Sina imani na Jaji mkuu wa tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sina imani na Jaji mkuu wa tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by johnmashilatu, Dec 23, 2010.

 1. j

  johnmashilatu JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  AGIZO la Jaji Mkuu Agustino Ramadhan la kupatiwa dhamana kwa raia wa Afrika Kusini, mwenye asili ya Kiasia Dawid Human (48), aliyehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela na faini ya sh milioni mbili, limefanikisha mfungwa huyo kuachiwa kwa dhamana.
  Dawid, ni Mkuu wa Kitengo cha ulinzi cha kampuni ya Geita Gold Mines (GGM); alikutwa na hatia ya shambulio la aibu hivyo kupewa adhabu hiyo Desemba 10 mwaka huu, baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, kujiridhisha kwamba mfungwa huyo alitenda kosa.
  Baada ya hukumu hiyo kutolewa, Dawid alikata rufaa na wakati huo huo Jaji Ramadha, aliagiza mfungwa huyo kupewa dhamana baada ya maombi ya dhamana yake kuwasilishwa kwa jaji huyo.
  Kwa mujibu wa maelekezo ya Jaji Ramadhan, Dawid alipewe dhamana hiyo kwa sababu za kibinadamu hivyo kutakiwa kuwasilisha mahakamani hapo pasi ya kusafiria na mdhamini mmoja aliyesaini mkataba wa dhamana ya sh milioni tano.
  Hata hivyo, Dawid alifanikiwa kutimiza masharti ya dhamana hiyo na hivi sasa yuko nje. Akizungumzia suala hilo kwa niaba ya Msajili Msaidizi wa Mahakama ya Rufaa, Janeth Masesa, ambaye pia ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyamaga, alisema Dawid akamilisha masharti ya dhamana yake Desemba 21 mwaka huu.
  Masesa, alisema raia huyo wa kigeni atakuwa nje kwa dhamana hadi hapo rufaa yake itakapoanza kusikilizwa. Hukumu ya Dawid ilitolewa na Jaji Aishiel Sumari wa Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
  Ilidaiwa kuwa Machi mwaka 2007 katika kijiji cha Mchauru, kilicho kwenye mgodi wa Geita, Dawid, alimshika matiti, sehemu za siri na makalio Adelina kwa nia ya kumnyangÂ’anya kitambulisho baada ya kufukuzwa kazi mgodini hapo.


  source:Tanzania daima

  My take.

  Tanzania ya sasa ina mambo kweli, yule mzungu wa enzi ya nyerere aliyedai kuwa serikali yake iko mfukoni mwake alikiona, lakini leo.

  nasema sina imani na jaji mkuu wa Tanzania Brigedia jenerali, Mwimba kwaya, mpiga kinanda, Augustino Ramadhan!

  pamoja na mengi namkumbuka zaidi katika uamuzi wake waketi alipoongoza jopo la majaji wenzake na kuikataa kuwepo kwa mgombea binafsi!

  Mimi sifahamu sheria, lakini kitendo cha kumpatia dhamana mzungu huyo kwa kisingizio cha ubindamu kinanishangaza

  vipi ubinadamu huo uonekane kwa Mzungu lakini usiwe kwa mama huyo ambaye alidhalilishwa na huyo kaburu?

  nakumbuka wakati fulani sam Six aliwahi kuikoromea idara yako kuwa inafanya ndivyo sivyo na yeye, akatafuta Forum ya kumjibu lakini nafikiri six alikuwa sahihi
   
 2. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tanzania sheria hazifuatwi, haijawahi kutoke mtu amefungwa alafu akikata rufaa anatolewa gerezani.

  Kama ni hivyo amtoe Liyumba, babu seya etc waje uraiani wakisubiri rufaa kusikilizwa.

  Yale yale ya kina ditopile na Zombe sheria kuanza kupindishwa kwa maslahi ya wachache.


  Hatudanganyiki tena.
   
Loading...