SIMULIZI: Tembele la uwani (EDGAR MBOGO)

Kumbe ni amri agizo kutoka juu🤓 watu walishaanza kumkisia vibaya Laylah
 
Kumbe ni amri agizo kutoka juu🤓
C nilikwambia,
Hana shida huyo, yupo kazini na ukizingatia tokea mwanzo barua ya jamaa ilipita kwa bahati mbaya.

Harafu tuachane na hayo, "jamani natafuta make wa kuoa, sharti awe hajui kusoma"🤣😂🔥😂🔥😂
Kazi Haina kipengele, na Soraya ndio atajileta shamba na mkataba tunasainia hukohuko. 🤣😂😂😂
 
TEMBELE LA UWANI
SEHEMU YA AROBAINI NA SABA
MTUNZI Mbogo EDGAR
ILIPO ISHIA SEHEMU YA AROBAINI NA SITA: Yap! waliposimama na kushuka toka kwenye gari mzee mahamud akaingia ofisini na Sorata akabaki ana mkabidhi Layla majina ya watu waliochagulia, kufanyiwa majaribio ya ajira, “Laylah, nadhani umemkumbuka yule kijana mpole” alisema Soraya kwa sauti ya chini iliyojaa kihoro, “tena nimeshangaa kusikia kuwa ndie aliemsaidia boss siku zile” alisema Laylah kwa sauti ya chini pia, lakini bado ikiwa na mshangao, “sasa hakikisha haingii humu ndani, muambie akupatie namba yake ya simu pia hakikisha kama kweli anaishi kule shambani Mahilo” alisema Soraya huku anampatia karatasi zenye majina ya watahiniwa …….. ENDELEA….
Hapo Laylah akashangaa sio kidogo, “we! Soraya, mwenzio si atakosa kazi na wakati baba amesema tuhakikishe anapata kazi?” aliuliza Laylah kwa sauti ya chini iliyojaa mshangao, “sitaki akutae na baba mpaka niongee nae mimi we fanya kama nilivyo kuambia” alisema Soraya kisha akaanza kuingia ndani akimuacha Laylah amesimama anamtazama kwa macho ya mshangao.
Soraya alipiga hatua kadhaa kisha akasimama na kugeuka nyuma akamuona Laylah amesimama anamtazama kama vile hakuelewa alichotakiwa kukifanya, hapo Sorya akarudi tena kwa Laylah, “usichoelewa nini Laylah?” aliuliza Soraya kwa sauti ya ile ile ya chini lakini iliyoonyesha kulalamika, “da’ Soraya, nayafikiria maisha ya yule kijana kwanini usimuache aingie halafu….” aliongea Laylah, lakini Soraya hakumuachia nafasi ya kumalizia akamadaka juu kwa juu, “Laylah, hii ndiyo nafasi yangu ya pekee ya kutimiza malengo yangu na ndoto yangu, ukikosea huyu kijana akaingia ndani hakika sito kusamehe hata kidogo” alisema Soraya kwa sauti kavu ambayo hata Laylah hakuwahi kuiskia hata siku moja, maana ilikuwa ya ukali na inayo maanisha, kisha akaondoka zake kuelekea ndani ya jengo la ofisi.
Soraya alimkuta baba yake akiwa pamoja na watu wengine watatu, ambao walikuwa na madaraka mbali mbali kwenye kampuni yao, yaani kama waajiriwa, huku kiti kimoja kikiwa kimebakia nae akakaa, “kama nilivyo waambia zingatieni majibu ya maswali mnayo uliza, si munajuwa kuna watu wanaleta janja janja, ameiba cheti cha ndugu yake anakifanya ni cha kwake ili apate kazi, akipata kazi unashangaa kama ni fundi anaharibikiwa na gari wanaanza kupiga piga simu tuwapelekee mafundi wengine wakawasaidie” alisema mze Mahamud kwa msisitizo, wakati wana wanasubiri watu waanze kuingia ili wawatahini, “hakuna shaka boss, tumejiandaa vizuri” walijibu wale watu watatu, huku muda wote Soraya akiwa kimya ametulia akiwaza juu ka kile alichomtuma Laylah, akiombea Laylah asije kufanya kitu tofauti.
Naam Laylah alirudi ndani na zile karatasi, akawaeleza kuwa tayari amesha waita walio hitajika na baada ya hapo akaelezwa kuwa aende akawaite mmoja baada ya mwingine waingie ndani” alisema Mahamud na Laylah akatoka nje, dakika chache baadae akaanza kungia ndani mtu mmoja baada ya mwingine, ambao walihojiwa na kuingia mwingine, huku wakichukuwa majina ya wale waliowakubali kwaajili ya kuingia kwenye awamu ya pili ambayo ingekuwa ni majaribio, ambapo ingefanyika siku mbili mbele.
Watu waliingia huku Soraya na baba yake wakimtazama kwa umakini kila alieingia wakiwa wanamtazamia mtu mmoja kwa mitazamo tofauti, wakati mzee Mahamud anatarajia kuona kijana aliemsaidia siku ile aliyovamiwa na vijana wawili waliokuwa na lengo la kumdhuru na kumpora fedha, huku Soraya alikuwa anaombea kijana huyo huyo asiingie mule ndani, maana hakutaka akutane na baba yake kabla hajakutana nae yeye.*********
Saa tano Talib alienda mwembe chai kwa Zido, na aliwakuta wakina Zido wakiwa pale nyumbani wanauguza majeraha yao waliyo yapata jana kule shambani kwa Soraya, “jamani hee mimi na mchongo, tusikae kuwaza juu ya yule fala” alisema Talib, huku ana sokota bangi, “Talib hebu achana na hizo mambo, unajuwa unapo mzungumzia yule dogo unamzungumzia mtu mwingine kabisa sio wa kipindi kile tupo shule” alisema Vitus ambae ni mmoja kati ya walioumia kidogo na kuwa na afadhari, “we ngoja uone nitakacho mfanyia usiku wa leo, nyie wenyewe mutajua kuwa mimi sio wa pole pole” alisema Talib kwa majisifu huku anawasha ile bangi yake na kuanza kuivuta, “Dah! Hebu achana na hiyo tupe mchongo mpya tuone kama unafaa” alisema Vitus, na hapo Talib akaanza kuelezea kuhusu fedha zilizopo kwenye kabati la ukutani la ofisini kwa baba mjomba wake, “sasa tutaingiaje mpaka ndani ya jumba lile mwanangu” aliuliza Zido kwa mara ya kwanza, “mutaingia mapema halafu mutajibanza chumbani kwangu, kwasasa nitahakikisha ninaiba funguo moja ya mlango wa nyuma wa nyumba kubwa, ambao tutaumia kuingilia na kiukweli mlango wa ofisi huwa haufungwi, hapo ni kazi kwenu kuchukuwa mkwanja na kutambaa zenu” alieleza Talib kwa namna ambayo ungesema ni kitu chepesi sana, “ni hivyo tu!?” aliuliza Vitus, kwa sauti ya mashaka, “kumbe je! unadhani kuna jipya basi, ni kama kumsukuma mlevi” alisema Talib huku akiendelea kuvuta bangi, “basi poa, wacha kwanza tukae sawa halafu tucheze na huo mkwanja” alisema Vitus, huku wenzake pia wakianza kupata matumaini mapya.**********
Naam kule kwenye masailiano ya ajira, Bahati iliangukia upande wa Soraya, maana wali wasaili wale watu walioomba kazi mpaka saa tisa za jioni, ambapo mtu wa mwisho aliingia pasipo kumuona Kijana mpole akiingia mule ndani, “unasema wameshaisha mbona yule kijana sijamuona?” aliuliza mzee Mahamud kwa mshangao, huku anamtazama Laylah aliekuja kutoa taarifa ya kuwa tayari watu wote walishaisha, “boss nadhani alipoona hajaitwa akaamua kuondoka” alisema Laylah huku akitazamaisha kichwa chini, “khaaaa! kwanini lakini, ilifaa umueleze mapema kuwa asiondoke” aliongea mzee Mahamud kwa sauti ya kulalamika, akionyesha wazi kuwa yule kijana kwake ni uhimu sana na hakutakiwa kukosa kazi, “baba wala hauhitaji kuwa na wasi wasi, madhari tumesha muona na kumfahamu basi tukimuona tena tutamueleza aje kukuona” alisema Soraya akionyesha kuwa mwenye furaha tofauti na alivyokuwa asubuhi.
Baada ya kuwa tangazia wale walioomba nafasi wakiwasoma majina wale waliopitishwa kwenye interview, Mzee Mahamud na binti yake wakaondoka pale ofisini huku Laylah akiendesha gari, muda wote Soraya alionyesha mwenye furaha isiyo na kifani, aliongea na kucheka kwa furaha hata wakiwa nyumbani pia alikuwa hivyo hivyo.
Masaa yalikatika huku Laylah, akionekana kusalia pale nyumbani kwa boss wake, na hata walipomaliza kuswali swala ya insha ndipo Mahamud aliposhangaa, “Laylah, hujachoka kwa kazi tuliyoifanya kutwa nzima, ni vyema kama ungeenda kupumzika nyumbani” alisema Mahamud na Soraya akadakia, “samahani baba, nimemueleza mimi abakie kuna jambo nilitaka nikuombe” alisema Soraya na kuwafanya baba yake na mama yake washtuke kidogo, maana haikuwahi kutokea Soraya akatoa ombi kwa msisitizo kama huu, “nini tena mwangu, kuna jambo umepungukiwa?” aliuliza Mahamud, ambae siku zote katika mali au vitu alivyojaaliwa kuwa navyo basi mwanae alikuwa anampenda na kumthamini kuliko utajiri wake wote, “baba… mhhhh! nilikuwa naomba niende kwa kina Laylah” alisema Soraya kwa sauti ya upole yenye mashaka mashaka, “mh! Soraya usiku huu, kuna jambo gani muhimu usiku huu?” aliuliza mzee Mahamud kwa sauti ya mshangao kama alivyoshangaa mke wake, yaani mama Soraya, “hakuna kitu baba, ila… ila tu… ninataka kubadili mazingira maana leo sijikii vizuri” alisema Soraya, ambae toka amepata akili hakuwahi kukataliwa kitu na wazazi wake hasa baba yake ambae alimkingia kifua pale mama yake alipohitaji kumnyima kile alichoomba.
Mzee Mahamud alitulia kidogo akiwaza juu ya ombi la binti yake, alitumia kama dakika mbili nzima huku Soraya ambae alikuwa amevalia gauni lake refu la kushindia pale nyumbani pamoja na Laylah ambae alikuwa kama alivyokuja asubuhi wakisubiri jibu, “sioni ubaya wowote, wacha akaone jinsi mwenzie anavyoishi” alisema mama Soraya baada ya kuona mume wake anakosa jibu, “sijawahi kufika nyumba kwa Laylah, vipi kuhusu usalama wake?” aliuliza mzee Mahamud, ambae alionyesha wazi kutoridhika na ombi la mwanae, huku ana mtazama Laylah, Soraya nae akamtazama Laylah ambae pia alikuwa anamtazama na macho yao yakakutana, “ndiyo boss, usalama upo mkubwa tu, isitoshe mtaani kwetu hakuna fujo wa la vijana wahuni” alisema Laylah ambae alishaanza kuhisi mpango wa Soraya, japo hakuwa amemueleza, “ok! basi kesho saa mbili muwe hapa nyumbani, na kila baada ya muda fulani Soraya utakuwa unapiga simu kunijulisha kama upo salama” alisema Mahamud kisha akaeleka chumbani kwake, akimuacha Soraya anaingia chumbani kwenda kujiandaa.
Hapo ndipo ungejua kuwa kuna jambo Soraya alikuwa amepania, maana alivaa zile nguo alizozi chukuwa kwa kijana mpole akidhania kuwa ni zawadi zake, alivaa gauni jepesi na fupi ndani ya baibui, alichukuwa vitu ambavyo alikuwa anahisi vinge msaidia kwenye safari yake, ikiwa ni pamoja na mswaki na dawa yake, baadhi ya mafuta anayo yatumia kila siku na kiasi flani cha fedha.
“Da’ Layalah, naomba iwe siri yako, nipekele kule Mahilo nataka kufika kwa kijana mpole” alisema Soraya wakati wanatoka kwenye kituo cha mafuta, Laylah akatoa macho kwa mshangao, “Da’ Soraya, nikupeleke Mahilo usiku huu?” aliuliza Laylah kwa mshangao,”ndiyo tukimpata utaenda kuniacha huko utanifuata asubuhi” alijibu Soraya, akionyesha kuwa amedhamiria kufanya vile, “lakini Da’Soraya huogopi kule porini” aliuliza Layla kwa mshangao huku anakanyaga mafuta kuelekea mashariki mwa mji wa songea, “wala siogopi najua yule kijana hawezi kuniacha kwenye matatizo” alisema Soraya kwa kujiamini, akionyesha mwenye shauku ya kukutana na kijana yule, “na kama akikataa usilale kwake?” aliuliza Laylah ikiwa ni kama tahadhari, “hawezi kunifukuza kwasababu wewe tayari utakuwa umeshaondoka” alijibu Soraya na hapo kikapita kimya kifupi, “hivi umesema anaitwa nani vile?” aliuliza Soraya, “anaitwa Higgno” alijibu Laylah, huku anaendelea kukanyaga mafuta.******
Naam hatimae walifika mashambani na kubahatika kukiona kibanda kimoja pembeni mwashamba moja kubwa, huku moto ukiwaka nje yake ikionyesha kulikuwa na mtu, nadhani patakuwa pale maana wale wafanyakazi wa kule shambani walionyesha kuwa anakaa huku” alisema Soraya, “kwahiyo una uhakika kuwa ndiyo pale” aliuliza Laylah huku anapunguza mwendo, hapo tunakumbuka wakati ule tuliomuona Higgno akilitazama gari likiwa lina punguza mwendo barabarani, “twende mpaka pale kama sio pale tutaulizia anapoishi si umesema anaitwa Higgno?” aliuliza Soraya, huku sauti yake ikianza kubadilika na kuwa yenye kihoro, mh! sawa lakini mwenzio naogopa” alisema Laylah, huku anatembeza gari taratibu kutafuta njia ya kuingilia, na alipoipata aka kata kulia na kuanza kufuata njia ile iliyoenda moja kwa moja mpaka kwenye kile kibanda kidogo cha udongo, ambacho nje yake kulikuwa na mtu amekaa karibu na moto huku zikionekana nyama na samaki wengi wakibanikwa juu yake, “ndio yeye” alisema kwa kunong’ona Soraya, huku yeye na Layla wanamtazama kijana mpole ambae sasa alishamjua jina kuwa ni Higno, ambae alikuwa analishangaa gari lile lililopandishwa vioo, lililokuwa linamulika kwa taa zake, “ndiyo ni yeye” alisema Laylah kwa sauti ya kunong’ona pia, “mwenzio naona aibu tushuke kwanza wote halafu utaondoka” alisema Soraya, kwa sauti ya kunong’ona huku anajichekesha kicheko cha chini chini kilichojaa aibu. Hatimae soraya yupo shambani kwa higgno je nini kitajiriiiii? Usikose kufuatilia mkasa huu hapa hapa JamiiForums bila kusahau kuwa talibu nae ana jambo lake usiku nyumban kwa mzee Frank.....ITAENDELEA.
 
Bikra mbili zinaenda kutana litakufa jitu😂
 
Higgno huwa ni fala fala tu hata kujielezea hawezagi
 
Ebwanae hatimae nitakuwa nareply. Nimesoma kimya kimya tangu enzi za ASALI HAITIWI KIDOLE kwa minjali ya kutokuwa na acount, leo nimeitengeneza bhana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…