Sina hamu na ndoa tena.

Sina hamu na ndoa tena.

Ndugu uliyeanzisha hii topic.
Zipo kero nyingi katika ndoa lakini hiyo kero ya kuonewa wivu na mkeo is almost negligible.
Mshukuru Mungu kwa kumpa mkeo wivu kwani anayekupenda ni lazma atakuonea wivu.
Note: Kuishi na Mwanamke inahitaji uvumilivu wa hali ya juu sana.

lakini wivu ukizidi,huwa ni kero,anaonewa wivu,huwa hana raha mara kwa mara.mara utaambiwa hiki,mara kile,ni adhabu kwa kweli,ukiangalia huna kibaya unachokifanya
 
Pole Garmii na masahibu yalokukuta, yaani mambo ya simu huwa yanaharibu sana mahusiano, nakumbuka hata mie nilikuwa hivyo nikaona naumia tu na kukosa raha muambie mkeo umuhimu wa private ya kila mtu kwenye simu ili yasimkute hayo ya wrong number. Jambo lingine pia mwanamke sio wa kumlaumu ni hiyo hali ya kutopata mtoto ndio inamfanya akupekuepekue akidhani atapata lolote yaan labda unatoka na msichana mwingine ambae unaweza kuzaa nae,miaka sita sio midogo nadani ya ndoa bila mtoto.
Poleni kwa kukaa kipindi kirefu bila kupata mtoto msikate tamaa endeleeni kutafuta.Watu wengi walikata tamaa wamefanikiwa tu.
 
imenikumbusha frnd wangu alikwaruzana na mr wake akapaki vitu vya ndani vyote akanda kwao akidhani mr atamfuta kumwomba arudi, aliikaa kwao miezi 3 akipiga cm mr hapokei, akituma sms hazijibiwi, mwishowe alijirudia tena na vitu vyake kavipaki kwenye kenta...haaa mpaka kesho anabanana na mr kwa nguvu zote, kwao ni kwenda na kurudi....hahaha maisha ya ndoa yana vituko vya kutosheleza....

UUuuuuwi ningekoma, yaani ninune niende home halafu nisifatwe? ndio maana tuliofundwa hatuondoki mwenzangu kuepukana na aibu kama hii
 
yan dena nampenda sn my wife hata yeye ndio maana nashindwa kupata maamuzi

Kama unampenda sana mkeo kwa nini umeweka heading kwamba huna hamu na ndoa tena, huwezi kukosa hamu if u still in love
 
yan dena nampenda sn my wife hata yeye ndio maana nashindwa kupata maamuzi

Mi nimesema Tangu mwanzo.
Mwataka amuache mke wake.
Mwajua anachompa??

Kaka fuata ushauri wa Rose na MM.... nani sijui,
Nimekuandikia kule.
Mbembeleze huyo mywife wako, upendo,
Na umueleweshe aelewe somo vizuri bwana.
 
Kama unampenda sana mkeo kwa nini umeweka heading kwamba huna hamu na ndoa tena, huwezi kukosa hamu if u still in love

Mwenzenu, mi nilishasoma ktk ya mstari zamaaaaaani.
Eti wivu wa mke wake, umfanye aichoke ndoa.
Mmmmh sio kweli.
Labda kuna kingine.
 
we watudanganya ....that can never hapen.. ila kwa inaotokea wawaeleze wake zao wa rudi katika viapo walivyoweka wakati waoana.....
 
Mi nimesema Tangu mwanzo.
Mwataka amuache mke wake.
Mwajua anachompa??

Kaka fuata ushauri wa Rose na MM.... nani sijui,
Nimekuandikia kule.
Mbembeleze huyo mywife wako, upendo,
Na umueleweshe aelewe somo vizuri bwana.

kinachompa head anajua nampenda kiukweli hapa nilipo nipo naye nampa mistar
 
Hebu kesho ukirudi home nenda na mwanamke aliyependeza saaana. ukifika jidai ulidhani ameshaondoka. just pick a former class mate au mfanyakazi mwenzio tell her/him the whole story and you both pretend you have been dating for sometimes but you do it for fun!! ILA HAKIKISHA NI MZURI KULIKO HUYO MKEO!! LAZIMA HESHIMA ITARUDI maana akina dada wakati fulani hutuona hatuwezi pata mwingine hasa tunapoonyesha kuwajali sana!!
 
Anahitaji muda na nafasi ya peke yake atafakari maisha yake na ndoa yenu....kuna kuchoka kwenye ndoa na kulemewa hasa kwa vile hana mtoto,anahofu pengine unahangaika kutafuta mtoto huko nje,self esteem yake iko chini.....msaidie mkeo,hakupenda kuwa hivyo....muulize tu kwa upole tatizo ni nini na umuambie kama anahitaji nafasi utampa kwa nia nzuri akapumzike na kutafakari....pengine akikaa na mama atapata nguvu na hekima zaidi ya kumudu stress zake.

Kuhusu hilo la mwanamke aliyekosea namba,sisitiza tu kuwa humfahamu na kama bado unayo hiyo namba waweza mpa azungumze nae yeye mwenyewe,asipokuelewa,kaa kimya,atatulia mwenyewe.
Pole sana,natumai Mungu mwema atakupa mtoto kwa wakati wake,zidisha imani na mshukuru Mungu kwa mema mengi aliyokukirimu!
 
Kama unampenda sana mkeo kwa nini umeweka heading kwamba huna hamu na ndoa tena, huwezi kukosa hamu if u still in love


Yaani hata mimi nashangaa sasa hiyo heading ilikuwa ina maana gani kumbe bado unampenda mkeo sana tena sana. Na kuna sehemu umeandika ugomvi si kila siku wakati mwanzo umesema kila siku ugomvi, watu wengine bwana inawezekana hata mke hana huyu
 
Matatizo hayakimbiwi, bali kupambana nayo.
Pole sana kwanza inabidi na wewe,upate msaada ili hamu ya ndoa irudi kwani wivu wa mkeo juu yako kupoteza wewe kutokuwa na hamu ya ndoa kazi ipo.

Sikubaliani na hao wanaokushauri kuwa umruhusu mkeo aende kupumzika mmeshakuwa mwili mmoja na hiyo siyo ajira useme kuna wakati wa kuomba likizo.

Kama wengine waliotangulia kusema kuhusu kupata mtoto/watoto linaweza kuwa ni tatizo ambalo mkeo analitumia kma mlango kupitisha matatizo mengine,kwani wengine message zinatujia wenyewe,tunapalangana na kuyaweka sawa,kwani kuna ninachopata kwa mume wangu sikipati kwa wazazi wangu.

Mbona hasira hupoa na kwisha tafadhali hebu jadili na mkeo ikiwezekana,mkapate chakula cha jioni nje ya nyumbani kwenu zungumzeni mweleze jinsi unavyompenda na kumthamini,na hili la mtoto unaweza kuligusia kwa maana kwa pamoja mnahitajika kujenga familia yenu.

GARMA hata tulipokuwa huko makwetu mbona tulipishana na kaka,dada,wadogo zetu na tuliyaweka sawa na kusonga mbele,iweje kwa mtu uliyeapa kuishi nye milele,na zaidi ukiumwa anakuhudumia na kufanya yote.

PENDA NDOA KWANI NI CHAMA AMBACHO HAKIFILISIKI,NA HIZO UNAZOONA KERO NI MITIKISIKO TU KWA AJILI YAKUANGALIA KAMA MSINGI UKO IMARA AU LA
 
Wana JF mm nimeoa 2005 na sijabahatika kuwa na mtoto na huyu mke wangu,tatizo la mke wangu ni moja tu huwa anawivu sn kupita maelezo.imefika hatua naona nikero kwn sina aman na ndoa hii,nimejitahid sn kwenda anavyotaka bado haridhiki,mkewangu pia huwa anatabia ya kushika cm yangu na hii style kwangu cjaona kma ni tatzo ila ucku wa kuamkia leo ameniamsha ucngzn nakunambia nijibu sms niliyotumiwa na mwnmke wangu wakti mm cna taarfa yyte km kuna sms.sms yenyewe iliandikwa hivi!BADO NAUMWA DARLING.ukwel nilishtuka sn kwn sikuwa na dem nje ya ndoa,nilichofanya nilipiga cm mda huohuo nakupokea mwanamke huku cm yangu ikiwa loud.yule mwnmke aliomba samhni kwn alikosea number za mwisho.sasa mkewangu hataki kuelewa anataka kwenda kwao.naomben mawazo yenu pls!

huo unaitwa "uchovu wa hisia" dawa yake muwe mballi kwa muda kidogo, haina maana muachane au kila mtu ashike hamsini zake lah hasha, mwambie unahitaji aende nyumbani kwa muda na ni lazima .
kisha Muombe Mungu, wako, sala ni muhimu katika kila jambo. unapokuwa peke yako unapata muda wa kufikiri vizuri na kumuomba Mungu wako,
kila la heri
remember there is no one can save your marriage but you two....
 
uimsemeshe ,mkatie nauli ,mpe na hela ya njiani mwambie awasalimie nyumbani..................nilisha mfanyia mke wangu hivyo alinitolea macho hakwenda kokote! sometimes wanatuchanganya sana akili wakati kuna mambo ya msingi ya kufanya...
 
Pole sana. Wote mnahitaji space. Mpe ruhusa aende akapumzike after a month mkutane muongee,kwa pamoja mtaamua hatma yenu.
 
Pole sana mkuu,hajiamini kwa kuwa bd hajapata dogo,angepata wa kudia wivu.Anadhani unatafuta dogo 'small house' ,yapo sana hayo kwny ndoa.Ikishindikana mpata ushauri kwa wataalam au akapumzike kdg kwao.
 
Rafiki,mie naona kama una tutaabisha bure...kimsingi yaonesha wewe huna misingi ya kuaminika,kwani huyo mke wako angelikuwa na matatizo tangu mwazo,usingefikia hata hatua ya kumuoa.Kutokana na matendo yako,amepoteza kabisa imani na wewe,na hayo ndio matokeo yake..

Katika kichwa cha habari,umesema huna hamu na ndo tena...lakini kimsingi,navyoona ni kuwa,huyo mke wako ndio hana hamu na ndoa tena,na ndio maana anahitaji kuondoka kwenda kwao...

Nakushauri,jirekebishe,acha utoto,na usimtese binti wa watu.Kuolewa nawe isiwe ndio mwanzo wa safari wa kifo chake.Na mara nyingi,nyie mnaokuwa wa kwanza kupiga kelele za msaada,ndio pia waanzilishi wavurugu..
 
Dah yaani 2005 no ng'eeeeeeeeee ndani ya house. Shida nini man! Mpe ugonjwa wa miezi 9 akitoka huko anakaa mwaka na nusu akiudhuria clinic baada ya hapo wewe huna nafasi tena itachukuliwa na huyo mgeni wenu. From zea no kelele tena atakuwa bize na mtoto.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom