Simulizi: Suprise ya mume wangu


May Day

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Messages
1,174
Points
2,000
May Day

May Day

JF-Expert Member
Joined May 18, 2018
1,174 2,000
Raha ya suprise ni kusupriseana.
 
kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Messages
4,064
Points
2,000
Age
34
kimsboy

kimsboy

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2016
4,064 2,000
SCRIPT ZA IMA

KUTOKA KWA:MSANII JOTO LA MOTO.


NYUMBANI KWA TONI-NDANI-MCHANA.
Toni, bwana wa makamo, 40,anaweka yaraka zake kadhaa kwenye mkoba, Pembeni yupo Sheila, Mwanamama mrembo, 34, akikunja shati kwa umakini na kuliweka vizuri kwenye begi dogo sambamba na nguo zingine zilizojaza begi, anafunga begi kisha anainua macho kumuangalia Toni ambaye bado anapanga nyaraka zake sawa sawa, Toni anashtuka na kugeuka kugundua Sheila anamuangalia, “vipi?” Toni anauliza, “hamna” anajibu Sheila, Toni anatabasamu nakumsogelea Sheila na kumkumbatia, “nitakumusi mke wangu” anasema Toni, “mimi na Watoto pia tutakumisi Toni” anajibu Sheila, kisha wanaachiana na kubaki wameshikana mikono wanaangaliana, “ukiwa huko ujichunge baba Gaspa” anasema Sheila kwa sauti ya upole iliyojaa mahaba, “baby” anasema Toni, “siku zote najichunga iweje hizo siku tatu zinishinde?” anauliza Toni,”sijasema zitakushinda baba Lisa” anasema Sheila, Toni anashusha pumzi, “mimi ni mtu mzima Sheila” anasema Toni, “kukucheat wewe labda nikutane na malaika” anasema Toni, “lakini sio binadamu” anaongeza Toni, “nilishakwambia babe..hakuna mwanamke mwingine mzuri zaidi yako anayeishi ulimwengu huu” anasema Toni, “mmh” anaguna Sheila huku akielekea ulipotundikwa mkoba wake nyuma ya mlango, anafungua na kutoa DVD, huku Toni akirudi kumalizia kupanga nyaraka zake, Sheila anarudi na kumuonyesha Toni ile DVD, Toni anageuka na kushangaa, “ni nini?” anauliza Toni, “ukaiangalie ukifika tu Arusha” anasema Sheila, “na kila asubuhi kabla hujatoka” anaongeza Sheila, “baby tutakuwa bize sana sidhani kama kutakuwa na muda wa kuangalia muvi” anasema Toni, “sio muvi na ina sekunde hamsini tu Toni” anasema Sheila, “ok” anasema Toni huku anaipokea na kuiweka kwenye mkoba na kuufunga “utatuletea zawadi gani?” anauliza Sheila, Toni anashusha pumzi, “nita ku surprise Sheila” anasema Toni, Sheila anatabasamu, simu inaita, Toni anaipokea na kuiweka sikioni, “nipo njiani Mak” anasema Toni huku akiinua mkoba wake, “ok” inasikika sauti ya kiume ikijibu kwenye simu, Toni anaitoa simu sikioni, “muda wa kwenda” anasema Toni, Sheila anabeba begi la nguo na wanatoka.

NYUMBANI KWA TONI-NJE-MCHANA
Toni na Sheila wanatoka getini na kuifikia gari ndogo, Toyota premior iliyosimama sambamba na geti, Toni anagonga dirishani, Dereva anashtuka na kupunguza sauti ya redio iliyokuwa ikicheza muziki kwa sauti ya juu, Dereva anafungua mlango na kufungua buti, Toni na Sheila wanaweka mabegi kwenye buti, kisha Toni anaelekea mlangoni siti ya mbele ya abiria huku Sheila akimfuata, Toni anageuka kwa Sheila, wanabusu, “niagie Gaspa na Lisa wakitoka shule” anasema Toni huku akifungua mlango na kuingia, gari inaondoka.

NYUMBANI KWA KWA MAKINI-NJE-MCHANA.
Makini, kijana Mtanashati, 38, akiwa na begi dogo, mkoba wa lap top na begi la mgongoni, amesimama nje ya geti. Gari inafika, kioo upande wa mbele wa abiria kinashuka, “sorry aise tumechelewa kidogo” anasema Toni akiwa ametoa kichwa dirishani,”kama kawaida mzee wa kuharibu” anasema Makini huku Dereva akiteremka na kwenda kumsaidia Makini begi, ,“itabidi utupeleke spidi tusije tukachelewa muda wa kuripoti pale airport” anasema Makini huku wakisaidiana na dereva kuingiza mabegi kwenye buti, “msijali” anasema dereva,wanaingia garini na gari inaondoka.

JIJINI ARUSHA-HOTELINI CHUMBANI KWA TONI-SAA MOJA JIONI.
Toni anavaa fulana, anachukua simu yake juu ya meza na kutoka.

JIJINI ARUSHA-HOTELINI-CHUMBANI KWA MAKINI-SAA MOJA JIONI.
Toni anafika mlangoni nakugonga, Makini yupo mezani akiitumia lap top, anashtuka kusikia mlango unagongwa, anainuka na kwenda kuufungua mlango, anamkuta Toni, “vipi?” anauliza Makini huku akirudi mezani kwenye lap top yake, “twende tukashtue moja moja alafu turudi tukiwa fresh” anasema Toni huku akiingia pale chumbani, “Toni tunawasilisha mada mkutanoni asubuhi” anasema Makini, “tunapiga moja moja fasta alafu tunarudi” anasema Toni, “safari moja itaanzisha nyingine Toni” anasema Makini, “kwa nini tusingoje mpaka keshokutwa baada ya mkutano?” anasema Makini, Toni anashusha pumzi na kujikuna kichwani kuashiria amefika kikomo cha hoja, “ok poa..ngoja na mimi nirudi chumbani nikaboreshe material yangu” anasema Toni huku anageuka na kuelekea mlangoni na kutoka.

JIJI LA ARUSHA MAKAO MAPYA-SAA NNE USIKU.
Mtaa maarufu katikati ya jiji kumechangamka vilivyo, idadi kubwa ya watu wa kaliba mbalimbali wakienda huku na kule, mabanda ya wapika chipsi, mishikaki, kuku n.k. yamesheheni na muziki mchanganyiko kutoka baa zilizopo maeneo hayo.

Toni amesimama pembeni ya kibanda cha chipsi, akiwa na chupa ya bia iliyojaa robo tatu mkononi, macho yamemtoka kuashiria kuwa kinywaji kimembamba vizuri, Muuza chipsi anamaliza kuweka chipsi mayai moja kwenye sahani na kumpatia jamaa aliyeketi jirani kisha anageuka kwa Toni, “bado hujachagua bro” anauliza Muuza chipsi, “nalitaka lile jeupe lilojazia” anasema Toni, “lile linalosinzia” anauliza Muuza Chipsi, “lenye jinsi ya bluu” anasema Toni, “andaa kaki yangu kabisa bro” anasema Muuza chips huku akielekea walipoketi kina dada watatu, Toni anabaki akipiga funda kadhaa kutoka chupa yake ya bia aliyoishika mkononi, Muuza chips anarudi na Chubu, mmoja wa wale kina dada waliokuwa wameketi, “mzigo huo” anasema Muuza chips huku akiwahi kugeuza mishikaki inayochomeka kwenye jiko lake, Toni anatoa noti ya shilingi elfu tano na kumpatia Muuza chips, “poa braza” anasema Muuza chipsi huku anaipokea ile noti ya elfu tano na kuiweka mfukoni, “twende” Toni anamwambia Chubu huku akiongoza njia kuelekea jengo la hoteli lililopo mita chache kutoka pale.

HOTELINI CHUMBANI KWA TONI-USIKU.
Toni na Chubu wanaingia, Chubu anaenda hatua tatu na kugeuka kumuangalia Toni, “naomba changu kabisa” anasema Chubu, Toni anaingiza mkono mfukoni na kutoa noti kumi za elfu kumi na kumpa Chubu, Chubu anapokea huku ameshikwa na mshangao,”zote zangu?” anauliza Chubu, “ukiweza kunisahaulisha mke wangu usiku wa leo nakuongezea” anasema Toni,Chubu anambusu Toni shavuni, “jiandae kaka leo nitakuonyesha kwa nini Arusha wananiita feti mauno” anasema Chubu huku akianza kuzungusha kiuno kama wacheza show wa bendi za kikongo, Toni akiwa katika hali ya ulevi anabaki anamuangalia Chubu kwa muda, “wee” anasema Toni kwa sauti ya ukali, Chubu anashtuka na kuacha kukatika, “sitaki hizo fujo zako..panda kitandani” anaongeza Toni, Chubu anaketi kitandani na kuanza kuvua raba zake, Toni anaendelea kumalizia bia yake mkononi.

HOTELINI CHUMBANI KWA TONI-SAA KUMI NA MBILI ASUBUHI.
Toni yupo kitandani, anafungua macho, anabaki ametulia kwa sekunde kadhaa kisha anapapasa mkono kitandani, anashtuka na kuinuka, anawasha taa ya mezani pembeni ya kitanda, inasikika sauti ya choo kinaflashi, anashusha pumzi, anakuja Chubu akiwa amekunja uso, “vipi?” anauliza Toni, “tumbo linaniuma” anasema Chubu huku akiketi kitandani na kuanza kuvaa nguo zake, “limekuanza saa ngapi?” anauliza Toni, “kwenye saa kumi hivi” anasema Chubu, “ila hamna shida nimeshameza frajili” anaongeza Chubu, Toni anashtuka, “frajili umezipata wapi?” anauliza Toni, “nilikuwa nazo kwenye pochi” anasema Chubu, “ina maana ulijua utaumwa na tumbo?” anauliza Toni, “huwa linaniuma mara kwa mara” anasema Chubu huku anainuka, “hiyo hali imekuanza lini?” anauliza Toni, “muda mrefu tu” anajibu Chubu, “karibu miaka miwili sasa” anaongeza Chubu, Toni anabaki kimya ameduwaa, Chubu anachukua mkoba wake, “mimi naenda” anasema Chubu, “hebu subiri” anasema Toni huku anainuka na kwenda kwenye kona ilipo ndoo ya takataka na kuchungulia, “kondomu tulizotumia ziko wapi?” anauliza Toni, “kondomu gani na ulikataa kutumia kondom” anasema Chubu, “na ukanitishia kunipiga..au umesahau” anaongeza Chubu huku akitoa pakiti mpya ya kondomu kwenye mkoba wake na kumuonyesha Toni, Toni anabaki ameduwaa, Chubu anarudisha pakiti mkobani na kwenda mlangoni, “unajua wewe ni shetani” anasema Toni, “ningekuwa shetani ungerudia mara tatu?” anasema Chubu huku anaufungua mlango na kutoka, “mara tatu?” Toni anaongea mwenyewe kwa sauti ya chini, anabaki ameduwaa kisha kichovu anaenda kuketi kwenye kiti akionekana kusongwa na mawazo, anabaki ametulia pale kwa muda kisha anachukua DVD aliyopewa na Sheila iliyopo pale juu ya meza, anaiingiza kwenye lap top, video inaanza, anawaona Gaspa, mvulana, 7, Lisa,binti, 10, na Sheila, wakiwa kwenye tabasamu zito “we love you daddy” wanasema Gaspa na Lisa, “we love you jembe” anasema Sheila huku wote wakipungia na kutoa ishara za busu, video inaisha, Toni analengwa machozi, anabofya Lap top DVD inatoka, anainuka, anaangalia huku na kule pale mezani, anafungua droo, huku akionekana kama ameshtuka na kuchanganyikiwa, anainua simu ya mezani, anaibofya mara kadhaa na kuuweka mkono sikioni, “halow..mwanamke aliyetoka chumbani kwangu ameniibia simu” anasema Toni, kunakuwa kimya kwa sekunde kadhaa “si ameshaondoka..mbona hukusema mapema kaka yangu” inasikika sauti ya kike kwenye simu, Toni anatoa macho kwa mshtuko, anaitoa simu sikioni na kuirudisha chini na kubaki kimya akishangaa, ile simu inaita, anashtuka na kuipokea kwa haraka, “Toni vipi..muda tayari twende” inasema sauti ya Makini kwenye simu, “mzee wewe tangulia mimi sijisikii vizuri Mak” anasema Toni, “imekuwaje tena?” anauliza Makini kwenye simu, “nitakwambia baadae” anasema Toni, “ok” anasema Makini kwenye simu, Toni anaitoa simu sikioni na kubaki amezubaa huku amejishika kichwa kwa mikono miwili.

WIKI MOJA BAADAE-JIJINI DAR ES SALAAM-OFISI YA TECHNO SKY.
Sheila na Mr Gebi wapo ofisini, Sheila akiwa ameshika simu ya sumsung akiikagua kwa umakini “ndio yenyewe..mimi ndiye niliyeinunua kwa hiyo naijua vizuri” anasema Sheila kwa bashasha huku akiinua mkoba wake uliopo chini, “ngoja nimpigie Toni” anasema Sheila huku anatoa simu yake na kuibofya, anaiweka sikioni, “baby njoo unipitie basi hapa mlimani city ofisi namba arobaini na tano” anasema Sheila, “sasa hivi?” inauliza sauti ya Toni kwenye simu, “ndio..sasa hivi baba G” anajibu Sheila,”kuna nini baby?” anauliza Toni kwenye simu, “ni surprise wewe njoo” anasema Sheila, “Ok baby” anasema Toni kwenye simu, Sheila anaitoa simu sikioni huku akiwa na tabasamu kubwa usoni, “hakujua hata kama niliwapa hii kazi” Sheila anamwambia Mr Gebi, “mmeipataje?” anauliza Sheila, “ulipotoa tu taarifa..tukaanza kufanya tracking..na ndio tumeipata” anasema Mr Gebi, “na imekuwaje imepatikana Dar na iliibiwa Arusha?” anauliza Sheila, “tuliyemkamata anasema huwa wakiiiba hizo simu za gharama soko zuri lipo huku Dar” anasema Mr Gebi, “kwa hiyo Mungu mkubwa ni kama amejileta” anaongeza Mr Gebi, Sheila anashusha pumzi, “naweza kuongea na huyo mliyemkuta nayo?” anasema Sheila, Mr Gebi anainua simu mezani kwake na kuobofya, “Bonge hebu mlete huyo mtu” anasema Mr Gebi na kuitoa simu sikioni, sekunde chache baadae wanakuja Bonge akiwa amemshika Chubu mkono, “kaa hapo” Mr Gebi anamwambia Chubu, Chubu anaketi huku Bonge akibaki amesimama pembeni, “ndio huyo” Mr gebi anamwambia Sheila, “naweza kumuhoji?” anauliza Sheila, “uwanja ni wako dada” anasema Mr Gebi, “mimi naitwa Sheila..sijui wewe mwenzangu unaitwa nani?” anauliza Sheila, “naitwa Chubu” anajibu Chubu, “dada hii simu uliipataje?” anauliza Sheila, “nilikutana na huyo Kaka kule Arusha” anasema Chubu, “mlikutana naye kivipi?” anauliza Sheila, “hotelini” anasema Chubu, “kwenye mazingira gani?” anauliza Sheila, “alinichukua tu kawaida kama mteja” anasema Chubu, Sheila anashtuka, “mteja?” anauliza Sheila kwa mshangao, “kwa hiyo mlilala nae?” anauliza tena Sheila, “eee” anajibu Chubu, “Mungu wangu” anasema Sheila huku akishusha pumzi nzito na kuweka mikono kichwani.

Huku nje Toni anafika, anasukuma mlango, anaingia na kumuona Sheila ameketi, “baby vipi?” anasema Toni na kuiona ile simu yake mkononi kwa Sheila, “hii ni ile simu?” anasema Toni kwa mshangao huku akiichukua ile simu mkononi kwa Sheila, na mara anagundua kuwa Sheila hayupo sawa, “Mama Lisa vipi?” Toni anamuuliza Sheila, Sheila anainua kichwa kumuangalia Toni, macho yakiwa yameiva kwa wekundu “huyu ni nani?” Sheila anamuuliza Toni huku akimuonyesha kwa Chubu ambaye Toni hakuwa amemng’amua mapema, Toni anapatwa na mshtuko mkubwa na kuiachia ile simu inaanguka chini.

OFISI YA TECHNO SKY-NUSU SAA BAADAE.
Mr Gebi, Sheila, Chubu, Bonge na Toni wapo ofisini, Sheila akiwa amejiinamia, Toni anashusha pumzi, “twende zetu nyumbani mama Lisa..tutayamaliza huko” anasema Toni, Sheila anashusha pumzi, anainua kichwa kumuangalia Toni, kisha anamuangalia Chubu “hebu naomba nikuulize Dada” anasema Sheila kwa sauti yenye majonzi mazito, kimya kinatawala kwa muda, “mlitumia kinga?” Sheila anamuuliza Chubu, Chubu anabaki kimya, Toni anatoa macho kwa hofu “naomba uwe mkweli Dada” anaongeza Sheila, “niseme tu ukweli dada yangu..hatukutumia” anasema Chubu, “uwii” anasema Sheila huku analegea mithili ya mtu aliyepigwa shoti ya umeme pale kwenye kiti.

MWISHO.
Huyo kwenye profile ni mama mndumi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Forum statistics

Threads 1,294,528
Members 497,971
Posts 31,178,700
Top