Mokes Junior
Member
- Aug 20, 2022
- 7
- 0
HEKALU LA WACHAWI sehemu ya 3
Mtunzi@NijoSenso.
Inaendelea.... Sitasahau siku bibi aliponiita ndani na kunikalisha kwenye ngozi nyeusi pale chumbani kwake. Siku hiyo ndiyo iliyobadilisha maisha yangu yote kwani hadi leo ninapoandika hii hadithi bado sipo huru nipo utumwani nimetekwa na uchawi. Asubuhi Moja bibi aliniita na kuniambia "mjukuu wangu Gonto, nadhani umeshakuwa mtu mzima sasa una miaka 15 ni muda mwafaka kuingia kwenye kundi letu" Kumbuka hapo Ilikuwa mwaka 2010 kipindi hicho nilikuwa nishaacha shule miaka mitatu nyuma. Nilimuuliza bibi kundi gani analomaanisha akanijibu la WACHAWI. Nilishtuka sana na kuogopa kwani nilikuwa mtu nayemkingia bibi yangu kifua pale wanakijiji walipomtuhumu kwamba ni mchawi Kumbe kweli alikuwa kigaguraaa!!!
Nilimkatalia bibi kata kata lakini jibu lake la mwisho lilikuwa lazima nijiunge na kundi lao nitake nisitake kwani nimechaguliwa na mizimu kuchukua nafasi ya bibi anayeelekea kuzeeka. Nililazimishwa kujiunga na HEKALU LA WACHAWI bila ridhaa yangu kipindi hicho mdogo wangu James alikuwa ametoroka nyumbani na kwenda machimboni Chunya. Hakika nilipata shida sana mwanzoni kwani tofauti na kutopenda kuwa mchawi pia nilikutana na watu ambao nilikuwa nawaheshimu Sana pale kijijini kumbe nao walikuwa WACHAWI!!!!
Bibi akishirikiana na WACHAWI wenzake walinifundisha Mambo mengi sana ya uchawi. Muda siyo mrefu nilizoea na kuupenda uchawi Yaani kiufupi nilinogewa na mechi pamoja na ibada za kichawi za kule hekaluni. Aisee jambo ambalo sitalisahau ni ile kafara!! Naam ni kafara ya mtoto mchanga iliyotolewa kwa ajili ya kunikaribisha na kunitakasa. Tukutane sehem ya nne.