Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,977
Mtunzi Juma hiza
Sehemu ya 01
Shauku niliyokuwa nayo ni jinsi nitakavyomuona dada na shemeji kwani mara ya mwisho ni siku ya ndoa yao iliyofanyika kwenye ukumbi wa New Msasani Club.
"Wengi wanasemaga mwanamke akishaolewa anapungua mwili, lakini mwanaume anaongezeka. Sijui ndivyo ilivyo kwa hawa shemeji na dada?
Niliwaza, wakati huo basi la Happy Nation nililopanda lilikuwa likisubiri taa ziwake pale Ubungo ili lipite kwenda stendi kuu ya mabasi.
Kila hatua ya basi picha ya dada na shemeji zilinijia kiasi kwamba nilijiuliza ni kwanini? Ni kwanini niliwakumbuka sana kuliko siku zote?
"Au labda kwa sababu nakwenda kukutana nao?" nilijiuliza.
Ndugu mbalimbali walikuwepo kituoni wakitumbulia macho ndani ya basi kutafuta nafasi ya haraka haraka kuwaona wageni wao. Na mimi macho yangu yalikwenda mpaka nje ambako yalikuwa yakitafuta watu walio wawili. Mtu mke na mtu mume. Yaani shemeji na dada.
Kwa haraka macho yalipowaona wanaume watupu sikushughulika nao, au wanawake watupu pia sikushughulika nao.
Niliyarudisha macho ndani kisha nikachukua begi langu na kuteremka nikijua labda shemeji na dada wamechelewa kufika stendi, hivyo nitawasubiri. Niliwaza.
Nje ya basi nilitembea na begi langu kuelekea kwenye kibanda kimoja kinachouzwa kadi za simu kwani wakati huo niko njiani nilichati sana na boyfriend wangu nikamaliza credit kwenye simu.
"Maria. Maria," nilisikia nikiitwa.
Niligeuka haraka huku kichwani nikitafuta sauti hiyo.
"Ha! Dada," alikuwa ni dada yangu Light yupo na mwenzake lakini sikujua kama ni rafiki yake, mfanyakazi mwenzake au mpangaji mwenzake.
Sijawahi kumsalimia dada shikamoo hata siku moja nyuma, sijuinni kwanini. Lakini safari hii tulipokutana baada ya kukumbatiana na mabusu kibao nilimsalimia.
"Shikamoo dada Light," nilimsalimia na mwenzake, naye akaniitikia. Lakini dada Light alionekana kufurahia zaidi shikamoo yangu. Kumbe alikuwa na hamu nayo sana.
Alinisaidia begi kwa kulibeba yeye kisha tukawa tunaelekea sehemu zinapopaki taksi.
"Basi mi mawazo yangu utakuwa umekuja na shemeji," nilimwambia dada Light.
*
*
Itaendelea