Sema Tanzania
JF-Expert Member
- May 18, 2016
- 251
- 466
Baba Neema alitupigia simu #116 baada ya kugundua mwanae kwa jina Neema, mwenye umri wa miaka 16 ni mjamzito na hivyo hatoweza kuendelea na masomo. Mwanzoni, Neema alisita kumtaja aliyempa ujauzito, lakini baadae alimueleza baba yake kuwa alibakwa na Askari Polisi na kupata ujauzito huo. Askari huyo alimtishia Neema baada ya kumbaka hivyo aliogopa kumueleza mtu yeyote.
Baba Neema alipopiga 116 kuomba msaada alisema, “Inasikitisha kuona kwamba watu tunaowaamini na kuwapa dhamana ya kulinda jamii zetu ndiyo hao hao wanaotuumiza.” Alikuwa amekwishafungua kesi lakini alihitaji tumsaidie kufuatilia na kuhakikisha haki inatendeka.
Tuliwasiliana na Kituo cha Polisi ambako mshukiwa wa tukio hilo alikuwa anafanya kazi na OCS alitujuza kuwa, afisa huyo alishasimamishwa kazi na uchunguzi unaendelea.