikuwa kifungoni?

Eeh bwana, tujitusi twenyewe tudogo tu hata mtoto wa .com hastuki, ila wenyewe wakabebea bango.
Nashukuru sana kaka mkubwa...
 
Doh! Mphamvu,
umelishwa nini jela jamani?

Ile jela ya kawaida ina ugali maharagwe, sana sana na kuliwa cha kopo.
Hii ya Jf inakupa uhuru wa kufanya mambo yako mengine, maana ukiingia humu unasoma habari tu.
 
Last edited by a moderator:
Ile jela ya kawaida ina ugali maharagwe, sana sana na kuliwa cha kopo.
Hii ya Jf inakupa uhuru wa kufanya mambo yako mengine, maana ukiingia humu unasoma habari tu.

Bado,toa na mengine uliyoyaficha,
mwaga yote Mphamvu,
kuna kitu umesahau...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mphamvu kabla hujapigwa BAN Madame B alikuwa wa ruttashobolwa but now she's mine. Pole sana na karibu tena ila acha tabia ya kugombana na mwenye nyumba ambaye huwa hakudai kodi.
 
Last edited by a moderator:
dah bora wewe ulipata pm july mie hata sikumbuki lini nilipata hiyo pm.... vipi na kule FB utaendelea kuwepo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom