Chilojnr
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 308
- 1,354
Sehemu ya 01.
Nataka nicheze mpira, niwe na mafanikio makubwa, kama yule aliyekuwa anachezea Brazil ambaye uliniambia sana kuhusu yeye!” alisikika kijana mmoja akimwambia mwanaume aliyekuwa amekaa pembeni ya redio yake akisikiliza mechi kati ya Simba na Yanga iliyokuwa ikichezwa Uwanja wa Taifa.
“Nani?”
“Yule Mbrazil!”
“Oh! Unamzungumzia Pele?”
“Ndiyo! Nataka nicheze mpira kama yeye!”
“Ni jambo zuri, ila soma kwanza!”
“Kwani yule alisoma?”
“Hakusoma! Ila wewe utatakiwa kusoma sana!”
“Na niliwahi kusikia ulikuwa ukicheza mpira tangu shule, ikawaje ukaacha?”
“Nilivunjika mguu, nikauchukia mpira!”
“Basi mimi nitacheza! Na nitakuwa mchezaji mkubwa sana,” alisema kijana huyo.
Walikuwa watu wawili waliokuwa wakizungumza kama mzazi na mtoto. Kijana wa miaka kumi na tano aliyeitwa kwa jina la Amon, alikaa pembeni ya baba yake aliyeitwa Stefano huku wakisikiliza mechi iliyokuwa ikiendelea Uwanja wa Taifa na kuzungumza mawili matatu.
Amon alikuwa mtoto wa mwisho wa mzee Stefano, kipindi hicho walikuwa wakiishi Manzese Kwa Mfuga Mbwa. Maisha yao yalikuwa ni ya shida, hawakuwa na pesa, katika mtaa huo, wao walikuwa miongoni mwa zile familia zilizokuwa na maisha ya dhiki kipindi hicho.
Hawakuwa wakila milo mitatu kwa siku, walipokuwa wakila asubuhi, kula tena ilikuwa ni usiku. Mzee Stefano alikuwa akifanya kazi za ujenzi ndani na nje ya Jiji la Dar es Salaam. Kila siku asubuhi alikuwa akipitiwa na wenzake na kwenda Mbezi Beach ama Goba kwenye ujenzi kwani kwa kipindi hicho mji ulikuwa unatanuka na kulikuwa na nyumba nyingi zilizokuwa zikijengwa.
Miaka hiyo ya nyuma wakati akiwa kijana mzee Stefano alikuwa na ndoto za kucheza mpira, alihitaji kuyajenga maisha yake katika mchezo huo. Alikuwa mchezaji mzuri, aliyejua kulisakata kabumbu na kumfanya kuwa nyota wa Timu ya Lipuli ya Iringa iliyokuwa ikitamba miaka ya nyuma.
Kupitia mpira, mwaka 1985 akafanikiwa kukutana na msichana mrembo, Zuri Michael Wambuli, msichana aliyekuwa akiishi Kariakoo. Kumsikia mtangazaji akitangaza mechi za Lipuli na kulisikia jina la Stefano kila wakati ikamfanya kutamani kuonana na mwanaume huyo, mbwembwe za mtangazaji huyo zilimfanya kuwa na kiu kubwa moyoni mwake.
Baba yake, mzee Michael Wambuli alikuwa shabiki mkubwa wa timu hiyo, kila alipokuwa akikaa sebuleni na kuzungumzia mpira, alimzungumzia sana Stefano kiasi cha binti yake huyo kutamani kumuona hata mara moja tu.
Moyo wake ukatokea kumpenda, alimpenda mwanaume ambaye hakuwahi kumuona alifananaje, moyo wake ukaanza kuburuzwa na mapenzi, kila alipokuwa akisoma, hakuwa akisoma kwa raha, alitamani sana kumuona mwanaume aliyekuwa akiutesa moyo wake.
Alitamani kumuuliza baba yake zaidi kuhusu huyo Stefano, alifananaje, alikuwaje, ni mzuri ama? Alikuwa na nywele nyingi zilizojulikana kama Afro ama? Alikuwa akivalia mabwanga kama wanaume wengine ama? Yaani kwa kifupi alitamani sana kuona mwanaume huyo alikuwa na muonekano gani.
Siku moja baada ya baba yake kununua gazeti la Mzalendo ndiyo siku aliyoiona picha ya Stefano kwa mara ya kwanza, ilionekana kwa ukubwa nyuma, kama alivyokuwa akitaka ndivyo mwanaume huyo alivyokuwa.
Kichwani alikuwa na nywele nyingi, alipigwa picha akiwa na amekaa kwenye kiti, suruali yake ilikuwa ni bwanga, zile za zamani ambazo kwa chini zilikuwa pana na alivalia shati ya mikono mirefu.
Muonekano ule tu ilitosha kumwambia Zuri kuwa mwanaume huyo alistahili kuwa mpenzi wake, ampende kufa na kuzikana, ampe chochote kile lakini mwisho wa siku waoane na kufunga ndoa.
Siku hiyo alilichukua gazeti hilo, akachana kipande kile kilichokuwa na picha ya Stefano na kuiweka ndani ya daftari lake, kila alipohitaji kumuona mwanaume huyo, alilichukua daftari lile, akaitoa picha ile na kuiangalia.
Mapenzi yakazidi kuchomoza, akashindwa kuvumilia, hakutaka kuona akiumia kila siku na hiyo ndiyo sababu iliyopelekea kumwambia baba yake kuwa alitaka kuangalia mpira, naye aende uwanjani.
Mzee Wambuli aliposikia hivyo alishangaa, hakutegemea kumsikia binti yake akimwambia naye alitaka kwenda uwanjani kutazama mpira, hakutaka kumkatalia, akakubali na hivyo katika mechi iliyofuata ambayo ilikuwa ikichezwa kwenye uwanja wa Taifa (Uhuru) wakaelekea huko.
Macho yake yakatua kwa Stefano, mwanaume huyo alikuwa na mvuto wa aina yake, mashabiki walikuwa wakiliimba jina lake, alikuwa mchezaji tishio ambaye kila mmoja alimuogopa, mwili wake ulijaza na alivalia pensi fupi iliyoyafanya mapaja yake manene kuonekana vilivyo.
Huo ndiyo ukawa muendelezo mwingine wa kumpenda mwanaume huyo, akampenda kupita kawaida na siku moja aliposikia timu ya Lipuli inakwenda kufanya mazoezi katika uwanja wa Shule ya Wasichana ya Jangwani kujiandaa na mechi dhidi ya Simba, akatamani kumuona.
Siku hiyo hakuondoka, alibaki darasani akijifanya kujisomea lakini lengo lake kubwa lilikuwa ni kumuona Stefano kwa mara nyingine tena. Hilo halikuwa tatizo, akafanikiwa kumuona mwanaume huyo, alimwangalia, alikuwa mtu wa mazoezi, alivutia kwa kila aliyekuwa akimwangalia.
Alikaa na kuvumilia, alipowaona wanafunzi wenzake wanasogea kwa karibu uwanjani, naye akajisogeza na kuanza kumwangalia kwa ukaribu zaidi, huyo Stefano alikuwa na mvuto kupita kawaida.
Mazoezi yalipomalizika, wanafunzi wakapata nafasi ya kwenda kuzungumza mawili matatu na wachezaji, haraka sana naye akamfuata na kuanza kuongea naye huku akijisikia aibu mno.
Ilikuwa ni lazima kufanya hivyo, kwa mtu kama Stefano ilikuwa vigumu sana kumuona sehemu na kuzungumza naye, alikuwa mkazi wa huko Iringa, alikwenda Dar es Salaam alipokuwa akicheza mechi tu, hivyo ilikuwa ni lazima afanye juu chini kuhakikisha anazungumza naye.
“Unajua sana kucheza mpira,” alisema Zuri huku macho yake yake yakiwa kwa mwanaume huyo.
“Ahsante sana!”
“Baba yangu anakupenda sana. Natamani hata siku moja uje kumuona!” alimwambia.
“Kweli?”
“Ndiyo! Aliniambia mengi sana kuhusu wewe,” alimwambia.
“Yapi hayo?”
“Kwamba unajua kucheza mpira!”
“Nadhani alikosea!”
“Hapana! Hakukosea! Unajua sana!”
“Ulishawahi kuona nikicheza?”
“Niliwahi kuja uwanjani kukuangalia!”
“Lini?”
“Mwezi uliopita! Unajua sana!” alisema Zuri.
Walibaki wakizungumza kwa dakika kama tano hivi, baada ya hapo Zuri akachukua namba ya posta kwa lengo la kumwandikia barua mwanaume huyo.
Hakutaka waishie hapo, ilikuwa ni lazima waendee kuwasiliana na lilikuwa jambo zuri kama wangefikia hatua ya kuandikiana barua kwani Zuri alitarajia kumaliza kidato cha sita mwezi unaofuatia.
Huo ndiyo ukawa mwanzo wa wawili hao kufahamiana, wakaandikiana barua, Stefano akapata nafasi ya kwenda kumtembelea, akakutana na mzee Wambuli, wakawa marafiki mpaka pale alipotangaza nia ya kumuoa msichana huyo ambaye alianza kufanya kazi katika Shirika la Reli Tanzania (TRL)
Mwezi mmoja baada ya kufunga ndoa ndipo Stefano akavunjika mguu na vipimo vilipofanyika, hakuruhusiwa kurudi uwanjani. Alikuwa na ndoto nyingi za kuendelea kucheza mpira, aende Ulaya, afanikiwe, apate pesa lakini ndoto yote hiyo ikafutika, ikafa moja kwa moja.
Ilikuwa ni huzuni kwake, moyo wake ulimuuma mno, alikuwa mtu mzima lakini hakuacha kulia, alilala kitandani usiku kucha akilia, alitamani kile alichoambiwa kiwe kwenye ndoto na atakapoamka basi aende uwanjani kujiandaa na mazoezi lakini haikuwa hivyo.
Wakahama Iringa na kuhamia jijini Dar es Salaam, alipofika huko, mke wake akamtafutia kazi hapo Shirika la Reli, akafanikiwa, na kwa kupitia jina lake kubwa, akakubaliwa na hatimaye kuanza kazi.
Je, nini kitaendelea?
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app