Nishaanguka sana mpaka nimekuwa sugu...nishajichokea na viumbe nyie!Nurse na wewe unaangukaga?.maana nakuona uko smart kweli kweli.
Nilikupenda sana emmanuel lakini katu hukuthamini penzi langu,ulipoumwa nilikubembeleza kwa maneno matamu uone jinsi gani nakujali na kukutakia uzima,ulipokasirishwa kazini bado nlikutia moyo,maumivu yako pia niliyabeba ili kukupnguzia uzito lakini wewe hukuthamini penzi langu katu..mapenzi yako kwangu yalishuka kila siku hupigi simu hadi nipige,tunaishi dsm hii wote lakini inapita hata miez 3-4 hatuonani hadi nibembeleze sana,kila nilichokuomba ulidai huna ilihali ulkuwa navyo.miaka yako 32 ilinifanya mwanzoni nkuone nmepata kuwa utawaza familia kumbe umri co tabia...machozi yangu hukuyajali wala kunithamini,nilikupenda sana emmanuel mwezi uliopita nilikutamkia tuachane nikajua ni gia ya kukubadilisha ndo kwanza ukasema nenda ili uendelee na wanawake wengine..(wanaume wapendeni wanawake wanaoonyesha kuwapenda kwa moyo kwani mtakuja kujuta baadaye)hyu niliyempenda hakunithamini ipo siku atanikumbuka..
Waoh.. pole sana mdada.
My dear haya ni maisha tu na huyo mwanaume wala hukuzaliwa nae, na amini kwamba huyo hakuwa wako, wako yupo njiani anakuja wakati tu haujafika wa kukutana nae siku ukikutana nae utajuta kwanini ulipoteza mda na machozi kwa mtu asiyejua thamani ya penzi lako, lakini haujapoteza mda hiyo ilikuwa ni hatua ya kupata uzoefu ili siku moja usilie kwa ajili ya mapenzi ila mapenzi ndo yatalia kwa ajili yako. Huu ndo mda wa kujipenda mwenyewe, kujithamini, kujiamini na kujitambua ili atakae kupenda atambua unajipenda mwenyewe, unajitambua, unajithamini na unajiamini.Pole...ukianguka unajikunguta vumbi na maisha yanaendelea!
View attachment 151972My dear haya ni maisha tu na huyo mwanaume wala hukuzaliwa nae, na amini kwamba huyo hakuwa wako, wako yupo njiani anakuja wakati tu haujafika wa kukutana nae siku ukikutana nae utajuta kwanini ulipoteza mda na machozi kwa mtu asiyejua thamani ya penzi lako, lakini haujapoteza mda hiyo ilikuwa ni hatua ya kupata uzoefu ili siku moja usilie kwa ajili ya mapenzi ila mapenzi ndo yatalia kwa ajili yako. Huu ndo mda wa kujipenda mwenyewe, kujithamini, kujiamini na kujitambua ili atakae kupenda atambua unajipenda mwenyewe, unajitambua, unajithamini na unajiamini.
mmmh kuna usemi unasema kupenda usipopendwa ni sawa na kusubiri boti uwanja wa ndege. Siku hizi haya mambo yapo watu hawana upendo wa moyoni unakuta tuu kuna kitu ametamani labda hela au papuchi. Hapo mtapendana mbaya zaidi mmoja yuko deep in love na mwingine ana mwadaa mwenzie. Baadae ni maumivu makali kwa yule aliyependa kwa dhati. Hizi situation zinakatisha tamaa sana ila ndo hivyo huwezi sema sipendi tena wakati unahitaji kupendwa.
pole mapenzi ndivyo yalivyo unampenda mtu, unamjali,unajitoa kwa moyo wako wote na kufumba macho kwa wengine lakin mwisho wa siku unaonekana -----.tulia mama Mungu yupo atakuletea mwingine atakae kujali.
Njoo kwangu sijawahi pata wa kunibembeleza jamani nasikiaga tu mmmh jamani!
pole mama wanaume ndo walivyo hata uwalambe bado wanamipango yao moyoni
Pole mwaya.. naimani ipo cku utampata akupendaye kwa dhati. Mapenzi ndivyo yalivyo ni kama kutia mkono kizani.
Labda yametokea hayo kwako ili tuwe pamoja, hebu njoo PM tujadiliane vizuri!