Simulizi: Tamaa ilinipeleka Kisiwa Cha Najini

Simulizi: Tamaa ilinipeleka Kisiwa Cha Najini

INAENDELEA...
" twende kwenye kile chumba alafu tunafanya kama
tulivyofanya sikuile" alisema yule mwanamke
wakijini na tukaenda kwenye kile chumba cha nguo
za wafalme tukavaa tukachukua fimbo tukaenda
sebuleni tukakaa na kunyoosha fimbo mbele ya
ukuta na ghafla picha ya kama video ikawa
inaonesha wale wachungaji na ndugu wameuchukua
ule mwili na kuupeleka nyumbani na kama nusu saa
hivi wakawa wanaingia nyumbani.
" tuondoke twende lodge usisahau na ile fimbo
uliyochukua kule lodge nilazima pia azikwe nayo"
alisema yule mwanamke wakijini.
Tulitoweka na kutokea lodge ambapo kila member
alipotuona alibaki akitushangaa maana Ndio Mara
ya kwanza kutuona na namna tulivyo vaa
tulipendeza sana kila aliye tuona lazma ajue
kupendeza kule sio kwa watu wa kawaida
" tuingie kwenye magari msafara uanze" aliongea
Mzee ambaye ni kiongozi wa ibada. Basi Mimi na
yule mwanamke wakijini tukaingia ndani ya gari yetu
ambayo atasijui ilifika saa ngapi.
" onhoo! Umewaona wale askari wakijini wale palee"
nilimwonesha yule mwanamke wakijini kupitia
dirishani.
" niliwaita, derava washa gari" alisema yule
mwanamke wakijini uku akimwambia dereva aondoe
gari, basi msafara wa magari ya members yalianza
kuondoka uku sisi tukiwa katikati, yalikuwa nimagari
meusi kulingana na suti walizo vaa kwa upande
wetu walipendeza sana ila kwa mtu wa kawaida
ilikuwa ni shida kidogo kwa kuwatizama wale
members. Tulipofika karibu kabisa na nyumba ya
marehemu kwa nguvu za kichawi tuliwasiliana kuwa
wote wanapaswa kufungua milango yao ya upande
wa kushoto na kushuka kwa mguu wa kushoto
kisha kusimama palepale ilikufanya watu wanao
tuona wajue kuwa sisi sio watu wakawaida.
"Jamani angalieni kule" watu walio kuwa pale
msibani walishtuana kutuangalia.
"Nini kinafuata? Nilimuuliza yule mwanamke
wakijini.
" jeneza lipo ndani kwaiyo toa ishara kwa members
waingie ndani na sisi tukifuata" alisema yule
mwanamke wakijini.
Nilinyanyua mkono na kuongea kwa sauti ya chini
na kuwafanya members wote waelekee ndani yaani
walikuwa kama wanakuwacontrolled na remote.
" hawa sio Freemason jamani " alisema
mwombolezaji mmoja pale msibani.
" mmmh! Kweli we wacheki mambo yao yanatisha
angalia walivyo vaa tena waone wale wawili"
aliongea mwombolezaji mwingine uku
akitunyooshea vidole Mimi na yule mwanamke
wakijini na pale msibani kukaibuka minong'ono,
lakini yote hayo tulipuuza kwamaana hawakuwa na
lolote lakututisha ila akili yetu ilikuwa kwa wale
wachungaji ambao...
Akili yetu ilikuwa kwa wachungaji ambao macho na
akili za wale majini yalikuwa juu yao kuwachukulia
uangalifu wasije wakaharibu utaratibu.
Tuliingia ndani tulimkuta mama wa marehemu, baba
yake na ndugu zake na watu wa chache wakiwa
wamelizunguka jeneza.
" tunaomba mtupishe kidogo" alisema yule
mwanamke wakijini na kuwafanya wale wazazi wa
marehemu na ndugu kutushangaa.
" nyie niakina nani" aliuliza baba Wa marehemu
akionesha ujasiri maana wengine wao waliingiwa na
woga.
" vizuri sisi ndio tulio muua uyu kwakuto fuata
masharti tuliyo wekeana na niongeze kitu apo tu uyu
kijana wenu ni member wa devil worship alijiunga
ila kuna shida kidogo ili tokea ndio maana
ameuawa kama ilivyo Sera yetu" alisema yule
mwanamke wakijini bila kuficha kitu na kunifanya
nimshangae kidogo.
" tunaomba sasa kwa ustaarabu mtumpishe tufanye
yetu kisha tutawaruhusu mka zike ila ibada yoyote
ya kikanisa hapaswi kufanyiwa" alisema zaidi yule
mwanamke wakijini na kusababisha mama wayule
kijana na Dada zake wapoteze fahamu kwa yale
maneno. Walikubali kutoka nje uku wale walio zimia
wakibebwa kutolewa kutupisha sisi tufanye mambo
yetu kisha wakazike. Tulipo hakikisha hakuna mtu
waziada nje ya sisi na wale members
waliochaguliwa kuingia ndani maana wengine
tuliwaacha nje kusaidiana na wale majini wengine
kama kutatokea hitaji la kufanya hivyo. Basi jeneza
likafunguliwa na ule mwili ukatolewa na kulazwa
chini kisha ibada ndogo ya kishetani ikafanyika na
Mara mtikisiko ukatokea katika lile eneo wakati
nguvu za kuzimu zikija kutwaa nafsi iliyo ndani ya
yule kijana maana kulingana na mkataba Alisha
saini kuwa roho yake ni ya shetani milele basi
lazima nafsi ichukuliwe iende kwa shetani kwaajili
ya siku ile kuu. Kitu kama kivuli kili toka ndani ya
ule mwili na kusimama pembeni ambacho hutoka
kabisa ndani ya mwili baada ya kufa kwa siku
arobaini lakini sisi pale tulikitoa ili kukipeleka
kuzimu kwa shetani mkuu, Beelzebub mwenyewe
aliingia pale na mtikisiko wake uliwafanya hata wale
walio kuwa nje wakijadiliana umbea kukimua mbio..
Beelzebub mwenyewe aliingia pale na mtikisiko
wake uliwafanya hata wale walio kuwa nje wakijadili
umbea kutimua mbio kutokana na kuhisi hali isiyo
ya kawaida, alifika Beelzebub na kukitwaakile kivuli
akakivisha vazi kama joho fupi lalangi ya kakhi joho
hili alipovikwa alitokea katika mwonekano halisi
kama roho na kumfanya Beelzebub kubadilika
umbile kutoka mtu wa kawaida adi kuwa wakutisha
sana alikuwa na mapembe marefu sana nyuma ya
mgongo wake alikuwa na mambawa kama yaliyo
ungua na miguuni alikuwa na kwato kama za
mnyama na sura yake ilikuwa na manyoya mengi
sana ambayo pia yalitapakaa mwili mzima na
macho yake yalikuwa kama moto alitisha sana kwa
ule muonekano wake.
"KAZI NZURI KIJANA UTAPATA ZAWADI YAKO"
alisema Beelzebub akinitazama na kutoweka na
kivuli au nafsi ya yule kijana.
Ibada iliishia pale na kisha tukaurudisha tena mwili
kwenye jeneza kisha tukaweka ile fimbo ndani ya
lile jeneza na kuwaita wazazi na ndugu wa
marehemu na kuwaonya wasilifungue lile jeneza
wala watu hawapaswi kufanya buriani vinginevyo
kutakuwa na matokeo mabaya sana.
"Nyie manasema hivyo kama nani" mmoja wa
wachungaji alisema.
" kama tulio muua" nilijibu hivyo maana sipendi
maswali sana tena yanayo ashiria ubabe.
" sisi tutafanya ibada na hakuna wakutuzuia"
alisema tena yule mchungaji.
" sikiliza baba Karen mtoto wa Mzee Daudi unaitwa
mchungaji Sebastian ila nani anajua mwengine kuwa
ulipokuwa kijana uliua mtu na kwasababu ya wivu
wako wakimapenzi ndio ulimuua na kukimbilia mjini
ambapo ulikaa na baadae ulipata uzamini
wakusoma chuo cha teolojia na sasa mchungaji je
ivi nikiuliza kuwa nani anajua mama stela
unatembea naye ndio yule mama Mzee wakanisa ee
uyo ivi mkeo anajua aya" alisema ivo yule
mwanamke wakijini na kumfanya yule mchungaji
achanganyikiwe.
" we..we..we ni nani? Alihoji yule mchungaji
akionesha kuchanganyikiwa sana.
" hahahaha ulizani humu ndani walioingia
nibinadamu kama wewe au unazani uyu marehemu
unamjua vizuri wewe? Aliuliza yule mwanamke
wakijini.
Basi kwa maneno yale sio tu wale waombolezaji
walio anza kurudi baada ya kukimbia
walichanganyikiwa Bali hata wachungaji wenzake na
mchungaji Sebastian walichanganyikiwa na
kumshangaa mwenzao.
" alafu sasa zingatieni hili hatuondoki hapa mpaka
maziko yamefanyika inaonekana mnaviburi sana
nyie" alisema yule mwanamke wakijini lakini wakati
wote uo wale majini bado waliendelea kuwaandama
wale wachungaji..
twendeni pale" alisema yule mwanamke wakijini na
si tukawa tunamfuata kuelekea sehemu yenye
matent maana yalikuwa hayana watu kwasababu
wengi walikimbia na wa chache wakawa wanarudi.
" kwanini umemsema vile mchungaji? Niliuliza
maana nilipenda alichokifanya.
" nilitumia uovu wake na siri yake kuzuia Neema
yake na kwa hatia aliyo tenda nyuma ndio hiyo
inamuhukumu na kwakuiangalia hatia hiyo hataweza
kuiona Neema aliyo nayo" alisema yule mwanamke
wakijini.
"Sijaelewa" nilisema.
" yaani pale ni kama nimemuumbua na kwauzaifu
wa binadamu amekwisha na Ndio maana ata wale
wachungaji wenzake wametulia kama unavyojua kila
binadamu anaile siri ambayo anajua yeye, shetani
na yule mkuu basi iyo hatia ndio inamletea mtu
shida ikitoka kama hivi" alisema yule mwanamke
wakijini.
"OK sasa nimeelewa" nilisema.
" Dawa ya watu ni kutoa siri zao" Niliongea.
" ndio ila kuna dini Fulani wao huwa wanasema ile
siri kwa mtumishi wa aliye juu kikawaida akisema
pale ile hatia anayoihisi utoweka na Ndio baadae
hufanya mapatano na muumba lakini iyo kwetu sio
muhimu" alisema yule mwanamke wakijini.
"Kama awa wachungaji wataleta shida shida kuna
hatari ya ile nafsi kurudi na ikirudi wote tutapata
adhabu kwa kushindwa kuwachukulia uangalifu"
alisema yule mwanamke wakijini.
" hii! Maneno gani sasa hayo" nilisema maana
niliona yule mwanamke wakijini kama anaombea
mabaya tu.
" nikweli ndio maana nakutaka uwe makini na ujue
tutafanyaje " alisema yule mwanamke wakijini.
" OK ngoja " nilisema uku nanyanyuka nilipokaa
kwani kichwani kuna wazo lilinijia, nilipo nyanyuka
kwa nguvu ya kishetani nilijigeuza kuwa mchungaji
katika mavazi yangu na kugeuza fimbo yangu kuwa
kitabu ambacho ukikitazama utazani ni biblia
kumbe hakuna kitu kama icho, nilipiga hatua mbele
nikaingia katikati ya majini walio wazunguka wale
wachungaji na Mimi nikajiunga na wale wachungaji.
" bwana asifiwe" niliongea kuwasalimu.
" amen" waliitikia wale wachungaji.
" samahanini jamani nimechelewa ila nahisi mambo
hayaja haribika nyie kuwepo hapa" nilisema.
samahanini jamani nimechelewa ila nahisi mambo
hayaja haribika nyie kuwepo hapa" nilisema ili nijue
nini wamepanga kutenda kwa muda ule na nizuie
kama kitakuwa hatari kwa maslahi yetu.
" kunashida bwana kubwa tu apa tulipo kuna nguvu
za giza zinatuandama" alisema mchungaji mmoja na
kunifanya nishtuke kidogo.
" unamaanisha nini"? Niliuliza.
" inamaana ujasikia kwanza apa tulipo huoni uzito
usio wa kawaida na pili angalia kule" alisema
mmoja wa wachungaji na kunyooshea kidole kule
alipokuwa yule mwanamke wakijini na member
wengine wa waabudu shetani.
" ndio naona kuna shida kwani pale"? niliuliza.
" ndio ipo wale sio watu wa kawaida ni waabudu
shetani " alisema yule mchungaji.
" tobaa! Sasa inakuwaje wawepo apa japo kuwa
najua marehemu alikuja kwangu akitaka ushauri
wakujitoa kwenye lile genge lakini sijui nini
kikatokea na Leo ndio nmepata habari amekufa
dah" nilisema kujifanya tu.
" inasemekana marehemu hakuacha kabisa ushirika
na lile kundi la shetani ndio maana wamemuua
kutokana na kuja kuomba uo msaada unaousema"
aliongeza mchungaji mwingine uku mchungaji
Sebastian akiwa kajiinamia hana chakuchangia.
" mmmmh hii hatari kama hakujiondoa sasa sisi
inamaana kuwepo hapa nimakosa kwa maana uyu
alimkataa bwana na kama alijivika mavazi ya
kondoo uku ndani ni mbwa mwitu mkali unadhani
bwana ata shuhulika naye kweli" nilisema ili
kuvuruga mambo.
" mmh sidhani ndio maana wale mapepo
yamesema hakuna ibada ya kikanisa wala yanini
maana uyu alikuwa wao wanajua" alisema sasa
mchungaji Sebastian.
" kweli kabisa sasa tutafanyaje kuondoka itaonekana
tumeshindwa" alisema mchungaji Sebastian tena.
" natukibaki pia tunaweza shindwa kama bwana
asipo tembea nasi maana uyu marehemu alimkataa
na yeye atamkataa tu" nilisema kuvunja nguvu
kabisa wazo la msingi.
" kama ndio hivyo tufanye nini" aliuliza mchungaji
mwengine.
" tukae tu tone mpaka mwisho apa kuna
chakujifunza" nilisema.
" nikweli mtumishi" walijibu wachungaji wote kwa
pamoja.
" basi twendeni pale tukakae" nilisema
basi twendeni pale tukakae" nilisema uku tukienda
eneo la pembeni kidogo nikiwa na wale wachungaji.
Basi mwongozaji wa mazishi alipoona watu
wamerudi na alipofanya mawasiliano na watu
waliokuwepo makaburini aliongea na ndugu na
kukubaliana wakazike, basi watu wakaingia kwenye
magari na msafara wa kwenda mazishini ukaondoka
kabisa ukiwa chini ya uangalizi wa yule mwanamke
wakijini na members waabuduo shetani na baadhi
ya majini ambayo yaliamua kupungua baada ya
kuona nimefanikiwa kwa kiasi Fulani kuwashawishi
wale wachungaji wasifanye balaa pale. Mimi na
wachungaji tulibaki nyumbani pale kwani
tulikubaliana kuwa kwenda mazishini nikukubali
masherti ya shetani basi tulibaki nyumbani uku
tukipiga story za kifo cha uyu kijana, tuliongea
mpaka pale waombolezaji waliporudi kutoka
makaburini na kisha Mimi na wale wachungaji
wengine tuliwaita wanafamilia na ndugu kuwauliza
kisa cha wao kukubali mtoto wao azikwe kishetani
namna ile.
" sisi tuliamriwa na wale watu na walitueleza kuwa
mwanetu alikuwa mwanachama wao kwaiyo
alishamkataa bwana" alisema baba mzazi wa yule
kijana.
" Mimi sikukubali jamani ila naomba tufanye
maombi angalau kidogo jamani na siku ya arobaini
naomba mfike tumfanyie ibada" alisema mama wa
marehemu akiungwa mkono na mabinti zake.
" haiwezekani uko nikumjaribu bwana na hakuna
Neema kwa waliokufa haipo kabisa jamani"
nilisema kwa msisitizo maana niliona kama watasali
basi hii ni shida.
" kama nyie hamta Fanya basi Mimi nitaenda ata
kwa Islamic kuomba msaada wamaombi.
" hata uende kwa malaika nani hakuna njia mama
kijana mwenyewe kaamua kuchagua njia yake wewe
huwezi leo kumfanya mkristu au Islamic" nilisema
maana niliona anataka kuleta matatizo yule
mwanamke.
Basi yule mama aliangua kilio cha kukata tamaa
pale pale akadondoka chini na kuzimia maana
alionekana mwenye uchungu mkali sana. Lakini
jambo ambalo wale wachungaji walifeli ni kuamini
Mimi ni mchungaji na kutokuwa na imani juu ya
sauti walizokuwa wakizisikia kwa maana Mimi
nilikuwa na onywa kila saa juu ya mabadiliko ya
wenzangu.
" jamani apelekwe sasa hospital " nilisema baada ya
yule mwanamke kuanza kutoka damu.
" nikweli tufanye hivyo" waliongea wale watumishi.
"Ngoja Nipige simu kuna doctor namjua atakuja na
ambulance" nilisema lakini kichwani nilikuwa
nimepanga kumpigia member wa devil worship
anaye miliki hospital ili..
kumpigia mmoja wa member wa devil worshippers
ambaye anamiliki hospital kubwa pale mjini.
Baada ya kuongea naye haikupita muda mlefu
ambulance ikawa imefika na kweli yule doctor
ambaye ndio mmiliki wa ile hospital alifika na
kumchukua yule mama ambaye alisindikizwa
hospital na mumewe na mabinti zake uku nyuma
wakituacha sisi YAANI Mimi na wale wachungaji.
"Uyu ni tajiri sana vipi mnajuana" aliuliza mchungaji
mmoja.
" hahahaha nimuuni wangu bwana ndio maana
ameona aje mwenyewe huu ni upako na neema
iwejuu yake" nilisema
" amen" waliitikia wale wachungaji na baada ya
muda kidogo mchungaji Sebastian aliamua kuaga
kuondoka na kufuatia na wachungaji wengine nao
kuniacha pale Mimi peke yangu.
Lakini baada ya muda kidogo kabla ile familia haija
rudi alikuja yule mwanamke wakijini n akujigeuza
naye kuwa ni mmoja ya wachungaji walioondoka.
" Kazi nzuri sana yaani umefanya kwa viwango
ndugu safi sana" aliongea yule mwanamke wakijini
na kunikumbatia kwa furaha.
" ila nimechoka nataka nirudi nyumbani namimi
nikapumzike siumeona umu ndani nipo mwenyewe"
nilisema
" upo peke yako ndani ila nje mbona bado wapo
watu wanao kaa kuanua matanga" alisema yule
mwanamke wakijini.
" sasa siwezi ongea na kila mtu tu maana Kazi
niliyo ifanya ni nzito nilitamani kufa apa mwili
umechoka sana" nilisema.
" sawa basi subiri warudi na sisi tuondoke" alisema
yule mwanamke wakijini.
Tulikaa pale kwa muda mrefu mpaka wale walio
enda hospital walipo rudi.
" mgonjwa anaendeleaje? Niliuliza.
" bado madaktari wamesema tunaweza kuondoka
wao wanamuhudumia haina shida " alijibu mume
wayule mama.
" OK sawa sasa Mimi na mwenzangu ngoja
tuwaache Mara moja tutazidi kuja kujuliana hali"
niliaga kwa staili hiyo.
"Sawa karibuni sana" walisema sasa yule baba na
binti zake.
"*Asante " tulijibu uku tukitoka nje na tulipo wapita
watu kadhaa waliokuwa pale nje tuli toweka na
moja kwa moja kutokea nyumbani.
nilijitupa juu ya kiti kwa uchovu.
" kaoge kwanza ndio ulale" alisema yule mwanamke
wakijini.
" OK " nilijibu.
niliinuka nikaenda bafuni nikaoga kisha nikaingia
chumbani nikajitupa kitandani na usingizi
ukanichukua nilikuja kuamka majira ya saa tatu
usiku nilipo amshwa kula na wale dada wakazi
wakijini.
" kuna siku uliniambia umundani wote ni majini
lakini sio wote ivi ulimaanisha nini? nilimuuliza uku
naamka kutoka kitandani.
" ndio sio wote maana wewe ni binadamu" alisema.
"ina maanisha mimi peke yangu ni binadamu
umundani? niliuliza tena nipate uhakika.
" ndio ni wewe peke yako" alijibu sasa yule
mwanamke wakijini kwa kuingilia mazungumzo.
basi nilikula na kuludi tena kulala mpaka asubuhi
niilipo amshwa na yule mwanamke wakijini
nijiandae kwenda kusaini ujenzi wa barabara.
" umesema nikasaini? nilimuuliza kwa mshangao.
"ndio ukasaini maana kwa sasa umepewa umiliki
kampuni kubwa ya ujenzi na kama utaendelea
kumfurahisha lucifer basi uta yafurahia maisha"
alisema yule mwanamke wakijini na kunifanya niwe
mwenye furaha sana kwa taarifa ile.
"ila na mashaka kidogo mimi sina elimu ya biashara
izo kubwa maana mimi nilikuwa zamani nafanya
kwa ujanja ujanja tu" nilisema ukweki japo nilifurahi
niliogopa pia kushindwa kuiendesha biashara.
"iusiogope sio wote unao waona wanamiliki
biashara kubwa wote wamesoma sana kuna
wengine wanasaidiwa na hekima ya yule aliye juu
maana yeye ndie kiongozi wa yote na pia kuna wale
wanaoongozwa nasisi ao pia majini ndio huwa
waamuzi wakila kitu kama ivi tenda walikutafutia
majini wewe ukasaini tu leo mbele ya rais" alisema
yule mwanamke wakijini.
"rais tena hii mbona kubwa " nilijibu kwa furaha
sana niliona zile ndoto zangu zakuwa tajiri mkubwa
zinatimia sasa.
"usijali sana sasa amka kajiandae unywe chai kisha
tuondoke " alisema yule mwanamke wakijini
nakunifanya kuruka kutoka kitandani adi bafuni
nilioga haraka nikanywa chai kisha nikawa nasubiri
muda ufike niondoke maana niliandaliwa vizuri na
wale wanawake wakijini na kunifanya muonekano
wangu uwe kama mtu aliyeshiba pesa kwa vile
nilivyokuwa.
"muda umefika tuondoke" alisema yule mwanamke
wa kijini. tulisimama na kutoka nje nilikuwa wale
wanawake wakijini ambao ni wahudumu wa kazi
wamevaa visuti vyeusi ambavyo vili wapendeza
sana.
"vipi na hawa tunaenda nao ? niliuliza .
"ndio hawa watakuwa kama wafanyakazi wa iyo
kampuni ndio watakao kuwa na document zote"
alisema yule mwanamke wakijini kisha tuka ingiia
ndani ya magari yetu ya kifahari na msafari
wakwenda kwenye ikulu ya kenya ulianza tulitembea
kwa muda wa saa kadhaa mpaka tulipoingia ndani
ya ikulu ya kenya lakini kwanza tulisimamishwa na
walinzi waikulu maaana mifumo yao ya ulinzi
ilishindwa kuonesha gari yetu ilipoingia wala idadi
ya watu kiufupi mifumo ya ulinzi haikutambua
chochote kilichofanyika katika mazingira yale ya
ikulu na kuwafanya walinzi kuingiwa na shaka na
gari yetu kwani walidhani imefungwa vifaa maalumu
vyakukwepa ulinzi. tlikaapale mpaka nilipo shuka
ndani ya gari kwenda na walinzi kwenye chumba
cha mahojiano maaana walikosa imani kabisa na
mimi, lakini ndani ya chumba chamahojiano
nilipofika kabla sijaulizwa chochote mmoja wawale
walinzi alipokea mawasiliano kuwa mifumo ipo
sawa na gari imeshafanyiwa uchunguzi shida ilikuwa
kwenye mifumo yenyewe. basi niliachiwa na
kuombwa radhi maana waliogopa kama nitasema
basi itaonekana wao kuwa niwazembe lakini ukweli
niliujua mwenyewe. baada ya ayo tuliingia ikulu
ndani ambapo tulilakiwa na waziri wa ujenzi wa
kenya ambaye alitupeleka mpaka ndani ambako
kwa mara yakwanza nilisalimiana na rais wa kenya
kwa bashasha na furaha ambapo kabla ya kuingia
mkataba na serikali yake tuliongea mambo mengi
sana yamaendeleo na pia yule mwanamke wakijini
aliahidi kuendeleza ushirikiano na serikali na kuahidi
kama kampuni tutapeleka maji kwenye moja ya
maeneo eldoreti na trukana na maeneo ya mkoa ya
pwani ambapo tuliahidi maeneo pia ya kisumu
tungejenga hospital kubwa sana, nilimweleza rais
kuwa nimeipenda kenya na ninamakza pale kenya,
rais alifurahi sana tulipoongea nae na baadae
tukaingia mkataba serikali yake kujenga iyo
barabara lakini hofu iliniingia pale nilipowaza kama
tukishindwa kutekeleza maana tuliahidi mambo
mengi sana mbele ya rais na mambo yenyewe ni
pesa nyingi na ukiangalia pesa zenyewe na tegemea
kwa majini.
"usiogope ayo tuliyo ahidi tutatekeleza" alisema yule
mwanamke wakijini maana aliyasoma mawazo
yangu.
"itabidi sasa utoe kafara"alisema yule mwanamke
wakijin.
"kafara!" nilishtuka maana nilishaingia na woga
nilijua kile ninachowaambia sikuzote wale
wanachama leo kinaenda kunitokea namimi.
"kwani na mtoa nani sasa mimi" niliuliza kipindi
icho tupokwenye gari tunaondoka zetu kutoka ikulu.
"kwani wewe ulitaka kumtoa nani" aliuliza yule
mwanamke wakijini.
" mimi sijui namtoa nani alafu kwa yote aya
niliyofanya napotu mnataka nitoe kafara? niliuliza
kwa kulalamika.
"kwani uoni makubwa yaliyo mbele yako pia huoni
leo mpaka umekutana na rais basi kama utajitoa
zaidi utapata makubwa zaidi" alisema yule
mwanamke wakijini.
" sasa mimi sina mtu wakumtoa nitafanyanyaje"
nilisema.
" unaye yule rafiki yako" alisema yule mwanamke
wakijini
"umaaanisha abdul" niliuliza kwa mshangao maana
abduli alikuwa ndio rafiki ndio ndugu ndio kila kitu
kwangu hata hii habari ya kufanikiwa kwangu
nilitaka aijue ili tufanye kufuru kwa stalehe alikuwa
kila kitu kwangu kiufupi
"hapana bwana badilisha mimi huyo hapana bwana
siwezi lazima ufikirie vizuri mimi kwa apo
nitashindwa" nilisema uku roho inaniuma sana
maana nilijua kitakacho mkuta abdul ni kuchinjwa.
" basi ukishindwa apo utawapoteza ndugu zako
wote" alisema yule mwanamke wakijini sasa akiwa
hana mchezo
Nipoteze familia yangu? Nilishtuka kutokana na
maneno ya yule mwanamke wakijini.
" ndio familia yako na heshima ulizopata
zitapukutika" alisema tena.
" kweli nimeamini kwanini huu utawala wa shetani
huwa unaanguka" nilisema.
" angalia maneno yako ayo" alisema yule
mwanamke wakijini.
" iyo kafara inaitajika leo usiku kama upo tayari
sema tuka mchukue" alisema yule mwanamke
wakijini.
" sipo tayari " nilisema.
" basi unaiponza familia yako" alisema yule
mwanamke wakijini.
" sikiliza wewe Mimi aya nafanya Mimi kama
mnahasira niguse Mimi nasio ndugu zangu"
nilisema.
" kama kuua nimeua sana kama roho za watu
nimezipeleka sana kuzimu lakini bado mnataka
mnipe hasara ya kuua watu wangu haiwezekani "
nilisema bila hata chembe ya mzaha uku kichwani
akili ikianza kugongana.
" hahahaha kwani maisha uliyokuwa ukiishi siku zote
unajua niya gharama kiasi gani? Aliuliza.
" maisha kwani unanipa wewe yupo anaye nipa ila
sio wewe" nilijibu kwa jeuri kama kufa nife tu lakini
sikuwa tayari kuua mtu wangu mwenyewe.
" unataka kuelekea kubaya" alisema yule mwanamke
wakijini na kunishika mkono na kutoweka ndani ya
gari hadi kisiwani Zanzibar ndani ya ofisi moja ya
kisasa.
" siwezi nmesema" nilimwambia yule mwanamke
wakijini baada ya kutokea mbele ya Abdul ndani ya
ofisi yake.
" hapana hatuna muda" alisema yule mwanamke
wakijini.
" kafara gani unalazimisha" nilisema.
" silazimishi ila ni lazima itolewe" tulibishana ndani
ya ofisi ya Abdul bila kuonekana wala kusikiwa na
abduli mwenyewe. Basi yule mwanamke wakijini
alipiga hatua kumfuata Abdul nikaona kama
nitacheza kidogo basi uyu mwanamke wakijini
anaweza Fanya kitu kibaya kwa jamaa yangu. Nika
ruka mpaka mbele kumzuia asipite lakini aliyeyuka
mbele yangu na kutokea nyuma yangu. Niliwaza
haraka sana nikaona nimshambulie kwa moto yule
mwanamke angalau kumzuia asifanye anachotaka,
nilirusha moto lakini ulipomkuta aligeuka kwa
hasira na kwa kasi ya ajabu akanikumba na kunitupa
chini uku akiwa amenikaba shingoni. Nilijitahidi
kujitoa lakini
Nilijitahidi kujitoa lakini hali ikawa ngumu
nikakumbuka kile walichokuwa wanakifanya
wanamaombi kule tunapo wafata kupambana nao
niliona nitumie njia yao kujikomboa maana ile
mbinu na maombi yao ni hatari kwa viumbe wa
kuzimu.
" usijalibu icho kutakuwa na matokeo mabaya sana"
alisema yule mwanamke wakijini uku akiniachia
shingo yangu.
Nilibaki nikikohoa tu pale chini uku nguvu zikiwa
zimeniishia. Nilimuona yule mwanamke wakijini
akimsogelea Abdul na kutaka kumgusa ili nibidi
nigeuke kama mtu wa kawaida ili angalau Abdul
anione.
" Abdul salii" Niliongea kwa kujivuta baada ya
kuonekana mbele ya Abdul lakini kama isivyo bahati
Abdul alishtuka kuniona mlendani nikiwa chini na
kutaka kusimama kukimbia akijua Mimi ni mzimu.
Lakini kabla ajasimama sawa sawa kwenye kiti
chake yule mwanamke wakijini alimgusa kichwani
na dakika hiyohiyo Abdul akashuka chini kama
mzigo na kupoteza fahamu.
" huyu ni sadaka usisahau hilo ila kwa matendo
yako nakuambia utaadhibiwa"alisema Yule
mwanamke wakijini. Basi yule mwanamke wakijini
akaja akanishika mkono na kuniinua juu.
" kabebe iyo sadaka yako muda ushaenda sana
tunatakiwa tukaitoe members wote wanatusubiri"
alisema yule mwanamke wakijini. Basi nilisogea
mpaka alipo lala abdul nikamnyanyua nikamweka
begani kisha yule mwanamke wakijini akaja
akanishika mkono wa kushoto na kwapamoja tuka
tokea lodge.
" kamweke chumba cha kafara" alisema yule
mwanamke wakijini, nikafanya ayo yote nikiwa
kimya bila kusema kitu.
Baada ya kumuweka mle nikaingia chumba cha
kubadili nguo nikavaa mavazi ya ibada kisha
tukatoka na yule mwanamke wakijini mpaka ukumbi
wa ibada na kuketi juu ya viti vyetu. Baada ya ayo
aliingizwa Abdul akiwa amwevikwa joho jeupe na
mikono yake ikiwa imefungwa kwa kamba ngumu,
nilipomuona roho iliniuma sana, basi alipigishwa
magoti na kuinamishwa kichwa chake na mchinjaji
akamsogelea nyuma yake tayari kwa amri yangu
Abdul achinjwe.
" LEO NAMTOA ABDUL RAFIKI YANGU
WAKIBINADAMU KAMA SADAKA" nilisema kujikaza
kama mwanaume tu ila roho iliniuma sana.
" Ha! Jack nimekufanyia nini ndugu yangu" alisema
Abdul baada ya kuisikia sauti yangu.
"HAKUNA ULICHOFANYA ABDUL ILA DAMU YAKO
INAMPENDEZA BWANA SHETANI" nilimjibu Abdul.
"Nisamehe ndugu yangu niachie jack nakuomba."
Alijitetea Abdul.
"SIWEZI KUKUSAIDIA ABDUL NENDA SHEOL
( KUZIMU)" nilijibu kwa mwangwi. Na baada ya
mchinjaji kusikia Sheol hakuwa na cha kupoteza
alimkanyaga Abdul mgongoni na kumfanya Abadul..
Baada ya IYO kafara tulirudi nyumbani kama
kawaida ila safari hii nikiwa nahofu kubwa moyoni.
" vipi mbona huna raha Leo? Aliuliza yule
mwanamke wakijini.
" nipo sawa mbona" nilijibu.
" unahofu ya kumtoa kafara rafiki yako? Aliuliza.
" ivi Leo yeye kesho simtasema ndugu yangu ?
Niliuliza.
" ee nawe aya mawazo yako tu" alijibu.
" kwaiyo haitatokea kutaka ndugu zangu" niliuliza.
" kunatiketi ya ndege inabidi uende America uko
utafanya kikao kule loss Angel kisha utapokea
adhabu yako" alisema yule mwanamke wakijini.
" adhabu ya nini tena" niliuliza.
" kwani ukuona ulivyokuwa unataka kuvunja
masharti ya ulimwengu huu" alisema na kunifanya
nikae kimya. Siku zilisogea mpaka siku ambayo
nilipanda ndege mpaka marekani ambapo tulishuka
kwenye ndege mpaka kwenye moja ya hotel tulio
amua kufikia tulikaa pale kwa siku tano na baadae
tulielekea kwenye moja ya mahall makubwa sana
ambako uko tuliingia kwenye hall la waabudu
shetani. Tulipoingia tu nilipokea kitabu kidogo na
kuongozwa mpaka viti vya mbele na kuketi,
nilipoketi nilikifungua kitabu ambacho kilijaa nyimbo
nyingi za kumtukuza shetani. Basi tulikaa mle ndani
kama masaa manne ambapo baada ya ayo masaa
wote tulinyanyuka na nyimbo sasa zikaanza
kuimbwa, kulikuwa na jopo la wanakwaya kabisa
ambao walikuwa wakituongoza kuimba zile nyimbo,
tuliimba na kadri muda ulivyokuwa unaenda
tulikuwa tukibadilika maumbo wote mle ndani na
sauti zetu zilizidi kuongezeka na mioyo yetu ilijaa
chuki isiyo ya kawaida na wala isiyo na sababu
yoyote dhidi ya binadamu wa kawaida.
" na damu ya mwanadamu imwagike milele "
ilikuwa moja ya shairi la wimbo ambao tulikuwa
tukiimba na kutujaza chuki dhidi ya binadamu
wakawaida. Tuliimba mpaka sasa tulipoanza kusikia
kama kinanda cha wimbo mzurii kikisikika, kwa
upande wangu niliacha kuimba ili nisikie uo wimbo
mzuri ni nani anaye taka kuimba maana mlio wake
ni mzuri hatari lakini hajabu ni kuwa kuta zote za
lilejengo tulilo kuwamo lilijaa mwanga mkali sana
na Mara mwanaume mrefu wa kadri aliingia
mwanaume mrefu wa kadri aliingia uku akiwa
amezingirwa na Vito vya thamani kila upande
alikuwa na mwendo wa taratibu sana na pozi nyingi,
hakuwa mwenye wasiwasi hata kidogo na alikuwa
mchangamfu sana, nilibaki kumshangaa kwani
sikuwahi ona mtu anaye pendeza namna ile japo
kuwa yule mwanamke wakijini alikuwa mzuri sana
lakini yule mwanaume aliyeingia pale alimzidi
kabisa yani, sikuwahi jua wala kuona mwaume
mwenzangu ni handsome nilikuwa sijui lakini yule
niliye muona kweli kati ya wanaume mahandsome
yule jamaa ni handsome.
" achakushangaa uyo Ndio shetani mwenyewe "
alisema mwanamke wakijini.
" mbona haendani na jina lake mbona anaonekana
mpole sana mstarabu na mwenye kupendeza"
nilijibu .
" ee basi uyu ndio shetani huu ndio muonekano
wake halisi" alisema yule mwanamke wakijini.
Wakati tunajadili ayo Mara mwanamke mmoja
mrembo wa kawaida akaingia kwa stahili ileile
aliyoingia nayo shetani.
" uyo mwanamke anaye enda karibu na shetani ni
nani au ni mke wa shetani " niliuliza.
" hapana sio mke wa shetani ila uyo ni Lilith
mwanamke wa kwanza kudai haki sawa mbele ya
mwanaume, uyo ni binadamu wakawaida kama
ulivyo wewe lakini tofauti yenu ni kuwa yule hafi"
alisema yule mwanamke wakijini.
" hafi! Kuna binadamu asiye kufa?niliuliza wakati
shetani bado yupo mbali kule akilakiwa kwa
shangwe.
" ndio hafi kwasababu uyo mwanamke alikataa
kumtii adamu akaondoka zake kwa vile yeye na
Adam waliumbwa sawa basi akaona kumtii
mumewe uyo sio sawa akaondoka na kujiunga na
shetani na basi baada ya Adam kuwa mpweke
ikabidi Eva aumbwe katika moja ya ubavu wa Adam
ili akatoka apo ataweza kumtii mumewe uyo lakini
kama unavyojua mwanamke Eva hakuwa na
mumewe hapo ndipo mmoja wa wenzangu
alimfuata na kumlaghai ale tunda na alipokula
akampelekea na mumewe ambaye ni adam lakn
adam hakushawishiwa na sisi ila yeye mwenyewe
aliamua kula kwa hiyali yake kwani aliogopa
kuendelea kuwa mpweke baada ya kujua Eva kala
lile tunda alijua lazima Eva atakufa tu Ndio adam
baba yenu akamua na yeye ale ili
Ndio adam baba yenu akaamua na yeye ale ili afe
na alipo kula tu wote walifunuliwa" alisema yule
mwanamke wakijini na kunifanya nishangae.
" lakini wakati uo yule Lilith hakuwepo sindio?
Niliuliza.
" ee hakuwepo alikuwa tayari amejiunga na shetani
na kuwa huru kutoka kwa mumewe wa kibinadamu "
alisema yule mwanamke wakijini.
" duh uo msala sasa! Kwaiyo saizi anaishi wapi uyu
mwanamke maana sijawahi sikia stori zake"
niliuliza.
" anaishi kuzimu na shetani " alijibu yule mwanamke
wakijini.
" hio ni baada ya Mimi na jeshi langu kukosea
kidogo tu na kupoteza ile vita mbinguni " aliingilia
shetani aliye kuwa amesimama umbali mlefu ndani
ya lile jengo na kwa maneno yake ukumbi mzima
ulitulia.
" vita! Vitagani? Nilijiuliza mwenyewe moyoni kwani
niliogopa kumuuliza.
" bado unawaza vita gani! Nitakuambia; Mimi na
wenzangu tuliamua kuchukua utawala wa mbinguni
lakini kuna kosa dogo tulikosea na pia aina ya
mashambulizi makali ya yule malaika mkuu ambaye
anafanya ulinzi kwa watu wako alitushambulia kwa
moto ambao sikupata kuuona kamwe ndio
tulizidiwa nguvu hapo na kusambaratishwa kabisa
mbinguni na mahali petu palifutika kabisa" alisema
shetani.
" mmmh! Ni yule mkuu nini? ndio aliwapiga"?
niliuliza.
" yule mkuu huwa hapigani na yoyote na hakuna
yoyote anaye weza kupigana naye" alisema.
Basi baada ya kusema ayo shetani alikuja mpaka
mbele kabisa aka keti na tafrija ikaanza kulikuwa ni
kuimba na kumtukuza yeye na baadae ripoti ya kila
kilichofanyika dunia ilitolewa ambapo wengine
walipongezwa na kupewa zawadi na wengine
nikiwemo na Mimi tulilaumiwa na kupewa adhabu
kulingana na makosa yetu, yule mwanamke wakijini
alieleza matendo yangu yote na kwa kupitia screen
iliyokuwepo pale ukutani kila kitu nilichofanya
kumzuia yule mwanamke wakijini asimchukue Abdul
kikionekana, basi kutokana na ayo matendo yangu
ambayo angalau yalionekana nafuu nilipewa adhabu
ya kuishi kuzimu kwa muda wa miezi mitatu niishi
kama msukule nikipangiwa Kazi ngumu mpaka
miezi iyo itakapo isha..
nikipangiwa Kazi ngumu mpaka miezi iyo itakapo
isha, upande wa wenzangu walihukumiwa kifo
kutokana na kutoa siri na kugoma kutoa kafara
kabisa waliwaelekeza watu wafanye kinyume kabisa
na sisi hata walio taka kujiunga na chama
waliwazuia kutokana na matendo yao walihukumiwa
kifo , na baada ya hukumu iyo walitokea viumbe wa
sio pungua mia moja walifika ndani ya lile jengo
walituchukua kila mtu kivyake walinifunga kamba
mikononi na miguuni kisha wakanibeba na
kutoweka nao Mimi mpaka kuzimu sehemu moja
ambayo sikuwa kufika wala sikujua kuwa kuna siku
nitafika. Lilikuwa ni eneo lenye mwanga hafifu
ambao ulitokana na giza zito na nguvu ndogo ya
mienge iliyo washwa mle ndani. Kulikuwa na watu
wengi sana mle ndani na wote walionekana
wamechoka mnoo maana walijilaza tu na kulikuwa
na harufu mbaya sana iliyokuwa pale, hewa ilikuwa
nzito sana na harufu mbaya ambayo baada ya muda
kidogo kupita toka niwekwe mle nilianza kuhisi
kuchoka na mwili kuishiwa nguvu na viungo vyangu
kulegea.
" nyanyukeni mkale sasa msipo amka na kula ni juu
yenu" alisema kiumbe ambaye hakuone vizuri
kutokana na hali ya hewa ya ugiza na mwanga
hafifu.
" amka twende tukale" nilimwamsha mtu mmoja
aliye kuwa jirani yangu, aligeuka kwa kujivuta na
kunitazama akajinyanyua kisha akasogea sehemu
mmoja hivi ambayo ilikuwa ni kama mlango au geti
akapita pale uku akipepesuka sana kama mlevi,
basi wengine nao walipomuona jamaa kasimama na
wote walisimama na kumfuata nikifuatiwa na Mimi.
" hiki ni chakula gani jamani? Niliuliza baada ya
kuona ni kama pumba limekorogwa na kupikwa
jikoni na kuchangwanywa na damu kiasi.
"Wewe kula kama hutaki ondoka " ilisikika sauti
nyuma yangu ikisema hivyo nilipo geuka nilistaajabu
kuwa muona mmoja wawale mashetani mekundu
nilikuwa naishi naye kule nyumbani akiniambia
Mimi maneno yale.
" yaani wewe kumbe ni msimamizi wa huku?
Nilisema.
" kula au uondoke" alijibu.
" Mimi sijazoe kula hivi kama mfugo unajua na kula
nini basi nisaidie nipate chakula kizuri" nilisema.
" kula au uondoke" alinijibu yule kiumbe.
kula au uondoke " alijibu tena yule kiumbe.
" lakini..aaaaaa!" Kabla sija maliza kuongea
nilichosema nilitandikwa na mkia wa taa alio kuwa
ameushika yule kiumbe na kunifanya nihisi maumivu
makali sana
" ondoka huku haraka " alisema yule kiumbe na
wakati najivuta kunyanyuka alinitandika tena naule
mkia nilihisi maumivu makali sana ambayo hata
sikuwahi ya hisi kabla alinitandika kila nilipokuwa
najivuta kutoka mle ndani ambapo misukule
mingine ilikuwa ikila. Nilipo fanikiwa kutoka nilienda
kujilaza chini mle ndani nikiugulia maumivu makali
ya kile kipigo.
" ondoka uende nje ungane na wenzako" ilikuwa ni
sauti ya kiumbe asiye onekana akinitaka nitoke,
basi nilijivuta kutoka nje nilipofika nilishangaa kuona
eneo moja kavu sana na kubwa sana kama hekali
elfu sita hivi na wale misukule wakilima huku
wakitandikwa na bakora kwa wale wanao onesha
ulegevu.
" chukua ilo jembe kaungane na wenzako" ilisema
tena ile sauti.
Na kunifanya nibebe jembe na kuungana na
wenzangu kulima. Nililima kwa nguvu nyingi
nikiogopa kupigwa na kuuliwa kama walivyo fanyiwa
wenzangu. Tulilima kwa muda mrefu uku sasa
nikihisi kuchoka na kiu ya maji na njaa Kali sana.
Wakati na endelea kulima kwa kuchoka na kwakiu
na njaa speed yangu ilipungua na uwezo wa kulima
vizuri ulitoweka sasa yule kiumbe msimamizi wa
mashamba alikuja na kunitandika fimbo
akinikazimisha niendelee kulima kwa nguvu na kwa
speed kama awali, lakini bila kujali kuwa
nilimwambia nahisi kiu na njaa na kuchoka.
" acha uvivu binadamu huku mbona utakufa usipo
weza kujisimamia" alisema yule kiumbe uku kipigo
kikiendelea kunihimiza nilime kwa nguvu.
Haliilikuwa mbaya siku ile yakwanza tu nimefika
niliwatizama wenzangu walio kuwa wamelala chini
wamekufa kwa kipigo na na kuchoka sana na kiu.
" kama mtatuua unazani nani atalima huku" nilisema
kwa uchungu na hasira ya maumivu ya kipigo
nilichokuwa nikikipokea na kunifanya ngozi yangu
kuchanika na kuwa na madonda kama wale
wenzangu.
* kwani wewe ukifa nani anajali inuka ulime au ufie
kondeni" alisema yule kiumbe..
kwani wewe ukifa nani anajali inuka ulime au ufie
kondeni umelala" alisema tena yule kiumbe
msimamizi wa mashamba. Basi niliinuka kulima
kwa kujikaza na kujituma huku mwili ukiwa
umechoka sana na unamaumivu makali sana ya
kipigo, nililima nikitegemea kuwa giza litakapo ingia
angalau tutapata nafuu ya kwenda kupumzika Kazi
ingeendelea siku inayo fuata lakini kwa kweli
haikuwa hivyo maana kule kuzimu hakukuwa na
usiku wala mchana na kulima ilikuwa ni bila
kupumzika zaidi ya kama dakika ishirini tu za
kwenda kula na kurudi kuendelea na kulima.
Baada ya kufanya Kazi ngumu na mateso ya kipigo
na chakula kisicho kuwa cha kawaida siku moja
nikiwa najiandaa Mimi na wenzangu kwenda kupata
chakula ili kuendelea na Kazi ambayo kimsingi
haiishi na wala hammalizi kuifanya nilimuona yule
mwanamke wakijini akiwa amesimama mbele
yangu akiwa mwenye uso wenye mashaka kiasi.
" kunanini mbona unaonekana hivyo" nilimfuata
kumuuliza maana niliona uwenda anataarifa mbaya
kuhusu Mimi.
" unahitajika kurudi duniani harka " alisema yule
mwanamke wakijini na kuufanya moyo wangu
kujawa na furaha isiyo ya kawaida ni kama vile
mkombozi amekuja kuniokoa. Basi alikuja na
kunishika mkono na moja kwa moja tulikokea kule
kule nyumbani .
Nilipofika duniani nilibaki kuangaza macho
kushangaa vitu maana japo nilikaa kwa muda
mchache kule kuzimu lakini ni kama nilikaa miaka
mingi kwa muda mchache mtu huweza kusahau vitu
vingi kuhusu dunia.
" kaoge kwanza baada ya apo utapokea jukumu
jipya" alisema yule mwanamke nikaenda kuoga
nilipo maliza walikuja wale Dada wakazi wakijini
kwaajili ya kuniandaa niwe na mwonekano mzuri
japo kuwa nilikuwa na nywele ambazo sasa zilianza
kupoteza mwonekano wake wa kawaida lakini
zilitengenezwa vizuri na kuwa safi na zakung'aa,
niliandaliwa vizuri nikavalishwa suti safi na kisha
nikatoka mpaka sebuleni alipo kuwa ameketi yule
mwanamke wakijini akitizama kipindi cha dini
kilichokuwa kikirushwa na kituo kimoja cha
television.
" umependeza sasa ila achana na makosa ya kijinga
maana...
umependeza sasa ila achana na makosa ya kijinga
maana kutoka kule ni kama bahati tu ila ukirudia
ukiambiwa ukae kwa siku ni sawa na umewekwa
kule mpaka ufe" alisema yule mwanamke wakijini.
"Sitofanya tena nimejutia! Haya nipe ilo jukumu sasa
nione nafanyaje" nilisema.
"Inatakakiwa ufuatilie sadaka za yule kijana alizo
ahidi kutoa na kuna watu wanapaswa kutengenezwa
kama wachungaji ilo la kwanza na lapili ni muhimu
alafu kuna jingine muhimu zaidi ambalo ndilo
utaanzanalo baadae kidogo ambalo ni muua
mchungaji Alex huyu kama ataendelea kuwepo
itakuwa ni shida ivi ninavyokuambia wanachama
nane wapo pale na tayari hatuwawezi ila kama ata
kufa basi hakutakuwa na hasara nyingine" alisema
yule mwanamke wakijini na kunifanya nishushe
pumzi kwa nguvu maana jukumu lililombele yangu
ni gumu mno.
" mchungaji mwenyewe ndio uyo kwenye TV ?
Niliuliza.
" ndio uyo baadae anatakiwa abaki story tu sawa?
alisema.
" sawa haina shida " nilijibu. Basi tulikaa mpaka
mida ya saa tatu usiku ambako tulitoka sasa mpaka
kwa yule mchungaji Alex kumtenganisha mwili na
roho yake. Tulipoingia tulimkuta yupo bize sana na
familia yake akiwaelekeza watoto wake maswala ya
shule basi yule mwanamke wakijini kwa nguvu ya
upepo alijigeuza joka kubwa linalowaka moto na
kutoka kwa kasi ya risasi kwenda kumvaa yule
mchungaji lakini ghafla alikuwa kama amegonga
chuma na kurushwa kwa nguvu ya ajabu na
kutoweka mle ndani. Nilipoona vile nijua kuwa sasa
inahitajika nguvu zaidi kumwangamiza uyu
mchungaji nilisogea mbele na Mimi kwa umbo la
nyoka lakini kabla sija mfikia nilisita baada ya
kuwaona wanaume wa wili waliovaa nguo nyeupe
sana wakiwa wamesimama mbele yangu na
mikononi mwao wakiwa wameshika mapanga
yanayo waka moto.
" hilo umbo sio lako na tabia hizi sio zilizokusudiwa
uzifanye" walisema wale wanaume wa wili kwa
pamoja na kunifanya ni rudi nyuma taratibu na
kutoweka ukunikiwaza kurudi muda mwingine
kwanza nikaangalie hali ya yule mwanamke wakijini
kisha tujadiliane juu ya wale wanaume wanaomlinda
yule mtu....
wetu.nilitoweka na kurudi nyumbani ambapo
nilimkuta yule mwanamke wakijini akiwa amelazwa
chini akiwa na majeraha mabaya sana mwilini
mwake.
" itabidi uongeze watu yule mchungaji anatakiwa afe
usiku huu" alisema mmoja wa wale watumishi
wakijini walio kuwa wamemzingira yule mwanamke
uku wakimtizama kwa huruma.
" msaidieni sasa apone uku Mimi nikipndoka na
kikosi kwenda kupambana" nilisema vile maana
niliona nikigoma basi nitarudishwa kuzimu kwenye
adhabu ambako nitateseka kule.
" huyu haponi tena atachukuliwa tena sio muda na
kwenda kufungwa kwenye gereza la roho hatatoka
huko mpaka kaiama" alisema tena yule mtumishi
wakijini na kunifanya moyo kunilipuka maana partner
wangu ndio anakwenda zake. Wakati tukiongea ayo
na kuwaza joto Kali mno ililikumba ile nyumba na
moto mkali unaotembea kwa kasi sana ulikuwa
ukitufuata na wote tulikimbia pembeni na kumwacha
yule mwanamke wakijini pale chini na moto ulipo
mfikia ulimtiwesha kabisa hapo ndio nikaamini hizi
Kazi za kichawi zinahatari sana na wakati
nikishuhudia hayo Mara joto lilizidi kutawala mle
ndani na Moto mkubwa mwekundu wenye kasi ya
ajabu ukawa unatufuata sisi pia kwa kasi.
" umechelewa tayari usinge rudi nakuambia
tutakwisha umelipoteza lodge la Freemasonry katika
Nairobi na watu watatakiwa kusali kwenye hall la
Tanzania ume leta madhara kwa kushindwa kwako
umekosea tunapoteza nguvu yetu Kenya" sauti ya
lawama niliisikia wakati hali mle ndani imeisha
kuwa mbaya sana nilicho waambia tu wale
wanawake wakijini ni kukimbia kila mtu kivyake
lakini hajabu hakuna aliye kimbia wote walipiga
magoti na kuinama chini na kuliwa na ule moto uku
wakinieleza kuwa saa imefika. Lakini kwangu
nilikuwa na ubinadamu wangu sikuona shida
nilitoweka mle ndani mpaka nyumbani Tanzania
tanga ndani ya nyumba ya wazazi wangu nilifika
ndani ya chumba changu na kukaa mle chumbani
lakini katika hali isiyo ya kawaida moto ulifumuka
kutoka ardhini juu ya bati na kwenye kuta za moto
kunishika mwilini. Nilikuja kushituka nikiwa
hospitalini..


MKASA; TAMAA ILINIPELEKA KISIWA CHA MAJINI
MWISHO
Nilikuja kushituka nikiwa hospitalini nikiwa
nimezungukwa na ndugu zangu wate. Marehemu
Jackson akiwa hospital aliwaadisia ndugu zake
mkasa huu na siku chache baada ya kuadisia na
kupatiwa matibabu aliamishiwa hospitali ya
muhimbili kwa matibabu zaidi juu ya kuharibika
vibaya kwa mwili wake na December 12 mwaka
2018 Jackson abel aliaga dunia akiwa hospitali.
Mkasa huu umehadisiwa na kaka yake mkubwa kwa
kuficha nakupunguza baadhi ya matukio ya kutisha
ila umeletwa kwetu angalau kujifunza mawili matatu
japo kuwa umefupishwa na kukata matukio ambayo
sio yote yanaweza kuandikwa.

Safi sana... Story nzuri....

Chapter Closed...



Cc: mahondaw
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni http://www.equatorstory.com/
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom