Simulizi Ya Kuvut

Asaelofficial

Member
Sep 5, 2017
30
35
NICE GUY OF CENTURY

SEHEMU YA 01

Ni katika supermarket moja alionekana Baba akiwa mke wake pamoja na mtoto wao mdogo wa mwisho katika uzao wao,mke alikuwa alilalamika kuwa hela hawana halafu mmewe amemleta sehemu ya gharama supermarket kununua keki ya birthday ya mtoto wao mkubwa wa kiume Asael,mtoto ambaye hana hata kazi tangu amalize masomo yake hakuwa ameajiriwa mpaka muda huo bado tegemezi nyumbani,
Baba alichukulia busara hakutaka kubishana na mke wake alimwambia...
"Mke wangu huyu ni mtoto wetu hata kama kwa sasa hana kazi ni tegemezi kwetu itafika tu wakati naye atapata kazi,na kuhusu kutumia pesa hata iliyobaki ya matumizi yetu nyumbani kumnunulia keki ya gharama mtoto wetu ambaye hana hata msaada kwetu kwa sasa sioni kama ni tatizo huyo ni mwanawetu hivyo ikiwa leo ni siku ya kuzaliwa kwake acha tutumie hata kidogo tulichonacho kuhakikisha mtoto wetu anapata furaha,ikiwa sisi tupo hai ni jukumu letu hili"
Hayo yalikuwa maneno ya mzee baada ya mkewe kulalamika kuhusu kijana wake kukosa kazi ya msingi tangu amalize masomo yake kutokana na tatizo la ajira kwa sasa.
Mkewe alimuangalia mmewe kisha akasema...
"nilijua tu utamtetea tu kijana wako,haya nunua hiyo keki twende"
aliongea mkewe,
mzee akajua huyu tayari nimeshamshinda ujanja,hayo yalikuwa ni maneno ya hapa na pale ya familia wakati wakiwa katika supermarket...
mara mtoto akaona mkate akamunyoshea mkono baba ake amnunulie...
Baba akawa anataka kumnunulia mtoto wake kwa siri ili mkewe asijue maana alijua tu lazima mkewe angemsema tena kuwa kawadekeza watoto wake....
Mzee alikuwa na tabia ya kutokukubali mtoto wake apate shida au ateseke ikiwa yeye anauwezo wa kumsaidia...

Walifika nyumbani walianza maandalizi ya kuandaa siku ya kuzaliwa ya kijana wao mpendwa walipanga kumfanyia surprise/mshitukizo hawakumpa taarifa,yeye mwenyewe haikuwa rahisi hata kuikumbuka hata siku yake ya kuzaliwa maana muda mwingi alikuwa akiutumia kufanya kazi ndogondogo mtaani akisubiri ajira kiufupi maisha hayakuwa sawa kabisa yalikuwa ya dhiki mtindo mmoja...

Wakati wao wakiandaa surprise aliyekuwa akiandaliwa hiyo surprise ndio kwanza wakati huo alikuwa akikabidhi guta alilokuwa akitumia kujiingizia kipato kwa boss wake,alikabidhi akapewa ujira wake kutokana na kazi aliyoifanya kwa siku hiyo,maana alikuwa akilipwa kwa kutwa,sasa alishangaa siku hiyo kulipwa nusu ya mapato yake alipohoji akaambiwa nusu ingine ilikuwa ibaki ili kukarabati guta alilokuwa akitumia,
Hakuwa na jinsi ilibidi tu akubaliane na matokeo alinishauri boss wake akaondoka....
Taratibu alikuwa akitembea kurejea nyumbani moyoni alijiuliza mateso na unyanyasaji huo uliokuwa ukimkumba ungeisha lini kazi ngumu mshahara mdogo,mtaani anadhaurika kuwa kasoma bure kaishia kuuza maji hakika hizo ndio zilikuwa changamoto kubwa kwake...
Aliingiza mkono mfukoni akatoa simu yake,alipotazama saa ilikuwa saa mbili usiku kama na dakika tano hivi alijiona amechelewa aliongeza mwendo akaendelea kukatiza katika vichochoro....

Nyumbani maandalizi yalikuwa tayari familia ilikuwa na furaha tele licha ya hali ya uchumi kutokuwa nzuri tangu Baba mwenye nyumba afukuzwe kazi katika kampuni alikuwa akifanya kazi kutokana na kuongoza wafanyakazi katika kudai haki zao kampuni lilichukua uamuzi wa kumfuta kazi na kumpa haki zake zote ili kuepusha asisambaze sumu iliyokuwa katika moyo wake ya kutetea wafanyakazi wenzake ili wapate haki zao za msingi hivyo alijikuta alifukuzwa kazi akarudi katika kazi yake ya kilimo cha mbogamboga za majani mpaka wakati huu....
Mama alianza kupata hofu akasema mbona kijana wake hakuwa na tabia ya kuchelewa nyumbani hivyo labda huko alipo alikumbwa na matatizo,
Mme akamsihi asiwe na hofu kijana wao angefika tu muda sio mrefu hivyo waendelee tu kumsubiri....

Upande wa pili ni kweli kijana wao Asael hakuwa kabisa na kumbukumbu kuhusu siku yake ya kuzaliwa,aliendelea kutembea ili awahi nyumbani....

Sasa wakati akiwa anatembea katika jengo moja alisikia kama kuna watu walikuwa wakiongea na vishindo vya hapa na pale ilimuwia vigumu kupita hilo eneo tena la mtaani kwake asijue nini hasa kiliendelea wakati huo,,,
Taratibu alijisogeza katika jengo hilo,aliamini wazi alikuwa sahihi kwa alichokusudia kuchunguza wakati huo kwa yeye alisomea masuala ya uwandishi wa habari sasa alitaka kujigeuza naye kama mwandishi halisi wa habari aliyekuwa akipeleleza habari kwa kina!
Rahasha kumbe haikuwa hivyo yeye akitokea katika kazi za guta hakuwa ameajiriwa kwa wakati huo licha ya kuwa kweli alikuwa na ujuzi huo...

Taratibu kabisa alipata upenyo akapenyeza jicho lake la kushoto bado ilionekana hajaridhika,alizidi kupepesa macho kwa harakaharaka aligundua kulikuwepo na makundi mawili ya watu ambayo yalisimamiana wima,alipotazama kwa umakini zaidi kiongozi mmoja wa kundi alimtambua,alikuwa ni Mr chalima mfanyabiashara mkubwa kabisa wa madini aliyejulikana sana hakuelewa kwa harakaharaka nini walikuwa wakikifanya usiku ule...
Baada ya muda gari iliingia mpaka eneo hilo gari ilikuwa imefunikwa turubai juu,Taratibu Mr chalima alisogea katika gari hilo akatoa amri vijana wafungue aone kilichokuwa ndani vijana walifanya hivyo...

Zilikuwa ni pembe za Ndovu aise!!!

Moyo wa Asael ulijawa na hofu sana kwa muda huo,hakuwahi kufikiria kuwa mtu kama mr chalima alikuwa akisifika kwa kutoa misaada katika jamii angesubutu kufanya biashara ya hatari kiasi kile tena wakishirikiana na maafisa wa polisi!!
mr chalima kwa wakati huo alikuwa na furaha sana hakuwa na wasiwasi kwa alitendalo...
ni wazi alikuwa ni mwenyeji na biashara hiyo,
Taratibu mwili ulimsisimka Asael akaitoa simu yake mfukoni aliona ni bora angebaki na ushahidi yeye kama mwandishi wa habari...
Alirekodi tukio hilo kwa simu yake ya mkono wakati mr chalima akikabidhi pesa kwa maafisa wale wa jeshi la polisi...
akajiona mshindi hakuta kuishia hapo alitaka apige na picha!!!

Nyumbani Bado alikuwa akisubiliwa
na familia yake ili waje kusherehekea siku yake ya kuzaliwa
mdogo wao wa mwisho alianza kulilia ile keki mama akaamua kumkatia kidogo..

Huku Asael akafanikiwa kupiga picha mbili za mwanzo,ila tayari alishaonekana mwanga wa simu ulimponza!!!

Akashangaa anaguswa kwa nyuma,akageuka mapema sana akafanikiwa kumtoroka huyo mtu ila aligundua ameshafamika alilaumu kimbelembele chake alijiona tayari ameiongoza familia yake matatani kwa muda wowote yule mtu angeweza kufika nyumbani....
akazunguka upande mwingine kusikia nini kingejili baada ya yeye kuonekana....

Alisikia kabisa mr chalima akitoa amri kwa kujiamini kabisa....
"kama amesikia haina budi sisi kumfunga mdomo asiongee mpaka mwisho,
na njia sahihi zaidi ya yeye kutunza siri ni kufa tu kabla hajafika nyumbani aeleze hili akiwatangulia kufika basi mmalize familia nzima siri izidi kuwa siri"
hii sauti Asael Alijisikia waziwazi kabisa kifo chake na cha familia yake kikipangwa na mr chalima....

Moyoni aliona ni bora awahi nyumbani akaiondoe familia yake mapema kabla wauaji hawajafika....

Wazazi wakiwa wamezubaa zubaa ghafla mwanao alifika akiwa na hofu iliyopitiliza
"baba,mama yatupasa tuondoke eneo hili mara moja wauaji wanakuja muda sio mrefu sitaki mniulize maswali kwa sasa nitawaeleza mbele ya safari"

Aliongea huku jasho likimtoka kama alitokea katika riadha marathon...

fataki zilianza kufyatuka picha yake mbele ndipo akakumbuka ilikuwa siku yake ya kuzaliwa!!

Alijilaumu sana kuwa na kiherehere...
walitoka akawasindikiza yeye akawahaidi kukutana mbele amalizie kuchukua vitu ndani....

Wakati tu anarudi kabla hajafika alishuhudia wauaji wakiingia ndani katika nyumba walipoishi wao....

Huu ni utangulizi tu wa mkasa huu...


Itaendelea hapahapa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom