Simulizi: Ulikuja kutafuta nini? (sehemu ya 01)

Pedrz

Member
Apr 2, 2021
27
75
Habari wana JF nawaletea simulizi nzuri ya Ulikuja kutafuta nini? Kama mtaipenda basi ntawaletea sehemu ya 02 sahivi tucheki hii sehemu ya 01.

Kweli hamna kinachoshindikana mbele za Mungu baada ya miaka miwili mtaani leo napata ajira katika shule ya msingi Nakoza nilifurahi sana, haya maisha ya mtaa yamenipeleka sana ukizingatia nyumbani nipo na mama yangu pekee ambae jicho lake lipo kwangu.

Basi nilijiandaa na safari na nilimweleza Mama kua baada ya siku mbili ntaanza safari kuelekea hapo shuleni, kilikua kijiji cha pili kwahiyo ilibidi nifanye maandalizi kabisa nilitamani kuondoka na Mama ila nikaona ngoja nikaweke mazingira mazuri kwanza alafu nitarudi kumchukua.

Nilimcheki rafiki angu masunga ambae alikua anaishi katika kijiji cha nakoza kama ntaweza kufikia kwake alijibu haina shida kabisa karibu sana. Baada ya siku mbili kuisha nilimwaga mama akanitakia heri katika safari yangu

Safari haikuwa ndefu sana mwendo wa masaa matatu na nusu nilifika katika kijiji hicho bila kupoteza muda masunga alinipokea na kuanza safari ya pili kuelekea kwake

Tulifika pale na hiyo siku tulipiga stori nyingi sana kiukweli masunga alikua rafiki angu mkubwa sana basi nilimwambia kesho nataka anisaidie kama ntaweza kupata geto, si unajua maisha ya vijana alicheka akasema haina shida kuna nyumba ya Bibi Chausiku ni nzuri sana ntakupeleka ukaione kesho

Usiku uliisha kesho asubuhi na mapema tulienda kwa Bibi chausiku haikuwa mbali sana kutoka kwa masunga ni mwendo kama wa dakika 20 tulifika tukamkuta akiwa amekaa kwenye mkeka tulimsalimia akatukaribisha tukaketi.

Basi Bibi na masunga walitoka kidogo kwenda kuongelea pembeni nilibaki kuwaangalia walikuwa wakiongea huku Bibi akigeuka akinitazama basi baada kama ya dakika tatu walirudi na Bibi aliniambia karibu mwanangu nilisema nashukuru

Masunga kashaniambia nadhani hamna jipya wewe karibu hata sahv basi kwa vile kashamaliza kila ktu mimi jioni ntakuja nilimjibu nikitabasamu, akasema haina shida karibu sana.

Tuliondoka huku nikiwa na hamu ya kuanza maisha mapya njiani nilimuuliza vipi kuna wapangaji wengine pale kwa Bibi

Masunga alinijibu hapana ni wewe tu, anakaa peke ake si unajua huku kijijini watu wanapita tu sio wakaaji. Ilinishitua kidogo ila nikaona kawaida alafu mbona kawaida tu huku kijijini nilijiambia moyoni. Nini kitaendelea katika sehemu ya 02 toa maoni yako kama unataka sehemu ya pili 02.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom