Simulizi Ya Kweli: Msako Wa Mange Kimambi

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,445
Image may contain: 1 person, smiling, text
 
SEHEMU YA KWANZA

“Uko wapi?”
“Magomeni.”
“Unafanya nini?”
“Niko ndani ya gari…kwenye foleni.”
“Mambo yameharibika huku.”
“Kivipi?”
“Kirusi kimekwishaingilia mafaili.”
“Sijakuelewa.”
“Ingia Instagram kwa Mange Kimambi” sauti ya mwanamke upande wa pili alisema kisha akakata simu. Alikuwa ni mke wa waziri. Scora Mtinika.
Stanley Massawe, mwanaume mfupi, mweusi, mwenye kitambi kilichotokana na ulaji wa kuku wa kienyeji, sanjari na bia mbili tatu za afya, alikuwa amekamata simu ile, kama vile ndio mara ya kwanza kukitia mkononi kifaa kile cha mawasiliano.
Alikuwa amebung’aa huku akihisi mapigo ya moyo yakimwenda kasi kuliko kawaida, ingawa ndani ya gari lake dogo, alikuwa amefungulia kiyoyozi, (Air Condition) jasho lilimchuruzika maungoni mwake kwa kasi kiasi cha kulowanisha shati lake la kijani alilokuwa amevaa na kuacha baka kubwa eneo la kwapani.
Sauti ya mtu aliyezungumza naye kwenye simu ilikuwa ikijirudia kichwani mwake.
“Kirusi kimekwisha ingilia mafaili….. Ingia instagram kwa Mange Kimambi” alikumbuka maneno yale.
Moyo ukawa unampwita kwa nguvu. Alimfahamu vema mwanamke yule, mwanaharakati anayetumia akaunti yake ya ‘Instagram’ kuibua mambo mazito ya wanasiasa, wafanya biashara, wasaniii, na watu mbalimbali mashuuri.
“Kaandika nini huyu kahaba” alinong’ona taratibu huku akiingia mtandaoni kuona kile kilichoandikwa na Mange Kimambi.
“Piii..piiii…piii..” sauti za honi za magari zilisikika nyuma ya gari lake.
Kabla hajanza kuperuzi alistushwa na honi zile. Askari aliyekuwa akiongoza magari alikuwa ameita magari ya upande wake.
Akasitisha kwa muda zoezi la kuangalia kile kilichokuwa kimeandikwa na mwanamke yule aishiye nchini Marekani.
Aliliondoa gari kwa kasi, akavuka mataa ya Magomeni, akaanyooka na njia ya Kinondoni, alipofika pale Magomeni Kanisani, alikata kushoto akashika barabara ya Tandale Uzuri.
Mita kama miamoja akaingia kwenye kinjia kilichochepuka, upande wa kulia ambapo kuna makaburi ambayo yapo mkabala na gereji bubu ya magari.
Akapaki gari lile aina ya Toyota Harrier ukingoni mwa ukuta wa makabauri. Akatizama mbele na nyuma kupitia kioo cha nyuma akaona hayupo katika njia ambayo angeweza kusababisha lapsha za hapa na pale.
Alinyakua simu ile aliyokuwa ameitelekeza kwenye dashboard, kisha akabofyabofya, punde akawa anaupitia ukurasa wa Mange Kimambi.
Hazikuzidi sekunde tatu kabla ya kuona habari. ambayo sio tu ilimstua lakini pia, ilimwogopesha.
“Mungu wangu!!!” alihamaki.
Macho yalimtoka kama mtu aliyefumaniwa akizini na mke wa mtu chumbani kwa mume. Alikuwa hapumui sawasawa kutokana na uzito wa habari ile ambayo ilipostiwa na mwanamke yule.
Akarudia tena kutizama habari ile, akaona kwa siku hiyo stori hiyo ilikuwa imepata ‘views’ ‘like’ na ‘Coments’ nyingi kuliko habari yoyote.
Habari iliyopostiwa na Mange ilimwonyesha yeye akiwa na mwanamke mmoja aitwaye Scora. Mke wa Waziri Hussein Mtinika. Wakiwa kama walivyozaliwa, ndani ya chumba cha Hotel moja ya kisasa huko Pemba visiwani Zanzibar.
Picha ile ya video iliwaonyesha wakiwa wametoka kuvunja amri ya sita, huku wakiwa katika mahaba mazito na mwanamke huyo wa Kigogo.
Katika video hiyo, Mange Kimambi alikuwa akimsifia kwa kejeli Stanley kwa kutembea na mke wa Waziri yule ambaye kwakwe, alikuwa ni kiongozi asiye na huruma na maisha ya watu.
“Hakika wewe ni mwanaume wa shoka, umeweza kumsuuza mke wa Waziri Hussein Mtinika….sema pamoja na yote, umeniangusha..unakibamia!! sidhani kama ulimsuuza vizuri!!” ujumbe ule ulisomeka hivyo.
“Nimekwisha!!...nasema nimekwisha mimi!!” Stanley alipayuka huku machozi yakimchurika.
Jambo lile lilikuwa ni zito mno maishani mwake. Kamasi lilimtoka, jasho jingi zaidi ya lile la awali lilimchuruzika. Wasiwasi ulikuwa umtenda moyoni mwake.
Kamwe hakutegemea kama tukio lile alilolifanya miaka saba iliyopita, ambalo alimini siri ile kamwe isingejulikana kwakuwa hapakuwa na yeyote aliyekuwa akifahamu uhusiano wake na mke yule wa waziri zaidi ya wao wawili.
“Sasa nani amevujisha siri hii kwa hiki kirusi cha Instagram??” Stanley alinon’gona.
Akiwa bado katika taharuki, simu yake iliiita, alipoangalia kwenye kioo cha simu ile akaona mpigaji ni Scora Mtinika, mke wa waziri.

Itaendelea
 
SEHEMU YA PILI

ILIPOISHIA…
Kamwe hakutegemea kama tukio lile alilolifanya miaka saba iliyopita, ambalo alimini siri ile kamwe isingejulikana kwakuwa hapakuwa na yeyote aliyekuwa akifahamu uhusiano wake na mke yule wa waziri zaidi ya wao wawili.
“Sasa nani amevujisha siri hii kwa hiki kirusi cha Instagram??” Stanley alinon’gona.
Akiwa bado katika taharuki, simu yake iliiita, alipoangalia kwenye kioo cha simu ile akaona mpigaji ni Scora Mtinika, mke wa waziri

ENDELEA NAYO…
Akasita kuipokea simu ile akawa akaitizama kama vile ndani ya kifaa kile kulitegeshwa bomu, simu iliendeleakuita kiganjani mwake.
Akakata shauri akabofya kitufe cha kupokelea nakuweka simu sikioni.
“Hallow” sauti nyembamba ilisikika
“Nakusikia”
“Umeona ?” scola, mke wa waziri mtinika alimuuliza.
“Nani ametufanyia huu unyama?”
“Sijui” scola alijibu.
Stanley akapiga kimya huku simu ikiwa bado ipo sikioni. Kisha akauliza kwa kwa sauti ya unyonge.
“Tunaweza kuonana?”
“Nini!!” Scola akahamaka kwa mshangao
“Tunaweza kuonana?” Stanley akauliza tena.
“Ili?”
“Tulizungumze hili”
“Hapana stanley, naogopa”
“Maji yamekwisha mwagika hatuna budi kuyaoga, Unapoendelea kuishi katika hofu ndivyo unayoikaribisha zaidi hatari maishani mwako” Alisema Stanley.
ukimya mwingine ukapita, kisha scola akazungumza simuni kwa sauti ya unyonge.
“Hatuwezi kuzungumzia kwenye simu?”
“Lakini kwanini hutaki tuonane?”
“Hebu kuwa mwelewa Stanley, kila kona sasa hivi wanazungumza jambo hili, kitendo cha kuonekana tukiandamana pamoja mtaani ni kuzidi kudhihirisha kile kinacho sambaa mtandaoni.
“Hufikirii ni hatua gani atachukua mume wangu dhidi yetu? Huna hofu kabisa na jambo hili Stanley, usisahau kabisa kwamba mimi ni mke wa waziri, na usijifanye hujui kwamba jambo hili limemdhalilisha mume wangu kwa kiwango kikubwa sana, na usidhani kwamba atalipuuza tu kama mwendawazimu, mimi na wewe kuanzia wakati huu hakuna ambaye yupo salama”
Scola alisema, Stanley alishusha pumzi ndefu, kwa mara nyingine alihisi tumbo likipata joto, hofu kubwa ikamvaa, alitamani ardhi ipasuke atumbukie ndani yake. Maneno ya Scola yalimwingia sawia mvulana yule chakalamu.
“Sasa naomba unisikilize kwa makini” Stanley alimwambia.
“Nakusikiliza” Scola akajibu.
“Waandishi wa habari wamekwisha kupigia kukuliza juu ya jambo hili.?” Stanley akamuuliza.
“Wamenipigia sana, lakini hadi sasa sijapokea simu yoyote, na sijaongea na mtu yeyote”
‘Vizuri sana, sasa unachotakiwa kufanya ni kulikanusha jambo hili kwa nguvu zote, likanushe kwa waandishi wa habari na kwenye akaunti zako mbalimbali za miotandaoni” Stanley alisema.
“Nitasema nini sasa wakati video iko wazi ikinionyesha mimi na wewe tukifanya uchafu ule”
“Unatakiwa useme picha hizo za video zimetengenezwa, shikilia msimamo huo,” stanley alisisitiza.
Ukimya mwingine ukapita baina yao, hatimaye scola akatikia kwa sauti ya taratibu:
“Sawa, nitafanya hivyo”
“Vizuri, hata mimi huo ndio utakuwa msimamo wangu, nitakukana popote pale niendapo”
Wakakubaliana hivyo.
Masaa machache badaye tukio la kuvuja kwa video ya Scola mke wa waziri na Stanley wakiwa katika mahaba motomoto ilikuwa gumzo nchi nzima.
Kila kona mada kuu ilikuwa ni kitendo hicho, vituo vya redio na runinga viliripoti jambo lile kadiri walivyoweza.
Mke wa waziri Mtinika, Scola mtinika alipopigiwa simu kutoa ufafanuzi juu ya ile sintofahamu alikana Kwa nguvu zote huku akiliweka tukio hilo katika muktadha wa kisiasa.

“Hizi ni hila anazofanyiwa mume wangu na maadui zake wa kisiasa kwa kunitumia mimi, kwakweli siwezi kukubali jambo hili linichafue kwa kiwango hiki, nimekwisha ongea na mwansheria wangu kwa ajili ya kupeleka jambo hili mahakamani. Na nina wahakikishia mange kimambi nitamtia adabu” Scola alijitetea mbele ya waandishi wa habari.
“lakini video inaonesha ni wewe, ukweli wa jambo hili ukoje?” mwandishi mmoja akauliza.
“Niwajibu mara ngapi kwamba hii ni hila ya mange kimambi, video hiyo ni ya kutengeneza, mtu ninaye husishwa naye simjui, na ifahamike mimi ni mke wa kiongozi mkubwa, kamwe siwezi kufanya uchafu wa kiwango hiki.” mwanake yule alizidi kujitetea.
Kwa upande wa waziri mtinika ambaye alikuwa ziarani nchini Marekani, alipotafutwa na waandishi wa habari kwa njia ya simu ajabu simu yake ilikuwa haipatikani, hata Scola, mke wa waziri huyo naye alipojaribu kumtafuta mumewe ili amweleweshe juu ya bomu lililolipuliwa na Mange Kimambi, hakumpata simuni.
“Mungu wangu nini kimempata mume wangu, kwanini hapatikani na siyo kawaida?” Scola alijiuliza kimoyomoyo.
Ndani ya muda huohuo mara simu yake ya mkonoi ilianza kuita, alipocheki kwenye kio cha simu akaona namba ya Stanely, moyo wake ukamdunda maana walikwisha kubaliana kutotafutana.
Simu iliita hadi ikakatika, mpigaji akapiga tena, mwisho alikata shauri akaona acha apokee:
“Hellow” alisema baada ya kupokea simu
“umeona kitu kingine alichoposti hiki kirusi”
“Kirusi gani?”
“Si Mange Kimambi”
“Kaposta nini tena?”
“ingia uangalie, alichoposti safari hii ni kibaya kuliko alichopost awali”
“Mungu wangu!!” Scola aliogopa.

ITAENDELEA
 
Back
Top Bottom