Simulizi za Mkatekumeni:Kikao Changu na Mh.Rais Pamoja na Baraza la Mawaziri

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,261
Reaction score
4,443
Habari za wakati huu;
Leo ninaendelea na sehemu ya pili ya Simulizi za Mkatekumeni Ni mwendelezo usio na mtiririko wa ndoto mbalimbali ninazoota hasa zinazohusisha viongozi na masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.Ili niandike andiko hili lazima niote Ndoto so Usipoona Andiko ujue sijaota ndoto au ndoto nilizoota hazijakidhi sifa ya kuandikwa katika simulizi hii.

Katika Ndoto ya Mwisho nilikuwa na Mh.Mwigulu Nchemba Katika Ndoto ya sasa kwa bahati nimeweza kuwa na ugeni wa Mh.Rais pamoja na Baraza la mawaziri katika kikao chake.Hata hivyo nitoe angalizo.Katika kikao hiki pembeni ya Mh.Rais sikuweza kutambua Sura ya waziri yeyote yule.Mawaziri walikuwepo waliongea hara hivyo hawakuwa wale ninaowafahamu ila niliwatambua kwa wizara zao.

Vile katika kikao hiki sikuwa mtu wa muhimu wa kuongea wala kutoa maelekezo.Muongeaji mkuwa alikuwa ni Mh.Rais.Mimi nilibahatika tu Kuongea na Rais kidogo baada ya Kikao kuisha

Kama unapenda kufuatilia basi tazama andiko la Kikao na Mh.Waziri Mkuu Simulizi za Mkatekumeni: Kikao changu na Waziri Mkuu Mwigulu

Sasa Tuendelee.

Ndoto imeanza tukia ndani ya Ukumbi wa mikutano katika ukumbi huu Mh.Rais ameketi na anazungumza na Mawaziri kwa upole na Taratibu akiwaambia:

Ndugu zangu,Nimewaita hapa kwa sababu ninataka nizungumze na ninyi wote kwa pamoja kabla sijaanza kuzungumza na kila mmoja wenu.Nilipowateua sikuwapa Uwaziri kama zawadi,sikuwapa uwaziri kama kulipa fadhila niliwateua kwa sababu ya uwezo wenu kwa kuzingatia changamotona vipaumble vya nchi na wizara zenu.

Rais aliendelea kusema,Nchi yetu iko katika hatua muhimu sana kihistoria,kijamii na kiuchumi.Kihistoria nchi yetu ipo katika Tipping Point.Tupo katika Tipping Point ya Kisiasa,Tupo katika tipping point ya kijamii na tupo katika tipping point ya Kiuchumi.

Kwa kawaida taifa linapokuwa katika tipping point huwa linayumba na hata linaweza kuanguka.Hata hivyo kuanguka katika hatua hii hakukwepeki ila tunaangukia upande gani?Tunaangukia Upande mzuri wa maendeleo na mafanikio kwa jamii yatu au tunaangakuia upande mbaya wa umaskini na mahangaiko kwa wananchi.

Mmekuwa mawaziri katika mgumu zaidi ila pia wakati bora zaidi.katika wakati huu utendaji wenu unaweza kuwaingiza katika historia kama viongozi BORA kabisa lakini pia unaweza kuwaingiza katika Historia kama viongozi wabaya kabisa kuwahi kutokea.Na changamoto hiyo inanihusu Pia mimi kama Rais,Makamu wa Rais pamoja na Viongozi wengine waandamizi na watumishi wengine wa umma.

Mimi kama Kiongozi wenu nataka sana tuangukie katika Upande mzuri wa historia.Nataka tutakapotoka katika kipindi hiki tutoke tukiwa kama taifa imara.Tutoke tukiwa wamoja lakini zaidi tusimuache mtuu yeyote nyuma.Sasa ili tufikie hayo malengo ni lazima tufanye kazi kwa pamoja.

Katika siku za karibuni nimeona kwa kiwango kikubwa sana ninyi kama mawaziri mmesahau majukumu yenu.Mmesahau hasa Majukumu yenu ya kisera na kiutendaji.Hili limienifanya nijiulize iwapo nimekosea kuwateua ama tu ni changamoto za kikazi.

Rais aliendelea kuongea na kusema."Ninapokuteua uwe waziri sikupi Probation,sikupi muda wa kujifunza,sikupa muda wa kujaribu.Maisha ya watanzania namaendeleo ya watanzania sio kwa ajili ya majaribio.Ninapoona mawaziri mnakuwa kama vile mnajifunza na kujaribu ninapata wasiwasi sana.

Kabla ya kuwaita nilifikiri kuwafuta kazi na kuteua mawaziri wengine.Fahamuni kwamba Ninayo majina ya kutosha kabisa ya watu ambao ninaweza kuwateua kuwa mawaziri hata sasa hivi.Ni suala tu la kumuambia Katibu mkuu achukue kundi X atoe hapo wizara 3 na kundi Y wizara zingine na atangaze baraza Jipya.Lakini kabla ya kufanya hivyo nimeona nizungumze na ninyi.

Ninapounda na kuteua wizara huwa ninatazama mahitaji ya kisera.Hata hivyo lazima pia nizingatie mahitajia ya kiuchumi,kisiasa na hata kijamii.Kunaa baadhi yenu ambao hatambui Hili.Jukumu lako kama waziri ni kuhakikisha unatambua mchango wa wizara yako Kimapato.Kila wizara ina kundi la jamii linalojishugulisha na shughuli za kiuchumi na ni lazima waziri ufahamu mchango wa wadau wa wizara yako katika Uchumi wa nchi

.Nataka kila waziri afahamu Je katika Mapato yanayokusanya na TRA mapato yanayotokana na wadau wa wizara yake ni kiasi gani?Nataka kila waziri afahamu pia katika mapato ya halmashauri Je mapato yanayotokana na wadau wa wizara yake ni kiasi gani?Nataka kila waziri afahamu Je mapato yanayokuswanywa moja kwa moja na wizara yake ni kiasi gani?Nataka Taarifa hizi kila wiki zifike kwa waziri wa fedha ili waziri wa fedha azifikishe kwa katibu mkuu na kisha taarifa zitolewe kwa wananchi na wadau.Na taarifa hii ifanyike pia katika matumizi ya wizara zenu.Natka Taarifa za matumizi ya wizara kila wiki.Kwa hivyi nitahitaji taarifa za mapato na matumizi za wizara kila ROBO mwaka na CAG nakuagiza uzifanyie ukaguzi taarifa Hizo.Sitaki tenda kuletewa taarifa za ukaguzi za mwaka nataka sasa taarifa za ukaguzi wa Robo Mwaka.

Eneo lingine la muhimu ambalo nataka kila waziri alitazame ni maeneo ya kimkakati.Ninaposema maeneo ya kimkakati nataka wewe kama waziri utambue Je ni Mikoa Gani katika nchi yana umuhimu wa kimkakati kati wizara yako?Hakikisha unayatazama kwa ukaribu maeneo hayo na kuhakikisha yanakuwa na mazingira sahihi na wezeshi.Kama taifa tuna maeneo ya Ukanda wa kilimo,ukanda wa madini na hata ukanda wa utalii.Ni lazima waziri uyatambue,uyafuatilie na kuyasimamia maeneo hayo ni kama ilivyokuwa hapo JUU kwenye Mapato unipatie TAARIFA za wiki,mwezi,Robo mwaka na Nusu Mwaka zinazolenga kunionesha mapato na matumizi yanayofanyika katika maeneo hayo pamoja na taarifa nyingine.

Ninyi kama mawaziri ni askari wangu.Ninapowatuma kwenda kufanya kazi nataka mfanye kazi.Ninafahamu kila waziri ana mtu wake wa media na ni lazima kila wiki angalau mara 2 waziri uzungumze na wadau wa wizra yako katika maeneo mbalimbali ya nchi.Mnapo wakuu wa mikoa,wilaya na wakurugenzi.Pangeni Ratiba Zenu za kuzungumza na wadau.Nataka waziri wa kilimo akiwa anazungumza na wadau wa kilimo Njombe waziri wa madini awe anazungumza na wadau wa madini Mererani na waziri wa biashara awe anazungumza na wadau wa biashara Dodoma ila nataka mzungumze na wadau wa wizara zenu na taaria za mazungumzo yenu ziwe sehemu ya taarifa rasmi za Baraz la mawaziri zikionesha mambo yaliyoibuka hatua zilizochukuliwa na zinzopaswa kuchukuliwa kama ni mabadiliko ya sheria,elimu zaidi kwa umma au kama ni kuongeza usimamizi na ufuatiliaji.Zungumzeni na wadau wa wizara zenu.

Kama mnavyofahamu tunaishi katika zama ambazo teknolojia za mawasiliano zinakuwa kwa kasi.Kama taifa ni lazima sasa tufanye uamuzi.Je Tunaweza kutumia kikamilifua fursa za kiteknolojia katika zama hizi?Kwanza kabisa tukianza tu na Swala kuusanya Taarifa Je mifumo yetu inasomana?Waziri unayesimamami hasa maswala ya TEHAMA nataka nifahamu tuahitaji nini ili tuweze kuwa na Full Digital Governance?Je tumeshawiza kuwa na uwezo wa Kumpa mwananchi namba moja ambayo anaweza kuitumia kwa maisha yake yote?Je tumeshaweza kuwa na Mifumo inayosomana kiasia kwamba mwananchi akiupodate Taarifa yake sehemu moja basi Nchi nzima kila kanzi data inakuwa na taarifa zake?Je Pale Nationa Data Centre tumefanya Uwekezaji wa kutosha?Tuna Backups za kutosha?tuna Redundancy ya kutosha.Nataka kila Mkoa uwe na Copy ya Primary Data za Kila Mkazi wa eneo hilo au mtu yeyote ambaye amewahi kupata huduma katika eneo hilo.Sitaki kabisa kuona wananchi wnapoanga Foleni kutaka huduma katika Ofisi ya Serikali Popote.

Hata katika Ofisi hizi kuwe na workstations ambazo mwananchi anaweza kufanya self service kama akihitaji,Tutumie AI kwa ajili ya kurahisisha mawasiliano na upatikanaji wa Taarifa.Nataka Tuwe na Digital Governance kwa asilimia 100.Hili ninataka kabla ya Mwisho wa mwaka liwe limetimia.Kama itabidi tuwarudishe watumishi wa umma Shuleni ila wakasoma IT pamoja AI basi tufanye hivyo ila hatutaki kabisa mwananchi akose huduma mtandaoni.Wananchi wawe na uwezo wa kupata huduma mahali popote pale wakati wowote ule.Zaidi mwananchi asirudie Taarifa mara mbili.

Uhamiaji nashangaa sana kwamba bado mifumo yenu haisomani na mifumo ya NIDA.Hakikisheni mifumo yenu inasomana.Nimeona TRA tayari mifumo inasomana,Halmashauri mifumo inasomana,Brela mifumo inasoma ninyi tu ndio bado mifumo yenu hasa ya kuhudumia wananchi haisomani.Mtu anapotaka Passport anapaswa tua aingize NIDA namba yake kisha aseme sababu ya Safari.Tuwaache watu wasafiri,waende duniani wakatafute FURSA dunia kwa sasa ni kijiji.

Wizara ya mambo ya ndani hasa Polisi.Mnapomkamata mtu mnahitaji muwe na mfumo ambao unaweza kumtambua mtu kwa alama ya kidole au namba yake ya nida.Mbona mitandao ya simu wanatumia NIDA na Vidole Gumba kusajili line za simu.Hizi teknolojia zipo ni suala tu ya kujifunza.Kama itabidi kuwarudisha Polisi wote shule wakajifunza hamna shida cha muhimu ni mtu akikamatawa basi tuwe na Digital Report Book ambapo taarifa za kukamatwa zitawekwa na sababu ya kukamatwa hatuwezi kuendelea kuwa na watu wanafichwa kwenye mahabusu ya Polisi bila ndugu kuwa na taarifa.

Wizara zote kwenye hili eneo la Tehama nawasisitiza sana sisi kama Serikali lazima tuwe mstari wa mbele.Ninasikia kuna mambo ya NFTs na sijui fedha za kidgitali Tazameni muone kama kuna fursa ya kuwainua wananchi na kuboresha hali za wananchi basi zitazameni vyema.

Nawasisitiza tena.Ninyi ni askari wangu wa mwamvuli.Wananchi wanwategemea,Mimi ninaategemea.Msinifanye nione kwamba nilikosea kuwateua nataka mfanye kazi na ionekana mnafanya kazi.Asanteni.

Baada ya kikao Mawaziri walielekezwa wazungumze na Katibu mkuu iwapo wana mambo au taaarifa za kumkabidhi.Nilibaki na Mh Rais tukijadili masuala binafsi na aliniuliza iwapo nimeshaamua iwapo niko tayari kuingia katika utumishi wa nchi yangu au la na iwapo nina lolote ambalo nimeona linahitaji kuwekewa mkazo.Nilimwambia kwa ninavyoona kila kitu kiko sawa ingawa kwa upande wa wananchi badi serikali inabidi ifanye zaidi ili kuhakikisha wananchi wengi wanaona matokeo ya utendaji bora wa serikali.
 
Achana na mada za kindoto ni za kipumbavu tu na hazina mvuto.

Huko nyuma ulikwisha andika pia lakini hakuna yeyote inayofika wachangiaji 5. Watu hawataki ku-discuss hisia
 
Achana na mada za kindoto ni za kipumbavu tu na hazina mvuto.

Huko nyuma ulikwisha andika pia lakini hakuna yeyote inayofika wavhangiaji 5. Watu hawataki ku-discuss hisia
Usijali nisipoota sitaandika.
 
Back
Top Bottom