Simulizi ya Kijasusi: Safari ya Gavin Luca

Simulizi ya Kijasusi: Safari ya Gavin Luca

Fasihinet ipo yote complete kwa wale ambao wanasoma kwa coin...


Na kwa wale wanao-soma kwa Softcopy pia ipo tayari yote bila kuwasahau wa vipande ✅

Ni wewe tu kuamua 🔥
 

Attachments

  • Screenshot_20250418-183635.png
    Screenshot_20250418-183635.png
    310.6 KB · Views: 36
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA TATU
SONGA NAYO................

“Kwa maana hiyo hakuna umuhimu wa wewe kuwa hai na familia yako kwa sababu hauna msaada wowote ambao utautoa kwangu”
“Hilo ndilo kosa ambalo hautakiwi kulifanya kwa sasa kwa sababu umepata mwanga wa kile ambacho unakitafuta. Hauwezi kuua watu wengi namna ile na kujiweka hadharani sura yako huku ukijua kabisa kwamba unaenda kutafutwa na taifa zima, haujaishia hapo umemteka jaji mkuu wa taifa halafu unataka kipuuzi tu uipoteze hii nafasi ambayo umeipata kusikilizwa na mimi?”
“Kama unahisi maisha yako yana thamani kubwa namna hiyo basi uanze kuongea mara moja na kunipa majibu ya jambo ambalo nimekuuliza”
“Ni miaka zaidi ya ishirini sasa tangu kwa mara ya mwisho familia hiyo ilipo onekana, kuipata tena haiwezi kuwa rahisi namna hiyo. Tangu yatokee yale matatizo ya mwanzo kama raisi kuweza kujiua na viongozi wengine wakubwa kufa ndipo ilikuwa mara ya mwisho familia hiyo kuonekana na kusikika. Miaka yote hii nimeitumia kuitafuta kwa udi na uvumba lakini sikufanikiwa kuipata ila kwa sasa nimeanza kuona mwanga wa kuwapata siku za hapa karibu”
“Umetumia miaka ishirini kuitafuta?”
“Unayo izungumzia hapa ndiyo familia tajiri zaidi ndani ya bara zima hili kwa miongo karibia mitatu sasa, unahisi inakuwaje rahisi kuwapata kwa namna ambayo unataka wewe?”
“Sababu ni ipi haswa ya wewe kuitafuta sana familia hiyo bwana jaji?”
“Sijajua ila huenda mimi na wewe wote tuna sababu moja ya kuweza kuitafuta, mimi nina shida na ule utajiri, ninataka kuzipata zile pesa zote ziwe kwenye mkono wangu kwa sababu najua nikiwa nazo basi nitakuwa mtu mwenye nguvu zaidi ndani ya bara zima. Nikiwa mtu mwenye nguvu maana yake ni kwamba kila mtu atakuwa chini yangu na kunisikiliza kwa kila jambo ambalo nitaliongea hivyo nataka niwe na hiyo nafasi ya kufanya ambacho nakitaka kwa muda niutakao mimi”
“Kwahiyo miaka yote hiyo umeipambania kwa ajili ya kutafuta utajiri tu kutoka kwao?”
“Ndiyo ndugu yangu, pesa ni kila kitu kwenye haya maisha. Pesa inatafutwa kwa miaka mpaka kuna watu wanazeeka bila kuwa nayo, unanishangaa vipi mtu ambaye nimeitafuta kwa miaka ishirini tu? Tena pesa ambayo ipo ni mimi kufanikiwa kuwapata wahusika tu ndipo niipate” maongezi ya jaji ndiyo yalimfanya Jopa naye kusogea kwenye kiti na kukaa, alionekana kuanza kuvutiwa na maelezo ya jaji ambaye alikuwa akijiamini mno.

“Ni kweli kwamba Gavin Luca mwenyewe alikufa?” swali la Jopa bila shaka jaji hakuwa amejiandaa kulipokea, lilimshtua kwa namna yake ikamlazimu kujifuta kwanza usoni maana jasho lilianza kumtoka.
“Unajua kwanini naishi haya maisha ya siri sana wakati naitafuta hii familia Jopa?” mwanaume huyo aliishia kumwangalia tu, ilikuwa ni ishara kwamba alitakiwa kuendelea na maongezi yake ambayo yalikuwa kwenye kichwa chake.
“Kwa sababu najua kosa moja tu liyatabeba maisha yangu”
“Nina uhakika haukuwa na taarifa yoyote juu yangu na watu wangu, sasa ulikuwa unahofia nani atayabeba maisha yako?”
“Kwa sababu mpaka sasa hakuna mtu ambaye ana uhakika kwamba Gavin Luca alikufa?”
“Unamaanisha?”
“Inawezekana kwamba bado yupo hai”
“Ilitangazwa kila sehemu kwamba amekufa, nimekuuliza ili nipate uhakika kwako kwa sababu ulikuwa karibu na mazingira ya watu wale wakati hayo mambo yanatokea kwa taarifa ambazo nimezipata awali”
“Hilo ni sahihi, nilikuwa karibu nikiwa gizani kiasi kwamba hakuna mtu alijua uwepo wangu ndani ya ule mzunguko kwa sababu niliwaza kwamba yangetokea yale ambayo yalitokea na mimi ningekufa kama ningetaka sifa za kujulikana lakini kuishi kwangu gizani ndiko ambako kumenifanya mpaka leo umenikuta nikiwa na afya njema. Dunia nzima ilitangaziwa kwamba amekufa lakini jambo la kushangaza ni kwamba haujawahi kupatikana mwili wake wala sehemu ambayo alizikwa bwana huyo. Kuna namna watu wanaiamini mitandao na mitandao ndiyo huwa inatumika kuwapumbaza watu hususani watu wapumbavu hivyo usije ukakaa na ukaamini kwamba Gavin Luca alikufa”
“Na vipi kama yupo hai?”
“Kama kweli anaishi basi naweza nikakusihi kwamba kimbia kwa namna yoyote ile ambayo unaiweza wewe usije ukaonekana tena kwenye haya maisha”
“Unanitisha mimi?”
“Mimi sikutishi, unaongea haya mambo kirahisi sana kwa sababu hukuwahi hata kumuona mtu huyo namna alivyo. Sio binadamu ndugu yangu ni jini lile, napokwambia kwamba kimbia kwa namna yoyote ambayo unaweza namaanisha kwamba hakikisha asije kujua kwamba unaitafuta familia yake kwa sababu ataua mpaka kizazi chako chote ila mbali na hilo basi ombea kwamba taarifa juu ya kufa kwake ziwe za kweli”
“Mhhhhh unaonekana una mengi unayajua kuhusu huyu mtu japo nina uhakika haunifahamu mimi ndiyo maana unaniongelea kwa wepesi wepesi namna hiyo”
“Sina uhakika kama kuna ulazima wa kukufahamu wewe kiundani linapokuja swala la hicho kiumbe”
“Nipe mazingira yake ya mwisho mahali ambapo alikuwepo na ilikuwaje mwili wake usipatikane”
“Mara ya mwisho alienda kumuua kiongozi wa THE IMMORTALS ndani ya Kigamboni karibu na yale maeneo ambayo walala hoi huwa wanaponda kokoto kwa ajili ya kuzilisha familia zao. Ndani ya lile eneo alifanya mauaji ya kikatili mno kwa walinzi ambao walikutwa wamekufa waliokuwa wapo nje lakini ndani ya yale mapango ambamo ndimo yalikuwa makao makuu ya watu wale, eneo lile lilititia chini kiasi kwamba palifunikwa
Kwa taarifa za mwanzo ni kwamba bwana yule Gavin alienda lile eneo kuifanya ile kazi mwenyewe na eneo lile lilititia naye akiwa ndani hajatoka lakini jambo la kushangaza ni kwamba wakati wanafukua mle ndani, waliikuta miili ya watu ambao iliharibika na kupondeka pondeka vibaya kiasi kwamba ilikuwa haitambuliki kabisa hivyo kilicho fanyika ni kwenda kupima DNA ya ile miili ambapo wahusika walitambulika isipokuwa mtu mmoja tu DNA zake hazikuendana na mtu yeyote yule.
Hapo ndipo yalizaliwa maswali mengi, kwa asilimia themanini na tano wengi waliamini kwamba ule ndio ulikuwa mwili wa Gavin Luca kwa sababu DNA yake haikuwahi kupatikana popote pale kabla lakini asilimia kumi na tano kuna watu waliamini kwamba ule haukuwa mwili wake kwa sababu ya eneo ambalo ulikutwa wakati wanayatoa yale mawe makubwa ambayo yalikuwa juu ya ule mwili.
Sasa hapo ndipo ilizaliwa sintofahamu kwamba amekufa lakini watu werevu huwa tunazingatia kila taarifa hata kama itakuwa ndogo. Zile asilimia kumi na tano ambazo zilisalia ndizo zilimaanisha kwamba yupo hai, zile themanini na tano zilithibitisha kwamba amekufa na kwa sababu ndizo zilikuwa nyingi, ndiyo maana uliona wakitangaza kwa imani kubwa kwamba kile kiumbe kimekufa rasmi na ukurasa wake ukafungwa pale pale.
Mimi kwenye maisha yangu yote nimeishi na zile asilimia kumi na tano kwa zaidi ya miaka ishirini sasa nikiamini kwamba yule bwana bado yupo hai ndiyo maana huwa nafanya mambo yangu gizani kwa sababu sitaki ufahari wa kuja kujulikana nikawa mfano. Napiga hatua zangu taratibu ili hata siku nikigundua kwamba aliishi niweze kumuua kirahisi, kwa maana hiyo ni kwamba hakuna mtu mwenye majibu ya uhakika mpaka leo kama yupo hai kweli au alikufa ni wewe unachagua wapi pa kuamini”

Mheshimiwa jaji alionekana kuwa na taarifa nyingi za familia hiyo jambo ambalo lilimpa umakini Jopa kuweza kusikiliza ili aweze kumuelewa bwana huyo.
“Kama kweli alifanikiwa kuishi, kwanini mpaka leo haijawahi kuonekana hata alama tu ya uwepo wake?”
“Hilo hata mimi sijui, ndiyo maana nimekwambia hakuna mtu anajua kwamba yupo hai ama amekufa na kufahamu hilo ni mpaka lipatikane kaburi lake ithibitishwe kwa vielelezo maalumu ila bila hivyo basi itakuwa ni ngumu kuamini kwamba alikufa. Lakini kwa akili ya kawaida mtu kama yule hata angekuwa hai isingekuwa rahisi kuweza kupatikana namna hiyo”

Ukurasa wa tatu unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 

Attachments

  • downloadfile-141.jpg
    downloadfile-141.jpg
    80.9 KB · Views: 41
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA NNE
SONGA NAYO................

“Kwa sababu zipi?”
“Alikuwa na familia tayari, siku zote mwanaume sehemu kubwa ya moyo wake inakuwa upande wa familia yake hivyo huenda hayo yote aliyafanya ili kuhakikisha familia yake inakuwa salama muda wote kwani yeye alijua kabisa kwamba kuna watu wanaweza wasiwe na nia nzuri kwa familia yake”
“Tunaanzia wapi na hii kazi kwa sababu umesema kukupata wewe umekuwa mwanzo wa mafanikio ya hii safari ambayo ninaifanya ya kuitafuta hii familia?”
“Hilo ni kweli kabisa lakini mimi binafsi siwezi kufanya kazi na watu ambao siwafahamu hivyo nahitaji kuwafahamu kwanza ndipo tujue tunaanzia wapi kuifanya kazi hii”
“Unataka kunifahamu mimi?”
“Sio wewe tu mpaka hao ambao wamekutuma wewe uje hapa”
“Hili jambo litakuwa hatari sana kwa upande wa usalama wako na maisha yako”
“Mpaka sasa sipo salama hivyo unaweza kuniambia tu nijue aina ya watu ambao naenda kuyaweka maisha yangu hatarini kwa ajili yao wapoje ili nisije kuwa napoteza muda wangu bila sababu zozote za msingi”
“Unalikumbuka jina la Gustavo Gaviria?”
“Unamaanisha yule muuza madawa ya kulevya ambaye aliwahi kutamba ndani ya mitaa ya PEENUGA kabla ya ujio wa Lucas Antony?”
“Ndiye huyo huyo”
“Hakuna mtu ambaye hamkumbuki yule bwana kwa sababu kwa kiwango kikubwa alifanya vijana wengi wakatamani kuingia kwenye hiyo biashara kwakuwa waliamini kwamba ndiyo ilikuwa njia rahisi ya kuweza kutoka kimaisha”
“Sasa huyo ndiye sababu kubwa ya sisi kuwepo hapa leo kuzungumza na wewe kuhusu jambo hili”
“Bado sijakuelewa unacho kimaanisha”
“Sio rahisi kunielewa ila nisikilize kwa umakini sana tena zaidi ya ambavyo unafikiria kwenye ubongo wako wa sababu hizi taarifa ambazo naenda kukupa hapa zinaweza kuyabeba maisha yako muda wowote kuanzia siku ya leo itategemea na namna ambavyo wewe utazipokea na kwenda kuzitumia.
Gustavo Gaviria aliuawa na DEA agent kutoka Marekani ambaye alipewa taarifa na mtu wa siri kuhusu uwepo wake kwa yule hawara wake ambako alikuwa anaenda kwa siri kubwa bila watu kufahamu lakini Gustavo kwa wakati ule alikuwa anamuamini mtu mmoja tu pekee ambaye ndiye huyo Lucas Antony ambaye ndiye alikuwa anakuwa na taarifa zake zote juu ya wapi atakuwepo, kitu gani ambacho atakifanya kwa muda fulani na biashara zote ambazo walikuwa wanazifanya, kiufupi ni kwamba hakuwa msaidizi wake tu bali mtu ambaye alimuamini kwa maisha yake yote.
Sasa wakati anaondoka usiku ule inadaiwa kwamba mtu ambaye alikuwa na taarifa za wapi atakuwepo alikuwa ni huyo msaidizi wake japo jambo hili limekuja kujulikana kwa baadae sana wengi hawakuwahi kulifahamu. Kabla ya hilo kutokea ni kwamba huyo msaidizi wake ndiye alikuwa amemtafuta huyo DEA Agent Rakeem ili amuuze Gustavo kwao kwa sababu walikuwa wakimtafuta kwa biashara yake ya madawa ya kulevya na nina uhakika unalitambua hilo namna Marekani wanavyo yapiga vita madawa ya kulevya kwa gharama ya namna yoyote ile.
Ile ndiyo sababu ambayo ilimfanya Rakeem kumuua Gustavo na ikaonekana kwamba lilikuwa ni jambo la kawaida tu. Ila kuna kitu Gustavo aliamua kuishi nacho moyoni kwa muda mrefu na ni watu wachache walikuwa wanakijua na watu hao walikuwa ni wanafamilia ambao hakuwa kwenye maelewano nao mazuri hivyo yeye siku zote alikuwa anjitangaza kwamba hakuwahi kuwa na ndugu. Hilo lilikuwa na faida zake na hasara zake, faida yake ni kwamba aliifanya familia yake kuwa salama muda wote kwa sababu hakuna mtu ambaye aliingia kuitafuta kwa namna yoyote ile kwani hawakuwahi kujua kwamba ilikuwa yake.
Lakini hasara yake ni kwamba alikufa akiwa mpweke bila ndugu yake yeyote yule kuhusika kwenye mazishi yake kwani yalisimamiwa na serikali. Sasa siri ambayo alikuwa nayo kwenye moyo wake ni kwamba bwana huyo alikuwa na mtoto ambaye alizaa na mwanamke mmoja ambaye alikuwa anajiuza huko kwao. Mwanamke yule aliwahi kumfuata Gaviria na kumpa taarifa ya mimba lakini aligoma kwa sababu ingeonekana kuwa aibu kwake kuweza kuzaa na mwanamke ambaye alikuwa anajiuza tena mtaani huku akiwa amefanya naye mapenzi kwa bahati mbaya tu tena akiwa amelewa.

Hali ile ilimfanya yeye kumpatia mwanamke yule pesa nyingi ili aweze kuitunza siri ile lakini alitakiwa kwenda kuitoa ile mimba hivyo makubaliano yao yakawa ni hayo ila mambo yalienda tofauti na yeye alivyokuwa amepanga kwani mwanamke yule hakuweza kabisa kuitoa ile mimba, aliamua kuitunza. Jambo hilo alilifanya kwa siri mpaka pale ambapo alijifungua na mtoto akaanza kukua ndipo alikuja kumtafuta Gustavo kwa mara nyingine na kumpatia taarifa ambazo zilimshtua sana ila hakuwa na namna kwa sababu jambo hilo lilikuwa limetokea na hakuwa na uwezo wa kuweza kulizuia tena.
Aliamua kukubaliana na hali kwa kuomba mwanamke huyo asije akavujisha habari hiyo yeye angemsaidia kwa kila kitu mpaka mtoto huyo anakua. Kwahiyo akawa ana mtoto kwa siri kubwa kiasi kwamba hakuna mtu ambaye alijua kuhusu hilo mpaka siku ambayo alikuja kufa ndipo wanafamilia wachache waliokuwepo wakazipata hizo habari baada ya mama wa mtoto kumpelekeka mtoto ili awafahamu ndugu wa baba.
Yeye baada ya kufika alihitaji kukutana na baba yake ndipo akapewa taarifa za kifo chake huku akiambiwa kwamba aliuawa na mtu ambaye jina lake baadae lilikuja kuwa maarufu sana. Kijana huyo hakukubaliana na hali hiyo alihitaji yeye na familia kwa ujumla waweze kumtafuta bwana huyo na alipe kwa yale ambayo alikuwa ameyafanya hivyo akatakiwa kufa kwa namna na kwa gharama yoyote ile.
Wakati huo bwana yule Rakeem alikuwa amerudi kwao Marekani lakini haikuwa tatizo la kumfanya aishi salama kwenye maisha yake. Mtoto wa Gustavo alidhamiria kumfanya mtu huyo apate mateso makali kwa kuipoteza familia yake aone jinsi maumivu yalivyokuwa makali, wakati huo naye alikuwa amefungua genge lake la siri kupitia jina la baba yake ili awe na nguvu kubwa naye akajikuta anaingia kwenye hiyo biashara huku moyoni akiwa ana shida kubwa na Rakeem aweze kulipa kwani aliamini kumpata Agent huyo ilimhitaji kuwa na watu kadhaa kwenye serikali ya Marekani na kuwa na watu wa namna hiyo inamhitaji mtu awe na mfuko mrefu, sasa kuhakikisha kwamba anakuwa na mfuko mrefu ndipo akaingia kwenye hiyo biashara akiamini kwamba ingempa pesa za kutosha.

Kwenye biashara alifanikiwa kwa kiwango kikubwa mno akawa anaingiza pesa nyingi ndipo sasa akatengeneza mfumo wake ndani ya Marekani ili kumpata bwana yule ambaye jina lake lilikuwa limepata thamani kubwa kwa kuweza kumuua muuza madawa ya kulevya maarufu ambaye taifa lake lilikuwa likimtafuta kwa kipindi kirefu.
Baada ya muda mrefu kupita alifanikiwa kuipata familia ya Rakeem ambapo alimtaka bwana huyo ampe taarifa za mtu aliye msaliti baba yake ili aweze kuiacha familia yake. Kama ulivyo nena hapo mwanzo kwamba sehemu kubwa ya moyo wa mwanaume upo kwenye familia ndivyo ilikuwa hata kwa Rakeem pia, hakuwa tayari kuona familia yake inauawa hivyo akalazimika kufanya jambo ambalo lipo kinyume na taratibu za kazi yake, kumtaja mtu ambaye alimpatia taarifa.
Sasa hapo ndipo kwa mara ya kwanza lilikuja jina la Lucas Antony kwenye masikio ya bwana huyo, jina ambalo lilikuwa la raia kutoka Tanzania. Licha ya Rakeem kuweza kutoa taarifa hizo lakini bwana huyo alimuua yeye na familia yake kwa sababu hakumuona kama ni mtu aliyekuwa anastahili kuwa hai kwa namna yoyote ile, alitakiwa kufa tena kwa mkono wake ndiyo maana aliua familia hiyo yeye mwenyewe huku akiwa tayari anajua hatua ambayo alitakiwa kuifuata kwenye karatasi yake ya maandishi ambayo ilikuwa inamuongoza wapi pa kwenda na nani wa kuweza kumfuata kwa wakati ambao alikuwa na uhitaji na ulazima wa kuweza kufanya hivyo.

Ndipo kwa mara ya kwanza alipo anza rasmi kutafuta taarifa za Lucas Antony, kumbuka kwamba wakati anafanya hayo yote muda ulikuwa umepita mrefu hivyo aligundua kwamba bwana huyo alikuwa mfu lakini kulikuwa na taarifa za uwepo wa familia yake na mwanae ambaye aliulaghai ulimwengu kwamba alikuwa amekufa.
Kwenye kufanya utafiti huo pia aligundua kwamba mwanae huyo alikuwa na nguvu za ajabu ambazo kwa mara ya kwanza zilikuwa ndani ya upanga ambao mpaka leo haujulikani upo mahali gani hivyo hapo akawa amedhamiria kumpata Gavin Luca. Ulitumika muda mrefu mpaka kupatikana kwa taarifa za bwana huyo lakini alifanikiwa kuzipata zote kwenye mkono wake hivyo akafanya maamuzi ya kuja Tanzania mwenyewe kwa mara ya kwanza kumtafuta mtu huyo lakini ndipo ikaja taarifa kwamba hakuwa hai, alikuwa amekufa japo taarifa hizo hazikuwahi kuwa na uthibitisho na ushahidi wa moja kwa moja.

Ukurasa wa nne unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA TANO
SONGA NAYO................

Kwake taarifa hizo alizipokea vibaya kwa sababu alikuwa anamhitaji Gavin akiwa hai, alikuwa anataka alipe ushenzi ambao aliufanya baba yake kumuua Gustavo lakini hakuwa na uwezo wa kufanya hivyo ila alibakia na mambo mawili kwenye kichwa chake, moja lilikuwa ni kupata shule na onyo kubwa kwenye maisha lakini jambo la pili lilikuwa ni kutafuta kitu ambacho alihisi ni haki yake ya msingi. Pesa.
Shule ambayo aliipata ni yale mambo ambayo aliyafanya Gavin Luca hali ambayo ilimfanya kuchukua tahadhari kubwa, sasa kwanini aliichukua hiyo tahadhari? Ni baada ya kugundua kwamba bwana yule alikuwa na familia lakini haikuwahi kujulikana tena kwamba familia hiyo ilipotelea wapi kwa kipindi chote hicho hivyo aliamini kwamba kama kuna binadamu alikuwa na zile nguvu basi kulikuwa na uwezekano mwanadamu mwingine akawa na nguvu za namna ile ile jambo ambalo huenda kwa baadae lingekuja kuwa hatari kwake yeye mwenyewe.
Baada ya kuligundua hilo ndipo aliamua kusafiri mpaka Japan na watu wake kadhaa, huko alienda kujitengeneza yeye na watu wake ili ikija kutokea siku akapata watu aina ya Gavin isijekuwa shida kuweza kupambana nao lakini wakati anafanya hayo yote ni kwamba kuna watu ambao aliwaweka kila sehemu ambao walikuwa wanaendelea kupeleleza kwa umakini kuhusu ilipokuwa familia ya mtu huyo ambayo alihisi ingemsaidia kukamilisha jambo lake ambalo alihisi ni haki yake yeye.
Kwenye kuitafuta familia hiyo jambo pekee ambalo alifanikiwa ama niseme tulifanikiwa ni kukupata wewe hapo. Kwenye ile orodha ya watu wote ambao walikuwa wanatafutwa na Gavin wengi kama sio wote walikufa huku zikibaki familia tu ambazo hazikuwa na hatia hivyo hata Gavin mwenyewe kama alikufa basi huko aliko anajua kabisa kwamba aliimaliza kazi lakini sisi tulitambua kwamba wewe bado unaishi jambo ambalo lilitushangaza kwamba wewe ulifanikiwa vipi kupona kwenye lile sekeseke? Ikawa sababu ya kuanza kuzitafuta taarifa zako zote hapo ndipo tukayagundua mengi ambayo ndiyo yamefanya hii leo mimi na wewe tufikie hapa.

Kwenye taarifa zile tuligundua kwamba wewe ndiye ulikuwa mtu wa karibu sana na raisi George kipindi kile lakini jambo hilo mlikuwa mkilijua nyie wawili tu. Wengi walikuwa wanajua kwamba bwana yule mtu wake wa karibu zaidi alikuwa ni mlinzi wake lakini haikuwa kweli, ulikuwa wewe hapo ambaye alikuwa anakutumia kukamilisha kazi zake nyingi ambazo asingeweza kuzikamilisha akiwa pale Ikulu kulingana na jina ambalo alikuwa nalo yeye na kuogopa kupata doa.
Wewe umehusika kwenye mauaji ya watu wengi kwa niaba yake, umehifadhi pesa nyingi ambazo zilikuwa zake na kila jambo ambalo yeye alihitaji ulifanye kwa ajili yake ulilifanya bila hata kuuliza. Tunajua kwamba pia alikuwa na sababu nyingine ya kuwa na wewe pembeni kwa siri kubwa kwa sababu alihitaji kuwapindua viongozi wake ambao pia hakuwa anawajua, raisi yule alikuwa anakutumia wewe uweze kuwatafuta watu hao kujua mfumo wao mzima kisha baada ya hapo angeweza kuwateketeza kisha yeye ndiye ajisimike kuwa kiongozi wa THE IMMORTALS lakini jambo hilo halikuwezekana kwa sababu kabla hajatimiza hayo yote ndipo alikutwa ameuawa wewe mwenyewe ukiwa hauna taarifa mpaka pale ulipokuja kuona kwenye vyombo vya habari.

Baada ya raisi kufa kwa sababu ulikuwa unazijua siri zake nyingi, kwa sababu ulikuwa unajua kila mambo yake ya siri zikiwepo akaunti zake za benki ambazo wewe ndiye ulikuwa ukizisimamia haukutaka kuishi kinyonge tena wala kuwa fala, uliamua kupotea na kila kitu ndipo ukaamua kuanza kuipambania nafasi ambayo mpaka leo upo nayo. Nafasi ambayo ulitumia pesa kuipata na hatimaye ukafanikiwa kuwa nayo, haya mambo hakuna wananchi wa huko nje ambao wanayajua zaidi ya sisi hapa ndiyo maana tukakutafuta kwa sababu taarifa hizi kama zikifika kwenye vyombo vya sheria ni lazima utahusishwa na kifo cha George.
Lakini baada ya kujua hilo kuhusu wewe tulijua kabisa wewe ungekuwa karata yetu ya mhimu kwa sababu unajuana na watu wengi lakini pia una taarifa nyingi za mambo ambayo yalitokea kipindi hicho hivyo tuliamini kwamba ungeenda kuwa msaada mkubwa kwetu ndiyo maana tuliamua kutumia njia yoyote kukupata. Sasa utajiuliza kwamba ni kwanini tumetumia njia hii?
Ukweli ni kwamba wewe ni miongoni mwa watu wagumu mno kukupata, mara kadhaa umekuwa ukionekana ukitokea Ikulu, jambo hilo limefanya tuchelewe sana kuweza kukufikia na ukiacha hilo, hata baadae baada ya kuyajua makazi yako, ilionekana wazi kwamba ni mtu mwenye ulinzi mkali mno kwa sababu serikali masaa ishirini na manne inaangalia usalama wako kwahiyo ingekuwa ni kazi kubwa kukupata na hata kama tungekupata kwa kule basi lazima kuna watu ambao na sisi tungewapoteza wengi na hatukutaka kufika huko kwa sababu tungekuwa tumetangaza vita vya moja kwa moja lakini pia tungeweza kutambulika kirahisi sana.
Hesabu ambazo zilikuja mezani ilikuwa ni kukupata ukiwa mahakamani kwa sababu ndiyo ilionekana kuwa njia rahisi zaidi kukamilisha jambo hili tena kwa haraka kubwa ndiyo maana tulianza kutengeneza mazingira mapema ya mimi kuwa na kesi kwa kuamini kwamba ungekuja pale mahakamani sasa mahakamani tungekukamata vipi? Ukiwa kwako au nje ya mahakama huwa unakuwa na ulinzi mkali zaidi ambapo kunakuwa na ule wa serikali lakini wakati huo huo unakuwa na ulinzi wako binafsi lakini pale mahakamani kunakuwa na ulinzi wa serikali tu pekee.
Urahisi ulianzia hapo baada ya kuanza kupandikiza watu wetu kwenye mfumo ili tukupate wewe ndiyo maana baada ya kuvamia pale umeona askari karibia wengi wamekugeuka na ambao walibaki ndiyo wale wamekufa mheshimiwa jaji. Mimi ndiye nilitakiwa kuifanya hii kazi ya kuhakikisha tunakupata na kufanya mazungumzo na wewe ya moja kwa moja kama hivi ili ujue umuhimu na ukubwa wa hili jambo kiasi kwamba kuna roho za watu zimetoka ili kuweza kufanya hili litokee, kamwe usije ukalisahau jambo hilo kwenye akili yako kwa sababu inaweza kukukosti.
Na jambo ambalo ulilifanya ni kwamba wewe una familia mbili ambapo moja mkeo mkubwa hajui kwamba una familia ya siri. Kwa sababu ulijua ni ya siri basi haukuipa ulinzi mkubwa ndiyo maana imekuwa rahisi mimi kuwapenyeza watu wangu mle ndani ila tambua kama utafanya jambo lolote la kijinga basi hakutakuwa na mazungumzo mengine ya amani kama ambayo umebahatika kuyapata leo kwa sababu watu ambao unaingia nao kwenye hii kamari sio watu wa kawaida bwana jaji hivyo hakikisha unayakumbuka maneno yangu kwa usahihi sana.
Nadhani nimekwambia jambo moja tu pekee la bwana huyo kuchukua tahadhari, lakini jambo lingine la pili ambalo alihisi ni haki yake kulipata ndiyo sababu amewekeza pakubwa kwenye kuitafuta hii familia ni kwamba ule utajiri wote unastahili kuwa wake kwa sababu ulipatikana kwa msaada mkubwa wa baba yake. Anataka kuhakikisha kama kuna wanafamilia wamebaki ahakikishe anawateketeza wote kisha baada ya hapo abebe fedha zote za hiyo familia ndipo anaweza kuhama moja kwa moja ndani ya taifa hili ila bila ya hivyo nadhani muda umefika sasa anaweza kuanza kuyaonyesha makucha yake hadharani. Nadhani ulidai kwamba unataka kutufahamu, umeweza kutujua kiufupi tu kuhusu maisha ya hapo nyuma na sababu za mhimu ambazo zimefanya mimi na wewe tupo kuongea hapa muda huu”
Mheshimiwa jaji alibaki ameduwaa, watu hao walikuwa wanafanya kazi kwa data ndiyo maana Jopa alimpa taarifa mpaka za kwake yeye mwenyewe ambazo zilikuwa za siri mno na aliamini kwamba siri hizo alibakia nazo mwenyewe tu kwenye kifua chake ila haikuwa kweli. Mheshimiwa jaji ndiye alikuwa mtu wa siri wa raisi George ambaye alikuwa anatumika kuweza kukamilisha kazi nyingi za bwana huyo hivyo baada ya George kufa iliaminika kwamba siri zote alibakiwa nazo yeye tu pekee kiasi kwamba akaamua kuzizika kwenye moyo wake lakini siku hiyo alikuwa anapewa taarifa za hizo siri. Alichoka.
Alihema na kushusha pumzi ndefu baada ya kusikia hiyo simulizi kutoka kwa bwana Jopa Magoma.
“Na vipi kama sitakuwa tayari kufanya kazi na nyie?”
“Utaziponza familia zako kisha wewe utawekwa mahali ukiwa hai ila utatamani ni bora ungekufa”
“Nahitaji kuonana na huyo kiongozi wako”
“Hilo ni jambo ambalo haliwezekani mpaka siku ambayo ataamua yeye kufanya hivyo ila kwa sasa utakuwa unawasiliana na mimi hapa kwa muda ambao nitakuwa nakutaka ama kama utakuwa na taarifa za mhimu kuweza kunipa”
“Umeniambia kwamba hata huyo bosi wako anazihitaji hizo pesa mbazo hata mimi nimepoteza miaka nikiwa nazitafuta, itakuwaje kuhusu nafasi yangu kwenye hizo pesa?”

Ukurasa wa tano unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 

Attachments

  • downloadfile-276.jpg
    downloadfile-276.jpg
    80.9 KB · Views: 30
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA SITA
SONGA NAYO................

“Kwa sasa unatakiwa kujali usalama wa familia yako kwanza, pesa zinaweza kukutokea puani lakini kama ukiifanya kazi vizuri nakuhakikishia utapewa bonus kubwa ambayo haujawahi kuifikiria kwenye maisha yako”
“Naruhusiwa kuondoka?”
“Hapana sio kirahisi hivyo bado kuna maelezo ambayo nayataka kwako” jaji alikuwa amenyanyuka tayari ili aweze kutoka ndani ya hiyo sehemu maana alihisi kama anaanza kuchanganyikiwa kwa mambo ambayo alikuwa anaambiwa hapo ila hakuwa na namna zaidi ya kuketi tena chini ili kuyapata hayo maelekezo aliyo ambiwa anatakiwa kupewa.
“Nataka kujua mambo kadhaa kuhusu mtu huyu, familia ambayo alikuwa nayo na watu wake ambao walikuwa wanamzunguka”
“Umenipa historia yenu, ni wazi mmefanya utafiti wa kutosha ndiyo maana mna taarifa zote hizo sasa unazungumzia kujua kuhusu familia yake ipi?” jaji alijibu mithili ya mtu ambaye hakupendezwa na aina ya swali ambalo alikuwa ameulizwa.
“Wewe ndiye mtu ambaye alikuwa karibu zaidi na raisi maana yake unayajua mambo mengi sana kuhusu huyu mtu na familia yake kwa ujumla. Mimi nimepewa ni taarifa ila pia nahitaji taarifa hizi nizisikie kwenye mdomo wako”
“Wakati zinatoka taarifa za kufa kwake Gavin, ilidaiwa kwamba aliacha mama, mke, babu yake, mlinzi wake mmoja pamoja na mtoto mmoja wa kike”
“Una uhakika na haya ambayo unayaongea?”
“Ndiyo”
“Huyo mlinzi wake ambaye alifanikiwa kuishi ni nani?”
“Othman Chunga”
“Naye bado yupo hai?”
“Sijajua ila nahisi hivyo kwa sababu huyu alimuoa yule mwanamke mwanajeshi ambaye alihusika kumuua mke wa George kipindi kile”
“Unamaanisha Sarah Martin?”
“Ndiyo”
“Na mtoto umesema wa kike?”
“Ndiyo”
“Kwa maana hiyo hana mtoto wa kiume kabisa?”
“Ndiyo hana”
“Kwa uelewa wako wa zile nguvu ambazo yeye alikuwa nazo kipindi kile, ni kweli kwamba zinaweza kuhama kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine?”
“Ndiyo inawezekana”
“Mhhhhhh hii familia inatakiwa kupatikana haraka sana kwa sababu naona kabisa kuna hatari kubwa hapo mbele na sitaki kabisa kumfelisha bosi wangu”
“Unawaza kuhusu bosi wako, unajua yale ambayo yanaenda kukutokea baada ya kile ulicho kisababisha mahakamani?”
“Ndiyo najua vizuri sana ila kwa bahati mbaya ni kwamba hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kufanikiwa kunikamata. Najua hiyo ndiyo habari kubwa kwenye taifa kwa sasa lakini ilikusudiwa iwe hivyo kwa sababu inaweza kuwa sababu nyingine ya kuyapata masalia ya Gavin Luca kama watakuwepo”
“Unamaanisha nini?”
“Yale mauaji ya halaiki namna ile kama kweli yupo hai ama kuna mtu kwenye familia yake atakuwa yupo hai na yupo karibu basi hataruhusu hali itokee halafu asifanye lolote, kwa maana hiyo nao wataingia kwenye huu mtego hivyo itakuwa rahisi kuwapata. Haya maisha unatakiwa uwe na mbinu nyingi za kuyafikia malengo yako ili moja ikifeli, basi unakuwa una njia ya ziada kuweza kurahisisha mambo zaidi. Washindi kwenye maisha mara nyingi hawajawahi kulitegemea jambo moja”
Jopa alionekana kuwa mtu mwenye mahesabu makali mno hali ambayo hata jaji yalianza kumtisha kwa sababu mara ya kwanza alikuwa na jeuri kubwa ila alikuja kugundua kwamba watu ambao alikuwa anaingia nao kwenye hiyo kazi hawakuwa wa kawaida.
“Mimi nitajitahidi kwa kila namna ya uwezo wangu kuhakikisha nafanya kila jambo ili taarifa za uwepo wao ziweze kupatikana haraka ila hakikisha unawatoa watu wako kwenye familia yangu kwa sababu sitafanya kazi na wewe kama utaendelea kuifanya familia yangu kuwa mateka wako hivyo haya mambo yaishie hapa”
“Hilo naweza kulifanya muda wowote kuanzia sasa, wala halina shida kubwa ila nataka uniambie jambo moja kwa sababu unaonekana kuwa na haraka sana. Unajua kwamba kwa yaliyo tokea kule serikali itakuwa inakutafuta sana na wewe ukipatikana wanategemea ueleze kwamba ulikuwa wapi na ulikuwa kufanya nini. Utahojiwa kila kona kwa sababu watu wengi wamekufa, je unajua ni namna gani unaenda kuielezea hii stori ili usije ukahusishwa moja kwa moja na jambo hili?”
“Hapana”
“Sasa una haraka ya kuwahi wapi?”
“Basi ni vizuri ukaniambia jambo ambalo napaswa kulifanya kwa huo ushenzi wako ambao umeufanya ambao umeniweka mimi kwenye hali mbaya kama hii. Kumbuka kwamba nipo hapa kwa ajili yako lakini sijaja kwa matakwa yangu, nipo hapa kwa sababu umeniteka jambo ambalo ni kinyume na sheria ya taifa hili”
“Kama ungekuwa unaijali hiyo sheria ambayo unataka kuanza kuihubiri hapa basi usingekuwa mtu mshenzi kwa taifa lako mwenyewe, ulitakiwa kutumika kama mfano kwa kuigwa kwa watu wengine. Kama watu wako watazipata taarifa juu ya maisha yako ya siri kwa zaidi ya miaka thelathini sasa, unahisi utaendelea kuwepo kwenye kiti ambacho umekikalia kwa muda wote huu bila kuwa na sifa stahiki?
Mimi sijali kuhusu hayo mambo kwa sababu taifa ni kama limeuzwa hili ila jambo la msingi ambalo sitaki ufanye makosa yoyote ni kwenye hii kazi. Ni usiku sana saivi, kuna watu watakusindikiza mpaka karibu na kituo cha habari na utatupwa hapo ukiwa hauna fahamu na wakati unashtuka hapo utakuwa mbele ya kamera ama hospitali ambapo utaeleza yale ambayo watu wangu wanaenda kukwambia”
Jopa alitoka humo ndani bila hata kuaga akiwa na wale watu wake wawili kwani maelezo na mazungumzo na jaji yalikuwa yamefika ukomo kwa wakati huo.






THE DARKNESS OF AN ANGEL
Ni jina la kitabu ambacho kilitakiwa kutoka usiku wa tarehe thelathini mwezi wa kumi lakini jambo hilo halikufanikiwa kama ambavyo lilikuwa limepangwa kutokea. Siku ambayo kitabu hicho kilitakiwa kuachiwa, ndiyo siku ambayo mahakama ilivamiwa na Jopa akafanya yale mauaji ya kutisha hadharani na watu wake, ndiyo siku ambayo hata jaji wa mahakama kuu aliweza kutekwa na kupotea jumla kiasi kwamba ikawa imebaki taharuki kubwa miongoni mwa wananchi na vyombo vya usalama kwa sababu kila mtu hakuwa akijua ni kipi kilikuwa kinaendelea kwani ni jambo ambalo hakuna aliyekuwa amelitegemea kwamba lingeweza kutokea.

Kitabu hicho mwandishi wake hakuwa akijulikana kabisa lakini kuna mwandishi wa habari mmoja ambaye alikuwa anahisiwa kwamba huenda ndiye alikuwa anahusika na jambo hilo na hata kama asingekuwa anahusika moja kwa moja basi ni lazima yeye angekuwa anamfahamu mhusika ambaye alikuwa mmiliki halali wa hicho kitabu husika.
Ni kitabu ambacho kilipata jina kubwa kabla ya kutoka kwake huku mwandishi akiwa hajulikani kabisa ila mvuto wake ulikuja kutokana na namna kilivyoweza kuelezewa kazi kubwa ikiwa inafanywa na mwandishi wa habari huyo ambaye alikuwa anahisiwa kuhusika na jambo hilo. Mwandishi huyo alikuwa anatumia mitandao yake ya kijamii kuweza kukinadi kitabu hicho na kudai kwamba kama watu walikuwa wanatamani kuyajua yale yote ambayo yalitokea miaka ishirini iliyokuwa imepita basi ilitakiwa kila mmoja wao ahakikishe anaipata nakala ya hicho kitabu.

Ukurasa wa SITA unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 

Attachments

  • downloadfile-276.jpg
    downloadfile-276.jpg
    80.9 KB · Views: 33
Nakukumbusha tu kwamba hii collection nzima ya GAVIN LUCA ipo tayari yote mwanzo mpaka mwisho.

Collection hii ina simulizi tatu
1. IDAIWE MAITI YANGU
2. SAFARI YA GAVIN LUCA (THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA)
3. SIKU ZA MWISHO.

Simulizi hizi zote unaweza kuzipata kwenye WhatsApp yangu +255621567672.

Lakini kwa wale ambao wanatumia coins Fasihinet unaweza kuzisoma zote zipo kule complete kwa link hii hapa 👇


Cha msingi wewe angalia cover husika hapo chini Kisha nenda Fasihinet itafute simulizi yenye cover husika ambapo lazima utaiona...

Enjoy 🔥
 

Attachments

  • FB_IMG_1745210598622.jpg
    FB_IMG_1745210598622.jpg
    180.2 KB · Views: 40
  • FB_IMG_1745210601464.jpg
    FB_IMG_1745210601464.jpg
    114.8 KB · Views: 23
  • FB_IMG_1745210606007.jpg
    FB_IMG_1745210606007.jpg
    132.5 KB · Views: 40
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA SABA
SONGA NAYO................

Umaarufu mkubwa wa hicho kitabu ulikuja baada ya kudokezwa kwamba kilikuwa kinazungumzia maisha ya Gavin Luca, kitabu hicho kilikuwa kinayaangazia maisha ya malaika huyo ambaye alikuja kuamua kuuonyesha upande wake wa giza na mambo hayakuwa mazuri kwa baadae. Uwepo wa hilo jina kwenye hicho kitabu ndiyo uliamsha msisimko mkubwa wa wananchi kuhitaji kukipata kwa namna yoyote ile.
Hilo ni jina ambalo lilikuwa maarufu nchini kwa muda mrefu, watu wengi walikuwa wanajifananisha na bwana huyo kiasi kwamba nguo zenye jina lake zilibadilika kuwa kama sare mtaani, wengi waliona kama bwana huyo alifanya mambo ambayo kwa miaka mingi hakuna mtu angeweza kuyafanya. Licha ya serikali kutumia nguvu kubwa kuhakikisha kwamba wanalizika jina hilo na linapoteza mvuto na umaarufu nchini lakini jambo hilo lilionekana kabisa kushindikana hivyo wakataka kudili na kila mtu ambaye ndiye alikuwa sababu ya jina hilo kuendelea kupata umaarufu.

Kitabu kilinadiwa kwamba kingetoa historia nzima ya maisha ya bwana huyo ambayo watu wengi hawakuwahi kuijua kwani ilikuwa inasimuliwa kwa mafungu lakini mbali na hilo pia watu waliahidiwa kwamba wangeelezewa sababu za msingi za kumfanya bwana huyo kuamua kuwa mtu katili na kuua viongozi wengi kwa wakati mmoja namna ile. Kitabu kilikuwa kinaenda kufichua ule uchafu ambao walikuwa wanaufanya viongozi wa taifa lao na wapate sababu za msingi za yale mambo yote kutokea lakini waliahidiwa kwamba kuna vitu vingi vya siri ambavyo vilikuwa vinaendelea nchini ila kupitia kitabu hicho kila kitu kilikuwa kinaenda kuwa wazi kabisa.

Ile hamu kubwa juu ya jambo hilo kuweza kutokea ndilo ambalo lilifanya watu wawe makini mno siku hiyo ukizingatia pia kulikuwa na kesi kubwa ya Jopa Magoma ambaye alikuwa anashtakiwa kwa kubaka na kuua kwa kukusudia. Ahadi ilikuwa ni kwamba siku hiyo majira ya usiku ndipo kitabu kilikuwa kinaenda kuachiwa rasmi na kila mtanzania angekipata kwa shilingi milioni moja. Pesa haikuonekana kuwa tatizo kwa sababu zilikuwa ni taarifa za mapema na watu walikuwa wamejiandaa kwa hilo hivyo kwao haikuwa tatizo ila walitamani kuona kile kitu ambacho kilikuwa ndani yake.

Saa kumi na mbili ya asubuhi ya siku hiyo iliachiwa cover rasmi ya simulizi hiyo ambayo iliamsha hisia kali na msisimko kwa watu ambao walikuwa wanakisubiri kwa hamu kubwa. Kwenye Cover kulikuwa na mwanaume ambaye alikuwa kwenye mavazi chakavu, mavazi ambayo yalichoka isivyokuwa kawaida lakini hakuwa na nuru mwanaume huyo. Ungemwangalia lazima ungemuonea huruma kwa sababu hakuonekana kuwa na hatia yoyote ile lakini kwenye macho yake alikuwa anatokwa na machozi ambayo yangemfanya mtu yeyote yule aweze kumuonea huruma. Mwanaume huyo alikuwa na nywele ambazo zilichakaa huku kwenye unyayo akiwa peku paku kabisa mwili akiwa ameuhifadhi ndani ya kaptula kuu kuu.
Kwenye mkono wake alikuwa ameshika upanga ambao ulikuwa umetapakaa damu nyingi, chini ya unyayo wake wa mguu wa kulia ambao ulikuwa mbele, alikuwa ameikanyaga noti ya shilingi elfu kumi ambayo ilikuwa imechanika pembeni huku ikiwa na damu kwenye baadhi ya maeneo. Mbele yake alikuwa amelala mwanaume ambaye alikuwa ndani ya suti, mwanaume huyo alikuwa hai lakini mwili wake ulikuwa umetapakaa damu huku akiwa na sura ya huruma bila shaka alikuwa anahitaji kuonewa huruma na mwanaume huyo mbele yake.
Pembezoni kabisa mwa huyo mwanaume mwenye upanga, walionekana watu waliokata tamaa ambao walikuwa wamepiga magoti huku wakiomba na macho yao yote walikuwa wameyaelekezea kwa huyo mwanaume ambaye alikuwa ameushika upanga kwenye mkono wake. Hiyo cover ndiyo ambayo iliongeza msisimko kuwa mkubwa zaidi na kuwafanya watu hao watamani kuweza kukisoma kitabu mapema iwezekanavyo.
Msisimko huo uliwafanya watu waweze kuifuatilia ile kesi mahakamani kwa hamu kubwa, walihisi huenda nayo ilikuwa sehemu ya mambo ambayo yalikuwepo kwenye kile kitabu kilicho ahidiwa na mtu ambaye hakuwa anatambulika lakini wao walikiamini kupitia mwandishi wa habari kwa sababu ndiye ambaye alikuwa anasisitiza sana kuwahakikishia wananchi kwamba walitakiwa kwa namna yoyote ile kuhakikisha wanakipata kile kitabu, kilikuwa ni mhimu kwao.

Mwelekeo wa ile kesi mahakamani ndio ambao ulivuruga kila kitu, kuvuruga mambo hayo ndiko ambako kulifanya upepo ubadilike ghafla kwa sababu hata yule mwandishi wa habari hakuonekana tena kwenye mitandao yake. Taifa lilikuwa limeingia kwenye simanzi kubwa ya kuweza kuwapoteza watu wengi mahakamani huku mtuhumiwa akidaiwa kwamba alifanikiwa kutoroka na jaji wa mahakama jambo ambalo lilizua utata na maswali mengine ambayo hayakuwa na majibu ya haraka kiasi kwamba wananchi wakawa wamebaki wametaharuki wasijue ni jambo gani ambalo lilikuwa linaikumba nchi kwani yalikuwa yanatokea yaliyo nje ya uwezo wao.
Jambo hilo lilileta picha mpya huku watu wakiwa hawaelewi ni jambo gani lilikuwa linaendelea, kwanza walishangaa kwamba inawezekanaje mahakama kuu ikavamiwa kirahisi namna hiyo wakati kuna ulinzi mkali? Hayo mauaji ya halaiki yalikuwa yamepotea kwa zaidi ya miaka ishirini sasa na watu walianza kusahau kabisa, Jopa alikuwa ni nani mpaka kuirudisha hali hiyo ndani ya taifa lao kiasi kwamba watu wakaanza kukosa amani tena? Hakuna hata mmoja ambaye alikuwa na jibu sahihi.

Saa kumi kamili jioni mwandishi wa bahari alitoa taarifa kwenye mitandao yake ya kijamii kwamba kile kitabu kisingeweza kutoka kwa siku hiyo mpaka pale ambapo mambo yangetulia. Alidai anasikitishwa sana na jambo ambalo liliwakumba watanzania kwa wakati huo na alitoa pole za dhati huku akiahidi kulifuatilia jambo hilo kiundani zaidi ili aweze kujua kwamba ni nani na nani walikuwa nyuma ya jambo hilo na mwafaka wake ungekuwa ni upi.

Jabari Malik, ndilo lilikuwa jina la mwandishi wa habari huyo ambaye alikuwa anakitangaza kitabu kwa nguvu zake, alikuwa anaitumia mitandao ya kijamii kuweza kuwasihi watu wahakikishe wanakipata bila kukikosa kwa gharama yoyote ile hivyo bwana huyo alipata umaarufu wa ghafla na kumfanya kuwa na jina kubwa kila kona kwa sababu alikuwa anafanya kile ambacho wananchi walikuwa wanamhitaji akifanye. Jambo moja tu ambalo kijana huyo wa miaka ishirini na mitano alikuwa nalo makini ni uhai wake, tangu aanze kutoa taarifa hizo alikuwa anapata jumbe za kutishia maisha yake kutoka serikalini na kwa watu binafsi huku wakimtaka kuachana na jambo hilo mara moja lakini hakuweza kuwasikiliza.
Kijana huyo licha ya kupata jina kubwa, tangu aanze kupokea vitisho hivyo hakuwa mtu wa kuonekana hovyo kila sehemu, sio kila mtu alikuwa anaweza kumuona na kumpata kwa wakati ambao angemhitaji hali ambayo ilifanya awe mtu wa kuonekana zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Tangu alipotoa taarifa ya kwamba kitabu kilikuwa kinaachiwa hiyo siku, alikuwa amepokea simu nyingi ambazo hazikuwa salama kwa upande wake na alipewa taarifa ya kuhitajika na vyombo vya usalama lakini hakuweza kutii wito huo kwa sababu alijua kwamba kufanya jambo hilo ingekuwa ni kama kujichimbia kaburi mwenyewe. Alikuwa anajua yale ambayo yalikuwa yanaendelea nchini hususani kupotea kwa watu ambao walikuwa wapo kinyume na serikali hivyo hata yeye alijua kabisa kwamba muda wowote kama watu hao wangempata basi wangempoteza kama wale wengine.
Alielewa vyema kwamba hata wananchi wake wasingeweza kumtetea kwa sababu wengi wao ni waoga na wajinga ambao hawana hata uwezo wa kufikiria jambo kwa akili zao ndiyo maana alielewa kabisa kwamba jukumu la kuyalinda maisha yake lilikuwa ni la kwake mwenyewe na sio mtu mwingine yeyote yule. Baada ya kuona anatafutwa sana siku hiyo, aliamua kuizima mitandao yake ya kijamii yote na hakuna mtu ambaye alikuwa anajua mahali alipokuwepo bwana huyo.

Jabari Maliki alikuwa ni mtoto wa tatu kuzaliwa kwenye familia ya watoto sita ambao walizaliwa kwa mfanya biashara Malik Mchambuzi ambapo baba yake alikuwa ni mfanya biashara mkubwa na zamani alikuwa ni mchambuzi na mshauri wa mambo ya kijeshi na kisiasa ila kwa wakati huo alikuwa ni mstaafu. Kijana huyo ndiye alikuwa mtoto wa pekee kabisa wa kiume kwenye familia yao hali ambayo ilipelekea yeye kupendwa sana na baba yake akamuweka kwenye hesabu zake kijana huyo kuwa ndiye mrithi wa biashara zake hivyo akatamani kuweza kumkuza kwenye hiyo misingi lakini jambo hilo lilikuwa gumu kwake.
Ugumu ulikuja pale ambapo mtoto alionyesha kuwa na mipango tofauti na ile ambayo alikuwa nayo baba yake, mtoto wake aligoma kuishi kwenye ndoto ya baba kwa sababu alidai anahitaji kuitengeneza ndoto yake yeye. Miaka kadhaa nyuma akiwa ni kijana mdogo zaidi aliwahi kushuhudia tasnia ya habari ikiwa inaenda kufa, tasnia ya habari ilikuwa imefikia sehemu mbaya kiasi kwamba vyombo vyote vya habari vilikuwa vikitumika kuwahadaa watu, kudanganya juu ya yale ambayo yalikuwa yanaendelea.

Ukurasa wa 7 unafika mwisho

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA NANE
SONGA NAYO................

Vyombo vya habari muda wote vilikuwa vinaisifia serikali hata kama ingeharibu na kuua watu, hakuona umuhimu wa yeye kuwepo kama asingeweza kufanya jambo hilo hivyo tangu anaenda kusoma elimu ya juu ndipo mahali ambapo walipishana yeye na baba yake kwa sababu baba yake alimtaka mwanae asomee mambo ya biashara na uchumi lakini mwanae akagoma kabisa na kwenda kusomea mambo ya habari. Jabari alimuweka baba yake nia yake ya kusomea jambo hilo, alihitaji kuwa mtanzania wa kwanza ambaye asingetumika vibaya na mfumo na kuwafumbua macho raia wake, ni mtanzania ambaye alihitaji kupigania uhuru wa vyombo vya habari kwa sababu vipo kwa ajili ya kupaza sauti ambayo wananchi hawakuwa na uwezo wa kuipata sehemu nyingine mbali na vyombo vya habari.

Maamuzi hayo ya Jabari yalimuudhi sana baba yake ukizingatia yeye ndiye alikuwa mtoto wa pekee wa kiume kwenye nyumba yake, maamuzi yake ndiyo yalimfanya akiwa na miaka kumi na nane tu baba yake amfukuze nyumbani kwake na kumkana kwamba hakuwa mwanae. Baba yake alimkataa kwa sababu aliamua kuifuata ndoto yake na hakutaka kuishi kwa kufuata ndoto ya baba yake lakini baba yake alijua kabisa mwanae ambako alikuwa anaelekea hakukuwa sawa kwa sababu haijalishi kama alikuwa sahihi au hakuwa sahihi ila kwenda kinyume na serikali alikuwa anakitafuta kifo.
Muda ambao alifanya kazi na wanasiasa mzee Malik alikuwa anawajua watu hao, hawakuwa wakijali lolote kuhusu raia wao bali kila mtu alikuwa anajali juu ya tumbo lake na familia yake tu. Aliamini kusubiri mwanasiasa akuletee mabadiliko ni ndoto ambayo unakuwa unaiota mchana wa jua kali kabisa hususani ndani ya taifa ambalo yeye alikuwa analijua vizuri zaidi kiundani.
Jambo hilo halikumtisha Jabari, kwa sababu baba yake alimfukuza nyumbani kwa kumpa sharti la kama anataka aendelee kubaki basi afanye kile ambacho baba yake alikuwa anamtaka akifanye vinginevyo angekatiwa kila kitu mpaka misaada kutoka huko kwao. Kijana huyu hakutishika na jambo hilo kwa sababu kwenye kichwa chake alikuwa anajua jambo moja kwamba ni heri ufe ukiwa unaishi kwa amani na furaha kwenye kile kitu ambacho kinakupa furaha kuliko kuishi muda mrefu kuitimiza ndoto ya mtu mwingine ambayo haina faida yoyote ile kwako.
Kuwa mfanyabiashara mkubwa haikuwa ndoto yake ile ilikuwa ni ndoto ya baba yake hivyo hakutaka kufuata huo mkumbo ili baadae aje kujutia na kuanza kuumia kwa kupoteza muda wake kuweza kuwafurahisha watu wengine badala ya kuipambania nafsi yake yeye mwenyewe. Hiyo ndiyo sababu kubwa ambayo ilimfanya yeye kuibeba njia yake ambayo aliona inamfaa na kuamua kutoka nyumbani kwao akiwa na miaka kumi na minane tu.
Aliishi maisha ya shida sana usingeamini kwamba alikuwa anatokea kwenye familia ya maisha mazuri, aliteseka mpakaa kamaliza elimu yake ya juu lakini wakati wote huo alikuwa anafanya kazi kwa bidii kubwa kuhakikisha kwamba siku moja anakuja kuwa msaada kwa watu. Kuna kipindi alipotea na hakuwahi kusikika tena kwa zaidi ya miaka miwili na baada ya kurudi baadae ndipo alirudi na jambo hilo la kitabu. Kitabu ndicho kilianza kumpatia jina kubwa zaidi, watu walivutiwa na mtu ambaye ndiye alikuwa mhusika mkuu ndani ya kitabu hicho, mhusika ambaye hawakuwa na majibu kama alikuwa hai au alikufa na mengine yakabaki stori tu lakini wengine walisikia kwamba bwana huyo alikuwa na familia. Watu walitamani kufanikiwa kuipata familia ya bwana huyo waweze kuwahoji kwamba walikuwa wanajisikiaje kuwa familia ya bwana huyo.

Miaka saba ya kuishi mbali na nyumbani akiwa ametengwa kwa sababu ya maisha ambayo yeye binafsi aliyachagua na kuona yalikuwa sahihi kulimkomaza. Alikuwa mwanaume shupavu ambaye hakuwa akimuogopa mtu yeyote yule ndiyo maana hata kazi yake alikuwa anaifanya kwa weledi mkubwa na kujiamini lakini jambo hilo halikuwa jema kwake. Halikuwa jema kwa sababu alikuwa amewagusa wenye mamlaka na baadhi ya watu ambao hawakupenda habari hizo ziweze kufika mahali ambapo yeye alikuwa anataka kuzifikisha.

Saa tano na dakika kumi usiku Jabari Malik alionekana akiwa ndani ya chumba mwenyewe akiwa amejifungia na kumpyuta mpakato yake. Alikuwa kimya akiwa anaangalia kwa umakini yale ambayo yalikuwa yanaendelea kwenye mitandao na lengo lake alihitaji kuweza kuwa na kila taarifa ambayo ilikuwa inaendelea lakini mitandao yake binafsi alikuwa ameizima kwa sababu alijua wangeitumia kuweza kumpata mahali ambapo yeye alikuwepo kwa wakati huo.

Kijana huyo alikuwa ameketi eneo hilo akiwa anayawazia maisha na namna yalivyokuwa yanaenda. Akiwa anaendelea kuperuzi taratibu, safari yake iliishia pale kwenye lile tukio ambalo lilitokea ndani ya mahakama, aliiruhusu ile video iweze kurudia tena kwa mara nyingine maana alikuwa ameiangalia kwa muda mrefu tu tangu tukio hilo liweze kutokea asububi ya siku hiyo. Alionyeshwa kusikitishwa mno na jambo hilo na hakulipenda kabisa kwa namna lilivyokuwa limetokea.
Akiwa kwenye hayo masikitiko yake aligundua kwamba meza yake ni kama inatetemeka ndipo akakumbuka kwamba kulikuwa na simu moja ndogo ambayo alikuwa anaitumia kuwasiliana na mpenzi wake. Alipo iangalia alitabasamu kwanza kwa sababu aliyempigia ndiye alikuwa tulizo la moyo wake, aliipokea kwa bashasha na kumfurahia mwanamke ambaye binafsi alimpenda kwa moyo wake wote kwa sababu mwanamke huyo alikuwa naye kwenye magumu na mabaya na walipendana sana.
Baada ya maongezi ya muda mfupi mwanamke huyo alihitaji kuonana na bwana huyo, alidai kwamba haukuwa muda mzuri wa wao kuonana lakini mwanamke huyo alisisitiza kwamba ilikuwa ni mhimu sana na hakuwa anategemea kupokea HAPANA kama jibu hivyo akawa hana namna tena ya kufanya zaidi ya kuweza kumkubalia mpenzi wake ambapo alimuelekeza eneo ambalo alikuwepo lakini akimtaka mwanamke huyo ahakikishe hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa anamfuatilia ndipo aweze kwenda eneo hilo kwa ajili ya usalama zaidi.

Alikuwa anamuamini sana mpenzi wake hivyo hakuwa na wasiwasi wa aina yoyote ule kuhusu yeye, ni kweli ni siku kadhaa hawakuwa wameonana hivyo wazo la kuonana muda huo lilikuwa zuri kwa wote wawili. Alijikuta anatabasamu kwa furaha kwa sababu muda mfupi ujao alikuwa anaenda kufurahia mapenzi ambayo yalikuwa yakiukosha moyo wake kwa kipindi kirefu hususani kwa mwanamke ambaye alikuwa akimpenda na kuhitaji kuwa naye kwenye maisha.
Licha ya kumwamini mpenzi wake lakini kazi yake haikumfanya kuchukua tahadhari kadhaa kwenye kila jambo ambalo alikuwa analifanya bwana Jabari. Alitoka ndani ya lile eneo na kwenda kusimama hatua kadhaa kutoka ilipokuwepo ile nyumba ili kuhakiisha usalama zaidi kwa sababu nyumba hiyo ilikuwa ipo pembezoni kidogo mwa jiji huku ikiwa imezungukwa na miti kadhaa lakini umeme ulikuwa unawaka vyema kiasi kwamba alikuwa akiona vyema kila ambacho kilikuwa kinatokea.
Baada ya muda kupita aliona kuna gari inakuja lile eneo, alikuwa anaijua kwa sababu ilikuwa gari ya mpenzi wake hivyo moyo ukawa na amani hususani baada ya kumuona mpenzi wake akliwa anashuka na kuanza kusogea taratibu kwenye ile nyumba. Alikuwa makini mno kwenye kila hatua ili awe na uhakika na mambo aliyokuwa anayafanya, baada ya kuona kila kitu kilikuwa sawa, taratibu alianza kutembea kuelekea alipokuwa yule mwanamke ambaye naye aligeuka baada ya kusikia hatua za miguu na ndipo akamuona huyo mpenzi wake.
“Nisamehe Jab……” yule mpenzi wake hata hakumaliza ile sentensi yake ambayo alikuwa anaitamka ilionekana tu damu ikiruka hewani baada ya kufumiliwa kichwa chake. Lilikuwa ni tukio la ghafla ambalo hata Jabari mwenyewe hakuwa amelitegemea kabisa, mpenzi wake alipigwa risasi ya kichwa na kufa pale pale mbele yake watu wakiwa umbali wa hatua kadhaa. Bado alikuwa kama amepagawa akiwa ametulia anauangalia mwili wa mwanamke yule ambaye alikuwa akimpenda sana ukiwa pale chini.

Maswali yalikuwa ni mengi kwenye ubongo wake, hakuijua sababu ya msingi ya mpenzi wake kuweza kuuawa na watu ambao walionekana kuja naye, hakuwajua hao watu na hakuwa na uhakika na sababu za msingi za wao kumuua mwanamke huyo. Jambo hilo lilimuuma kwenye moyo wake kwa sababu alijihisi kuwa na hatia ya kusababisha mauaji ya huyo mwanamke ndipo akili ikamrudi akawa kama amekurupuka wakati huo alikuwa anawaona wanaume watatu wakiwa wanakuja mbele yake.
Kukurupuka kwake ndiko kulimpa taarifa haraka kwamba hakuwa salama, mahali hapo kwake palikuwa ni zaidi ya sehemu ya makaburi kwa ajili ya kuzikia watu lakini wakati anayakumbuka hayo yote muda haukuwa rafiki kwake. Alikuwa amechelewa Jabari hivyo akataka kugeuka nyuma ili ayaokoe maisha yake lakini nako upande wa nyuma yake alikuwa anakuja mwanaume mwingine. Alitambua kwamba wanaume hao walishukia mbali kidogo na eneo lile kisha wakaanza kulizunguka hilo eneo, hawakuwa wajinga.

Ukurasa wa nane unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA TISA
SONGA NAYO................

Hapo ndipo akatambua kwamba alikuwa na namna moja tu ya kuweza kutoka hai ndani ya eneo hilo, kuyapigania maisha yake. Hakukuwa na namna ya kumtoa pale hai kizembe, alijua ni lazima afe au watu hao waondoke naye jambo ambalo kwake lilikuwa ni hatari zaidi hivyo kwake mambo ya mhimu zaidi yalikuwa ni mawili, kufa ama kufanikiwa kukimbia ndani ya eneo hilo ila sio kukamatwa na hao mabwana, mwisho wake ulikuwa unaenda kuwa mbaya zaidi na alikuwa akilitambua hilo vizuri.
“Jabiri unaikumbuka hii sura?” alitamka mwanaume mmoja ambaye alikuwa ameshika bastola kwenye mkono wake, bila shaka waliwahi kukutana kabla ya siku hiyo na walikuwa wakifahamiana.
Jabari aligeukia ule upande ili aweze kumuona vizuri bwana yule ambaye ndiye alikamilisha lile zoezi la kuweza kumuua mpenzi wake. Baada ya bwana yule kumkaribia karibu ndipo sura ile akaikumbuka vyema, haikuwa ngeni kwake kwa sababu watu hao walikuwa wakifahamiana kabla lakini kufahamiana kwao ilikuwa ni kwa ajili ya masuala ya kazi. Mara ya mwisho wawili hao kukutana ilikuwa ni mwaka mmoja ambao ulikuwa umepita nje ya mahakama, walikutana wakati mwanaume huyo akiwa anashtakiwa kwa kosa la kufanya mauaji kwa kukusudia.
Kukutana kwao ilikuwa ni kwa sababu ya kesi hiyo ambapo Jabari alikuwa anakaa nje ya mahakama kila siku ilipokuwepo kesi ya bwana huyo ili kupata maudhui ya kuweza kuyasambaza mtandaoni ili azidi kupata jina. Ilifikia hatua bwana huyo akawa amemkariri vyema kijana huyo kwani kila alipokuwa anaenda mahakamani ilikuwa ni lazima waweze kuonana. Lakini stori yao haikuishia hapo tu bali mtu huyo kupitia mwanasheria wake alimtafuta Jabiri ili aweze kufanya kazi chini yake ambapo alidai angempatia jina kubwa zaidi ya lile ambalo alikuwa nalo lakini kazi yake kubwa ilikuwa ni kuhakikisha kwamba anampambania bwana huyo kwa kuweza kulilinda jina lake.

Kazi hiyo ambayo aliahidiwa pesa nyingi Jabari aliikataa kabisa kwa kuwa alidai kwamba yeye alikuwa anaisimamia misingi ya kazi yake kwahiyo hakuwa tayari kabisa kuweza kuwasaliti watanzania kwa sababu tu ya mtu huyo, alitaka kuifanya kazi yake kwa weledi mkubwa. Kukataa kufanya kazi na mtu huyo ilimpa jazba kali bwana huyo ila kwa kipindi kile hakuna na la kufanya kwa sababu alikuwa na kesi nzito mbele yake ila alimuahidi Jabari kwamba kuna siku angekuja kujutia uamuzi wake wa kuweza kugoma kufanya kazi pamoja na yeye.
Ile kesi ambayo bwana huyo alikuwa anahukumiwa nayo, alikutwa na hatia hivyo akafungwa jela miaka kumi na mitano hivyo mpaka wakati huo Jabari hakuwa na wazo kabisa kwa sababu alijua kwamba bwana yule yupo jela. Jambo la kushangaza ulikuwa ni mwaka mmoja tu umepita tangu afungwe jela lakini wakati huo walikuwa wanakutana mtaani tena kwa mara nyingine akionekana kabisa kwamba mtu huyo alikuja kwa ubaya ndiyo maana alimuua mpenzi wake.
“Nakukumbuka wewe, kwa sababu niligoma kukusaidia ndiyo maana umemuua mpenzi wangu?” aliuliza akiwa anamsogelea bwana huyo kwa tahadhari kubwa.
“Bwana mdogo nilikupa nafasi ya dhahabu ukaipiga teke, kwa sasa ungekuwa ndiye mwandishi wa habari tajiri zaidi ndani ya taifa hili ila ulikubali kubaki na hayo maisha ya kuhangaika hangaika. Kwa sasa sijaja hapa kumuua yule malaya kwa sababu hiyo, jambo ambalo limenileta hapa ni wewe hapo hivyo ongoza mpaka kwenye gari tuweze kuondoka wote kwa sababu sina mpango wa kutoka jasho kukuua muda huu hili eneo” alionekana kuwa mjivuni bwana huyo na sio ujivuni tu bali aliona kabisa kwamba uwezo alikuwa nao mkubwa wa kufanya lolote lile mahali pale.
“Unahisi kila mtu ananunulika sio? Unajua ni shilingi ngapi ambayo ninayo kwenye akaunti zangu za benki? Kumuua yule mwanamke haikuwa busara kufanya jambo hilo kwa sababu siwezi kukuacha ukiwa mzima. Unatakiwa kufa mpuuzi mkubwa wewe” ndita zilikuwa zimejichora wakati anatamka hayo maneno yake, alikuwa ni mwandishi wa habari tu hivyo hawakuwa na wasiwasi naye kabisa lakini aliwashangaza, huenda hawakutegemea kukutana na mtu wa namna kama hiyo.

Jabari kwenye mguu wake alivaa buti la kahawia ambalo lilikuwa na kisigino kirefu kiasi, alikigusisha chini akiinamia kwa mbele, alijigeuza na sarakasi ya mbele kile kisigizo kikawa kimelenga kwenye paji la uso la yule mwanaume ambaye hakuwa amejiandaa kwa sababu hakutegemea kukutana na jambo la namna hiyo. Ila alipokuja kushtuka lile buti lilikuwa linashuka kwenye paji lake la uso jambo ambalo lilimfanya kujivuta nyuma kwanza lakini alichelewa kidogo kwa sababu kile kisigizo kilimbaraza na kuacha alama ambayo ilianza kutoa damu lakini akiwa anayumba yumba ule mkono ambao ulikuwa na bastola ulikutana na mguu mwingine bastola ile ikawa imerukia mbali kutoka ilipokuwepo kwenye lile eneo. Watatu wale ambao walikuwa wamezunguka kila upande walimkaribia Jabari ili kuweza kukabiliana naye kwa sababu ila hali ambayo aliionyesha pale iliwapa tahadhari, hakuwa mtu wa kawaida kama ambavyo walijua.

Kumsogelea karibu yake lilikuwa kosa kubwa kwao kwa sababu aligeuka akiwa ameshika kisu kwenye mkono wake ambacho alikitoa kiunoni na kwa sababu hawakuwa mbele yake hawakuona hivyo yule ambaye alikuwa mbele alikutana nacho usoni. Kilichimba kwenye uso wake kuanzia lilipo paji la uso mpaka kwenye jicho lake hali ambayo ilimfanya aendelee kupiga makelele huku akidondokea chini.
Wakati analitekeleza tukio hilo alikuwa amezunguka ili kuukwepa mguu ambao ulikuwa unakuja kwenye mbavu yake, alifanikiwa kuudaka mguu huo na kuupindisha kwa mkono wake kisha akajivuta na kuzamisha kisu kwenye moyo wa bwana huyo na alipo kitoa hakuwa na uhai tena alikuwa mfu bwana huyo. Yule aliyekuwa chini akipiga makelele alikutana na kisu cha koromeo ambacho kilirushwa na Jabari akabaki anatapa tapa mwenyewe mpaka alipotulia huku wanaume wakiendelea na kazi.

Ni wawili tu walibakia ila Jabari alimuona mwanaume yule ambaye alikuwa anajuana naye akiinama na kuibeba bastola yake hivyo akajua kabisa kwamba anaenda kupigwa risasi kama akifanya uzembe. Jambo ambalo alilifanyi ni kuruhusu yule mmoja aliyekuwa naye karibu amzamishie ngumi kwenye mwili wake kwa sababu alijua wangekuwa karibu hivyo ingekuwa nafasi yake kupona kwenye hizo risasi kwa sababu lilikuwa eneo la wazi na kuifikia miti zilikuwa ni hatua kadhaa ambazo alikuwa anatakiwa azipige kwa mahesabu makali isivyokuwa kawaida.
Yule mwanaume baada ya kufanikiwa kuizamisha ngumi yake ndani ya mwili wa Jabari alidakwa mkono na kuvutwa kwa nguvu kubwa ambayo ilimfanya akose balansi. Jambo hilo lilipelekea mtu huyo kupigwa roba ya nguvu tena ya ghafla na kugeuziwa kule ambalo alikuwepo bwana yule mwenye bastola na tayari alikuwa ameanza kuzirusha risasi kwa fujo kubwa kuelekea alipokuwepo Jabari. Risasi zilikuwa zinamfikia mwenzake hivyo akatoa bastola nyingine na kuanza kushambulia kwa kutumia zote mbili ambapo aliamini kwamba zingempata tu Jabari.
Baada ya kuona hali hiyo Jabari aliusukumia mwili ambao alikuwa anautumia kama ngao mbele ili ukutane na hizo risasi kisha yeye akaanza kukimbia kwa spidi kubwa kuelekea kwenye ile miti. Alisikika akitoa mguno wakati akifanikiwa kujificha nyuma ya mti mmoja, mwanaume yule ambaye alionekana kuwa na usongo naye alikimbilia mpaka eneo hilo akiwa na bastola yake kwenye mkono wake, hakuonekana kuitegemea bastola tu bali ni kwamba Jabari alifanikiwa kwenye mahesabu yake ya kumuwahi na kumdharau bwana mdogo huyo ndilo jambo ambalo lilikuwa limemfanya ampoteze kizembe.
Alipo uzungukia mti huo kwa nyuma yake, hakukuwa na jambo la maana lolote zaidi ya damu ambayo ilikuwa kwenye mti huo. Alijua kabisa amemjeruhi hivyo angeenda kuhitaji msaada. Alisonya bwana huyo na kuondoka kuelekea ndani ya ile nyumba ndogo ambayo ilikuwepo pale. Ndani yake hakukuta jambo la maana lolote zaidi ya kompyuta mpakato moja ambayo ilikuwa mpya tu na haikuwa na la maana ndani yake na kitanda kimoja basi, moja kwa moja alijua kwamba amesha mpoteza mtu wake kwa hiyo siku huku akiwa amewapoteza vijana wake watatu kama utani. Aliitoa simu ndogo kwenye mfuko wa suruali yake na kupiga mahali ambapo alikuwa anapajua yeye mwenyewe.
“Amefanikiwa kukimbia ila sio yule mwandishi wa habari ambaye tulikuwa tunamdhania”
“Una maana ipi?” ilisikika sauti ya mkwaruzo upande wa pili
“Ni muuaji”
“Bila shaka unanitania?”
“Hapana, hapa ninapokwambia ni kwamba ametumia dakika moja tu kuwaua vijana wote watatu na ambaye nipo hai mpaka muda huu ni mimi pekee japo nimempiga risasi na anavuja damu”
“Una uhakika ni yeye?”
“Namjua vizuri sana kwa sababu sijafahamiana naye leo. Inawezekana kuna jambo kubwa lipo nyuma yake, mwandishi wa habari hawezi kuwa namna hii huenda kuna mchezo anaucheza”
“Nahitaji huyo mtu apatikane haraka sana”
“Sawa kiongozi” baada ya maongezi mafupi na upande wa pili bwana huyo aliikata simu yake na kutoweka hiyo sehemu kwa sababu hakukuwa na jambo lingine tena la kuweza kulifanya hapo.


Ukurasa wa tisa unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA KUMI
SONGA NAYO................

TAZARA
Ndani ya kituo kikubwa cha treni cha nchi, majira ya saa kumi kasoro jioni muda ambao treni ilikuwa inajiandaa kuelekea mkoani, alionekana mwanaume mmoja akiwa amekaa kwenye holi kubwa ambalo lilikuwa linatumika kwa abiria kuweza kupumzikia kabla ya safari. Ndani ya holi hilo kulikuwa na watu wengine ambao wengi wao walikuwa wakiongea na kubadilishana soga huku wengine wakifahamiana kwa mara ya kwanza kiasi kwamba zikawa zinazaliwa kelele ambazo zilifanya eneo hilo lisiwe na utulivu wa kutosha.
Ni kawaida sana uwapo ndani ya eneo hilo kukumbana na hali hiyo kwa sababu watu huwa wanatawanyika kila mmoja akienda upande wake ilimradi tu muda uweze kwenda waweze kuondoka na usafiri huo ambao huwa una utulivu wa kutosha ndani yake na kila mtu anaishi kwa namna atakayo yeye awapo ndani.
Ndani ya hilo eneo kwenye kiti kimoja kuna mwanaume alikuwa amejitenga mwenyewe, kweye mkono wake alikuwa na gazeti ambalo alikuwa ameliinamia kwa utulivu mkubwa, bila shaka hakuwa anataka bugdha ama kelele kutoka kwa watu wengine. Mwanaume huyo kwenye mwili wake alikuwa amevaa koti jepesi la blue, shati safi ya blue na suruali nyeusi. Kwenye mguu wake alikuwa na viatu vyeusi ambavyo vilishabihiana moja kwa moja na soksi zake.
Upande wa juu alikuwa amevaa kofia nyeusi aina ya pama pamoja na miwani myeupe ambayo ilikuwa inamuwezesha kuona vizuri kila lililokuwa linaendelea humo ndani. Lakini hakuonekana kuvutiwa sana na mambo yote zaidi ya kuyaelekezea macho yake kwenye gazeti ambalo lilikuwa kwenye mkono wake akiwa analisoma na kulifunua taratibu miguu yake akiwa ameiwekea nne, hakuwa na pupa, alionyesha kuwa mtu ambaye alikuwa anajiamini kwa ukubwa zaidi.
Aliyainua macho yake na kuangalia mbele yake ambako kulikuwa na maaskari kadhaa waliokuwa wanahakikisha usalama ndani ya eneo hilo huku ile sehemu ambayo alikuwepo yeye akiwa pekeyake na pembezoni kidogo mwa ile sehemu kulikuwa na mizigo kadhaa ya wasafiri wengine ambao walikuwa wanasafiri bila shaka. Aliyapeleka macho yake kwenye saa yake ya dhahabu na kutikisa kichwa chake kisha akaangaza kila upande lakini alionekana kabisa hakukiona kile ambacho huenda alikitarajia kwa wakati huo. Aliyarudisha macho yake kwenye saa na kuangalia katikati ya miguu yake sehemu ambapo ilikuwepo begi ya ofisini ya mkonini kisha akalikunjua tena gazeti lake kuweza kuendelea kukipitia kile ambacho kiliyabeba mawazo yake kwa mara ya kwanza.

Nje kabisa ya eneo hilo, upande wa chini ambako huwa kunatumika kukatia tiketi alionekana mwanaume mmoja ambaye alikuwa kwenye haraka. Licha ya kuwaona watu wengine wakiwa wanazunguka kila sehemu ndani ya hilo eneo lakini yeye binafsi alionekana kabisa kuwa nyuma ya muda wake hivyo alihitaji kuwahi mahali ambako alikuwa anapajua mwenyewe.
Alielekea moja kwa moja kwenye dirisha la tiketi na kujitambulisha kwa mhudumu mmoja mwanaume ambaye umri wake ulikuwa kwenye miaka hamsini akidai kwamba ni yeye ambaye alipiga simu kituoni hapo kuomba kuwekewa tiketi moja ya daraja la kwanza ndani ya treni na alilipia mapema kwenye mtandao. Usoni alivaa kofia yake safi na kitambaa cha kuziba uso wake hususani mdomo na pua na haikuwa ajabu kwa sababu ni wengi walikuwa wanafanya hivyo kwa ajili ya kujilinda na magonjwa ambukizi.
Alivaa koti ya jinsi ambayo ilimkaa vyema huku ikionyesha ndani t-shirt yake nyeupe ndani ambayo ilikuwa inaendana moja kwa moja na kiatu chake, alivaa suruali ya jeans ambayo ilifanana na koti lake ila kofia na kitambaa vilikuwa vyeusi. Mwonekano wake ulimfanya kuwa kijana wa kisasa zaidi ambaye aliwafanya watu wengi kumshangaa kiasi lakini hakujali kwa sababu baada ya kutoa vielelezo na kupatiwa tiketi alianza kupandisha ile sehemu ya kuweza kusubiria kwani muda ulikuwa unazidi kuyoyoma ni kama robo saa tu ilikuwa imebakia waweze kuondoka.
Alikuwa akipandisha ngazi akiwa makini kuangalia ile sehemu ambayo watu walikuwa wamekaa akionekana kabisa kutafuta kitu na baada ya sekunde kadhaa macho yake yalitua sehemu. Ni sehemu ile ambayo alikuwa amekaa yule mwanaume ambaye alikuwa anasoma gazeti, naye aliinua macho mara moja tu wakagongana kisha akajifanya kuendelea kusoma gazeti lake kama mwanzo.
Mwanaume yule ambaye alionekana kuwa kijana mdogo tu alitembea mpaka ile sehemu ambayo alikuwepo yule mwanaume akaketi kwa pembeni yake na kujifanya kama anampa salamu.
“Umechelewa sana kufika hapa, hii sio ishara nzuri, ulitakiwa kufika mapema kabla ya wakati kama huu”
“Hawa watu wananitafuta kila sehemu, wameweka watu wao ndiyo maana nilitaka kuwa na uhakika na usalama wangu kwanza ndipo niweze kuja hapa”
“Vipi hali yako kwa sasa unahitaji daktari wa kukusaidia ukiwa safarini?”
“Hapana, niliitoa risasi ilikuwa moja tu hivyo kwa sasa nipo sawa sioni kama kuna shida”
“Hapa kwenye miguu yangu kuna begi, begi hili ndani lina mzigo ambao unatakiwa kuufikisha mahali na hakikisha mzigo unafika kwa namna yoyote ile ambayo utaiweza kama unaona hali yako kwa sasa sio nzuri niambie ndani ya hizi dakika niende mwenyewe”
“Nina uhakika nitaufikisha mzigo ukiwa salama japo sijui naupeleka wapi”
“Unaenda kukutana na Ghost”
“Unamaanisha naenda kukutana na bosi?”
“Anahitaji kuonana na wewe kwa mara ya kwanza hivyo huo mzigo unaenda kumpelekea mwenyewe. Haukatazwi kuutazama mzigo huo ila hakikisha unafika mahali husika”
“Sawa kiongozi naenda kuulinda kwa nguvu zangu zote”
“Mahali ya kuupeleka na wapi unatakiwa kushukia utakutana na maelezo ndani ya begi hivyo nikutakie safari njema tutaonana wakati mwingine” mwanaume huyo alikuwa anaongea huku ameinama mithili ya mtu ambaye akili yake ilikuwa kwenye gazeti lakini ukweli ni kwamba hakuwa anasoma lolote zaidi ya kuongea na kijana ambaye alionekana kumtii kama kiongozi kwake.
“Roger that” alijibu lakini wakati huo mwanaume yule alisimama na kuanza kuondoka mithili ya mtu ambaye anaenda uani na angerudi ila ilikuwa ni safari ya moja kwa moja kwa sababu hakurudi tena na baada ya muda kijana yule kuhakikisha kwamba hakuna mtu ambaye alikuwa amemzingatia alisogea kwenye lile begi na kulishika kwenye mkono wake, wakati huo watu wote waliambiwa wapange mstari kwa ajili ya kuingia ndani ya treni kwani safari ya kuondoka ilikuwa imewadia.

Kijana huyo hakuwa na papara na kazi yake alionekana kuijua vizuri lakini wakati hayo mambo yote yanafanyika, kuna mtu mmoja ambaye alionekana kuwa na mashaka naye, alikuwa akimwangalia kwa umakini sana kijana huyo. Mtu huyo alimshtukia kijana huyo tangu anafika na kwenda kukaa karibu na yule bwana mtu mzima na bwana huyo baadae akapotea, kwake hakuona kama ni kawaida, alihitaji kumfuatilia na kumjua kiundani kwamba ni nani na kwenye begi lake kulikuwa na kitu gani. Udadisi ukazalisha jambo jipya kwenye treni.

Watu wote waliingia kwenye mabehewa yao, kuanzia watu wa daraja la tatu, watu wa daraja la pili mpaka wale wa daraja la kwanza ambao kijana huyo asiye julikana alikuwa mmoja wao. Muda wote hakuwa na taarifa kwamba kuna mtu alikuwa anamfuatilia, bwana yule ambaye alikuwa anamfuatilia, alitulia mpaka alipo hakikisha namba ya behewa ambalo kijana yule aliingia huku yeye akiwa hana habari wala taarifa yoyote juu ya mtu mwingine kuweza kumpa umakini mkubwa wa uwepo wake hapo.
Alipata behewa moja na wanaume wenzake watatu jumla wakawa wanne, kila mmoja alipewa kitanda chake kwa mfumo wa namba. Wenzake walikuwa wanatambulishana kiundani zaidi ila yeye hakuwa na bahari nao kabisa akalala na begi lake upande wa juu na hakutaka kusumbuana na mtu yeyote yule mpaka ulipofika usiku wa manane ndipo aliamua kubeba begi lake na kwenda nalo chooni ambapo njiani alikutana na mhudumu mmoja akauliza eneo ambalo walikuwepo kwa wakati huo. Alikuwa ndani ya muda mwafaka kabisa.
Lakini akiwa anaelekea uani aligundua kwamba choo ambacho alitakiwa kukitumia kilifungwa kwa ndani na wakati anagundua hilo na kutaka kuondoka hapo mlango ukafunguliwa. Ilikuwa ni ghafla na hakutegemea kukutana na jambo kama hilo, alivutiwa ndani ya bwana yule ambaye alionekana wazi kwamba alikuwa anamsubiri kwa hamu kubwa. Hakujiandaa kukutana na hali kama hiyo hivyo alishtukia akiwa amenyooshewa bastola na mtu huyo ambaye alikuwa mgeni kwake.

Ukurasa wa kumi unafika mwisho.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA KUMI NA MOJA
SONGA NAYO................

“Wewe ni nani na hilo begi lina nini ndani yake?” lilikuwa swali la bwana huyo ambaye alikuwa siriasi sana.
“Tunafahamiana kabla mheshimiwa?”
“Unatakiwa uvue kitambaa ili tufahamiane”
“Kwahiyo unamvamia mtu ambaye hata haumfahamu kwa sababu tu unataka kumfahamu yeye ni nani? Kwenye treni sijaja kwa bahati mbaya, nimelipa pesa kwanini unataka nianze kujitambulisha ndani ya taifa huru hili kwa kila mtu?”
“Bwana mdogo tusipotezeane muda, nimekuona tangu kule kituoni ukiwa unabadilishana hili begi na mtu ambaye bila shaka alikuwa anakusubiri hivyo nataka kujua kwamba wewe ni nani haswa na hilo begi lina nini, isije kuwa umebeba bomu ukateketeza treni”
“Nionyeshe kitambulisho chako” kijana huyo bila shaka aligundua kwamba bwana huyo alikuwa mtu wa serikali kwa maelezo yake tu ndiyo maana akamtaka amuonyeshe kitambulisho. Hakuwa mbishi baada ya kuonyesha kitambulisho alivua kile kitambaa chake ambacho kilishonwa vizuri na kuwa barakoa iliyo mziba vyema na kumfanya asitambulike.

Yule mwanaume ambaye alikuwa amemshikia bastola alibaki ameduwaa baada ya kitambaa kutolewa, aliyekuwa anamuona mbele yake alikuwa ni mwandishi wa habari maarufu sana ndani ya Tanzania Jabari Malik na ndiye huyo ambaye alikuwa mtu wa kukipa nguvu kitambu kipya cha THE DARKNESS OF AN ANGEL. Kijana huyo ni kwa muda alikuwa amepotea na yeye ndiye ambaye alitoa taarifa za kughairi kutoka kwa kitabu hicho siku ya jana yake baada ya bwana Jopa Magoma kuvamia ndani ya mahakama na kumteka jaji wa mahakama kuu.
Mshangao wake ulienda sambamba na namna walivyokutana kwani hakuamini kabisa kumuona bwana huyo ambaye mpaka wakati huo alikuwa anatafutwa na mamlaka za ulinzi na usalama lakini hawakujua kwamba wangempatia wapi na jana yake usiku alikumbana na balaa la kuweza kuuawa ambapo alipona akakutana na risasi tu ila kwenye jaribio hilo alimpoteza mpenzi wake kipenzi ambaye alitumika kuweza kujua mahali ambapo alikuwepo.

“Kumbe ni wewe Jabari Malik!”
“Umesha iona sura yangu na bila shaka najua jambo ambalo unaenda kulifanya hapa, kutaka kunikamatisha”
“Mimi ni askari ndiyo lakini ni moja ya hao watu ambao wanakutafuta kwa sababu pesa imebadilisha maisha ya watu ndugu yangu na leo sikutegemea kama ningeipata bahati hii ya kusafiri kisha nikakutana na wewe kirahisi namna hii jambo ambalo linaenda kunipa sifa kubwa kwa wakubwa zangu kufanikisha kukukamata. Mungu ni mku……” alijisahau akaanza kujielezea sana lakini wakati huo alikutana na jambo ambalo hakulitarajia kabisa kwenye akili yake.

Ile barakoa ilirushwa kwenye uso wake na kumfunika uso kiasi kwamba alijikuta anaachia risasi bila kutarajia kabisa na ni zile kelele za mtetemeko na muungurumo wa treni ndizo ambazo zilifanya risasi isisikike mbali. Wakati anarusha zile risasi mkono wake ulikutana na kisu kidogo ambacho kiliugawa mshipa wa damu kiasi kwamba damu ikaanza kumtoka kwa wingi na hata ile bastola yake ilidondokea mbali.
Hakuwa mnyonge mwanaume yule, alikuwa amefanikiwa kuitupa barakoa na kuupanga mkono wake baada ya kumkosa Jabari na buti lake ambalo lilitua kwenye sinki la maji mpaka likapasuka na kudondokea pembeni maji yakaanza kutoka kwa wingi humo ndani. Jabari alimrushia lile begi bwana yule ambaye wakati anataka kulipangua alikutana na mguu wa goti uliomfanya akakosa balansi nzuri ya kuweza kusimama jambo hilo lilimfanya kuyumba kiasi kwamba akakutanishwa na ngumi tano za uso.
Alishindwa kuona mbele akawa anarusha ngumi hovyo hovyo mwisho alichomwa na visu vingi kwenye mbavu zake mpaka akakosa kabisa nguvu za kusimama akashuka taratibu na kukaa akiwa ameegamia kwenye vyuma vya treni maji yakiwa yanampita na kumlowanisha ila hakujali kabisa kama sio kukosa uwezo wa kuyamudu. Jabari alisogea karibu zaidi na kumuinamia yule mwanaume akiwa anamkagua kila sehemu ya mwili wake ikiwemo kwenye waleti yake ambayo hakukutana na jambo la ajabu ndani yake zaidi ya vitambulisho, kadi za benki na pesa taslimu.
“Ningekupa nafasi ya kuishi lakini kufanikiwa kuiona sura yangu ni jambo ambalo halikupi nafasi hiyo ndugu yangu hivyo naomba tusameheane kwa hilo na nina imani utanielewa kwamba sikupenda kufanya hivi ila mpaka hapa sina namna nyingine zaidi ya hii”
“Wewe ni nani Jabari? Unaonekana sio yule ambaye watu wanamjua kwenye mitandao ya kijamii kama mwandishi wa habari ambaye kazi yake ni kushika kalamu ya wino na notebook kisha kuziandika habari na kwenda kuripoti”
“Kwa muda huu hata kama utanifahamu haina umuhimu wowote ule kwa sababu unaenda kufa hivyo ni mara mia usiweze kunifahamu”
“Haya unayo yafanya yamekuweka kwenye nafasi mbaya huenda haujui tu, kama siku wakifanikiwa kukupata basi hakuna binadamu atakuja kukuona tena”

“Hilo ni sawa japo sina uhakika na hayo maneno yako kwa sababu haujui ni nani yupo nyuma yangu na yupoje. Ila hata kama itatokea hivyo basi sio kwa kukamatwa na mtu dhaifu kama wewe, wewe unatakiwa kuwa mfano kwa wapuuzi wengine ambao wanazipuuza haki za wananchi na kujali kuwasujudia hao viongozi. Ni wazi unajua kabisa sina hatia yoyote ile lakini ulitaka kunikamata bila hata kunihoji na kibaya zaidi unataja pesa kabisa kiasi kwamba haujali kama unavunja haki za raia wako hivyo wewe ni mshenzi ambaye unanunulika. Haufai kuishi”
“Hapana nisikil….” alipigwa ngumi kwenye shingo yake ikavunjika akafa pale pale, kisu kidogo ambacho alikuwa nacho Jabari kwenye mkono wake alikirushia nje kwenye dirisha, treni ikiwa inaendelea kutembea kwa kasi kubwa. Alisogea mlangoni na kugundua mlango uliegeshwa tu hivyo akaufunga na kurudi ndani ya choo tena, alisogea pale ambapo maji yalikuwa yanaendelea kutoka akanawa kuitoa damu ambayo ilikuwa kwenye mkono wake mmoja. Alisimama kwa muda wa dakika tano akiwa anajiangalia kwenye kioo kwa umakini mno, maisha yake yalikuwa yamebadilika isivyokuwa kawaida, kutoka kuwa mwandishi wa habari wa kawaida tu mpaka kuwa muuaji wa kutisha namna hiyo kiasi kwamba anaweza kuua mtu na ikaonekana kuwa jambo la kawaida tu kwake.

Baada ya kunawa alilifungua lile begi ambalo alikuwa amepewa na yule mwanaume akiwa kwenye kituo cha treni. Begi lilikuwa na namba maalumu za kufungulia ambazo alikuwa nazo kwenye kichwa chake na jambo hilo alilifanikisha kwa ukubwa. Baada ya kulifungua alikutana na vitu viwili ambavyo vilimshtua kiasi kwamba akameza mate kwa shida na kuangalia kule mlangoni kama kuna mtu alikuwa yupo karibu, baada ya hapo aliyageuza macho yake kwenda nje akagundua kwamba ulikuwa usiku mkali na wakati huo walikuwa wanapita kwenye pori zito. Baada ya kuridhika na hali ya usalama, aliyarudisha macho yake tena kwenye lile begi kuangalia vizuri vitu viwili ambavyo aliviona.

THE DARKNESS OF AN ANGEL, aliyaona maandishi hayo kwenye cover kubwa ya kitabu ambacho kwa muda mrefu alikuwa akikipigia kampeni kwenye mitandao. Hata yeye licha ya kukinadi sana kwa muda mrefu lakini ukweli ni kwamba hakuwahi hata siku moja kukiona hicho kitabu kwa macho yake wala kukishika bali alikuwa anapewa taarifa za kuzisambaza na kile ambacho angetakiwa kuwapatia wafuasi wake. Alibaki ameganda akiwa anakitazama kwa umakini, kilikuwa na cover ile ile ambayo hata yeye alikuwa nayo lakini ilikuwa imeongezewa maneno upande wa juu kabisa ambayo yalikolezwa kwa rangi ya damu kukiwa na maandishi yaliyo someka THE ODYSSEY OF GAVIN LucA.
Alijikuta moyo wake unamuenda mbio isivyokuwa kawaida, hata yeye hapo ndipo alijihakikishia kwamba ni kweli ndani yake huenda kulikuwa na historia ya maisha ya Gavin ambaye mpaka wakati huo hakuwa akijulikana alikuwa wapi lakini sio yeye tu hata familia yake haikuwa inatambulika mpaka wakati huo ilikuwa ipo wapi na kwa sababu ipi ilipotea kwa muda mrefu bila taarifa yoyote ile. Lakini jambo ambalo lilimshangaza zaidi ni kwamba safari yake hiyo ilikuwa ni kwenda kukutana na GHOST mtu aliye daiwa kuishi gizani kwa muda mrefu ila ndiye alikuwa kiongozi wa watu hao ambao alijikuta anafanya nao kazi kwenye mazingira ya kutatanisha bila kuwa na taarifa nyingi za kutosha kuhusu wao wala kuyajua makazi yao yalikuwa yapo wapi.

Ukurasa wa kumi na moja unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA KUMI NA MBILI
SONGA NAYO................

Alikuwa akiogopa kwa sababu hakuwa na taarifa sahihi juu ya huyo GHOST, hakuwa anajua kabisa kama huyo GHOST ndiye alikuwa Gavin mwenyewe au alikuwa mtu mwingine. Je kama alikuwa Gavin, kwa historia ya bwana huyo ilivyokuwa ya kutisha angeongea naye nini? Na kama sio yeye basi angekuwa ni nani huyo haswa? Maswali yake ambayo alikuwa anajiuliza mwenyewe yalimfanya aanze kutokwa na jasho bila hata yeye mwenyewe kupenda.
Mikono yake ilikuwa inatetemeka wakati anakigusa kitabu hicho ambacho hata sababu za kuandikwa kwake hakuwa anazijua zaidi ya zile ambazo aliambiwa na alikuwa ana uhakika kwamba watu hao hawakuwa wamemwambia ukweli, na kama lengo lilikuwa ni kukiachia, ni kwanini baadae walighairi halafu yeye ndiye akapewa kukipeleka kwa kiongozi wa watu hao? Kwamba yeye aliaminiwa sana? Jibu likawa hapana, hakuwa na uhakika huo kwa sababu hata mwanaume ambaye alikutana naye Tazara angeweza kukipeleka mwenyewe, sasa kulikuwa na sababu zipi nyuma yake na akaruhusiwa hata kuufungua ule mzigo? Alikosa kabisa jibu ndipo akaamua kuhamishia macho yake kwenye kitu cha pili ambacho alikiona.

Kitu cha pili lilikuwa ni vazi, vazi jeusi ambalo kwenye kifua lilikuwa na nembo ndogo ambayo ilimtaka mtu kuwa karibu ili aweze kuiona vizuri. “GL” ndiyo ilikuwa nembo hiyo ambayo aliiona mbele yake ikiwa na alama ndogo kama upanga unao waka moto, alitumia dakika nzima mpaka kuja kugundua kwamba hiyo nembo kilikuwa ni kifupi cha muasisi wa hayo mambo Gavin Luca na huenda wakati wa kukutana na kiongozi huyo, alitakiwa kuwa ndani ya hilo vazi. Hakuona kitu kingine humo ndani zaidi ya kikaratasi kidogo ambacho kilikuwa na taarifa za wapi alipo takiwa kuwepo kikiwa na ramani yake pembeni hivyo akaamua kulifunika begi hilo na kuirudishia barakoa yake usoni baada ya kujisafisha na kufuta jasho ambalo lilimnyima utulivu. Aliivuta pumzi kwa shida kisha akaufungua mlango wa humo ndani na kuweza kutoka lakini hakurejea tena kwenye behawa lake.

Wakati kunaanza kupambazuka zilisikika kelele, kelele ambazo zilitoka kwa bwana mmoja ambaye alikuwa ameenda uani kuweza kujisaidia, alitoka akiwa anakimbia na kuanguka huku akitoa kilio kikali kisichokuwa cha kawaida kiasi kwamba kilianza kuwatoa watu kwenye mabehewa yao na kusogea nje ili waweze kuona jambo ambalo lilikuwa linaendelea ama kufanyika.
Zile kelele zake ziliwatoa askari ambao walikuja mkuku mkuku wakiwa na silaha zao tayari kwa kukabiliana na hatari yoyote kuhakikisha watu wapo salama ndani ya treni. Bwana yule alidakwa na askari mmoja wakati amejikwaa akiwa anarukia behewa lingine wakati treni inayumba. Alikuwa anahema huku akiwa analalamika kudai kwamba anaogopa, alionekana hakuwahi kukutana na jambo kama hilo kabla kwenye maisha yake.

Alitulizwa na askari lakini hakuongea jambo zaidi ya kunyoosha kidole chake kuelekea pale ambalo kilikuwepo choo, jambo hilo liliwafanya maaskari kujongea pale taratibu wakihisi kwamba huenda kulikuwa na uvamizi lakini baada ya kufika pale hata wao hawakuamini, walibaki wanashangaa wasijue jambo lile lilifanyika muda gani.
Mwili wa mwanaume mmoja ulikuwa hauna uhai huku akiwa na majeraha kwenye sehemu kadhaa za mwili wake, maji yalikuwa mengi ndani na bado yalikuwa yanaendelea kutoka ni kwa vile tu mengine yalikuwa yanapitiliza chini ndiyo maana hayakujaa ila kama isingekuwa hivyo huenda yangesambaa kwenye sehemu kubwa ya treni kwa sababu yalionekana kutoka kwa muda mrefu kwani mhusika alionekana alikufa muda mrefu ambao ulipita kwa sababu alikuwa wa baridi.

Iliwazimu kumuita yule bwana ambaye alikuwa anakimbia kwa hofu ili aweze kuelezea tukio lile zima, yeye alieleza kwamba alikuwa ameamka muda ule na kuhitaji kwenda kupunguza uzito mwilini lakini ajabu baada ya kufika eneo lile alikutana na mlango ukiwa umeegeshwa tu huku maji yakionekana ndani hivyo moja kwa moja yeye alijua kwamba huenda aliyekuwa ameingia kwa mara ya kwanza alisahau kufunga koki ya maji ila baada ya kuingia ndani alikutaja na jambo la ajabu.
Mwili wa mtu ambaye alikuwa amekufa ndio ambao ulimfanya asiwe na utulivu, alishtuka na kuogopa kwa wakati mmoja hivyo kwake aliona njia bora ni kukimbia na kuanza kupiga kelele kwa sababu ya uoga ambao alikuwa nao. Bwana huyo alikuwa na wasiwasi kubwa mno na habari za tukio hilo zikaanza kusambaa kila kona ya treni jambo ambalo liliwafanya watu kuhitaji treni hiyo kusimama ili kila mtu aweze kushuka kwani hawakuwa na imani tena na treni hiyo lakini hilo jambo lisingewezekana kwa sababu polisi walitakiwa kufanya uchunguzi kwanza.

Kila mtu alirudishwa ndani ya behewa lake ili ufanyike upekuzi wa kujua huyo mtu aliuawa na nani na ni nani hakuwepo ndani ya hiyo treni. Jambo ambalo liliwapa hasira zaidi polisi hao ni baada ya kugundua kwamba yule ambaye alikuwa amekufa alikuwa ni askari mwenzao, hiyo haikuwa vita ya mauaji tu pekee bali vita ya mhusika na jeshi zima la polisi.

Baada ya uchunguzi mkali kufanyika, iligundulika kwamba kwanza kwenye treni ni mtu mmoja tu ambaye hakuwepo. Zilifuatiliwa taarifa zake bwana huyo baada ya kufuatiliwa utambulisho wake makao makuu ila kwa bahati mbaya hata kamera hazikuinasa sura yake halisi kwa sababu alivaa barakoa muda wote ambao aliingia TAZARA. Bwana huyo hata majina ambayo alijitambulisha nayo hayakuwepo kabisa kwenye mfumo wa utambulisho wa taifa hali ambayo ilizalisha maswali mengi kwamba alikuwa ni nani na kwanini alimuua yule mtu ambaye alikuwa ni askari? Ndipo wakaanza kufautilia video za kwenye cctv.
Bwana yule wakati anaingia Tazara hakuwa na kitu mkononi lakini ndani ya treni aliingia na begi dogo ambalo hawakujua alilitoa wapi na ndani yake kulikuwa na nini hasa. Baada ya kuchunguza kwa umakini ilionekana kwamba kuna mtu ambaye alikutana naye pale Tazara ambaye ndiye alimpatia begi na walifanya mazungumzo ya muda mfupi kisha bwana huyo akatoka, maana yake kulikuwa na mpango mkali kabla ya kufanikisha jambo hilo. Sasa ni kipi kilikuwa kinaendelea? Kikawa kitendawili kingine kisicho na majibu halisi.

Jambo ambalo lilifanyika kwa wakati huo ikawa ni kutafuta sura ya bwana yule ambaye aliacha begi pale Tazara kama kungekuwa na mfanano wake lakini sura yake haikutoa taarifa zozote zile ikiwa ni ishara kwamba bwana huyo hakuwahi kupiga picha yoyote kabla na wala hakuna taarifa zozote ambazo ziliwahi kupatikana kumhusu yeye, alikuwa ni kama Ghost ambaye hatambuliki kama yupo hai. Jeshi la polisi likawa na kesi nyingine mkononi ambayo mbele yake ilikuwa na kiza kinene huku watu wakiwa wanataka taarifa kwani walikuwa na wasiwasi na usafiri huo wa treni kwamba huenda mhusika alikuwa anahitaji kuweza kulipua jambo ambalo lilizalisha mashaka mengi.

Utata huo ambao ulizaliwa na kuibuka kwa jeshi la polisi haukuwa na majibu, wakati huo kulikuwa na kesi kubwa ya mauaji ambayo yalitokea mahakamani hivyo Jopa Magoma alikuwa anatafutwa kila kona.
Jambo hilo likiwa hata halijaisha ndipo yanaibuka mengine ya bwana huyo kufanya mauaji ya askari polisi ndani ya treni, mambo hayo yalikuwa yamepotea kwa miaka mingi mno, kwa muda mrefu ndani ya Tanzania matukio hayo ya kutisha yalipotea na kufanya watu kuishi kwa amani na kujisahau lakini ghafla kutoka mahali kusiko julikana, zile nyakati za giza ambazo ziliwahi kuwepo huko nyuma zilianza kujirudia taratibu na kuufanya umma kuanza kugubikwa na wasiwasi na hisia nzito ila hilo halikufanya bwana huyo kupatikana. Alikuwa amepotea Jabari Malik, mwandishi wa habari ambaye alijikuta anaingia kwenye matatizo mazito na serikali kwa sababu alisimamia kile ambacho aliona ni sahihi na wananchi wanastahili kukijua ila haukuwa mwisho mzuri kwake japo wahusika pia hawakuwa sahihi kumtafsiri kijana huyo kwani alionekana kuwa mtu tofauti na ambavyo walikuwa wakimjua.

Ukurasa wa kumi na mbili unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA KUMI NA TATU
SONGA NAYO................
********
Hisia zilimpa ishara kwamba alikuwa hai lakini mwili uligoma, ni wakati ambao alikuwa anasikia kelele kwa mbali ambazo hakujua kama ni za duniani ama upande wa dunia nyingine ambako alikuwepo kwa wakati huo kutokana na yeye binafsi alivyokuwa akiamini. Sauti hizo alikuwa akizisikia kama watu wakipishana kuongea haraka haraka huku wengine wakisisitiza kwamba alikuwa ni yeye mwenyewe hivyo alitakiwa kuwahishwa hspitali. Yote hayo yalikuwa ni kama ndoto ila ulikuwa ni uhalisia wenyewe.
Nje ya jengo kubwa la kituo kikubwa cha habari cha taifa ndiyo sehemu ambayo ilikuwa na hizo kelele ambazo mtu mmoja alikuwa anazihisi kwa mbali sana. Jaji wa mahakama kuu alikutwa eneo hilo asubuhi na mapema akiwa ametupwa, ni wale wafanyakazi ambao waliwahi sana ndio ambao walimkuta hapo na mshtuko huo uliwajaza watu kadhaa ambao wengine walikuwa wakipita karibu na maeneo hayo kila mtu akihitaji kumuona kiongozi huyo mkubwa kipindi ambacho gari ilikuwa inasubiriwa ili kuweza kumpeleka hospitali lakini hata polisi walikuwa wamearifiwa juu ya tukio hilo hivyo walikuwa wanakuja kwa wingi ndani ya hilo eneo.
Sehemu hiyo ilijaa kamera kwa muda mfupi kiasi kwamba kila kitu kilikuwa live na kwa wale ambao walibahatika kuwasha televisheni zao mapema basi walikuwa wakilishuhudia jambo hilo moja kwa moja. Mheshimiwa hakuonekana kuwa fahamu zake, alihitaji kupata msaada wa haraka lakini jambo hilo lilikuwa gumu kwa sababu watu wengi walikuwa wamezingira ndani ya hilo eneo mpaka pale ambapo polisi walifika na kuwatawanya raia hao kisha wakaondoka na jaji kumuwahisha hospitali kwa ajili ya usalama wake.
Ilikuwa ni habari nyingine yenye gumzo kubwa watu wakiwa kwenye vilio vya msiba mzito ambao ulitokea mahakamani, msiba ambao ulimtoa raisi hadharani akatangaza siku saba za maombolezo na bendera kupepea nusu mlingoti kwa ajili ya kuwaenzi watanzania wenzao lakini wakati huo jeshi la polisi likifanya kazi kubwa ya kuweza kuwatafuta wahusika ambao walitenda tukio hilo.

Kupatikana kwa jaji kulizua taswira mpya tena ndani ya taifa, mtu huyo ndiye pekee ambaye alikuwa hai mpaka wakati huo kwa wale wote ambao walikuwepo ndani ya mahakama hivyo wananchi wengi walijazana nje ya ile hospitali wakiwa wanahitaji kupata majibu kutoka kwa bwana huyo. Hata wale ambao walikuwa mbali na eneo lile, walizua taharuki kwenye mitandao ya kijamii wakitaka kupata taarifa kwamba yeye alikuwa wapi, kwanini ni yeye pekee alikuwa hai, hao watu ambao walimteka ni akina nani na walikuwa wanahitaji nini kwake! Ni maswali ambayo waliamini kwamba mtu pekee wa kuweza kuwajibu alikuwa ni jaji ila kwa wakati huo lilikuwa ni jambo ambalo halikuwa linawezekana mpaka pale ambapo afya yake ingetengamaa.

Yalipita masaa mawili tangu awe kwenye ile hali akiwa anapata matibabu, hatimaye aliyafungua macho yake baada ya muda kuwa yamefumbwa. Kuyafungua kwake ndiko ambako kulimtaarifu kwamba alikuwa sehemu tofauti na ile ambayo alikuwa na wale mabwana kwa mara ya kwanza, sehemu ambayo alikuwepo wakati huo ilikuwa ni hospitali. Alitoa tabasamu hafifu kwenye uso wake lakini wakati anafanya hilo alishtuka baada ya kuona anatazamana na mtu ambaye naye alitabasamu.
Alikuwa nesi ambaye bila shaka alikuwa humo ndani kuhakikisha mheshimiwa anakuwa salama na anarudi kwenye hali yake.
“Nimekaa kwa muda gani humu ndani?”
“Ni masaa mawili na nusu mpaka sasa mheshimiwa”
“Kuna mwanafamilia wangu yeyote ambaye amefanikiwa kuja kuniona hapa?”
“Hapana mheshimiwa”
“Hawana taarifa au?”
“Taarifa nadhani wamechelewa kuipata na taarifa ambayo tumeipata ni kwamba mkeo yupo njiani anakuja saivi”
“Okay, kuna jambo gani huko nje nasikia makelele mengi”
“Ni wananchi wamejaa wakiwa wanatamani kupata majibu kutuka kwako”
“Majibu kutoka kwangu?”
“Ndiyo mheshimiwa, lile tukio ambalo lilitokea mahakamani limeacha hisia nzito sana kwa watu hivyo wanatamani kujua kwamba wale watu ni akina nani, wanatamani kufahamu kwamba kwanini ni wewe tu pekee ndiye ambaye umefanikiwa kuwa hai mpaka wakati huu? Lakini wengi zaidi wanataka kujua kile ambacho kimetokea ukiwa huko kwa hao watu”
“Mhhhhh nilitamani kuona watu wakifurahia kuniona nikiwa hai lakini jambo la kushangaza kati yao wote hakuna hata mmoja ambaye amefurahishwa na mimi kurudi nikiwa hai zaidi wote wanataka kuanza kunishushia lawama, kuna wakati kuwatumikia wananchi inataka moyo sana kwa sababu unayatoa maisha yako halafu hata hawajali wanakuja kutafuta sehemu wakupe lawama” nesi hakuwa na jambo la kuongezea mbele ya mheshimiwa zaidi alimuacha ateme nyongo yake akiwa anainuka kabisa kuelekea dirishani kuangalia upande wa nje kilichokuwa kinaendelea akiwa juu ya ghorofa.
“Mheshimiwa kuna mgeni wako”
“Mgeni?”
“Ndiyo”
“Muda huu?”
“Ndiyo”
“Anajua kama sipo vizuri?”
“Ndiyo ila amesema kwamba ni dharura hivyo ni lazima muonane” alijifikiria sana mheshimiwa lakini hakuonekana kuwa na namna nyingine zaidi ya kumruhusu mtu huyo aweze kuingia. Ndani ya wodi ambayo yeye alikuwepo, aliingia bwana mmoja ambaye alikuwa kavaa suti ya blue na tai yake nyekundu, alikuwa mwanaume shupavu kwa kumuangalia kwa macho ya kawaida lakini sura yake haikuwa na utani hata kidogo.
“Liam Sebastian, nakufahamu wewe” aliongea jaji akiwa anasogea kwenye meza sehemu ambayo ilikuwepo juisi safi ya matunda na kuimimina.
“Shukrani kwa kuwa na kumbukumbu na mimi mheshimiwa na unisamehe kwa kukuingilia kipindi ambacho huenda ulitakuwa kupumzika lakini nina imani unaelewa itifaki za kazi zetu, sina namna”
“Usijali kuhusu hilo, nakumbuka vizuri ulipambana sana kwenye kesi ya Jopa, ni wewe ambaye upelelezi wako ulifanya bwana yule apatikane na makosa na hatia ambazo moja kwa moja zilitakiwa kumfanya anyongwe mpaka kifo kwa ule ushenzi mkubwa ambao alikuwa ameufanya kwenye maisha yake ambao kiuhalisia ni kwamba ulikuwa kinyume kabisa na ubindamu”
“Asante kwa kulitambua hilo mheshimiwa lakini hii kesi sistahili kupewa pongezi kwa sababu ni kama ndo kwanza inaanza upya baada ya mhusika kutoka kwenye mikono ya jeshi la polisi na kufanya yale mauaji na utekaji mbele ya mahakama yako tukufu. Hiyo ndiyo sababu ya msingi ambayo imenifanya mimi kuwepo hapa muda huu”
“Mhhhh kwanini usingeniacha nikapumzika kwanza kwa hilo?”

“Tupo nje ya muda mheshimiwa, tangu nimepata taarifa za wewe kupatikana nimewahi hapa hivyo nilikuwa nasubiri tu ufumbue macho yako ili tuweze kuongea kuhusu hili kwani ni mhimu sana ukizingatia hata wananchi wanatamani kuusikiliza upande wako wa stori upoje. Ni jambo ambalo linashangaza kwa sababu ukiangalia mtiririko wa yale matukio inaonekana kabisa bwana yule alikuwa pale kwa ajili ya kukupata wewe halafu kirahisi namna hii anakurudisha ukiwa hai tena kwa muda mfupi? Hili linashangaza mheshimiwa”
“Kwahiyo na wewe ulitamani nirudi nikiwa kama maiti?”

“Sina maana hiyo, nimekuwa kwenye hii kazi kwa muda sasa hivyo hapa naongea na wewe uhalisia ambao ndio ukweli wenyewe hata wewe nina imani unalijua hilo, sio rahisi muuaji ambaye amekupata kwa gharama kubwa namna ile akuache tu kirahisi kama hivi. Kama hautajali unaweza ukanishirika kwenye huu upande wa hiyo simulizi yako ambayo upo nayo mpaka wakati huu”

Ukurasa wa kumi na tatu unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA KUMI NA NNE
SONGA NAYO................

“Mhhhh Sebastin mbona umekuja kwangu kama mimi ndiye mtuhumiwa wakati mimi ndiye ambaye nilitekwa?”
“Hizi ni itifaki za kazi, wewe sio mtuhumiwa ila wewe ndiye ambaye umekumbana na mtu huyo hivyo kupitia wewe kuna uwezekano ukawa na msaada mkubwa wa kuweza kumpata kwa sababu wewe ndiye ambaye ulikuwa naye kabla ya kukuweka huru tena”
“Una miaka mingapi bwana mdogo?”
“Sioni hata ya miaka kuhusika kwenye hili mheshimiwa”

“Mimi nikiwa na umri kama wa kwako nilikuwa nafanya kazi kubwa ya kulilinda taifa hili ila kwa bahati mbaya nilikuwa naishi nyuma ya kamera hivyo ni watu wachache tu ndio ambao walikuwa wanatambua kuhusu jambo hilo. Lakini maisha yanabadilika kwa sababu baadae nilikuja kugundua kwamba nilikuwa natakiwa kufanya zaidi ya pale, muda sio rafiki kabisa kwenye maisha ya binadamu huenda kama ningefanya zaidi ya pale leo hii mimi nisingekuwa hapa ila huenda pia nigekuwa kaburini.
Kuwa makini na kila jambo ambalo nilikuwa nalifanya kwa wakati ule ndiko ambako kumenipa nafasi ya kuishi kwa muda mrefu tofauti na wenzangu wengi ambao nilikuwa nao kwenye hii safari. Bwana mdogo mimi ni mtu wa nne kwa ukubwa ndani ya taifa hili kwenye nafasi za uongozi wa juu. Ukimtoa raisi, makamu wake, waziri mkuu ambaye kimsingi sina uhakika kama ni mkubwa kwangu pamoja na katibu mkuu kiongozi ambaye naye hana mamlaka yoyote kwa upande wangu basi nakaa mimi kwenye hiyo nafasi. Kisha baada hapo ndipo wanafuata watu kama spika wa bunge na wenzake huko chini.
Kwa hizo sifa zangu ambazo nimekupatia hapa unaona ni sawa mimi kuhojiwa na kijana kama wewe hapo?” aliongea maelezo ambayo yalikuwa yamenyooka sana lakini yalikuwa na ukali wa kumaanisha ndani yake akiwa amemkazia macho mwanaume aliyekuwa anatambulika kama Liam Sebastian.

“Najua kwamba wewe ni jaji mkubwa zaidi ndani ya taifa hili, naelewa nafasi yako kubwa ambayo unayo ndiyo maana nimekuja hapa kwa heshima zote lakini tukiachana na jambo hilo, kwenye mstari wa kazi zetu hivi vyeo tunavivua kwanza kwa sababu hapa sijaja kama Liam bali nimekuja kwa mamlaka ambayo yananiongoza na kila jambo ambalo linaendelea humu ndani natakiwa kuliandika kwenye ripoti kisha niipeleke sehemu husika na ripoti huyo itatumika kama ushahidi baadae ila naona sio chaguo sahihi kugoma kunijibu kwa sababu kama nikiandika kwamba umenigomea na hili likajulikana nadhani utakuwa kwenye nafasi ngumu zaidi mheshimiwa”
“Kama nimekusikia vizuri ni kwamba unanitisha?”
“Hakuna mahali nimekutisha ila mimi binafsi najaribu kuhakikisha naifanya kazi yangu kwa usahihi”

“Mhhhh, unatakiwa kuziangalia sana hatua zako bwana mdogo. Jambo moja ambalo vijana wa umri wako huwa wanachelewa kulifahamu ni kwamba mfumo huwa haupendi mashujaa ambao wanakuja hadharani mbele ya viongozi wakubwa kama mimi na kuleta hizo tambo zako. Unaweza ukaja kulikumbuka hili ukiwa umechelewa, hii haitakuwa nzuri sana kwa upande wako”
“Hilo nalielewa mheshimiwa na nilisha likubali tangu siku ambayo nilikula kiapo cha kulitumikia taifa hili na katiba ya nchi yangu. Nadhani sasa ni wakati wa kunijibu maswali ili uwe na muda mzuri wa kupumzika na familia yako, ninavyotoka hapa wananchi wanaenda kutangaziwa kwamba majibu yao yamepatikana kwa hivyo watatakiwa kurudi makwao kusubiri taarifa sahihi kwahiyo naomba ujitahidi kuyakumbuka matukio yote kwa usahihi kiongozi” kijana huyo alionekana kujiamini isivyo kawaida lakini ujio wake ndani ya hilo eneo bila shaka ulimtengenezea adui mpya bila yeye kujua.

Jambo ambalo alikuwa analifanya kwa wakati huo ni kwamba alikuwa sahihi kabisa, alikuwa sahihi kwa kila kitu kwa sababu kwenye jambo la mhimu kama hilo vyeo vilikuwa vinawekwa kando kwanza kuhakikisha taifa lipo salama lakini habari hizo hazikuwa njema kwa wakubwa kwa sababu walitaka kujitawala na mambo walitaka yaende vile ambavyo walikuwa wanataka wao.
“Unataka tuanzie wapi?” aliongea mheshimiwa akiwa na hasira ambazo aliamua kuzimezea ndani, lazima angezitumia baadae kwa kijana huyo.
“Kuanzia wakati unatekwa na yote ambayo yalikwenda kutokea huko ambako ulikuwa hadi dakika ya mwisho unakuja kutupwa nje ya ofisi zile za habari”
“Hili tukio unarekodi?”
“Ndiyo mheshimiwa” aliuliza hivyo ili asije akaingizia maneno mabaya katikati ya vitisho ambayo yangeuonyesha ule upande wake mwingine ambao hakutaka wananchi waweze kumuona nao. Na wakati anajibiwa hivyo mwanaume huyo alibonyeza rasmi kamera ambayo ilikuwa kwenye shati yake hivyo tukio lote hilo lilikuwa linarekodiwa ikiwa ni ishara kwamba kila ambalo angelisema mheshimiwa huyo lingetumika kama ushahidi wa maelezo kwa baadae, alikuwa mtaalamu, hakuwa mjinga kuharibu hayo mambo hivyo aliketi kitandani kwa ustadi ili aweze kuyadadavua ambayo yalikuwa nyuma ya pazia.

“Kwanza naweza kuitumia nafasi hii kumshukuru kila mmoja ambaye kwa namna moja ama nyingine alifanikisha kuniombea na kuhakikisha narudi nikiwa mzima kabisa wa afya. Kwangu hii ni zawadi bora mno lakini jambo la pili ni masikitiko yangu makubwa juu ya jambo ambalo lilitokea ndani ya mahakama yangu. Kila jaji anapenda kuona haki inatendekea mahakamani, mahakamani ni sehemu ya watu kupata haki zao lakini kwa wale ambao wameliasi taifa ile ni sehemu ya kuhakikisha wanapata zile adhabu ambazo wanastahili ili kuwa funzo kwa watu wengine.

Lakini kile ambacho kilitokea pale kinasikitisha, ni jambo la aibu kuona hata baadhi ya askari ambao taifa liliwaamini wakiwa wanaisaliti nchi waziwazi namna ile, lile ni jambo baya zaidi kuwahi kulikumba taifa letu kwa zaidi ya miaka kumi na tano ambayo imepita. Wakati nashuhudia ule ukatili nilikuwa nayawaza maisha ya wale wanyonge wananchi ambao hawakuwa na hatia yoyote, akili yangu ilipata mawazo makali na fikra za mbali ambazo ziliufanya moyo wangu kububujikwa na machozi.
Wale watu kwa namna yoyote ile hawakustahili kufa kwa sababu hawakuwa na hatia wala kosa lolote lile lakini yule mshenzi ambaye alitakiwa kufa ndiye ambaye aliufanya ushenzi huo nina imani jeshi letu litakuwa limewapata watu wa baradhuli yule na kama hawajawapata basi wanatakiwa kutolala ili wahakikishe kwamba watu hao wanapatikana kwa gharama na kwa namna yoyote ile kwa sababu wameliingiza taifa letu kwenye majonzi mazito mno ambayo huenda yataishi miaka na miaka bila kufutika ama kupata mtu wa kuweza kuyafuta.

Kama ambavyo kila mtu anakuwa na shauku ya kutaka kujua jambo ambalo lilitokea basi hata mimi wakati nazinduka kutoka kwenye usingizi mzito wa kifo nilitaka kujua, pindi akili zangu zinarudi kwenye hali yake ya kawaida nilitamani kuonana na bwana yule niweze kumhoji kwamba ni kwanini aliufanya ukatili wa namna ile ingali alikuwa mkosefu na sheria ilitakiwa kumuadhibu? Nilihitaji anijibu swali hilo akiwa ananitazama usoni, nilitamani kujua alijisiaje baada ya kuua zile nafsi ambazo zilikuwa pale ila nilijua hilo lisingewezekana.
Lakini kubwa zaidi nilitamani kujua sababu za mimi kubakishwa hai, kama aliwaua watu wote mbele ya mahakama ile maana yake hata mimi alitakiwa kuniulia pale pale ndani bila kuruhusu nitoke nje ya lile eneo, sasa nilishangazwa na mimi kubakia huru nikiwa nazijutia nafsi zile ambazo zilikufa bila kuwa na hatia. Nilijiona kuwa mhusika na kujikuta na hatia ambayo mpaka sasa inanitesa, kuwa jaji ni miongoni mwa kazi ambazo zinaenda kuniachia historia ya ndoto mbaya kwenye maisha yangu ila sina namna nyingine naweza kuifanya zaidi ya kukubali yote haya ambayo yanatokea.

Kwa bahati mbaya sikufanikiwa kabisa kuonana na huyo bwana, sikufanikiwa kumuona tena Jopa mpaka wakati huu ambao nimejikuta nipo hopsitali nikipatiwa matibabu, kila nikikumbuka yote ambayo yalitokea, moyo wangu unabaki unatetemeka, sina amani wala furaha, sina uhakika na usalama wa familia yangu kwa sababu mimi binafsi mpaka wakati huu najihesabia kama mfu.
Watu wale baada ya kunipata mimi walinipeleka sehemu ambayo sijui ni wapi, eneo ambalo nilishtuka nikiwa sina nguo hata moja kwenye mwili wangu ndipo akaja bwana mmoja ambaye sikuwahi kumuona wala simfahamu. Bwana yule nilimuomba kuonana na Jopa ili nimuulize maswali na nimsihi ajisalimishe mwenyewe lakini sikupewa hiyo nafasi kwa sababu jibu ambalo alinijibu bwana yule ni moja ambalo lilinishtua mpaka pale ambapo alinionyesha video ya mjongeo ndipo nikaja kuiamini.

Ukurasa wa kumi na nne unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
HADITHI: THE ODYSSEY OF GAVIN LUCA (LIONELA)
MWANDISHI: FEBIANI BABUYA
STORYTELLER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP: 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+

********************
UKURASA WA KUMI NA TANO
SONGA NAYO................

Bwana yule alinipa taarifa kwamba Jopa amekufa, Jopa alikuwa amepigwa risasi kumi kwenye kifu na kwenye kichwa jambo ambalo mara ya kwanza lilinichanganya kwa sababu yeye ndiye alikuja pale mahakamani na kuweza kuutenda ule ushenzi halafu naambiwa kwamba amekufa, kivipi tena? Ndipo yule bwana akanipa maelekezo kwamba yule alitumwa kufanya kazi ya kunikamata mimi tu baada ya hapo hakuwa na kazi kwao tena ndiyo maana wakamuua.

Bwana yule aliendelea kujipambanua kwa kuniambia kwamba Jopa kuwa hai ungekuwa kama ushahidi wa wao kupatikana, walikuwa wana imani kwamba huenda kuna siku angekuja kufanya kosa mamlaka zikampata hivyo kama angepatikana basi ingekuwa ni hatari kwao huenda angesema siri zao, ili kuondoa huo utata wakaamua kuyabeba maisha yake. Jambo hilo kwa mara moja lilinishtua na kunikera, lilinikera kwa sababu yule mshenzi hakutakiwa kufa kirahisi namna ile, alitakiwa kuitumika adhabu yake kubwa kwa ushenzi ambao ameufanya ila sikuwa na uwezo wa kuzuia jambo lile kutokea kwa sababu mimi mwenyewe niliamini kwamba nilikuwa naenda kufa” mheshimiwa jaji alitulia kidogo akiwa ameinama kwa masikitiko kisha baada ya hapo akauinua uso wake ili aendeleze yale maelezo ambayo yalisalia.

“Baada ya hapo ndipo alihamia kwenye sehemu ya pili, sehemu ambayo nilikuwa nahitaji sababu ya wao kunikamata mimi kiasi kwamba kukamatwa kwangu ikawa sababu ya kumuua mapaka mtu wao ambaye alionekana kutengenezwa kwa gharama lakini pia hilo lilienda sawa na kuhitaji kuwafahamu kwamba wao ni akina nani. Jambo ambalo aliniambiwa yule bwana lilinishtua sana, nina uhakika hata watanzania wote ambao watafanikiwa kulisikia litawashtua kwa kiasi kukubwa kama ambavyo ilikuwa kwangu.
Bwana huyo alinitaka mimi nimpe taarifa za wapi alipo Gavin Luca na familia yake. Niliogopa mno kwa sababu hizo ni taarifa za zaidi ya miaka ishirini ambayo imekwisha kupita, Gavin Luca kila mtu anajua kwamba alikufa na kila sehemu ilithibitishwa hivyo lakini mwanaume huyo nilipo mpatia hilo jibu alionekana kuwa na hasira huku akinihakikishia kwamba bwana huyo yupo mzima wa afya kabisa hivyo nilitakiwa kumpatia maelekezo.

Baada ya kuona anamaanisha sana jambo lile ikabidi kwanza nimuulize kwanini anahisi kwamba mimi najua ilipo familia hiyo na jambo la pekee ambalo alinijibu ni kwamba kuna taarifa mahali zilimwambia kwamba mimi kama jaji nilikuwa na taarifa hizo kwa sababu nina taarifa nyingi mezani. Binafsi nilimwambia kwamba ni kweli kabisa kwamba nina taarifa nyingi lakini sijui kitu kuhusu bwana huyo na sijui lolote pia kuhusu familia yake kwakuwa familia hiyo ilipotea kwa zaidi ya miaka ishirini sasa na serikali ilifanya jitihada za kuitafuta lakini haijawahi kufanikiwa kujua mahali ambapo wapo watu hao.
Licha ya maelezo hayo yote bado alionyesha msimamo wa kwamba familia hiyo ilikuwa ipo mahali na serikali inajua hivyo inawalinda watu hao, akafika mbali na kudai kwamba hata Gavin Luca bado yupo hai ila amejificha mahali ambapo anahisi kwamba hawezi kupatikana hivyo kunikamata mimi walikuwa wanatoa ni onyo kwa serikali kuhakikisha inawapatia majibu sahihi juu ya taarifa hizo.

Kutekwa kwangu walikuwa wanataka kuionyesha serikali kwamba wakitaka muda wowote wanaweza kumpata kiongozi yeyote yule wa serikali na wakamuua. Amedai kwamba muda mwingine hawatafanikiwa kunirudisha nikiwa hai tena bali nitakuwa maiti lakini pia walikuwa na watu wao ambao waliwapandikiza kwenye ulinzi wangu wa nyumbani hivyo hata familia yangu haitakuwa salama tena baada ya jambo hili ambalo limetokea kuanzia siku ya jana mpaka leo hii.

Lakini hawajaishia hapo, wamesema kwamba kuanzia sasa yataanza kufanyika mauaji ya watu wengi kwenye maeneo tofauti mpaka pale ambapo watapata taarifa juu ya ilipo familia hiyo na mimi nimeachwa hai kama mjumbe wa kuweza kufikisha malalamiko yao kwa taifa zima na vyombo husika vya mamlaka kuhakikisha wanamtafuta mtu huyu Gavin Luca na familia yake mpaka wampate ndipo wao wataweza kuondoka kabisa ndani ya taifa hili na kwenda mbali ila kama jambo hilo litashindikana basi itakuwa ni hasara kubwa kwetu kwani kuna uwezekano tutawapoteza watu wengi kwa muda mfupi ambapo itakuwa historia mbaya zaidi ya ile ambayo ilitokea kwenye mahakama yangu.
Watanzania wote kwa sasa tunatakiwa kushikamana na kuwa wamoja, watu hawa wametoka sehemu ambayo haijulikani na baadae wameanza kututishia kwenye taifa ambalo lina ulinzi bora na amani ambayo tumeilinda miaka na miaka hivyo hatutaweza kuruhusu wapuuzi wachache waje kuiharibu, hawa watu ni lazima wapatikane na wapate adhabu ya mauaji ambayo wameyasababisha kwenye taifa letu bora.

Mbali na hilo pia natoa rai kwa vyombo vya usalama kuhakikisha kwamba zitafutwe taarifa za huyu mtu wa kuitwa Gavin Luca na familia yake. Familia hii pia ni moja kati ya familia ambazo zimehusika kwenye uhalifu mkubwa mno na uharibifu amani wa muda mrefu ambao uliliweka taifa gizani kwa takribani miaka kumi. Hii ndiyo familia ambayo ilisababisha jaji mkuu Emilia Clark kupoteza maisha, hii ndiyo familia ambayo ilisababisha shirika letu la kijasusi la TIGI kuyumba kwa kiwango kikubwa.
Ni hii familia ambayo ilisababisha mkurenzi wa shirika hilo kuuawa pamoja na majasusi wanne wa shirika hilo kupoteza maisha. Familia hii ilihusika kwenye mauaji ya makamu wa zamani wa raisi, walimuua mkuu wa majeshi lakini mabaradhuli hawa wakaona haitoshi wakaamua kudiriki kumuua mpaka raisi wa Tanzania, kesi ambayo imebaki kuwa kesi isiyo na majibu kwa sababu tu mhusika alitangazwa kwamba amekufa lakini hata familia yake inatakiwa kulipa kwa hili.

Familia hii imeharibu kizazi chetu kwa ile biashara yao haramu ya madawa ya kulevya hivyo kuendelea kuwaangalia ni kama kulikosea taifa letu heshima, ni lazima waweze kulipa kwa hili ambalo limetokea. Sisi kama taifa hatutakiwi kuruhusu jambo lolote lile ambalo litatufanya turudi gizani kwa muda mrefu kwa mara nyingine hivyo tunatakiwa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha tunalimaliza hili.
Kama kuna mtu yeyote atakuwa na taarifa za watu hawa basi asisite kuzitoa polisi kwa ajili ya msaada zaidi. Lakini napenda kuitumia nafasi hii kuwapa pole watanzania wote na familia ambazo zimepoteza wapendwa wao, wote tumesikitishwa na jambo hili ila kwa sasa naomba Mungu azipokee nafsi zao, sheria itatenda haki kwa ajili yao. Mungu ibariki Tanzania” mheshimiwa alimaliza maelezo yake na kutulia, wakati huo Liam aliizima ile kamera yake kwani maelezo ya mhimu yote yalitolewa humo hivyo hiyo ndiyo ingekuwa taarifa ambayo ingewafikia wananchi moja kwa moja.

“Mheshimiwa maelezo yako ni kama haukuwa unanijibu maswali yangu, umeelezea kana kwamba unaongea na wananchi!”
“Nikikumbuka maelezo yako ya kwanza ulisema kwamba hili ndilo ambalo unataka kuwafikishia wananchi hivyo nadhani ulitakiwa kunishukuru kwa sababu nimekurahisishia kazi, wewe huoni hilo?”
“Hiki ulicho kizungumza ndicho ambacho kilitokea?”
“Whaaaat?”
“Swali langu umelisikia mheshimiwa”
“Bwana mdogo hivi unajiona nani labda?”
“Nafanya kazi yangu, sitakiwi kupeleka taarifa ambayo ina ukakasi, naweza kupoteza kazi yangu kiongozi”
“Kwahiyo umekaa hapa ukiamini kwamba mimi naweza kuipika hii taarifa?”
“Sina maana hiyo”
Nimekujibu maswali yako hivyo unaweza ukaenda, nahitaji muda wa kupumzika”
“Sawa mheshimiwa, asante kwa muda wako mimi naenda ila kama utahitajika kutoa ushirikiano basi ni matarajio yangu utakuwepo kwa ajili ya kuwapigania watanzania maana wewe ndiye wanakutegemea kupata mwafaka wa hili ambalo limetokea” alingea mwanaume huyo akiwa anapiga saluti kama heshima kwa kiongozi huyo mkubwa kisha akaanza kuondoka. Akiwa ameshika kitasa cha mlango ili aweze kutoka alisikia sauti ambayo ilimfanya asite kufanya jambo lile na kugeuka.

Ukurasa wa kumi na tano unafika mwisho.

FEBIANI BABUYA.
 
Usisahau kwamba hii simulizi ipo yote mwanzo mpaka mwisho..

Unaweza kuipata yote kwa pdf lakini wake wa Fasihinet pia kule ipo yote.
 

Attachments

  • downloadfile-286.jpg
    downloadfile-286.jpg
    80.9 KB · Views: 28

Similar Discussions

Back
Top Bottom