Simulizi ya Kijasusi: Safari ya Gavin Luca

Simulizi ya Kijasusi: Safari ya Gavin Luca

HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA KUMI NA SITA
SONGA NAYO................

“Kuna kipindi niliwahi kuwaza kwamba kwanini kuna watu wanakufa mapema! Jambo lile liliwahi kuniumiza kichwa kwa muda mrefu ila baadae nilipata jibu moja rahisi la jumla. Watu wanakufa mapema kwa sababu wengi wanastahili kufa, kuna watu wanatakiwa kutokuwepo duniani ili dunia iwe sawa na mambo yaweze kwenda kama ambavyo watu wamejipangia ila baadhi ya watu hao wakiendelea kuwa hai unaweza kuwa mwanzo mbaya wa baadae ya taifa hili” hayo ni maneno ambayo yalitoka kwenye kinywa cha jaji na ndiyo ambayo yalimfanya mwanaume huyo kusita kutoka na kugeuka ili ayasikilize kwa umakini zaidi.
“Hiki ambacho kimetokea hapa ni kazi mheshimiwa, sio mambo personal kama ambavyo unahisi wewe. Mimi nalipwa ili kufanya hii kazi na ndiyo inanitambulisha popote pale hivyo kama unaona nimevuka mipaka kwenye hili naomba unisamehe sana”

“Shilingi imetengenezwa kwa kutofautishwa na pande mbili, upande mmoja unafahamika kama kichwa na upande mwingine unafahamika kama mkia. Ambao waliitengeneza hawakuwa wajinga wala wapuuzi kuzitofautisha hizo pande mbili, zilitofautishwa kwa sababu kuna maana kubwa kuweza kufanya hivyo ila sio watu wote ambao huwa wanalizingatia sana jambo hili, wengi huwa wanahisi kwamba aliye kuja na hilo wazo alipoteza muda tu.
Lakini sio kweli mtu huyu aliwaza mbali sana na siku ambayo wewe utakuja kuelewa utofauti wa hizo pande mbili, ndiyo siku ambayo utakuja kunielewa yale ambayo nimeyazungumza hapa siku ya leo ila huenda muda hautakuwa rafiki kwako zaidi ya kutamani ungeelewa mapema. Nakutakiwa siku njema afisa, unaweza kwenda kwa sababu nahitaji muda wa kupumzika”
Aliambiwa maneno mazito ambayo hayakuwa na maana nzuri kwenye tafsiri, alijua kabisa mheshimiwa alikuwa anamaanisha nini kusema vile ila asingeweza kushindana naye kwa sababu alikuwa ni kigogo na kumgusa hovyo ilikuwa ni hatari kwake yeye na kwa kazi yake kwa ujumla. Alitoka ndani ya hilo eneo akiwa ameimaliza kazi ambayo aliona kabisa hata taarifa ambayo aliipata kwa mtu yule ilikuwa ya uongo ila sio kila mtu angelitambua hilo, wananchi walikuwa wanaenda kuiamini ila sio yeye, alijua kabisa kiongozi huyo alikuwa na mengi nyuma ya pazia ambayo hakuyasema juu ya tukio lile ambalo lilikuwa limetokea. Kwa bahati mbaya hakuwa na huo uwezo wa kumlazimisha.


LUGALO MILITARY BASE.
Moja kati ya maeneo ambayo yanaogopeka na kuheshimika sana ndani ya mipaka ya Tanzania, ni eneo ambalo linamilikiwa na jeshi na ndipo yalipo makao makuu ya jeshi la ulinzi la wananchi ya Tanzania JWTZ. Linapo ishia eneo la jeshi hilo barabara itokayo mwenge kwenda Tegeta kuna daraja kubwa ambalo watu huwa wanalitumia kuvukia kutoka upande mmoja kwenda upande mwingine. Pembezoni mwa daraja hilo ndipo kuna hifadhi ambayo inamilikiwa na jeshi na ukiingia kwenye hifadhi hiyo unakuwa umeingia eneo husika moja kwa moja. Eneo hilo huwa lipo kama hakuna watu mpaka pale ambapo utatia maguu yako ndani ya eneo hilo ndipo unakuja kuelewa sababu ya kwanini watu wengi huwa wanapaogopa sana.

Usiku wa saa saba na dakika zake hamsini na tisa, pembezoni mwa mti mmoja ambao upo karibu na barabara karibia kabisa na ulipo ukuta mfupi wa chuma ambao umeandikwa kwa rangi ya damu ya mzee kwa maandishi makubwa LUGALO MILITARY BASE, kuna mwanaume alikuwa amekaa kwa kuegamia mti huo pembeni yake akiwa na upanga mmoja mkali ambao ulikuwa unaonekana kwa mbali kutokana na jinsi ulivyokuwa mkali.

Bwana huyo alikuwa ameweka bastola moja juu ya paja lake huku nyingine ikiwa kiunoni, kwenye mwili wake alikuwa amevaa nguo zote nyeusi za jeans na buti ambalo lilikuwa linafanana na nguo zake. kwenye uso wake kulikuwa na kofia nyeusi aina ya pama ambayo ilimziba kumfanya asionekane kwa mtu ambaye angekuwa mbali. Hapo alipokuwa ameketi alifanya mwanga kumulika kwa mbali kiasi kwamba mtu angehisi ni wale wadudu watoao mwanga nyakati za usiku wanapokuwa wanaruka ruka hewani lakini kwake ilikuwa ni tofauti na jambo hilo.
Kwenye mkono wake wa kulia alikuwa anaivuta sigara na ndiyo ambayo ilikuwa inatoa mwanga ambao ulikuwa unaonekana, sigara hiyo alikuwa anaivuta kwa msisimko mkubwa kana kwamba kuna jambo la mhimu alikuwa analisubiri eneo hilo kwa nyakati hizo. Hakuwa na wasiwasi kabisa juu ya ujio wake hilo eneo, alionekana kuwa kwenye mahesabu yake na alijua jambo ambalo alikuwa analifanya kwa nyakati zile ndiyo sababu kubwa ambayo ilimpa imani ya mahesabu yake.
Akiwa lile eneo alisikia hatua kwa mbali na mazungumzo ambayo yalitoka kwa watu ambao walioekana kujuana kiundani na vizuri zaidi. Watu hao walionekana kuwa ni zaidi ya watu wawili lakini sauti zile zilipungua zikawa za chini zaidi na ndiyo sehemu ambayo alikuwa anaisubiria kwa hamu zaidi. Utulivu ule ulimpa jibu kwamba wale watu walikuwa wameugundua uwepo wake ndani ya lile eneo hivyo ulikuwa ni muda mwafaka wa kufanikisha jambo ambalo lilimpeleka pale nyakati zile za usiku.

Ni kweli ule mwanga wa sigara yake ndio ambao ulitoa taarifa juu ya uwepo wa mtu eneo lile, ule mshtuko uliwafikia wanajeshi ambao walikuwa zamu kuhakikisha usalama wa eneo hilo. Walikuwa wanaamini hakuna mtu mwingine ambaye alitakiwa kuwepo eneo hilo zaidi yao kitu ambacho walikuwa sahihi kabisa lakini hali ya pale ilionekana kuwa tofauti kidogo hivyo wakahisi huenda alikuwa ni mvuta bangi wa mtaani ambaye walitakiwa kukesha naye na kumnyoosha.
Sababu hiyo ikawafanya wanajeshi wawili tu kujongea kuelekea eneo la tukio, bwana yule alikuwa nyuma ya mti hivyo kwenye tochi ya mwanajeshi mmoja ambayo alikuwa ameimulika, bwana huyo alikuwa anaonekana kwenye mabega yake tu. Licha ya kusikia zile hatua za watu zikielekea ule upande bado hakuwa na shaka wala hofu, aliendelea kuivuta sigara yake kwa utulivu akiwa anauachia moshi hewani kwa mbwembwe nyingi.
Wanajeshi walikuwa wawili, mmoja alipita upande mmoja na mwingine alipita upande mwingine hivyo wakatokezea kwa mbele yake, hakuwa na eneo la kukimbilia ila huenda hawakuwa na uelewa kwamba mtu huyo hakwenda pale kwa bahati mbaya wala hakwenda pale ili kuweza kuwakimbia watu hao ila wasingeweza kulijua hilo kwa haraka namna ile, walihitaji muda jambo ambalo halikuwa rafiki kwao.
“Unajua upo wapi hapa?” aliuliza mwanajeshi mmoja akiwa anammlika na tochi usoni ambayo ilionekana kumkera kwa sababu alifumba macho akizikunja ndita zake.
“Lugalo”
“Unaelewa sheria za hili eneo?”
“Ndiyo, hakuna raia anaruhusiwa kuingia hili eneo vinginevyo atakumbana na adhabu kali”
“Kwahiyo wewe ni kidume mpaka ukata kuja kutuvimbia kwenye eneo letu siyo?”
“Mpo wangapi hili eneo?” alijibu mwanaume huyo kwa sauti nzito zaidi akiwa hana hata wasiwasi lakini swali lake lilionekana kuwa kichekesho. Yule mwanajeshi ambaye alikuwa amemlika ile tochi yake alihisi kama kuna kitu amekiona pembeni ya eneo lile hivyo akalazimika kuweza kuhamisha mwanga ndipo alishangaa kuona upanga ambao ulikuwa unang’aa sana huku kwenye paja la mwanaume yule pakiwa na bastola. Alishtuka na kugundua kwamba bwana huyo hakuwa kibaka wala mvuta bangi bali alikuwa ni muuaji, jambo lile ndilo ambalo lilimfanya atake kupiga kelele kuwashtua wenzao ila muda wa kufanya maamuzi haukuwa rafiki kwake.

Ni wakati ambao alipokea buti zito la goti akakosa balansi na kutaka kuangukia mbele kwani hakutarajia huku akiachia tusi zito kulaani shambulio lile lakini wakati anainama, ule upanga ulishikwa na kuzungushwa ambapo ulipita kwenye shingo yake. Mwenzake alipuliza filimbi aliwa anarusha buti lake ambalo lilidakwa na kwa mbele ule upanga ukasokomezwa kwenye sehemu zake za siri bwana yule akasimama ambapo alirusha ngumi yake ikatua kwenye taya na kuzivunja. Mwanajeshi yule alitamani kuweza kujinasua ndipo ile bastola ilipo tumika, alipigwa risasi mbili kichwani kutoka kwenye bastola ambayo haikufungwa kiwambo cha kuzuia sauti kiasi kwamba ule mlio wa risasi ulisikika mbali na pale na hayo yote mhusika alionekana kuyafanya makusudi kabisa kwa hesabu zake.
Hakujulikana alikuwa ni nani na kulikuwa na sababu zipi mpaka yeye kuvamia ndani ya kambi ya jeshi na kuanza kufanya mauaji ya namna hiyo. Ile filimbi na mlio wa risasi uliwafanya wanajeshi ambao hawakuwa mbali na lile eneo kusogea wakiwa na silaha zao tayari kupambana na hatari yoyote ambayo ingekuwepo ndani ya eneo lile. Walifika pale pakiwa kimya, ni miili ya wenzao tu ambao ilikuwa imetapakaa pale mhusika akiwa hayupo.

Ukurasa wa kumi na sita unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA KUMI NA SABA
SONGA NAYO................

Kumuua mwanajeshi ni kosa kubwa ambalo kusameheka kwake ni labda ufe, walikuwa wanne wanajeshi wale ambao kila mmoja alionekana kufura kwa hasira na kutamani kukutana na mtu ambaye aliyafanya hayo yote. Wakiwa wanaendelea kuangaza kila kona bila kuzungumza jambo, mmoja alihisi kama kuna ujio wa mtu nyuma yake, aligeuka lakini hakuona kitu ndipo akakumbuka kwamba ni kama alipishana na mtu.
Alijigusa kwenye tumbo lake akakutana na damu, upanga ulikuwa umepita kwa nguvu na kulitoboa vibaya tumbo lake ila hilo aliligundua baadae wakati mhusika alisha pishana naye. Alishuka chini taratibu tena kwa utulivu mkubwa kabisa, mwisho wake haukuwa mzuri sana,
Ule mshindo wa kudondoka kwake ndio ambao uliwapa wenzake taarifa ya kwamba hawakuwa salama, muuaji bado alikuwa aneo hilo jambo ambalo lilikuwa ni kweli. Bwana huyo alikuwa amesimama nyuma ya mti mmoja akiwa anawaangalia watu hao walivyokuwa wanahaha kujua alipo. Kwa mbali aliona kuna taa nyingi zinakuja mahali kule na hilo lingekuwa ni tatizo kubwa kwake. Alijitokeza nyuma ya mwanajeshi mmoja ambaye aligeuka na bastola akiachia risasi lakini alipishana na bwana huyo ambaye alizungusha mguu wake ukatua kwenye mbavu za mwanajeshi huyo na alipotaka kudondoka bwana huyo alimpokea na buti la kichwa akajibakiza kwenye jiwe kichwa kikapasuka.

Mwanajeshi mwenzake alimulika kule akihitaji kuwa na uhakika na mtu ambaye anamshambulia lakini haikuwa bahati kwake, alikutana na upanga ambao ulirushwa kwa nguvu na kuitoboa shingo yake kiasi kwamba akapoteza maisha akiwa amesimama. Ni mmoja tu ambaye alikuwa bado amesimama akiwa haelewi mhusika alikuwa wapi, alijaribu kumulika kila sehemu mpaka pale ambapo aligundua kwamba yule muuaji alikuwa nyuma yake, alitaka kugeuka ila kwa bahati mbaya hakupewa hiyo nafasi, alipigwa risasi nne kwenye kichwa chake kukamilisha idadi ya vifo vya wanajeshi sita ndani ya muda mfupi.

Wanajeshi wengi walifika hilo eneo wakiwa na vifaa vingi ambavyo vilikuwa na mwanga wa kutosha kiasi kwamba eneo hilo likawa jeupe tofauti na vile ambavyo lilikuwa mara ya kwanza ambapo maeneo mengi kiza kilikuwa kimetawala kiasi kwamba ilikuwa ni ngumu mtu kuweza kuona tukio ambalo lilikuwa linaendelea kwa sababu hata zile taa za barabarani karibu na eneo hilo zilikuwa zimezima ikionekana wazi kwamba ni mtu alizizima kwa makusudi kabisa kwa sababu alijua kile ambacho alikuwa anahitaji kukifanya ndani ya hilo eneo.
Ilikuwa imesambaa miili ya wanajeshi sita ambao waliuawa kikatili isivyokuwa kawaida na muuaji alionekana kabisa kudhamiria kutekeleza jambo hilo. Miili yao ilikuwa bado ya moto kabisa na damu zilikuwa zinaendelea kuwatoka ikiwa ni ishara kwamba muuaji hakuwa mbali na eneo hilo hivyo ilitolewa amri kwamba atafutwe sehemu yoyote ile ambayo alikuwepo lakini hawakufanikiwa kabisa kumpata.

Jambo la pekee ambalo walilipata na liliwashangaza pakubwa ni vitu ambavyo walivikuta pale, waliikuta shilingi moja ambayo ilikuwa inang’aa sana. Shilingi hiyo iliwakumbusha mbali, hapo zamani iliwahi kuwa utambulisho kwa mwanaume ambaye alipata kuitwa Gavin Luca lakini kwa wakati huo alikuwa ni mfu. Ni asubuhi tu ya siku hiyo ambapo jaji alitoka kuhojiwa akidai kwamba watu ambao walimteka walikuwa wanazitaka taarifa za bwana huyo. Wote walibaki kwenye mshangao mkubwa, iliwezekana vipi bwana huyo kuwa hai? Walipigwa na butwaa.
Lakini wakati huo ambao dunia iliendelea kuwashangaza ndipo wakakutana na jambo lingine la kushangaza zaidi ya lile la mwanzo, karatasi ngumu nyeupe ambayo iliandikwa kwa kutumia damu “GAVIN LucA”.

Wanajeshi sita walikuwa wameuliwa ndani ya military base ya Lugalo, lisingekuwa jambo ambalo lingefanya mambo kuisha kirahisi namna hiyo, ilikuwa ni lazima yawepo malipo kwa wahusika ambao walifanya jambo hilo. Ilikuwa ni aibu kubwa kambi kuu ya jeshi la wananchi kuvamiwa, wanajeshi kuuliwa na kisha muuaji asipatikane, ni jambo ambalo lilikuwa gumu isivyokuwa kawaida.
Taarifa ile ilifika makao makuu kabisa usiku ule ule, jambo ambalo lilifanya viongozi wa ngazi za juu kuweza kupaniki na kujiuliza hilo jambo liliwezekanaje? Hawakuwa na jibu kwa wakati huo. Wanajeshi walisambazwa kila kona, wanajeshi waliifunga mitaa kuanzia Makumbusho mpaka Tegeta, hakuna gari ambayo iliruhusiwa kuondoka wakati huo na hata wale vijana ambao walikuwa kwenye makundi ambayo hayakuwa yakieleweka waliwekwa kwenye kikaango huku wakila adhabu kali.

Waliamini kwamba ilikuwa ni lazima wampate mhusika wa hilo tukio kwani bila hivyo isingekuwa ishara nzuri kwao na ilikuwa ni aibu jeshi kudhalilishwa namna hiyo. Hilo tatizo ambalo liliwapata ndilo ambalo lilifanya taarifa zifike kwa bosi wa watu hao, mkuu wa majeshi ambaye alikuwa ni mwanamama mwenye roho ngumu na kwa wale ambao hawakuwa mashabiki wakubwa wa kufanya kazi kwa bidii walidai mwanamama huyo alikuwa na roho mbaya. Elizabeth Danzek Thorne, mwanamama huyu ndiye alikuwa mkuu wa majeshi wa kwanza mwanamke ndani ya Tanzania.

Nafasi hiyo hakuipata kwa bahati mbaya bali kwa kazi kubwa tukuka ambayo alikuwa ameifanya kweye safari yake ambayo alikuwa ameitumikia kwenye jeshi. Mwanamama huyo alikuwa ni shupavu, jasiri na asiye muogopa binadamu yeyote yule, ile misimamo yake mikali ndiyo ilikuwa sababu ya wanajeshi wengi kumuogopa Meja Jenerali Elizabeth Thorne.
Wakati tukio la base ya Lugalo kuvamiwa, mwanamama huyo alikuwa juu ya kiuno cha kijana mmoja ambaye aliipata hiyo bahati akiwa anashusha miguno ya raha, mwanamke huyo hakuwa na mume kutokana na historia mbaya ambayo iliwahi kumpata huko nyuma hivyo alitafuta kijana mmoja ambaye alimuamini kwa ajili ya kumalizia shida zake. ilikuwa akiwa na mawazo anamuita kijana huyo ambaye alikuwa anapewa kila kitu na jambo hilo lilikuwa ni siri kubwa sana kati ya wenyewe wawili na walinzi wake kadhaa ambao ndio walikuwa wakienda kumfuata kijana huyo.

Hakuwa gwiji tu kwenye kazi yake bali alijua kukitumia vyema kiuno chake, mapenzi ni sanaa ili muyafaidi wote mnatakiwa kuwa wasanii, alilijua hilo. Mwanamama huyo alikuwa makini kwenye hiyo sekta kwa sababu hakutaka kumpoteza kijana huyo kirahisi, alihitaji kijana huyo alijihisi kufika kwake. Alikuwa anagugumia kwa raha mpaka pale ambapo alianza kutoa machozi akiwa anaelekea kufika kileleni ndipo alishtushwa na simu binafsi, hiyo ni simu ambayo ilikuwa inapigwa kukiwa na dharura tu pekee.
Aliruka kutoka kwenye kiuno cha yule kijana ambaye alikuwa amekolea hivyo akaishia kutoa lawama na kuibeba simu yake kwenda bafuni akiwa uchi bila nguo hata moja kwenye mwili wake kisha akaipokea simu yake. Ujumbe ambao aliupokea kwenye simu yake ndio ambao ulimfanya atoke bafuni akiwa amebadilika sura yake, alimtaka kijana huyo aondoke haraka sana kuna mtu angemsindikiza, alikuwa anamjua mwanamama huyo akibadilika hivyo lazima kunakuwa kuna shida mahali hivyo hakutaka kabisa kukosana naye akaondoka kimya kimya.

Mwanamama huyo alivaa haraka na kuondoka nyumbani kwake kuwahi Lugalo ambapo alikuwa na msafara wenye ulinzi mkali. Alitumia muda mfupi kufika kwa sababu barabara ilikuwa nyeupe kabisa kutokana na kwamba ilifungwa, hakuna magari ya raia ama binafsi ambayo yalikuwa yanaruhusiwa kupita. Alifika hapo na kupokelewa na wasaidizi wake ambao walimpeleka moja kwa moja mpaka eneo husika la tukio na kile ambacho alikiona hata yeye hakuweza kabisa kuamini kama kilikuwa ni kweli.
Wanajeshi wake waliuawa kama mbwa, walidhalilishwa vibaya tena ndani ya kambi yao na mtu wasiye mfahamu kwamba alikuwa ni nani na kulikuwa na sababu ipi hasa ya yeye kuweza kuingia ndani ya eneo hilo.
“Mmempata mhusika?”
“Hapana mkuu, tumefika hapa wakati hayupo, tumezunguka maeneo yote na tayari wanajeshi wamejaa kila sehemu kama ambavyo ulitoa maelekezo kwenye simu lakini bado hakuna dalili za mtu huyu kuwepo hapa”
“Haya maeneo kuna kamera za siri?”

Ukurasa wa kumi na saba.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA KUMI NA NANE
SONGA NAYO................


“Kamera ambazo zilikuwepo ni za barabarani pale ambazo zimeunganishwa na taa lakini taa zote zilizima ikiwa na maana kwamba mhusika alikuwa anajua jambo ambalo alikuwa analifanya na alitambua ni namna gani anaweza kuingia na kutoka bila kujulikana”
“Umewasiliana na familia za mashujaa wetu?”
“Hapana kiongozi, tunasubiri kwanza kukuche ndipo tutoe taarifa”
“Nahitaji huyu mtu au hawa watu wapatikane haraka, haiwezekani mtu anakuja ndani ya kambi ya jeshi na kufanya huu ujinga halafu anategemea kwamba ataondoka kirahisi na kwenda kutudhihaki huko atakakokuwa na wenzake. Hii ni aibu kwangu lakini huyu nataka awe mfano wa haya yote ambayo yametokea”

“Sitalala mkuu mpaka nihakikishe huyu mtu anapatikana hapa”
“Isifike asubuhi, tuma vijana kila kona, kila mtaa, kama kuna mtu hawamuelewi wahakikishe anasema yeye ni nani na usiku wa leo alikuwa wapi. Kama kuna wahusika ambao watakuwa na mashaka zaidi hao nitawahitaji mimi hapa kuwahoji mwenyewe” mwanamama huyo aliongea kwa jazba mno, ilikuwa ni aibu kwake kukutana na hali kama hiyo kwenye utawala wake kwa sababu ilikuwa inaenda kuonyesha kwamba ni kwa namna gani jeshi ni dhaifu, yaani mtu aingie Lugalo, afanye jambo ambalo analitaka na kuondoka kwa namna ambayo anaitaka yeye? Kwake aliona jambo hilo halikuwa likiwezekana kabisa, ilikuwa ni lazima mhusika apatikane kwa gharama yoyote ile.

Akiwa anasonya ndipo aliona kuna karatasi inaletwa na sarafu moja ambayo ilikuwa inang’aa, akiwa kwenye hiyo taharuki ya kuweza kuangalia vizuri alisita kwanza baada ya simu yake kuanza kuita kwa fujo. Aliitoa simu yake na kuiangalia kwa muda kabla ya kuiweka kwenye sikio lake, simu ilikuwa inatoka kwa mkubwa wa nchi.

“Sawa mkuu nakuja” alitoa jibu moja tu kwa simu ambayo ilitoka upande wa pili, hakuonekana kufurahishwa nayo kwa sababu kuitwa na raisi ilikuwa na maana kwamba alikuwa na taarifa na yale ambayo yalikuwa yametokea na alijua kabisa kwamba mtu huyo lazima angedai majibu ya matukio yote ambayo yalikuwa yamefanyika. Sasa alikuwa anaenda kumwambia nini raisi tukio kama hilo kutokea kwenye mkono wake? Aliogopa kwamba unaweza kuwa mwisho wake wa kuwa kwenye hiyo nafasi, raisi hakuwa na utani kabisa kwenye jambo ambalo linabeba usalama wa taifa zima na raia wake.
Alihema akiwa na hofu usoni, hofu ambayo iligubikwa na hasira ndipo akashtuliwa na sauti ya msaidizi wake ambaye ndiye alikuwa ameshikilia kile kimfuko ambacho kilikuwa na vile vitu ambavyo aliviona kabla ya kupokea simu ya raisi.
“Hiki ni nini?”
“Hatumjui mhusika lakini hivi ndivyo vitu ambavyo tumevipata kwenye tukio na ni alama za muuaji” alishtuka kusikia jambo hilo, muuaji anaua halafu anaacha alama za kubaki kwake ndani ya eneo hilo? Haikumuingia akilini ila ikamlazimu kuzitazama kwanza ndipo mambo mengine yangefuatia.

Alipata mshtuko wa wazi kwenye uso wake baada ya kuufungua ule mzigo kiasi kwamba ilimlazimu kurudi nyuma hatua moja. Ni baada ya kuiona ile shilingi pamoja na lile jina ambalo liliandikwa kwa damu “Gavin Luca”, mwanamama huyo hakuwa mgeni wa hayo mambo, hiyo shilingi alikuwa anaifahamu vizuri na alikuwa akimjua mhusika lakini pia alipo liona lile jina pale alipata hofu ambayo ilikuwa wazi kwenye uso wake. Aliogopa kwa wakati mmoja Elizabeth.
“No, no, no hili haliwezekani. Huyu mtu amekufa kwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita, hata familia yake imesahaulika kwa sasa japo ndiyo familia ambayo ipo namba moja kwenye kumbukumbu za matukio ya kutisha ndani ya taifa hili”
“Hilo ni jambo ambalo hata sisi limetushtua mkuu kwa sababu tunajua ni mfu, sasa inawezekana vipi mtu huyu atokee tena? Muuaji anaua aina ya mauaji yale yale ya Gavin kipindi kile akiwa hai hivyo moja kwa moja ni yeye”
“Mhhhhh, sidhani kama hii ni kweli, kwa kipindi kile alikuwa anaelekea miaka arobaini, mpaka sasa atakuwa na sitini au sitini kasoro. Kwa miaka hiyo ni ngumu kufanya matukio kama haya na hata kama angekuwa amefanya sidhani kama angekuwa na hiyo nguvu ya kuweza kukimbia haraka namna hii kiasi kwamba tusijue kaingia wapi”

“Kwahiyo unahisi ni nani mkuu ambaye kafanya haya? Moja kwa moja shilingi inamdondokea yeye, nina uhakika hakuna mtu mwingine ambaye angekuwa na uwezo wa kuyafanya haya zaidi yake” Elizabeth alimsikilza vyema msaidizi wake lakini ni jambo ambalo halikuonekana kuiteka akili yake, hata yeye alikuwa kachanganyikiwa kwani kila ambalo lilikuwa linatokea hapo lilikuwa kama ndoto ambayo muda wowote ingeisha na mambo mengine yakaendelea.
“Fanya upelelezi mkubwa mpaka huyu mtu apatikane hapo tutajua kwamba ni nani huyu ambaye anayafanya haya, haiwezekani mfu aje kuua watu duniani tena kwa mara nyingine na kwanini ipite miaka yote hii ndipo haya mambo yaanze kurudi tena? Naenda kukutana na mheshimiwa raisi muda huu, nina imani mpaka namaliza naye kikao utakuwa na majibu ya kuweza kunipa” aliondoka baada ya kutoa maagizo, safari yake ilikuwa ni kuelekea Ikulu kwa ajili ya kukutana na bosi wa nchi ambaye alikuwa anamhitaji kwa ajili ya kulitolea taarifa vyema tukio hilo.


***********
Ndani ya jumba jeupe, mheshimiwa raisi alikuwa amekaa kando ya bwawa moja la kutengeneza. Bwana hilo lilitengenezwa kwa sababu alikuwa anapenda kukaa akiwa na mawazo yake anaenda kuvua samaki eneo hilo kwa sababu isingewezekana raisi kupelekwa sehemu nyingine kwa ajili ya usalama wake kwahiyo ikaamuliwa litengenezwe bwana hilo kwa ajili yake.

Ilikuwa inaelekea saa kumi ya alfajiri, mheshimiwa hakuwa na usingizi kabisa, alikuwa eneo hilo akiwa anaendelea kuvua huku kila kona kukiwa na ulinzi mkali. Alijua kabisa kwamba wakati kama huo kupata samaki lilikuwa ni zoezi gumu lakini alipenda kufanya jambo hilo, eneo hilo lilikuwa limetengenezewa mifumo bora ya umeme hivyo kulikuwa na mwanga wa kutosha hata kama mtu angekuwa mbali eneo ambalo linaonekana vizuri basi angefanikiwa kuona mandhari hiyo ya kuvutia.

Alikuwa hapo akiwa anamsubiri mkuu wa majeshi aweze kufika wafanye maongezi, taarifa ambazo alizipokea hazikuwa njema kabisa kwa upande wake, ilionekana kuwepo kwa tatizo mahali hususani kwenye hiyo base kubwa zaidi ya jeshi. Mkuu wa majeshi aliingia Ikulu usiku huo akiwa ana wasiwasi kwa sababu hakujua mwafaka hasa wa jambo hilo ambalo lilikuwa limetokea na hakuwa na majibu ya moja kwa moja ya kuweza kumpatia raisi jambo ambalo aliona kwamba ilikuwa ni hasara kwa upande wake yeye.
Alikuwa ndani ya kombati ambayo ilimpendeza na buti safi jeusi ambalo lilikuwa linang’aa kwenye mwanga. Walinzi wake walibakia yeye akachukuliwa na kitengo maalumu cha ulinzi wa raisi kwa ajili ya kwenda kukutana na bosi wake. Alihema baada ya kuona mheshimiwa amekaa karibu na lile bwawa lake la kutengenezwa akiwa anaendelea kuhangika na ndoano yake.

“Heshima yako kiongozi”
“Haya maisha ya uvuvi yananikumbusha mbali, nimezaliwa kwenye familia ambayo baba yangu alikuwa anawategemea samaki ili tuweze kuishi. Ni maisha ambayo sikuwahi kuyapenda kwa sababu nilitamani kuishi kama wenzengu ambao baba zao walikuwa wamefanikiwa tayari kwenye maisha lakini ni maisha ambayo yamenipa somo kubwa namna ya kuishi sehemu yoyote ile na kuyamudu mazingira.
Niliwahi kumlaumu baba yangu kwamba ni kwanini yeye hakufanikiwa kama wenzake ila kadri umri ulivyokuwa unazidi kwenda niligundua kwamba nilikuwa namkosea sana baba yangu kuweza kumlaumu. Haya maisha fomula ya kuweza kufanikiwa ni ngumu mno na kuna wakati haiwafai watu wenye roho safi, ukiwa na ile roho ya kutaka kupendwa na kusifiwa na kila mtu kwamba wewe ni mwema basi mafanikio inaweza kuwa hadithi ya kufikirika kwako.
Ukurasa wa kumi na nane unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA KUMI NA TISA
SONGA NAYO................

Mafanikio kwa asilimia kubwa yanawataka watu ambao wamejikana, watu ambao wao wanaamini kwamba duniani hakuna kuonekana huruma, mtu wa kukuonea wewe huruma ni yule ambaye alikuumba pekee, wengine tunatakiwa tuishi kwa kila mtu kuangalia namna bora ya kuweza kuwa hai na maisha yake kwenda. Baba yangu alikuwa mtu mwema kupitiliza, hata kama angepata kidogo basi angehakikisha kwamba kila mtu anapata kikubwa tu awe na uhitaji, hakuelewa kwamba kuna wakati ili ufanikiwe lazima uonekane una roho mbaya na kuwa mchoyo.

Baba yangu aliamini maisha ya umoja na kugawana na wengine hata kile kidogo ambacho unakipata akasahau kwamba wanadamu hawana kumbukumbu hivyo aliishia kusifiwa huku familia ikiwa haina mwelekeo sahihi. Simlaumu kwa sababu yeye aliamua kutanguliza utu kwanza mengine aliamini yangekuja yenyewe, nimekuja kumuelewa baada ya kuwa na kila kitu kwenye maisha yangu ndipo nikagundua kwamba kuna muda mafanikio yako yanaweza kukufanya wewe ukawa mtumwa. Kuna wakati ukiwa hauna kabisa unatamani kuwa pale juu ukihisi ukiwa pale wewe ndiye unakuwa binadamu mwenye furaha sana duniani, unakuwa unaamini kwamba kila jambo linawezekana ila jambo la kushangaza ni kwamba mafanikio yako yanaweza kukufanya ukawa mtu mwenye mawazo zaidi duniani na ukakosa hata watu wa kuwa nao karibu kwa sababu wengi watakuwa wanakuogopa na wale wachache ambao wataamua kusimama kwako ni kwa sababu kuna kitu wanakipata.

Yale maisha ndiyo huwa yanafanya namkumbuka baba yangu kwa sababu yeye kuwa na pesa nyingi halafu hana msaada aliona kama sio sawa. Huenda hakuwa sahihi kwa sababu maisha ya sasa yanakutaka uwe na pesa kwa namna yoyote ile lakini kwa zama zake alikuwa sahihi. Ile zawadi ya uvuvi nadhani ndiyo zawadi bora mimi kuwahi kuipata kuliko hata hii nafasi ya kuwa raisi.
Hiyo ndiyo sababu huwa inanifanya nisipokuwa sawa nakuja hapa kukaa na kuvua nikiwa nawasubiri raia waamke asubuhi ili waende kulaumu kwenye mitandao ya kijamii na wengine kwa sababu ya mawazo na njaa zao kuanza kutukana viongozi bila sababu za msingi. Huenda unaweza ukawa haujanielewa sababu ya mimi kukwambia haya yote meja” raisi aliongea na kutoa historia fupi ya maisha yake huku akiwa anaikunja ndoano yake na kumkabidhi mlinzi wake mmoja kisha akamtaka meja Elizebeth kumfuata watembee tembee kidogo.

“Sababu ya mimi kukwambia haya yote ni kutaka kukupa picha nzima ya uongozi na namna uongozi ulivyo na vile ambavyo unatakiwa kuwa. Kuwa kiongozi sehemu yoyote ile ni kazi ngumu kwa sababu watu wote wanayaweka maisha yao rehani wakiamini wewe utayalinda, sasa kwenye kuyalinda maisha yao kuna wale ambao wanakuwa makini kukupa msaada wa kuyalinda na kuna wale ambao hata maisha yao hawayajali kabisa bali huwa wanaamini raisi lazima utoke Ikulu ukawalinde hata kama wanafanya upuuzi na baada ya hapo wanakuja kukutukana hadharani kwamba hauwajali.

Uongozi ni jukumu gumu kwa sababu kuna aina mbili za watu ambao wanapatikana kwenye hilo neno; kuna wale ambao wanashika nguvu ya kuendesha lakini kuna wale ambao wanaongoza watu kwa kuwahamasisha na kuwavutia kwa namna bora kuhakikisha wanaamini kwenye sera zao na maono yao bila kutumia nguvu kuwalazimisha watu wapi pa kuamini na wapi pa kukosoa.
Baba yangu alikuwa kiongozi bora wa familia ndiyo maana hakuwa na utajiri mkubwa lakini alitoa elimu kubwa ambayo imenifanya mimi leo kuwa raisi wa taifa hili. Hivyo ndivyo uongozi unakutaka uwe, ile alama ambayo utaiacha siku ambayo utakuwa haupo ndiyo itakutafsiri kama ulikuwa unawalazimisha watu kuamini kwenye maono yako au wao walihamasika na wewe.
Hili linakuja kwetu mimi na wewe, mimi ni raisi lakini wewe ni miongoni mwa watu wa ngazi za juu zaidi kwenye taifa hili hususani kwenye kuhakikisha mipaka ya taifa hili ipo salama kwa namna na kwa gharama yoyote ile. Mimi natuliza kichwa kufanya maamuzi yaliyo bora kwa ajili yenu wote lakini wewe ni moja ya watu ambao wanatakiwa kuyatekeleza mawazo yangu ambayo nikiyatoa yanageuka kuwa sheria.

Mimi na wewe tukiwa kama viongozi tunaubeba msalama wa jambo lolote ambalo linatokea, kesho watu wakipata habari jambo la kwanza itakuja sura ya raisi kwao, unajua ni kwanini? Kwa sababu wataamini mkuu wa majeshi amefeli kazi yake ndiyo lakini nani alimuweka pale? Jibu ni mimi hapa, hivyo hata mimi naingia kwenye doa la jambo ambalo ulitakiwa uwepo wewe na vijana wako. Ndiyo maana nimekwambia uongozi ni jambo gumu sana kwa sababu huwa wanapata madhara na ambao hawakupaswa kuyapata lakini watafanya nini? Unaweza ukanipa ripoti ya jambo ambalo limetokea huko kabla ya hiyo asubuhi muda mfupi kuanzia sasa jina langu kuanza kusambazwa vibaya kwenye mitandao ya kijamii?”

Maelezo yote ambayo alikuwa anapewa mkuu wa majeshi na raisi yalikuwa yanamhusu yeye na alilielewa hilo, tatizo ambalo lilitokea lilikuwa kwenye mkono wake lakini lingewaharibia wote wawili kwa pamoja. Raisi kumuita hapo alikuwa na maana yake kubwa ya kupewa taarifa juu ya hatua madhubuti ambazo zilikuwa zimechukuliwa mpaka wakati huo.
“Kwanza naomba unisamehe kwa kutokukupatia taarifa ya kwanza mimi kiongozi, nimepatiwa taarifa hivyo nikahitaji kwenda eneo la tukio niwe na taarifa kamili ndipo nikupigie ila kwa bahati mbaya nikiwa ndio kwanza nafika pale ndipo ukapiga simu”
“Achana na hayo mambo nahitaji ripoti la jambo hilo haraka muda huu”
“Ni kweli wamekufa wanajeshi sita, wote wamauawa na mtu mmoja tena kwa kuuawa kikatili kisha mtu huyo akaondoka bila kufahamika”
“Ni ndani ya eneo la jeshi?”
“Ndiyo”
“Unajua kama ile ndiyo military base kubwa zaidi Tanzania na ndipo yalipo makao makuu ya jeshi la nchi?”
“Ndiyo kiongozi”
“Sasa inawezekana vipi mtu aingie lile eneo na kutoka bila kukamatwa?”
“Hilo ni jambo ambalo nalifanyia kazi mpaka muda huu kuhakikisha anapatikana kwa namna yoyote ile”
“Unajua kwamba jambo hili linaenda kutuvua nguo”
“Hilo nalielewa ndiyo maana nafanya kila namna kumpata”
“Unajua ni nani ambaye kahusika?”
“Hapana ila kuna ushahidi ambao tumeupata”
“Upi huo?” mwanamama huyo aliutoa ule ushahidi na kumpatia raisi ambaye alishtuka na kusimama, hata ule uwezo wa kuendelea na ile safari ya kutembea hakuwa nao tena. Alisogea kwenye kiti ambacho kilikuwa pembeni ya mti mdogo akaketi huku naye mkuu wa majeshi akisogea karibu na bosi wake lakini yeye alikuwa amesimama.
“Kivipi awe yeye?”
“Hata mimi ni swali ambalo mpaka sasa ndilo linanimiza kichwa sielewei imekuwaje ikawa hivi’’
“Mmevipata wapi hivi vitu?’’
“Ni vya muuaji na tumevipata eneo la tukio ambapo ameviacha baada ya kufanikisha kuwaua wanajeshi wangu”
“No way Gavin yupo hai. Huyu amekufa muda mrefu na kila mtu analijua hilo”
“Umeongea na jaji wa mahakama kuu kiongozi?”
“Hapana nimepanga kuongea naye kesho”
“Nina uhakika umeyasikia maelezo yake muda ule, anadai watu ambao walimteka wamemhakikishia kwamba Gavin yupo hai hivyo inawezekana ni kweli. Ni ngumu kwa mtu wa kawaida kuingia ndani ya lile eneo la jeshi halafu akaua watu na kutoweka kwa muda mfupi namna ile, tukio kama hili linamhitaji mtu mwenye uwezo mkubwa ambao umevuka uwezo wa wanadamu wa kawaida”
“How and why?”
“Hayo maswali majibu yake hata mimi kwa sasa sina, kuna haja ya kuanza na moja kuyachunguza maisha ya mtu yule na familia yake kwa ujumla”
Ukurasa wa kumi na tisa.

FEBIANI BABUYA.
 

Attachments

  • downloadfile-105.jpg
    downloadfile-105.jpg
    80.9 KB · Views: 33
Hapo patamu kiongozi.ila nina ombi moja tu kwako nayo ni kujitahidi ili mwendelezo uache kukawia kwa mda mrefu
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA ISHIRINI
SONGA NAYO................

“Familia yake unajua ilipo?”
“Hakuna mtu hata mmoja ambaye anajua ipo wapi”
“Sasa hata tukisema ni yeye, huoni kama kwa sasa umri utakuwa umekwenda sana? Na kwanini asubiri ipite miaka mingi namna hii ndipo aweze kurudi? Hili jambo linanipa ukakasi kwa sababu ni muda mfupi mahakama imevamiwa na watu kuuawa lakini wakati huo huo jaji akatekwa na kupotea. Baadae anarudi kwenye mazingira ya kutatanisha na wakati huo huo yule mwandishi wa habari Jabari naye anadaiwa kuua watu na kupotea. Taifa halijakaa sawa kuna mauaji yamefanyika ndani ya treni, wakati ambao natuliza kichwa kuweza kuyamaliza yote haya napata taarifa ya kambi ya jeshi kuvamiwa!

Tena mvamiaji anadaiwa kuwa Gavin mtu ambaye amebakia kwenye vitabu tu vya historia ya taifa hili? Hapana kuna jambo halipo sawa hapa” raisi alikuwa anakaa na kunyanyuka akionekana kabisa kuvurugwa. Alihisi kwamba kuna sehemu hesabu ilikuwa inafeli, sasa ilikuwa ni wapi? Hakuwa na jibu sahihi kwa wakati huo, alihisi moto unawaka ndani ya moyo wake ambao ulikuwa unaenda kwa kasi kubwa bila yeye mwenyewe kuweza kupenda.
“Unahisi kwamba kutakuwa na kitu gani mheshimiwa?”
“Nadhani huyi sio yeye”
“Aina ya mauaji ni yale yale, alama zake ni zile zile ambazo zimeandikwa kwenye vitabu vya historia ya taifa hili, kwanini unahisi sio yeye?”
“Kipindi yule bwana analipelekesha hili taifa kwa namna ambayo alikuwa anaona yeye nilikuwepo sema nilikuwa mtu wa pembeni sana hivyo hakuna mtu ambaye angeweza kunizingatia kwa namna yoyote ile. Lakini mimi niliwahi kuwa miongoni mwa watu ambao waliwahi kumfuatilia yule bwana kiundani kupita kiasi.
Kumfuatilia kwake nilikuwa natamani kujua siri ya yeye kuwa na usongo wa kuua watu kikatili namna ile lakini mpaka namaliza utafiti wangu mpaka mwisho niligundua jambo moja kubwa. Gavin hakuwahi kumuua mtu ambaye hana hatia hata siku moja, yaani kwenye mauaji yote yale ambayo aliwahi kuyafanya, hakuna hata mmoja ambaye alionewa. Ni ngumu kusema hili kama raisi lakini ndio ukweli, watu wale walikuwa wanalipa kwa yale ambayo waliyafanya kabla hivyo haikuwa kwa bahati mbaya.

Sasa nikiunganisha zile doti na kipindi hiki hata kama angekuwa ni yeye jambo ambalo kwangu naona haliwezekani kwa sababu amekufa lakini kulitakiwa kuwepo na sababu ya yeye kuua wanajeshi hawa. Sasa kuna tatizo lolote baina yake na jeshi tena wanajeshi ambao hata hawafahamu walikuwa kwenye ulinzi? Jibu ni hapana. Ni miaka zaidi ya ishirini imepita kwa sasa na hakuna hata kiashiria cha uwepo japo wa familia yake hivyo kusema yule alikuwa ni yeye hapana sio kweli.

Hakuna sehemu jeshi limemkosea tangu amuue mkuu wa majeshi Medrick Savato ambaye alikuwa ni mmoja wa watangulizi wako. Kwa maana hiyo kama jeshi halijaikosea hiyo familia, basi kusingekuwa na sababu ya wao kufanya hayo yote. Kwahiyo naweza kukuthibitishia kwamba huyu sio yeye bali kuna mtu anayafanya haya kwa mgongo wake kwa sababu kubwa mbili. Sababu ya kwanza anataka kutengeneza ugomvi mkubwa baina ya serikali na hii familia huku yeye akinufaika katikati lakini sababu ya pili anataka kuiibua hiyo familia kokote kule ilipo na hapo atakuwa ameshinda hii mechi kirahisi”

“Mheshimiwa, mbona kama umefika mbali kuwaza kuhusu hili?”
“Ni kwa sababu wewe mwenyewe umeniuliza kuhusu maelezo ya jaji, anadai watu ambao walimteka wanaitaka hiyo familia na Gavin mwenyewe. Kwa kuunganisha haya matukio wewe huoni kabisa kwamba watu hawa wanaweza kuwa sehemu ya haya mambo kutokea huku wao wakiwa pembeni kutuachia sisi kuifanya kazi hii kwa kuua watu wetu na kuanza kuitafuta hiyo familia?”
“Na vipi kama hautakuwa sahihi kwa hili kiongozi?”
“Basi mimi mwenyewe nitaongoza hii oparesheni ya kuwatafuta hawa watu na familia nzima kwa ujumla na nikiwapata nitafanya maamuzi magumu ambayo yataishtua dunia. Sitaki yale makosa ya miaka ile yaje kurudi kwenye taifa langu, kwa sababu yatasababisha damu ya watu wasiokuwa na hatia kumwagika bila sababu za msingi na mimi sipo tayari kuona jambo kama hilo linatokea, kwa gharama yoyote ile sitoruhusu yajirudie kwa mara nyingine, hili naapa kwa nafsi yangu”

“Kwa sasa natakiwa kufanya jambo gani?”
“Mhusika atafutwe kwa gharama yoyote kwa sababu atakuwa na majibu sahihi lakini kuna pande zingine ambazo zinatakiwa kuangaliwa. Upande wa kwanza tunamhitaji yule mwandishi wa habari akiwa hai kwa sababu anaweza kuwa ana mengi ambayo anayafahamu na yatakuwa msaada mkubwa kwa hapo baadae. Lakini upande mwingine tusikae tu kuhangaika na hii familia, pia hawa watu wengine wanatakiwa kutafutwa na kulipa kwa yale ambayo yameyafanya mahakamani na wanaonekana kwamba wanaenda kuwa sababu ya taifa hili kupoteza amani jambo ambalo pia sipo tayari kuona linatokea mbele ya uso wangu”

“Mambo yatakuwa ni mengi kwa wakati mmoja mheshimiwa”
“Hilo nalijua, ndiyo maana vyombo vya usalama vyote naenda kuvituma mtaani ila tunawahitaji TIGI. Ni kwa muda sasa hawajafanya shughuli ya hatari tangu kumpoteza mkurugenzi wao na wale majasusi wao”
“Kwa hilo sitokupinga mheshimiwa kikubwa tu hawa watu wasije wakaingia kwenye njia yangu wakati naifanya kazi yangu”
“Wote wanakufahamu vizuri kuanzia IGP, DcI mpaka mkurugenzi wa hilo shirika hivyo hakuna ambaye anaweza kuja kwenye njia yako”
“Shukrani kwa kulielewa hilo lakini nadhani kuna watu ambao tunawahitaji sana kwa sasa”
“Wapi hao?”
“wakati kundi lile la majasusi sita likisambaratika inadaiwa kwamba kuna majasusi kama wawili walifanikiwa kuishi kwa wakati ule hivyo hawa nitawahitaji mheshimiwa kuonana nao. Kuna sehemu ya kuanzia kupitia kuonana nao”
“Unamaanisha unataka kuonana nao ana kwa ana?”
“Ndiyo”
“Sasa hili halipo kwangu, wasiliana na mkurugenzi wao ndiye anaweza kujua kwamba kwa sasa wako wapi kwa sababu ni miaka mingi imepita na hakujawahi kuwa na taarifa zao zozote mpaka leo”
“Sawa mheshimiwa”

“Kwa sasa unaweza kwenda, mimi nangoja kupambazuke nikutane na jaji, haya mambo yanaonekana kuwa mabaya tofauti na nilivyokua nayaona kwa mara ya kwanza” mwanamama huyo hakuongea jambo lingine zaidi ya kupiga saluti na kutoweka eneo hilo kwenda kuyatekeleza majukumu yake. Lakini alisisitiza anahitaji kuonana na wale majasusi wawili wa THE INVISIBLE ambao walifanikiwa kuishi wakati ule kati ya wale sita ambao walikuwa ndiyo msingi mkuu wa shrika la kijasusi la TIGI.
Majasusi wale hawakueleweka kwamba mpaka wakati ule walikuwa wapi hivyo alitakiwa kukutana na mkurugenzi wa wakati huo kuweza kumuomba taarifa za watu hao kama wapo aweze kukutana nao, hao waliyaishi yale maisha ya Gavin na walikuwa wahanga wakubwa wa lile tukio hivyo aliamini kwamba kupitia wao kuna sehemu kubwa ya kuanzia kazi yake angeipata hususani kumtafuta mtu ambaye kwa maelezo ya raisi alidai hakuwa yeye hivyo kuna watu wengine ambao waliingilia huo mchezo katikati na walitakiwa kupatikana haraka iwezekanavyo.



*********
Kulikuwa na sababu za msingi za jaji kuweza kudanganya kuhusu kifo cha Jopa, yeye na mwanaume huyo kuna makubaliano ambayo waliyafanya, makubaliano ambayo yalipaswa kuwa siri yao wenyewe kwa sababu hakuna mtu mwingine yeyote ambaye alikuwa anatakiwa kuyafahamu. Yeye alikuwa ni miongoni mwa masalia ya watu wa siri ambao dunia iliwasahau, mtu ambaye dunia ilimuona kuwa kiongozi wa kawaida kama ambavyo walikuwa wengine waliokuwa wamepita lakini haikuwa hivyo.

Ukurasa wa ishirini unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA ISHIRINI NA MOJA
SONGA NAYO................

Bwana huyo alikuwa na mengi kwneye moyo wake ambayo aliyajua na wengi hawakuwa na ufahamu nayo lakini kwake hilo halikutosha, alihitaji kuzipata zile pesa za ile familia ambayo ilidaiwa kuwa ndiyo familia tajiri zaidi ndani ya bara zima la Afrika huku akiwa hajui atawapatia wapi. Alitumia zaidi ya miaka ipatayo ishirini kuhakikisha anawapata watu hao lakini lilionekana kuwa zoezi gumu kwa upande wake, akiwa anaendelea na zoezi lake hilo ndipo alipopata ugeni huo wa ghafla.

Watu hao walikuwa na taarifa zake yeye na waliamini kupitia yeye kuna mambo mengi wangeyafahamu kuhusu watu hao hivyo walimpa nafasi ya maisha yeye na familia yake lakini alitakiwa kuwafanyia watu hao kazi yao tena kwa haraka kubwa ili waweze kulimaliza zoezi lao ambalo liliwaweka nchini mpaka wakati huo. Bwana huyo alifanikiwa kurudishwa nyumbani kwake baada ya hali yake kutengamaa vizuri.
Alikuwa amepata wasaa wa kuketi na familia yake, baada ya muda mrefu kupita alihitaji kupumzika mwenyewe ili kupata wasaa wa kuweza kuwaza kuhusu mustakabali mzima wa maisha yake yeye na hizo pesa ambazo alikuwa anazihitaji. Hizo pesa yeye alikuwa anataka kuzipata kwa njia ambayo ingemfanya asije kutambulika kwa sababu alielewa kuutafuta umaarufu wa kufahamika mwisho wake huwa ni mbaya, mpaka wakati huo alikuwa maarufu kila sehemu na hakutaka kabisa jambo hilo liweze kutokea.
Ilikuwa ni asubuhi na mapema, alizama kwenye mawazo mazito hasa ya namna ya kuipata hiyo familia huku pia akiwa na mashaka kuhusu uhai wa Gavin. Akiwa hapo mwenyewe anapata kahawa yake na ule upepo wa asubuhi kutoka baharini, alipokea taarifa ambayo alitumia dakika nzima kuweza kuitafakari hatimaye akakubali kwa sababu jambo hilo lingemsaidia yeye kusafisha jina lake na kumfanya watu wamuonee huruma na kumuona kama ni mtu ambaye alionewa pakubwa kuweza kutekwa.
Ilikuwa ni taarifa ya ujio wa mwandish wa habari ambaye alidai kuwa shabiki mkubwa mno wa kiongozi huyo na alikuwa akimuona kama shujaa kwake. Alihitaji kupata taarifa fupi tu kutoka kwake ili awafikishie wananchi hususani wale ambao walikuwa wanamhusudu. Alifika mwandishi wa habari wa kike jambo ambalo lilikuwa nje ya matarajio yake kabisa kwani hakutegemea. Alikuwa ni mwanamke mrembo mno kiasi kwamba hata yeye alijikuta anaanza kumeza mate kwa shida baada ya walinzi kumsindikiza mrembo huyo kufika hapo alipo kuwepo.

Kabla ya kumfikia mheshimiwa, walinzi walihitaji kumkagua mwanamke huyo lakini aliwazuia kwa kigezo kwamba wangemdhalilisha mwanamke, mwanamke ni mama bwana! Uliwahi kusikia wapi mwanamke anashikwa shikwa kirahisi hivyo? Walinzi wakawa wapole kama maji kwenye mtungi.
“Mheshimiwa pole sana kwa kila ambalo limekukuta, sisi kama watanzania tumesikitishwa kwa ukubwa na hili jambo kiasi kwamba watu wana mashaka na wanahitaji kuijua hali yako kwa wakati huu ili wawe na imani na uwaahidi kama utaendelea na kazi kwani wengi wanakuona wewe kama shujaa ambaye wanajifunza vingi kwako”
“Shukrani kwa moyo wako ambao unafanana na urembo wako ulio nao, nimejisikia faraja kubwa kuja kunitembelea hapa. Watu hawatakiwi kuwa na wasiwasi kwa sababu mimi nimerudi salama lakini jambo la msingi zaidi ni kuwaombea wale ambao wamekufa na naweza kukuthibitishia kwamba sitaondoka kwenye nafasi yangu hivyo nitaendelea kuwapambania watanzania na kuwanyoosha wapuuzi kama hawa ambao waliniteka na huu utakuwa mfano kwa wahalifu wote ambao watapita kwenye mkono wangu, hakuna hata mmoja ambaye mimi nitamruhusu atoke salama”
“Maneno ya kishujaa kabisa mheshimiwa, pia tunatamani kupata stori juu ya watu hawa lakini na hiyo familia ambayo walidai kwamba wewe unaweza ukawa una taarifa nayo. Watu wanatamani kujua kama je ni kweli una taarifa za hao watu? Huyo Gavin bado yupo hai? Na hao watu ambao walikuteka labda unajua namna ya kuwapata?” kidogo maswali hayo yalimfanya kumwangalia kwa umakini mrembo huyo ambaye kila alipokuwa anamtazama aliishia kufurahi.
“Mhhhh ukweli ni kwamba Gavin mimi naamini alikufa lakini mpaka sasa nimebaki na maswali mengi juu ya kauli za bwana yule, huenda naye ana mtazamo tofauti na hilo kiasi kwamba sasa tunaziacha mamlaka husika zitoe majibu sahihi. Binafsi mpaka sasa sijui kama familia hiyo ipo wapi, ni jambo ambalo lilikuwa nje ya uwezo wangu. Hao ambao waliniteka natamani wapatikane haraka waweze kupewa adhabu kali”

“Watu wengi wanaamini kwamba huenda kuna jambo la hatari mheshimiwa ndiyo maana watu wale walihakikisha wanamuua hata mtu wao Jopa ambaye alikuwa anatakiwa kutumikia adhabu yake kutokana na hukumu ambayo aliipata mahakamani. Huoni kama huenda walikuwa wanadanganya kusema kwamba mtu huyo kafa?”
“Kwa hilo sijajua jambo lolote lile”
“Vipi leo kama ukikutana na familia ya Gavin utaiambia nini?”
“Hii ni moja ya familia ambazo zimefanya mambo mabaya ndani ya taifa hili hivyo mimi nitawataka watumikie adhabu kali hata kuuawa kwa sababu wao ndio sababu kubwa ya matukio kama haya kuweza kufanyika”
“Huoni kama tunatumia uharaka kuwahukumu hawa watu mheshimiwa? Huenda hawakuwa na hatia na kuna taarifa zinasema kwamba kuna watu ambao walikuwa kwenye nafasi kubwa za serikali ndio ambao waliifanyia ubaya familia yao kisha wao wakaja kuyalipa yale baadae!”
“Hapana huo sio ukweli, ni uongo mkubwa. Wale walifanya yale kwa manufaa yao wao ndiyo maana kwa kuogopa kutumbuliwa upuuzi wao wakaamua kumuua hadi raisi kwa kuwahonga watu wake wa karibu jambo ambalo linaikuta hii familia na hatia ya maisha hivyo siku yoyote wakipatikana kwanza wana kesi ya kumuua raisi wa nchi, kosa ambalo kwa namna yoyote ile halisameheki”
“Mh….” Mwanamke huyo alikuwa anasogea zaidi alipo mheshimiwa ambapo harufu yake ya marashi ilizidi kumpa ladha safi jaji, alimgusa mkono wake ambao ulikuwa laini huku mwanamke huyo akiendelea kuuliza maswali magumu lakini kwenye mkono wake alikuwa na kalamu ndogo ambayo aliivuta kwenye kola ya suti yake, aliifungua kwa kubonyeza batani moja, ilikuwa na makali kwa mbele mithili ya wembe, bila shaka alikuwa anahitaji kumuua kiongozi huyo lakini zoezi lilisimamishwa na mlinzi ambaye alikuja spidi eneo hilo kiasi kwamba jaji akamgeukia akiwa anaonekana kabisa kukereka na hali hiyo.

“Bosi mheshimiwa raisi anataka kukuona?”
“Raisi?”
“Ndiyo”
“Nitaenda Ikulu baadae”
“Yupo hapa”
“Whaat?”
“Amefika na msafara wake wapo nje” ni jambo ambalo hakulitegemea hivyo lilimshtua kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba alianza kutokwa na jasho jembamba mwilini”
“Mruhusu aingie, nakuja kumpokea dakika moja tu” aliongea akiwa anasimama na kumgeukia yule mwandishi wa habari huku akiwa anatoa tabasamu ambalo halikuwa na furaha ndani yake.

“Naomba unisamehe kwa leo inatosha, naomba uache mawasiliano yako kwa msaidizi wangu kwa sababu baada ya hapa nitakuwa na maongezi binafsi na wewe”
“Sawa mheshimiwa, muda wowote ambao utanihitaji mimi nitakuja popote ulipo” alitabasamu akiwa anamwangalia mwanamke huyo kwa matamanio makubwa. Mwandishi huyo alipita njia tofauti na aliyokuwa amepitia jaji kwenda kumpokea raisi.
Mwandishi huyo wa habari alisimama sehemu kuwaangalia wanaume hao wawili walipokutana, huenda ilikuwa mara yake ya kwanza kumuona raisi wake kwa ukaribu zaidi ndiyo maana alimwangalia kwa umakini japo hakuonekana kuwa na muda naye kabisa kwani baada ya kukamilisha hilo alitoweka haraka mno. Baada ya kufika nje na umbali kadhaa kutoka lilipo jumba hilo kubwa, alisimama na kugeuka nyuma akiwa analiangalia jumba lile kwa umakini na kwa mahesabu makubwa.

Hakufahamika kama alikuwa na lengo lipi na mheshimiwa na yeye alikuwa ni nani mpaka akaishia kutoa silaha ambayo bila shaka ilikuwa ni ya mauaji ila aliona muda haukuwa rafiki, kwa siku hiyo alifeli ila alikuwa na uhakika kwamba ipo siku jaji angejaa kwenye mkono wake ukizingatia alikuwa amechanganyikiwa na ule urembo wake na alimuachia mawasiliano kwa ajili ya siku nyingine kuonana.

Ukursa wa ishirini na moja unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA ISHIRINI NA MBILI
SONGA NAYO................

***
“Tangu umerudi mimi binafsi sikupata nafasi ya kuweza kuonana na wewe na kukupa pole zangu ila nina imani kwamba unaendelea vizuri kabisa”
“Ndiyo mheshimiwa raisi, kwa sasa namshukuru Mungu nipo vizuri na kwa sababu nilipata tu mshtuko ndiyo maana haijapita muda mrefu mimi kurudi kwenye hali yangu ya kawaida tena”
“Ni jambo zuri kwa sababu wewe ni miongoni mwa watu ambao ni mhimili mkubwa kwenye taifa hili, linapotokea jambo la hatari kama hili kwenu inakuwa inaathiri mfumo mzima wa uendeshaji nchi. Ulipo toweka jeshi la polisi halijalala kukutafuta wewe kwa sababu hata familia yako ilikuwa na wasiwasi kubwa ila kwa sasa u mzima wa afya.
Sasa bwana jaji sijaja hapa ili kupoteza muda na wewe, kuna jambo ambalo limetokea alfajiri ya leo na ni hatari kwa usalama wa hili taifa. Jambo hili limefanywa kuwa siri kwanza ili mhusika atafutwe vizuri na kutoleta taharuki kwa wananchi wangu ila uhalisia ni kwamba hali sio nzuri. Alfajiri ya leo kuna mtu ambaye amevamia Lugalo ambapo ameua wanajeshi sita na kutoweka bila kufahamika kwa sababu wakati wanajeshi wengi wanafika ndani ya eneo la tukio hakukutwa.
Wanajeshi wamesambazwa muda ule ule kila kona ya mji na mipaka imefungwa kuanzia Makumbusho mpaka Tegeta kule ila bado imekuwa kazi kubwa kupatikana kwake japo maeneo hayo yanakaliwa na wanajeshi kwa wingi. Tukio hili linakuwa mwendelezo wa matukio haya kutokea tangu mahakama yako iweze kuvamiwa na wewe kutekwa na watu ambao hawajulikani kabisa wakidai wanaitaka familia ya Gavin.
Sasa kwa hesabu zangu naona kabisa kwamba haya matukio yana uhusiano wa moja kwa moja na wewe hapo unaweza kuwa msaada mkubwa kwenye hili. Hili jambo linaleta sintofahamu kwa watu na mali zao, watu wanapoteza imani tena ya kuwa na amani, taifa letu limejengwa kwa umoja, amani na mshikamano kwahiyo kama kimojawapo kikitoweka hapo tunakuwa tunaenda nje ya misingi ya taifa letu tangu waasisi wetu walipo tuvesha taji la ushindi wa uhuru” maelezo ya raisi yalikuwa marefu tena ya kueleweka vizuri kabisa wakati ambao alitulia kwanza akionekana hana papara na jambo lake.

“Umeongea jambo ambalo ni sahihi kabisa mheshimiwa, sasa sijajua hapo unataka nisaidie kwenye upande upi?”
“Kwanza kabisa nataka kujua ukweli wa kilicho kutokea huko ambako ulikuwa”
“Sijakuelewa mheshimiwa, taarifa yangu nimeitoa mapema kabisa na afisa yule amesha ipeleka kwa wananchi tayari.”
“Wakati ule ulikuwa unaongea na afisa Liam na kuwapa taarifa raia wa taifa hili ila kwa wakati huu unatakiwa kuripoti taarifa ya kweli na sahihi kwa mkubwa wa nchi” jaji alikaa vizuri, alielewa kabisa kwamba alikuwa anaulizwa swali la mtego na kama angejichanganya basi ingekula kwake mazima.

“Wakati wananichukua sikujua jambo ambalo liliendelea kwa sababu nilipoteza fahamu lakini baada ya kuzinduka, nilikuwa ndani ya chumba kikubwa kilicho gubikwa na kiza kinene lakini mwanga ukiwa hafifu sehemu ndogo tu ya eneo lile. Nikiwa kwenye maswali mengi ndipo akatokea mwanaume mmoja, mwanaume ambaye alionekana hakuwa na utani na ile kazi yake ungehisi kuna kitu alikuwa ananidai. Bwana yule ndiye ambaye alianza kunihoji mimi huku akiwa anaamini kwamba nilikuwa an taarifa za ilipo familia ya Gavin pamoja na kujua alipo Gavin mwenyewe, hap……”
“Kwanini unahisi waliamini wewe utakuwa na taarifa za hiyo familia?”
“Kwa sababu mimi ni jaji mkuu wa taifa hili, wanajua nina historia pana ya sheria kwa maana hiyo pia walikuwa wanaamini kwamba nina taarifa za kutosha ndiyo maana wakawa wanahisi kwamba mimi najua yote ambayo yalitokea na nina taarifa za watu hawa”
“Ni kweli kwamba una hizo taarifa?”
“Hapana mheshimiwa, jambo hili ningelifikisha kwako muda mrefu kama nilikuwa nalifahamu kwa undani namna hiyo”
“Una uhakika?”
“Ndiyo mheshimiwa”
“Nakusililiza”

“Baada ya kumpatia majibu kwamba kwa taarifa ambazo mimi ninazo ni kwamba familia hiyo haipo hai, bwana yule alionekana kukasirishwa na habari ile huku akiniaminisha kwamba mhusika yupo hai kabisa na familia yake ipo mahali”
“Kivipi alikuwa na huo uhakika?”
“Alidai kwamba hakuna sehemu ambayo ilithibitika moja kwa moja kwamba Gavin amekufa zaidi ya miili ya watu kadhaa ambao walikutwa eneo lile ambao nao hakukuwa na uhakika kama alikuwepo yeye”
“Alijuaje haya mambo?”
“Kwa sababu upanga ule haukupatikana. Kwa maelezo yake ni kwamba Gavin aliingia eneo lile akiwa na upanga, kama angekuwa amefia pale maana yake ule upanga ungeweza kupatikana lakini jambo la kushangaza ni kwamba hata ule upanga haukupatikana kabisa hivyo atakuwa hai”
“Mhhhh, huyu mtu unamfahamu au umewahi kumuona sehemu yoyote ile?”
“Hapana mheshimiwa”
“Wewe umeziamini hizo taarifa zake?”

“Sina uhakika nazo lakini zimenipa ukakasi, kuna namna nimezielewa hoja zake kwamba huenda mtu huyu ni mzima wa afya ila inawezekana akawa amedanganya kifo chake”
“Kwa sababu zipi labda mpaka afanye hivyo?”
“Huenda alikuwa anakwepa kuiingiza familia yake kwenye matatizo, akakubali kubeba lawama kisha ionekane amekufa nazo. Yule bwana aliua viongozi wengi sana wa serikali kesi ambayo alijua kabisa kwamba asingeweza kupona, sasa unahisi lingetokea jambo gani mheshimiwa kama angepatikana au kama familia yake ingepatikana? Hilo lilikuwa ni kosa la wao kuweza kuuawa hadharani kabisa. Kwenye ile kesi walinzi wa raisi pekee ndio ambao walipewa hukumu zao ngumu hivyo kwa maana hiyo ni kwamba wahusika wenyewe mpaka leo hawajaadhibiwa kabisa, inaweza kuwa sababu kubwa ya yeye kuweza kuigiza kama amekufa”

“Sasa kama shida yao ilikuwa ni yeye, wakakuta wewe hauna hatia na haujui kuhusu taarifa hizo, kwanini wakuachie kirahisi namna hii? Wote tunajua kwamba wangekutumia wewe kama kinga ama ngao yao ya kuishinikiza serikali kufanya yale ambayo wao wanayataka. Nina uhakika mpaka wanafanya jambo hili walikuwa wanaelewa kwamba kwa nafasi yako serikali inaweza kufanya jambo lolote lile kufanikisha kupatikana kwako, kwanini iwe kirahisi namna hii?”

“Kwenye hilo sijajua mheshimiwa kwa sababu hata mimi nimejiona kwamba ni mfu, watu wale niliwaomba kwamba kama wanataka kuniua mimi ni sawa lakini wasije wakaigusa familia yangu kwa sababu haina uhusiano wowote na kazi yangu lakini walidai kwamba muda wa mimi kufa haujafika, walikuwa wanatoa ni tahadhari kwa serikali kwamba wanaweza kumfikia mtu wao yeyote na kwa wakati wowote ule ambao wanautaka wao hivyo tuhakikishe tunawasaidia kupatikana kwa familia hii vinginevyo matukio kama yale ambayo yalitokea mahakamani yataendelea kila sehemu”

Raisi alikuwa makini kuyasikiliza maelezo ya bwana huyo, ni kama alikuwa anayathaminisha ila hayakuwa yakimuingia akilini, bwana huyo alikuwa bingwa wa saikolojia hivyo mtu anapo mdanganya alikuwa anajua kirahisi na jambo hilo aliliona kwa jaji wake hali ambayo ilianza kumpa mashaka ambayo hakuwa na sehemu ya kuyapatia majibu sahihi kwa wakati huo na hakutakiwa kukurupuka kufanya maamuzi.
“Unahisi hawa watu wanahitaji ni kuipindua serikali yangu bwana jaji?” jaji alishtuka, hakutarajia kama angeulizwa jambo la namna hiyo.
“Taifa letu lina ulinzi mkali mno, hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kuthubutu kuja na wazo la namna hiyo kwa sababu litahesabika kama usaliti”
Ukurasa wa ishirini na mbili unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA ISHIRINI NA TATU
SONGA NAYO................

“Na kwanini umedanganya kuhusu Jopa?”
“Kivipi mheshimiwa”
“Una uhakika kwamba amekufa?”
“Kwa video ambayo nilionyeshwa inaonekana ni yeye na ameuawa kabisa”
“Una uhakika kwamba jambo hilo ni kweli?”
“Sina uhakika kwa asilimia zote”
“Umeliwasilisha kana kwamba una uhakika wa asilimia zote”
“Ni kwa sababu nilikuwa nina presha bado mheshimiwa, nilikuwa naiwazia sana familia yangu hivyo nilikuwa na wasiwasi mno. Sina jibu la moja kwa moja na kama angekuwa hai kwanini wadanganye?”
“Jaji tutaonana wakati mwingine, kwa sasa wewe pumzika mimi nina majukumu mazito mbele yangu” raisi aligundua kabisa kwamba jaji alikuwa muongo anamdanganya ndiyo maana aliamua kuyakatisha mazungumzo hayo kwa sababu jambo ambalo lilimleta hapo alilipatia majibu kwenye ubongo wake. Jaji alibaki ameduwaa akiwa haelewi, hata yeye hakuwa na imani na raisi wake, alimwangalia kwa umakini mpaka alipo tokomea zake.



********
THE GLs’
Inasimama kwa niaba ya ufupisho wa Gavin Luca (GL) huku muda mwingine ikitumika L pekeyake ikiwa na maana ya The Lucas’. Jamii ya watu wa siri ambao kupatikana kwao ulikuwa ni mtihani na hata huo utambulisho wao huo ulikuwa wa siri kubwa kiasi kwamba ni watu wa kuhesabika ambao walikuwa wanautambua vizuri.
Hayo yalikuwa ni masalia ya mwanaume ambaye alipata kuishi na kuitikisa nchi miaka kadhaa ambayo ilikwisha kupita zaidi ya ishirini. Gavin Luca kwenye kuishi kwake aliacha kumbukumbu bora ya maisha yake na kwa watu wake wa karibu ambao aliapa kuwalinda, mwanaume huyo kwa mara ya mwisho watu hao walifanikiwa kumuona ndani ya Mlandizi alipokuwa anamalizia kazi ya kumuua Mavambo. Baada ya hapo ilibaki historia kwenye taifa yeye na ndugu zake kwani alipoenda Kigamboni ndipo zilirudi taarifa kwamba bwana huyo alikuwa mfu.

Watu hao hawakuwa wakionekana kirahisi wala kutambulika kwamba walikuwa wapi, ni familia ya bwana huyo ambayo ilitafutwa na serikali mpaka serikali yenyewe ikawa imekata tamaa moja kwa moja kuweza kuwapata. Hawakuwahi kuonekana wala kufanya kosa la namna yoyote lile kuwafanya watu ambao walikuwa wanawatafuta waweze kujua mahali ambapo walikuwepo, jambo hilo liliwafanya wasionekane tena kwenye maisha yao.

Baada ya maisha kwenda na muda kupita ndipo zilitengenezwa hizo alama za vifupisho, hazikuwa kwa ajili ya kufurahisha bali watu hao walikuwa wanalienzi jina la Gavin Luca ambaye alipata kuishi kwa miaka mingi ambayo ilipita lakini pia ulitumika kama utambulisho wa wao kutambuana popote pale. Huko ndiko ambako Jabari alikuwa anapaswa kufika kwa ajili ya kuonana na watu hao ana kwa ana pamoja na kukutana na kiongozi wa watu hao ambaye alidaiwa kwamba anaitwa Ghost. Hakuna jambo la maana sana ambalo alikuwa analifahamu mwandishi huyo wa habari kuwahusu watu hao lakini aliamini kwamba huenda ni muda ulikuwa umefika japo alikuwa anaogopa.

Baada ya kusababisha mauaji kwenye treni kabla hakujapambazuka, alishuka kwa kuruka kwenye treni baada ya kufika mahali ambapo ramani yake ilikuwa inampa maelekezo kwamba alitakiwa kushukia. Yalikuwa ni maeneo ambayo yalikuwa mbali sana na mji lakini pia hayakuwa mbali na misitu na milima milima ambayo ilifanya usiku kuwe na kiza kinene. Aliangalia ramani yake vile ilikuwa inamuelekeza ndipo mbele akaona barabara kubwa ya vumbi ikiwa inaenda mahali ambako hakuwa na uhakika kama alikuwa na ufahamu nako ila hakuwa na namna zaidi ya kuifuata ramani.
Alitembea kwa muda mrefu mpaka akajihisi kuchoka, lakini wakati anaelekea kukata tamaa kwani hakujua mahali ambako alikuwa anaelekea ndipo aliona mwanga mkali kwa mbele yake ukiwa unakuja mahali ambako yeye alikuwepo. Alipigwa na butwaa baada ya kugundua kwamba ulikuwa ni msafara wa magari jambo ambalo lililiwa geni kwake kwani hakuelewa porini na milimani kama kule gari hizo zilikuwa zinatokea wapi ila ikamlazimu kuwa mpole.

Hakuwa fala, siku zote yeye ndiye ambaye anapaswa kuyalinda maisha yake kabla ya mtu yeyote yule kufanya hivyo, alijongea kwenye mti mmoja ambao ulikuwa kando ya barabara na kujibanza huku akiwa makini kuangalia ule msafara ili ajue ulikuwa unaelekea wapi. Jambo la kumshangaza yeye ni kwamba ule msafara ulisimama hatua kadhaa kutoka mahali ambapo alikuwepo yeye, aliona kuna mwanaume anashuka na kuangalia kwenye simu yake kisha akawa anaelekea mahali ambapo yeye alikuwepo.
Hakuelewa inakuwa vipi mtu huyo ajue kama yeye yupo pale, alizidisha hofu baada ya kuona kwamba mwanaume huyo hakuwa mtu wa kawaida, alikuwa amevaa mavazi meusi kwenye mwili wake na kitambaa usoni, mavazi yale yalikuwa yanafanana na yale ambayo yeye aliyavaa pia kwa sababu yalikuwa kwenye begi na alitakiwa kuwa nayo kwa namna yoyote ule ndio ulikuwa utambulisho wao.
Licha ya kuendelea kushangaa na kuduwaa lakini hakutaka kumuamini mtu huyo kirahisi kwa sababu kwanza hakujua amefanikiwa vipi kujua kama yeye yupo maeneo yale hivyo akasubiri kuona jambo ambalo bwana yule angelifanya. Msafara ulikuwa wa gari tatu na nje ya yale magari kulikuwa na wanaume watatu kwenye kila gari hivyo walikuwa tisa na yule ambaye alikuwa anakuja kwake alikuwa ni wa kumi.
Bwana yule aliangalia tena kwenye simu yake na kugeuka kwa nguvu kuelekea pale ambapo alikuwepo Jabari, alishtuka baada ya kukoswa na ngumi ambayo ilibandua mpaka gome la mti, alijivuta nyuma lakini alikutana na ngumi ya shingo mpaka begi lile likamdondoka. Alitaka kunyanyuka, alisita baada ya kugundua kwamba alikuwa anaangalia na bastola uso kwa uso hivyo akawa mpole.
“Unatakiwa kufanya mazoezi kuanzia kesho, bado wewe ni mlaini sana, shukuru Mungu hakuna mtu amejua kwamba una hilo begi”
“Nyie ni akina nani?”
“Shika begi lako tuondoke, kiongozi anakusubiri. Welcome to the GLs’” alimeza mate kwa shida, hilo neno lilikuwa geni lakini aliangalia kwenye vazi la yule mtu, lilikuwa sawa na lile vazi yake kwa sababu kwenye kifua kulikuwa na alama hiyo ya GL pamoja na alama ya upanga ikiwa na maana ya jina la muasisi wa hayo mambo. Hawakuonekana kuwa watu wa kawaida kwa upande wake na hakuwa na uhakika kama angeweza kwenda nao sawa, alikuwa na wasiwasi mno lakini hakuwa na namna kwa sababu alitakiwa kuufikisha mzigo mwenyewe ambao alipewa kwa namna yoyote ile na hata baada ya kukutwa hapo begi aliambiwa yeye ndiye alibebe.
Alibaki ameduwaa na kujiuliza watu hao walijuaje kama yeye alikuwa hapo? Aliangalia begi lake kwa umakini mkubwa ndipo akagundua kwamba huenda mle ndani kulikuwa na kifaa cha mawasiliano. Alijihakikishia hilo kwa sababu alisisitizwa kwamba lile begi lilikuwa la mhimu mno hivyo asingeachiwa aende nalo kirahisi mpaka huko hivyo watu hao walikuwa wanajua alipo na hata kama angeamua kukimbia nalo basi wangemkamata tu. Alitabasamu kuona watu hao walivyokuwa makini na kazi yao, hawakuwa wanabahatisha, ni hesabu zilikuwa zinatumika kwa asilimia kubwa.

Alifungwa kitambaa Jabari hivyo hakuelewa mahali ambako walikuwa wanaelekea ni wapi, baada ya kufika sehemu gari hizo zilizungushwa kama mara tatu ndipo zikaendelea na safari yake kwenda huko ambako yeye alitakiwa kufika. Ulipita muda ambao hakuutambua kwamba ulikuwa ni muda gani mpaka kufanikiwa kufika mahali ambapo alifunguliwa uso wake kuweza kuona mbele.
Ilikuwa ni milimani ila sehemu ambayo ilikuwa inavutia kuitazama kwani ilitengenezwa na kuwa kama tambarale nzuri ya kumfanya mtu atulize akili. Kwenye jiwe kubwa kulikuwa na ile alama ya GLs’ na hata kwente miti kadhaa ambayo alikuwa anaiona mbele yake, kulikuwa na hizo alama. Kutoka hapo hawakutembea sana akaanza kuona mwanga kwa mbali, zilikuwa ni taa za kisasa ambazo zilifungwa hapo akagundua kwamba sehemu hiyo ilikuwa ipo katikati ya milima kwani ukiwa mbali usingeweza kuona jambo lolote huko.

Ukurasa wa ishirini na tatu unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA ISHIRINI NA NNE
SONGA NAYO................
Waliingia sehemu ambayo ilikuwa kama geti kubwa ambalo lilijhengwa kwa mawe ya kutosha na baada ya kufika ndani huko, kuna sehemu magari yalisimamishwa kisha ghafla sehemu ambazo magari hayo yalisimama pakaanza kushuka chini, bila shaka sehemu hizo zilifunguka na kujiachia zenyewe baada ya hapo zikajifunga. Huko ndani ulikuwa ni kama mji, kulikuwa na barabara kabisa ya lami ambayo ilitengenezwa kwa ustadi mkubwa.
Kulikuwa kunavutia kwa sababu kulipambwa kwa vitu vya gharama mpaka pale ambapo gari hizo zilifika sehemu ambayo yeye alitakiwa kushuka pamoja na yule bwana ambaye ndiye alimvamia kwenye ule mti kisha zile gari zikaendelea na safari asijue zilikuwa zinaenda wapi. Sehemu ambayo hata hakuitarajia ndipo ulikuwepo mlango wa eneo hilo, mwanaume yule alisogeza jicho lake pale kisha akasubiri kama dakika moja ndipo lango zito likafunguka.
Aliyo yaona ndani alishindwa hata kutembea tena, alihisi wanadamu ni viumbe kwa kutisha kuliko hata ambavyo yeye aliwafahamu kupitia kazi yake ya uandishi wa habari. Aliingia sehemu ambayo ilikuwa ni kama jumba kumba la kifahari, akilini mwake bado hakuwa akiamini kama alikuwa milimani na hata hakujua eneo sahihi ambalo alikuwepo kwa wakati huo hata kama angefanikiwa ni kutoweka hilo eneo.

Ndani kulikuwa kuzuri mno, alibaki anaduwaa akiwa anaangalia vito vya dhahabu vilivyo sheheni ndani ya hilo jengo ambalo lilikuwa chini ya ardhi. Alikuwa anatembea kwa uoga, kosa lake moja lingeyabeba maisha yake na hata isinge julikana kama aliwahi kuwepo binadamu kama yeye. Sasa hapo ndipo alielewa ambavyo watu huwa wanasema ndugu yetu amepotea tumemtafuta miaka na miaka lakini hatujawahi kumpata, sasa kwa eneo kama lile mtu huyo ungempatia wapi? Hakukuwa na sehemu hiyo, ungekufa huko na kuzikwa basi hakuna mtu hata mmoja ambaye angefanikiwa hata kukisia.
Alikuwa anatembea kwa mashaka kwani eneo lilikuwa tulivu mno, mwanaume yule ambaye alikuwa naye alimsimamisha na kumkagua kwenye mwili wake na kifaa maalumu mpaka alipo jiridhisha kwamba yupo sawa ndipo akamruhusu kuingia sehemu ambayo ilionekana kuwa ya pekee kabisa. Aliingia naye huko kisha yeye aliinama kutoa heshima na alimtaka hata kijana huyo kufanya hivyo, hakuwa mbishi, alifuata maagizo na kisha mwanaume huyo ambaye alikuja naye alitoka humo ndani lango likajifunga na kumuongezea hofu kubwa kwenye moyo wake.

Heshima ambayo walikuwa wanaitoa, ilikuwa ni kwenda kwa mwanaume mmoja ambaye alikuwa amegeukia ukutani karibu na sehemu ambayo ilikuwa inawaka moto kwa mbali huku kwenye mkono wake kukiwa na kitabu ambacho bila shaka alikuwa anakisoma kwa utulivu mkubwa. Mtu huyo alionekana kuwa mtu mzima japo alikuwa amempa mgongo Jabari.
“Habari yako bwana mdogo” aliisikia sauti nzito kutoka kwa mwanaume huyo ambayo ilikuwa ya kiutu uzima wakati mwanaume huyo anafunga kile kitabu.
“Salama kiongozi shikamoo” alijikuta anatoa hiyo salamu kwa wasi wasi mkubwa akiwa anatetemeka. Mwanaume yule hakujibu jambo lolote zaidi ya kiunuka alipokuwa ameketi akiwa na kanzu kwenye mwili wake na kugeuka. Jabari alitaka kukimbia baada ya kumuona bwana huyo, umri wake ulikuwa umesoga lakini sura ilikuwa ni ile ile na ndipo alipokumbuka hata kumwangalia kichwani ambako alikuwa na dredi zilizokuwa zimetunzwa kwa ustadi mkubwa huku zikionekana kuwa za miaka mingi sana.

Sura ya mtu yule haikuwa imebadilika kabisa na alikuwa ana uhakika kabisa kwamba haikuwa mara yake ya kwanza kuiona sura hiyo. Alikuwa anaifahamu vizuri kwa sababu wamekuwa wakiisoma tangu wakiwa watoto na sura ya mtu huyo imewahi kusambaa kwenye kila kona ya nchi kwa sababu alikuwa ni muuaji. Akiwa anaendelea kuikumbuka sura hiyo alikumbuka miaka mingi ambayo ilikuwa imepita kwenye tukio la mwanaume mmoja ambaye alifanya mauaji ya kutisha mchana wa juakali ndani ya jiji ambapo alisababisha mauaji ya waziri wa mambo ya ndani wa wakati ule Slyvester Mboneka.

Yule muuaji aliimbwa kwa miaka mingi na alidaiwa kuwa Ghost na ndilo jina ambalo lilikuwa maarufu mitaani kwa sababu bwana huyo hakukuwa na taarifa za kuwahi kuishi kwake duniani ndiyo maana wakampa hilo jina. Sasa huyo muuaji ambaye alikuwa akimkumbuka ndiye huyo ambaye alikuwa akiangaliana naye ana kwa ana mbele yake, yule bwana ambaye alifanya lile tukio ambalo wamesimuliana mno wakiwa watoto wadogo ndiye huyo ambaye alikuwa mbele yake. Othman Chunga ndiye mwanaume aliyekuwa mbele yake, ndiye mtu ambaye alikuwa amebahatika kukutana naye wakati huo jambo ambalo yeye binafsi bado hakuwa akiliamini kabisa, alihisi kwamba anaota Jabari.

Alikuwa na historia za watu hao kwa sababu yeye alikuwa ni mwandishi wa habari, aliwahi kuwasoma kwa undani kipindi anazisaka taariza zao ili aweze kupata jina lakini hakuwahi kutarajia kama anaweza kukutana nao kwa namna kama hiyo. Aliyakumbuka yale maneno ya mwanaume ambaye alimpatia begi kule Tazara ambaye alimwambia kwamba kwa sasa anaenda kukutana na GHOST ambaye ndiye kiongozi mwenyewe wa watu hao. Hakuwa ameelewa wala kumfahamu huyo ghost mpaka pale ambapo alifika mbele yake, alijikuta anatokwa na jasho kila sehemu ya mwili wake.
“Bila shaka umeshtuka ama hukutarajia kuweza kuniona hapa si ndiyo?”
“Ndiyo kiongozi, kwenye akili yangu haukuwepo kabisa, nilihisi huenda ulikufa kwa miaka mingi ambayo ilikwisha pita”

“Haya ndiyo maisha Jabari, maisha haya ni marahisi tu kama ukizingatia kanuni zake ila kama ukitaka kushindana na kanuni basi maisha lazima yawe magumu kwako. Naishi kwa muda wote huo wanadamu wengi hawajui kama nipo hai au nimekufa jambo ambalo linanifanya niwe na amani wakati wote kwa sababu nayafanya mambo yangu kwa amani na hakuna jambo ambalo limenipa presha kwa miaka yote hii mpaka hivi sasa ambapo imenilazimu nijitokeze hadharani kwa sababu taifa linaenda kuingia kwenye matatizo mengine makubwa ambayo hata mimi sikuyatarajia.

Kabla haujapewa utaratibu na kukupatia sababu za msingi za wewe kuwepo hapa na wewe mwenywe kunikabishi mzigo wangu, una swali lolote ambalo unataka kuniuliza Jabari?” Jabari bado alikuwa kama ameduwaa, hakuwa na uhakika kama ile ilikuwa ni ndoto ama lilikuwa jambo la kweli kiasi kwamba ikamlazimu kuweza kujipiga kibao kuona kama bado yupo hai.
“Ndiyo ndiyo, nina maswali mengi sana kiongozi”
“Ni muda wako kuuliza kwa sababu unaweza usije kuipata nafasi kama hii tena na sio kila mtu anaruhusiwa kuniuliza maswali ila nimekupa nafasi hii kwa sababu maalumu ambazo utazijua siku za mbeleni”
“Ni kweli kwamba Gavin Luca bado yupo hai? Natamani sana kulifahamu hili. Natamani kujua kama familia yake yote bado ipo? Lakini jambo lingine ni kwamba kwanini mlipotea kwa hii miaka yote kiasi kwamba hakukuwa na alama yoyote ya uwepo wenu kwenye maisha ya watu wengine na mkaja kuishi ndani ya eneo kama hili?”

“Mhhhh, watu wengi wanatamani kulijua jibu la swali lako namba moja, sio wewe pekee bali ni ulimwengu mzima. Nimeona habari hizo kwa miaka karibia ishirini kila mtu akiwa anauliza hilo swali lakini hakuna ambaye amewahi kuwa na majibu sahihi hivyo limebaki fumbo ambalo kulitatua kwake ni jambo gumu isivyokuwa kawaida. Kuhusu maisha ya bosi inaweza kukushangaza hata mimi ambaye ndiye kiongozi wa hawa watu sina majibu sahihi ya kukupa ila jibu rahisi kwako ni kwamba alishakufa.
Hii sio hadithi ambayo inapendwa kusimuliwa kwa namna moja ama nyingine kwa sababu inatisha, tangu siku ile ambapo aliniaga kule Mlandizi hata mimi sijawahi kufanikiwa kumuona wala kuongea naye tena. Kuhusu familia yake nakujibu hili swali kirahisi ila madhara yake yanaweza kuwa makubwa kuliko ambavyo unafikiria kwa sababu yanaweza kuiponza familia yako yote na yakafanya ukaipoteza.

Familia yake yote ipo salama tena ni wazima wa afya na muda mfupi ujao utafanikiwa kuwaona baadhi ambao itakuwa na ulazima wa wewe kuwaona lakini kuna mmoja ambaye ndiye anasubiriwa na kila mtu anafika siku ya kesho kwa sababu kuna hii dharura imejitokeza ndani ya taifa hili”
“Samahani, naweza kuuliza kwamba ni nani?”
Ukurasa wa ishirini na nne unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom