Inaendelea...sasa mnafanya nn usiku wote huu"? niliuliza nikimgeukia.
" tunaenda kuzimu kupanga mipango ya siri" Alisema.
" siri ipi" Nilimuuliza
" hapana kalale wewe ni binadamu mengine kujua haitawezekana" Alisema .
" isiwezekane kivipi na wakati tunafanya kila kitu pamoja vipi tena tunaanza kutengana" nilisema ayo kwa lengo lakutaka kujua tu wanachofanya.
" unakifua wewe"? Aliniuliza.
" ndio ninacho" nilisema.
" basi nifuate " Alisema.
Nilimfuata tukaingia ndani ya moja ya chumba ambamo ndani yake kuna viumbe vinatisha sana walikuwa wekundu kama damu na wembemba sana walikuwa hawana nguo wala hawana jinsia kama binadamu walikuwa na jicho moja katikati ya kipanda uso na mikono myembamba yenye kucha ndefu kama zatai, miguuni Ilikuwa kama desturi yao walikuwa na kwato na pua walikuwa na tundu moja nalo lilikuwa kama tundu la fuvu la mtu walikuwa na meno marefu kama ya simba , walipotuona tunaingia walirudi nyuma wote wakawa wanatutizama
" fungueni mlango enyi mashetani wekundu" Alisema yule mwanamke wakijini na Mimi hapo ndio nikafahamu kuwa wale ndio red devil, mlango ulifunguliwa kutokea chini ambako kuli kuwa kunafuka moshi mzito sana kama kule chini kuna moshi.
" sasa ndio tunaenda wapi" niliuliza maana niliona pale apapitiki na atapita nani kwenye moto.
" iyo ndio njia nauo unaouogopa ni moshi wakuzimu lakini kwa sasa usijali hauna shida labda baadae " Alisema yule mwanamke.
" baadae kivipi wakati wa kurudi au? Nilimuuliza.
" hapana bwana tuachane na ayo ngoja nitangulie" Alisema yule mwanamke na kuingia mlendani na Mimi nikifuata kwanyuma. Tulipoingia tulijikuta tukielea juu kwa muda wa kama dakika 30 na baadae kutua eneo tulivu lililotulia sana,
" unaliona ilojengo refu"? Alisema yule mwanamke.
" ndio naliona mbona lipo ivyo? Nilisema maana lilikuwa kimuonekano ni jengo lakini ukilitazame tena ni kama mtu yaani halikueleweka ni kitu gani maana lilikuwa likibadilika badilika.
" iyo nyumba ndimo baadhi ya watu Fulani ambao hawataki kujiunga na dini yetu ila wanataka miujiza huja hapa kupokea izo nguvu
.....sasa nifuate" Alisema tena.namimi nikawa namfuata baada kama ya atua kadhaa nilishangaa kuona joka kubwa likiwa mbele yetu nikisema kubwa na maanisha kubwa kweli basi ilinibidi nisimame tu nikilitazama
" ngoja baada ya muda ataufungua mdomo wake nayeye atatupeleka mpaka ukumbini maana wenzangu wameshawasili " Alisema yule mwanamke na kweli baada ya izo dakika akafungua mdomo na sisi tunaingia kama tunaingia pangoni na kisha akaufungu mlango, nilitarajia kuona giza mlendani lakini mambo yalikuwa ni tofauti na mategemeo yangu kwani miale ya moto Ilikuwa ikiangaza mlendani ya mdomo wa lile joka utasema tumboni mwake anawaka moto.
" usishangae huyu sio nyoka wakawaida" alinieleza yule mwanamke wakijini
"Ni jini na yeye ? Niliuliza.
" ndio ila yeye yupo kwenye sekta ya usafirishaji" Alisema .
" ha! Kwaiyo sekta ya usafirishaji wewe mwenyewe ndio unakuwa msafirishaji? Niliuliza.
" ndio uku sio kama uko duniani mtu akipewa nafasi basi ni mapumziko kwake badala ya wajibu" Alisema yule mwanamke.
" anha! Sawa bwa....niliishia hapo baada ya kuona mdogo walile joka unafunguka.
" tumefika? Niliuliza.
" hapana ila nahisi kunashida " Alisema yule mwanamke wakijini.
" shida! Kivipi? Niliuliza.
" mmh tutoke kwanza" Alisema yule mwanamke. Tulitoka nje lakini nilishtuka baada ya kuona moto ukitoka juu unashuka chini.
" tukimbie" nilisema baada ya kuona ali sio nzuri.
" hapana usijalibu kukimbia tulia hapo ngoja tuone kitakacho tokea" Alisema yule mwanamke wakijini. Moto ule ulikuja kwa nguvu ya ajabu na kuingia chini ya shimo lililokuwa mbele yetu na kurudi juu kwa kasi ile ile na kusababisha wote kutupwa pembeni maana ule moto ulikuja kwanguvu ya ajabu ambayo ili tutawanya wote tuliokuwa tukishangaa.
" amekombolewa tayari" Alisema yule mwanamke wakijini kwa masikitiko.
" nani? Niliuliza uku nikijinyanyua kutoka pale chini nilipokuwa nimetupwa Mimi na viumbe waliokuwa kule chini.
" acha bwana sio muhimu kwa sasa" Alisema yule mwanamke akiwa amejilaza pale chini alionekana amekata sana
acha bwana sio muhimu kwa sasa" Alisema yule mwanamke akiwa amejilaza pale chini alionekana amekata sana tamaa kwa kile kilicho kuwa kimetokea.
"Mbona unaonekana umefadhaika sana" niliuliza ili nione atajibu nini.
" alikuwa ni muhimu lakini kabla hatujaja kumjadili namna ya kumtumia Bwana wa roho zote ametuma nguvu imuokoe dah! tumepoteza apa dah" aliongea kwa masikitiko makubwa sana na nilipotupa macho kutizama kila upande niliona pia wale viumbe wa kuzimu wakiwa wamekaa chini uku wamejiinamia na kunifanya NA Mimi kuwa na hamu ya kujua ni nani aliye twaliwa apa na alikuwa anaumuhimu gani adi asababishe huzuni kutawala uku kuzimu,
" twende basi uko kikaoni muda siunaenda" nilisema hivyo maana nilijua nikifika uko ukumbini ningejua nini kinaendelea maana nilijua swala lile lazima lingejadiliwa kikaoni mle.
" turudi tu duniani" Alisema yule mwanamke wakijini uku akijinyanyua.
" kwaiyo kikao hakipo? Niliuliza.
" ndio sasa apa tujadili nini?alijibu.
" kwanza tukio pili ajenda iliyo takiwa kujadiliwa" nilisema maana nilikuwa na hamu ya kuwajua vizuri mashetani.
" hapa sio duniani kama kitu kikitokea unaweza kutafuta njia ya kukitatua huku tatizo likitokea ujue lipo nje ya uwezo wetu na halina njia ya kulilekebisha kama ambavyo tulikosea tulipokuwa mbinguni na hakuna njia ya kupona basi ujue hata ili lililotokea ujue hakuna njia na kama ukijitia unauchungu sana kama ni mwanadamu ujue umekufa na kama ni shetani ujue unafungwa kwenye giza la kiroho maisha yako yote ukisubiri ili siku na kuhusu ajenda ndio iyo iliyoondolewa mbele ya macho yetu wote na usiniulize alitwaliwa vipi maana umeona" Alisema yule mwanamke wakijini na kunifanya ni baki na shangaa tu huyu Bwana wa roho zote basi anatisha sanaa maana kilicho tokea ni hatari tupu.
"Tulitembea hatua kama kumi kisha wazo likanijia kuhusu wale watoto wawana maombi tulio wachukua kwaajili ya kafara.
" vipi kuhusu wale watoto kule nyumbani? Nilimuuliza.
" nyumba ipi yenye watoto? Aliniuliza kwa kunishangaa.
" he! Unashangaa
..."he! Unashangaa nakuniuliza wapi kwenye watoto kwani umeshasahau kilichotokea Leo mchana? Namimi nilieleza kwa njia ya swali huku nikimshangaa.
" kama kuna watoto nyumbani ngoja tukawaone"aliongea yule mwanamke wakijini na kunifanya ni baki namshangaa.
"Au kile kichapo alichokipata pale kwenye mapigano kimemuondolea kumbukumbu vizuri nini"? Niliwaza mwenyewe.
" Mimi kumbukumbu ninazo vizuri ila nataka na Mimi nikaone ao watoto" alijibu yule mwanamke wakijini akijibiza mawazo yangu.
"Mmmmmh" niliguna baada ya kuona amegundua mawazo yangu.tulitembea kwa umbali Fulani kisha tukashikana mikono na kuanza kupaa taratibu tukirudi duniani, tulipo fika umbali wa kama mita mia toka kwenye ardhi ya kuzimu tuliongeza kasi na ghafla tukajikuta nje la lango ambalo lilifunguliwa na wale mashetani wekundu.
" twende tukawaone ao watoto " Alisema yule mwanamke wakijini.
"OK twende kule kwenye kile chumba" nilisema na kuanza kuelekea mle chumbani.
" vipi mbona una shangaa" Aliniuliza yule mwanamke wakijini baada ya kuona nimepigwa na butwaa kushangaa kile kilicho kuwa kule ndani.
" inamaana hawa watoto waliondolewa humu ndani? Niliuliza.
" yaani mambo yote yale ulitegemea uwakute umu ndani kama wewe nani" Alinijibu hivyo lakini sikupendezwa na namna alivyokuwa akinijibu nilijua Wenda mambo yaliotokea kule ndio maana kajikela.
" naenda zangu kulala wewe kawange" nilijibu na Mimi kwa hasira maana alinikera kwa majibu yake.
" unanambiaje" aliuliza.
" umesikia achakiburi basi" nikajabu uku naingia zangu chumbani.
" mfyuuuuuuu" alisonya kwa hasira lakini wala hatasikugeuka nikaingia chumbani na kujirusha kitandani. Haikupita dakika usingizi ulinipitia maana nilikuwa nimechoka sana.
" mpaka saivi unalala amka unywe chai" Alisema yule mwanamke wakijini na kunishtua kutoka usingizini.
"Ooh za asubuhi? Nilimsalimia.
" mbaya kiasi kunamtu anareta mchezo kati ya wale wanachama wapya mmoja analeta utani anasahau kiapo chake" Alisema yule mwanamke.
" nani uyo na kwani kafanyaje? Niliuliza.
Amekiuka kiapo chake usiku wa kuamkia Leo amekusanya wa chungaji akidai kuwa amebadilika na mbaya zaidi wamekubaliana kutoa ushuhuda kwenye kanisa lao kesho kwenye ibada yao ya jioni" Alisema yule mwanamke wakijini uku akinitazama usoni.
"Nini!? Niliuliza kwa hamaki kwani niliona kijana anampango wakunipanda kichwani.
" ndio hivyo" alijibu yule mwanamke wakijini.
Nilisimama kwa hasira nikapiga goti kama ilivyo kawaida nikaongea maneno ya kufuru kuu kisha nikatoweka kutoka mle ndani.
"Sasa ndio unafanyaje? Alisema yule mwanamke wakijini baada ya kutokea nyuma yangu ndani ya lodge.
" nataka nimfuate uyu mjinga hawazi tupanda kichwani ivi" nilisema kwa jazba.
"Usijali swala lake Lucifer mwenyewe kaliona ataagiza nguvu zaidi na baadae utaiongoza iyo nguvu uko kwenye ibada yao watakayo ifanya nanafikiri wataifurahia maana wameyakoroga nauyo mpuuzi akitiwa mikononi itabidi achinjwe mbele ya member wa hii lodge" Alisema yule mwanamke wakijini na kuja kunishika mkono na Mara tukatokea nyumbani.
"Kunywa kwanza chai alafu punguza hasira maana ukiwa na hasira utashindwa kuwa na maamuzi mazuri " aliongea yule mwanamke wakijini nikabaki namshangaa toka lini mashetani yakahimiza mtu asiwe na hasira.
"Wewe kunywa chai usiwaze sana" alijibiza mawazo yangu yule mwanamke wakijini kisha akaniaga anatoka Mara moja hato kawia kurudi kisha akatoweka, nilimaliza kunywa chai nikaoga nikatoka nje kwenye bustani nzuri ya maua nikaenda kukaa chini ya mti uku nikisoma kitabu cha kishetani cha mashujaa wakishetani nilikaa pale mpaka nilipoitwa kuwa chakula cha mchana tayari nilikula lakini ajabu yule mwanamke wakijini haukuwepo bado nyumbani, moyoni nilianza kuingiwa na hofu Wenda amekumbana na wanamaombi uko au mtu anayesali akawa kwenye kwenye matatizo.
" ili jini lipo wapi lakini? Nilijiuliza mwenyewe.
"Mimi hapa" alitokea yule mwanamke wakijini nyuma yangu.
" ulikuwa wapi wewe? Niliuliza kwa ukali kiasi kwani Mimi mtu kunifanya nimhofie huwa sipendi kabisaa.
....." nilienda kufwatilia wale wachungaji na yule kijana" Alisema.
"Haya umegundua nini sasa? Niliuliza.
" sio nilienda nigundue kitu ila nilitaka kufwatilia mienendo yao wote ili baadae saa kumi na moja wakikutana tuwaoneshe nguvu " Alisema yule mwanamke.
"Sasa ungesema ungechelewa basi maana nikajua tayari uwenda ushakutwa na matatizo uko" nilisema.
" matatizo ni kawaida ila Mimi usiniofie sana siwezi kufa" Alisema yule mwanamke wakijini. Basi tulikaa tukipiga stori za kawaida mpaka pale tulipoona nyumba inatikisika kama kuna tetemeko kubwa.
" nini hii" nilijisemea huku nikijinyanyua kwatabu nikitaka nikimbilie nje kukwepa kudondokewa na nyumba.
" usijali tulia tu izo ni nguvu tayari zimetumwa kwaiyo ngoja kutulie kisha unifuate" alisema yule mwanamke wakijini na baada ya kama nusu saa ivi kukatulia na yule mwanamke wakijini alinyanyuka na kunipa ishara nimfuate, nikamfuata mpaka ndani ya chumba kimoja kilichokuwa mle ndani tulipoingia nilishangaa kidogo kuona kila kitu mle ndani ni chekundu kwanzia kuta adi sakafu na vyote vilivyokuwapo kule ndani.
" vua izonguo zako vaa izi" alisema yule mwanamke wakijini uku akinipa nguo nyekundu sana ambazo zipo kama joho Fulani lakini uo ni muonekano tu lakini kulivaa ni kama ovaloli lakini ukinitazama nikama nimevaa joho.
" hii ninguo ya namna gani!? Niliuliza
" hii ni nguo ya ushindi nguo ya nguvu ambayo uvaliwa siku za hatari kubwa sana kwaajili ya vita kubwa na kwa vile wale wachungaji hawana nguvu sana basi Leo wataifurahia nguvu yetu wao niwatu wania mbili basi watajutia kupita kwenye njia iliyofungwa" alisema yule mwanamke wakijini. Basi nilivaa nikavaa na viatu vilivyoundwa kwa ngozi ya binadamu na ya nyoka kwa muonekano viatu ivi vilikuwa kama buti za askari ila tofauti ya izi buti nikuwa hazina soli kiufupi kiatu kizima kili kuwa kama nimevaa soksi tu.
"Vaa ichi kitambaa " Alisema yule mwanamke wakijini.
" mbona kinamatusi matupu? Nilimuuliza yule mwanamke.
" ndio kwani yule mnyama umemsahau yule aliye vaa vile vilemba? ALIULIZA..
"Vaa ichi kitambaa " Alisema yule mwanamke wakijini.
" mbona kinamatusi matupu? Nilimuuliza yule mwanamke.
" ndio kwani yule mnyama umemsahau yule aliye vaa vile vilemba vya makufuru? Alisema.
" nmekumbuka" nilisema.
" basi yule aliruhusiwa kupigana vita juu ya watu wayule mkuu nakuwashinda, alipewa mamlaka juu ya kila kabila,ukoo,lugha na taifa. Wote waishio duniani watamwabudu isipokuwa tu wale amabao majina yao yameandikwa tangu mwanzo wa ulimwengu katika kitabu cha yule mkombozi wao , basi aliye na masikio na asikie , yule aliye pangiwa kuchukuliwa mateka lazima atatekwa, wakuuawa kwa upanga atauawa kwa upanga. Hivyo watu wa yule mkuu wanapaswa wawe na uvumilivu na imani.
" beba na hii" Alisema yule mwanamke wakijini uku akinipa fimbo ya dhahabu ambayo nilijua Kazi yake.
" haya tutoke" Alisema baada na yeye kuvaa kama Mimi.
Tulitoka nje nilichokiona uzalendo ulinishinda nilitamani kurudi ndani kwa woga.
Kulikuwa na watu kama maiti walikuwa wameviligwa sanda mwili mzima adi usoni hakuna kilicho kuwa kikionekana zaidi ya macho ambayo yalikuwa yanawaka moto, kila saa walikuwa wakitoa sauti za ngurumo za kutisha sanaa na nyuma yao walikuwa na mikia kila mmoja.
" tuondoke wanatusubili sisi ao " Alisema yule mwanamke wakijini.
" aisee mbona wanatisha sana" nilisema.
" achana na ayo wewe upaswi kuogopa" Alisema.
" haya tuondokeni jamani" nilisema uku nikijikaza kama mwanaume lakini wale viumbe walinitisha sana maana toka mdogo naogopa sana viumbe wanao onekana ivi.
Walianza wao kuondoka kwa kasi ya ajabu na kusababisha upepo kuvuma sana eneo la pale nyumbani na kila walikokuwa wakipita wali sababisha vumbi na upepo mkali sana.
Wakati wao wapo mbele sisi tupo nyuma tunawafuata kwa kasi ile ile.
Lakini moyoni nikiwaza namna ya kumfanya uyu kijana aliyetusaliti na kutaka kutoa siri zetu kama ushuhuda mbele ya waamini wenzake na mbele ya wachungaji.
"Tubadili uelekeo kunja uku kushoto" Alisema yule mwanamke wakijini uku nayeye akifanya kama alichonambia nifanye.
"tunaelekea wapi? Niliuliza.
" kunamtu tunapaswa kumzuia kabla hajafika kule kanisani maana kama atafika basi hakuna tutachokifanya" Alisema yule mwanamke wakijini.
" nani? Niliuluza.
" ni muumini ambaye sasa ivi tunamkaribia lakini huyu ni hatari kwetu na inapaswa tumzuie na hivi ndivyo tunavyo Fanya" Alisema yule mwanamke wakijini na kutua katikati ya barabara ya rami ambapo magari yalikuwa yakipita kwa kasi.
" nishike mkono " Alisema yule mwanamke baada ya Mimi pia kutua pale pale katikati ya barabara.
Nilipomshika mkono Mara kitu kama shimo likatokea katikati ya barabara na moja ya gari la abiria basi lilipojaribu kukwepa lile shimo moja kwa moja liliserereka na kudondoka na kuiziba njia ambapo ili sababisha foleni kubwa sana.
" sasa jigeuze binadamu na ukachomoe Betrii kwenye ile pale gari yenye (no.K...) Nilijigeuza binadamu kama kawaida nikaifwata ile gari ambayo dereva wake alishuka kwenda kuangalia ajali iliyotokea ambayo ili sababisha foleni.
Nilifungua boneti nikachomoa nyaya kwa uangalifu kisha nikatoa betri nikarudi mpaka pale alipokuwepo yule mwanamke.
" haya Kazi nzuri sasa tuondoke wenzetu wameshafika kanisani tayari" Alisema yule mwanamke wakijini.
" sasa ili betri lanini Mimi? Niliuliza uku tukiwa angani taratibu tukianza safari ya kuelekea kanisani.
" utalitupa mbele ila kazi imeenda vizuri" Alisema yule mwanamke.
" kwani yule ni nani na kwanini tumefanya yote haya" niliuliza
" yule ni muumini wa kawaida ila hakuna anaye jua uhatari wake kwaiyo pale tumesababisha foleni ambayo itamchelewesha kuja kanisani na pia kuchomoa betri ni kumkatisha kabisa tamaa kuwa hawezi kuja kanisani kwa vile gari yake vyovyote vile haiwezi kutembea bila betri na hawezi kuiacha pale barabarani kwaiyo atatakiwa aivute mpaka nyumbani na wakati wote uo sisi tunamaliza Kazi kule bila shida" Alisema yule mwanamke wakijini na kunifanya nijue kuwa sio kila kitu kinacho tokea ni bahati mbaya ila huwa kinakuwa kinapangwa kwa ustadi mkubwa tu.
"Unaweza kuliachia" Alisema yule mwanamke wakijini baada yakufika mita chache kutoka kanisa lilipo..
Unaweza kuliachia" Alisema yule mwanamke baada ya kufika mita chache kutoka kanisani.
Nikaliachia na kuendelea na safari kufika pale kanisani.
"NIKWELI UPO TAYARI KUYAPOTEZA MAISHA YAKO ULIYO MZAWADIA LUCIFER KIRAHISI HIVYO" Niliongea katika mazingira ya kutoonekana lakini kimsingi nilikuwa Mimi na wale mashetani tulikuwa tayari tumejazana mle ndani na kusababisha joto Kali kwa wote walio kuwa mle ndani maana hata feni hazikumudu kitu zilipo washwa.
Yule kijana msaliti alipo sikia hivyo alikurupuka mpaka kwa wachungaji ambao muda ule walikuwa wanajiandaa kwaajili ya neno baada ya kusifu na kuabudu kumalizika.
Kila mtu pia mle ndani alinyanyuka kwani waliingiwa na hofu baadaya kusikia sauti nzito na yakutisha iliyoongea kwa utaratibu sana.
" hamuwezi kumchukua Mwana wa aliye juu nyinyi mashetani waovu" Alisema mmoja wawachungaji.
" hahahaha unamjua uyo kijana vizuri au unaongea tu" alijibu yule mwanamke wakijini kwa swali.
" nawaamuru mtoke kwa jina la.....puuuuuuuuuuuuuu! Moto ulifuka mle ndani na moshi mzito ulio mfanya yule MCHUNGAJI na wenzake washindwe kumalizia sentence yao maana walichotaka kutufanya kilikuwa ni kitu kibaya sana.
" muue yule MCHUNGAJI kisha tuondoke na target yetu" nilimwambia yule mwanamke wakijini afanye vile maana niliona mambo yatakuwa magumu kama yule MCHUNGAJI jeuri atabaki hai.
"Slash" yule mwanamke wakijini Alisema na Mara kichwa na kiwili wili cha yule mchungaji vikatengana.
" muwahi adui kabla haja kuwahi" Niliongea huku nikitabasamu niliona nimepata mafanikio makubwa duniani ambayo nilikuwa hata sijui niyasemeje.
" tuondoke wale mashetani wengine watamalizana na wale waimbaji wanao sumbua pale" Alisema yule mwanamke wakijini uku akiwa amemviriga yule kijana kwa mkia uliomuota nyuma yake.
Sekunde chache tulikuwa nje yakanisa tukitokomea zetu baada ya kufanya tukio la kutisha sana.
" mfungie umo ndani" Alisema yule mwanamke wakijini baada ya kufika kwenye lodge ndani ya chumba cha kafara. Basi nilimfungia kisha tukaondoka zetu kwenda
mfungie umo ndani" Alisema yule mwanamke wakijini baada ya kufika kwenye lodge ndani ya chumba cha kafara. Ee nilimfungia kisha tukaondoka zetu kwenda nyumbani uku moyoni nikiwa mwenye furaha sana.
"Tulikaa nyumbani tukisubiri muda ufike mida ya saa tano usiku member wote wanapaswa washuhudue kifo cha msaliti.
" KANISA LA..... LAVAMIWA NA WATU WANAO SHUKIWA KUWA MAGAIDI WALIMUUA MCHUNGAJI MWENYEJI NA KUWAUA WACHUNGAJI WAGENI NA KULICHOMA MOTO KANISA ZIMA NA KUUWA WATU WANAOKADILIWA KUFIKIA MIATATU" moja ya channel ili kuwa ikieleza tukio la kutisha ambalo lilitokea kanisani pale ambapo tulienda kupambania mtu wetu.
" Leo nitofauti na sikuile" nilisema uku nikimtazama yule mwanamke wakijini.
" ndio ni tofauti kutokana hatukufanya kosa alafu pia ni kutokana na nia za wale wachungaji yaani walikosea pa dogo sana ndio maana tumeshinda Leo" Alisema yule mwanamke wakijini.
"Walikosea wapi? Niliuliza.
" walitaka wawemaarufu kupitia uyu kijana msaliti walisahau sheria ya yule mkuu kuwa hapendi mtu kujikweza ndio maana umeona tumeweza kuwapa kipigo cha haja wale wachungaji na waumini wao" Alisema yule mwanamke wakijini.
" basi balaa inamaana watu wote wale mtu aliye imara ni yule jamaa tulio mzuia kule barabarani" nilisema
" ndio unajua wengi wao huenda kule kanisani wakiwa wanamatatizo yao sio kuwa wanamwabudu yule mkuu sana ila wao uenda kupata uponyaji tu nje ya apo ni wachache sana wanao enda kwaajili ya kumshukuru na kujifunza vitu vipya na maagizo mapya kutoka kwa yule mkuu sana" Alisema yule mwanamke wakijini. Tuliendelea kupiga story mpaka saa tano usiku ambapo tuliondoka nyumbani kwa njia za kishetani adi kwenye lodge letu la ibada kwa shetani.
" mleteni yule kijana msaliti apewe haki yake na kwahaki yake litakuwa funzo kwenu na kwa yoyote atakaye kiuka kiapo chake"Niliongea baada ya nusu saa toka tufike pale lodge na kuingia mle ndani kuendesha ibada za kishetani.
Aliletwa yule kijana akiwa amevalishwa joho jeusi lenye picha ya Lucifer aliye chukuia mbele ya kifua chake kisha..
Aliletwa yule kijana akiwa amevalishwa joho jeusi lenye picha ya Lucifer aliye chukuia mbele ya kifua ya lile joho.
" Leo damu ya uyu msaliti itafanywa kinywaji ndani ya lodge hili na atachinjwa kama njia ya kuongeza wafuasi wapya kwa kila tone la damu yake italeta mtu mpya kwa Lucifer " Alisema yule mwanamke wakijini katika mazingira tuliyo zoea yakutoonekana kwa wale member wa ile jamii ya siri ya kishetani.
Alipigishwa magoti yule kijana na bakuli kubwa jekundu likawekwa mbele yake akainamishwa kichwa kuelekea kwenye bakuli lile na kisu kikali chenye mpini wa mifupa ya mtu kilitolewa na kumeremeta kwa mng'ao wake, basi mchinjaji alikinyanyua juu na kisha kukipeleka taratibu shingoni mwayule kijana na kuanza kumchinja yule kijana mpaka alipokitenganisha kichwa na kiwili wili cha yule kijana na kukinyanyua juu uku akiacha damu za kile kichwa zikimwagika chini ya sakafu ya lile lodge la shetani, aliweka kichwa chini na kumshika vizuri yule kijana aliye chinjwa uku akielekeza shingo yayule kijana ndani ya lile bakuli ambalo lilijaa damu ambayo ilikuwa ikiruka kutoka kwenye mishipa ya shingoni ya yule kijana aliye chinjwa. Kitendo kile kilinifanya nijisikie vizuri mpaka kufikia hatua ya kumnyanyua yule mwanamke wakijini na kumkubatia mlendani ya lodge.
"Jamani mmeona kilichotokea hii sio kwa wenyeji ila nikwenu wageni ivi ndivyo msaliti anavyopaswa kutendewa hakuna upendo kwa yeyote asiyempenda Lucifer nakuyafanya maislahi ya Lucifer kuwa kwenye tisho uyo atakatwa kichwa tu na hakuna namna" alisema yule Mzee mwongoza ibada ambaye anaonekana.
" kila mmoja wetu atakunywa damu ya uyu mwenzetu na kesho asubuhi itabidi wote tukauzulie mazishi yake uko kwao ambapo taarifa za kifo chake kilisha tangazwa tayari kwaiyo prince of Kenya na madam wasio onekana kesho wataonekana wakiwa mochwari kuuanda mwili kwaajili ya maziko na pia watakuwapo kila hatua mpaka uyu mwenzetu atakapozikwa kisha jioni tutafanya maziko yetu humu kwenye lodge" aliongeza kusema yule Mzee kiongozi wa ibada..
Basi baada ya yote yale tulirudi nyumbani na asubuhi kama kawaida yule mwanamke wakijini alikuja kuniamsha nikaoga nikanywa chai tayari kwa safari ya kuelekea mochwari kwaajili ya kumuandaa marehemu.
" unajua Mimi aya mambo sijawahi Fanya ujue" nilimweleza yule mwanamke wakijini baada ya kufika mochwari.
" sio wewe tu ata watu wengine wa kawaida hawajawahi Fanya ila sasa wewe utafanya" alisema yule mwanamke wakijini. Alimgeuza yule marehemu akamlaza kifudifudi aka mchana kwenye uti wamgongo na kumwingiza nyoka maeneo ya mgongoni kisha akaniambia niambia nimshone yule marehemu kwa kutumia nyuzi zilizokuwamo mule ndani, basi nilimshona kama alivyonielekeza na yeye akawa anachanganya vitu atasikufwatilia alichanganya nini na baada ya kama nusu saa nilimaliza na yule mwanamke wakijini alimgeuza tena yule marehemu na kumpasua kifuani upande wa moyo kisha akachomoa moyo na kunikabizi nishike alafu akachukua nyoka mwengine akamweka pale ulipokuwa moyo kisha akanipa Kazi ya kumshona, nilimaliza kumshona kisha tuka chukua maji ambayo yalichanganywa na Dawa tukaanza kumuosha na kukinga maji yanayo mwagika kutoka kwenye ule mwili tunao uosha, tulipo maliza yule mwanamke wakijini alitoweka na kurejea kama dakika tano baadae.
" weka uo moyo umu alafu tumvike suti hii nyeusi yenye nembo yetu na Pete kisha, basi nilifanya kama alivyo sema na kuanza kumvalisha suti na pete, baada ya ayo alichuku ule moyo yule mwanamke na kutoweka na tena ndani ya dakika tano alirudi akiwa na jeneza kichwani nikampokea kisha tuka mweka yule marehemu mule ndani na kulifunga jeneza.
" ha! Unajua tumesahau kitu" alisema yule mwanamke.
"Kitu gani? Niliuliza.
" fimbo ni muhimu ile itazuia watu wasione maeneo ya shingo kuwa alichinjwa" alisema Yule mwanamke wakijini.
"Nenda lodge kachukue ile fimbo utakuta imechorwa alama nyekundu katikati ujue ndio iyoiyo ilete nakusubiri" alisema yule mwanamke wakijini na Mimi nilitoweka kama kawaida yangu.
"Nipofika kwenye chumba cha kafara nikakuta iyo fimbo ikiwa pembeni kidogo ya fimbo nyingine basi nikachukua na kutoweka kurudi mochwari sasa ile naingia nilibaki kushangaa kile nilichokiona.
" walifika wachungaji atasijui ilikuwaje maana tulisha toa angalizo maziko tungefanya sisi kama wazamini lakini hata sikujua pale wachungaji walifwata nini na mbaya zaidi walilifungua jeneza kabla ya sisi atujaweka ile fimbo mle ndani.
Nilitupa macho kuangalia vizuri mlendani kumtafuta yule mwanamke wakijini nilimwona amejikunja kwenye kona akinitingishia kichwa kunizuia nisifanye chochote kile. Basi niliganda wale nilipokuwa uku nikitazama wale wachungaji wanachofanya.
" he hiii shingo yake vipi? Aliuliza mmoja wa wachungaji.
" ha! Alichinjwa inamaana? Alijibu mchungaji mwengine uku akishangaa.
" kwani yule nesi tuliekuja naye yupo wapi? Aliuliza mchungaji wa kwanza.
" alitoka ila uyo anaingia" alisema mchungaji watatu na kunifanya nitupe macho mlangoni kuangalia. Aliingia nesi kweli na mwanaume mwingine aliyevalia kama daktari.
" uyu marehemu aliletwa apa akiwa amechinjwa au? Aliuliza mchungaji wa kwanza.
" hapana sisi tulimpokea kutoka kwawasamalia wema tukamleta uku" alisema daktari.
" kwaiyo huwa amumwangalii mtu akiletwa sasa hamuoni mnaweza mleta mochwari mtu aliye zimia? Aliuliza Yule yule mchungaji wa kwanza.
"Hapana bwana mchungaji sisi tulimwangalia ila ukweli kuhusu kuchinjwa ilo na Mimi naliona saizi" alisema daktari.
" aha! Lakini ndugu tunaomba radhi kwa kilicho tokea mtusamehe sana kwakuto kugundua tatizo Ilo mapema" alisema tena daktari.
"OK haina shida ila huu uzembe usijirudie bwana" walisema kwa pamoja wale wachungaji.
" lakini kuna wazamani walikuja kufanya maandalizi ya maziko kwa marehemu mmekutana nao?" aliuliza nesi.
" hapana mbona sisi hatujakuta mtu humu" walisema wale wachungaji.
" lakini tulisikia kuwa kuna wazamini ndio maana tumekuja ila tumekuta marehemu ameshaandaliwa kwaiyo tunatakiwa tuondoke na mwili kwaajili ya ibada " waliongeza wale wachungaji.
Basi milipomtizama yule mwanamke wakijini alinifanyia ishara tuondoke kweli nikaondoka nikatokea nyumbani na sekunde tu na yule mwanamke wakijini akawa naye anaingia.
" tutafanyaje sasa? Nilimuuliza uku nikijua mambo tena yanataka kuwa magumu.
" tuwaache waubebe waupeleke nyumbani kwa marehemu kisha sisi tutaenda lodge kule kuchukua members wengine na tutaita jeshi la ulinzi litakaa angani kwani hii ni vita sasa " alisema yule mwanamke wakijini..... Itaendelea