Simulizi: Sijaona kama wewe

josephdeo

Member
Nov 23, 2015
95
196
Tuna safari ndefu sana katika maisha na kila mmoja anakutana na mikasa yake. Lakini katika yote hayo yaani safari ndefu na mikasa ambayo tunakutana nayo kuna kitu kimoja tu ambacho kinatufanya wotr tuendelee kupenda kubaki katika ulimwengu huu. Kitu hicho si kingine bali ni mapenzi.

Mapenzi yamekuwa chachu ya watu kung'ang'ania kubaki ulimwenguni hata baada ya mikasa ambayo anakuwa anapitia. Pia mapenzi ndio silaha kubwa ambayo imefanya ulimwengu kubaki kuwa mahala salama na sio risasi wala nyukilia.

Ni majira ya asbuhi ambapo anga lilipambazuka vyema na kuonesha kuwa hizo ni moja kati ya siku njema ambayo anga limeamua kujinasibu. Nilishtuka toka usingizini na hii ni baada ya kusikia kelele nje ya chumba ambacho nilikuwa nimelala. Kiuvivu uvivu niliamka na kutazama kelele hizo zilisababishwa na nini?

Huku nikiwa na ghazabu za kuniharibia usingizi wangu ambao niliukosa kwa usiku mzima na ilipotimu saa kumi na moja alfajiri ndio niliupata na sasa saa mbili asbuhi naamshwa na kelele.

Nilikwazika sana na kufungua mlango wa chumba nilichokuwa na ulitii amri yangu na kufunguka. Ulipofunguka tu pamoja na kuwa na mawenge ya usingizi ila niliona kitu kinakuja upande niliopo kwa kasi sana niliamua kurudisha mlango ili kuufunga na kile kitu kiligonga mlangoni. Lilikuwa jiwe na hapo sasa nilipata kitu kilochochochea zaidi hasira zangu.

Awamu hii niliufungua mlango kwa kasi na kutoka nje mzima mzima huku kwa sauti kubwa nikiuliza.
"ni mjinga gani aliyeponda jiwe kwenye mlango?". Waliokuwa nje wote walibaki wananishangaa kana kwamba naongea lugha ambayo ni ngeni kwao.

Niliamua kuita kwa jina mdogo wangu wa kike aliyenifuatia mimi "Neema nani aliyepiga jiwe kwenye mlango wakati mimi nimelala" alinitazama tena na kuniambia.

"kaka Emma anapigana sijui na kina nani?". Sikutaka kusubiri moja kwa moja niliuliza ugonvi huo uko wapi na nilirudi ndani na kuchukua panga na kisha kutoka nikiwa kifua wazi na chini nilivaa pensi tu.

Bila kuchelewa nilifika sehemu ya ugonvi na kukuta tayari kaka yangu huyu alikuwa kawadhibiti aliokuwa anapambana nao na mimi nilifika pale nakuwaangalia wale watu ambao idadi yao walikuwa watatu na kuuliza.

"wamefanya nini hawa". Kwa utaratibu huku akilazimisha utulivu akasema.
"hawa jamaa nimewakuta na demu wangu".

Nikauliza "nani huyo?". Kwa maana na yeye alikuwa na idadi kubwa ya wanawake.
Akanijibu huku sasa akishindwa kujizuia "kwani demu wangu humujui au na wewe unataka kuniletea uchuro". Nilinyamaza kwa kuwa nilisha mfahamu mwanamke aliyekuwa akiongelewa pale na mimi niliondoka kwa kuwa alikuwa tayari kashawadhibiti na watu wengine wa mtaa wetu walikuwepo.

Hayo ndio yalikuwa maisha ya Mabatini bila kuwa na nguvu basi hauwezi kuishi kwani kila mmoja alikuwa mbabe hivyo ukiwa mnyonge watakunyonga na haki zako wasikupe. Baada ya sekeseke hilo kuniondolea usingizi nilirudi nyumbani na kuchukua kikombe cha uji ambao tayari ulikuwa umeshakuwa tayari.

Ilikuwa kama sheria amabayo ilipitishwa na ilitumika pale nyumbani kuwa tukiamka tu lazima kuwepo na uji na kisha chai itafatia kama itapatikana kwa siku hiyo lakini uji ulikuwa ni wa kila siku.
 
Unawezakupata muendelezo wa riwaya hii kupitia group hili la WhatsApp bure kabisa...



Au tuma ujumbe kwenye namba hii ili iwe tukuunge... +255 655 500 516
 
Unawezakupata muendelezo wa riwaya hii kupitia group hili la WhatsApp bure kabisa...

Au tuma ujumbe kwenye namba hii ili iwe tukuunge... +255 655 500 516
 
Ndani ya group mambo yapo mbio mno kuliko haya maelezo natayari tuko na riwaya mpya.

Tembelea group hili kwa gharama ya bure kabisa karibu

Screenshot_20220806-212122.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom