Simulizi : Salamu kutoka kuzimu

Simulizi : Salamu kutoka kuzimu

Maji Chai

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2018
Posts
266
Reaction score
367
sehemu ya 01

Sikumbuki nillifikaje nyumbani, ila nakumbuka mara ya mwisho nilikuwa safarini kwa ajili ya likizo ndefu ya mwezi wa kumi na mbili. Ila si tu kufika nyumbani, nilifikaje nyuma ya mlango? Wakati yote hayo nilisikia vilio nje, sikutaka kupitwa na vilio hivyo kwani hata shuleni nilitambulika kama 'Baba sipitwi'.

Niliusukuma mlango ule wa mbao uliokuwa umechoka na ghafla kukaribishwa nje na wingu kubwa la watu waliokuwa wakiangua vilio. Ikafatwa na sauti ambayo haikuwa ngeni maskioni mwangu, ilikuwa sauti ya mtu ambaye nilikuwa kondoo wake naye alikuwa mchungaji wangu Haris. "Mavumbini tumetoka, na mavumbini tutarudi".

Maneno yake yakanitia woga, yakanikumbusha hali niliyokuwa nimemwacha nayo mama aliyekuwa si wa maji wa chai. Machozi yakaanza kunitirika huku nikielekea kwa Haris aliyekuwa kasimama mbele ya jeneza. Muda wote huu nilikuwa nikimlaani vikali aliyekuwa kaniweka nyuma ya mlango kwani nilijua fika alikuwa akitaka nisiuone mwili wa mamangu kipenzi Bi.Zakish.

Nilikaribia kwenye jeneza tayari kumtizama mamangu kwa mara ya mwisho, alikuwa ni mwanamke mwenye uzuri wa aina yake. Nywele ndefu kama singa ya farasi, ngozi nyororo yenye rangi ya mtume na midomo ambayo haikuwahi kaukiwa mate uliojawa meno yaliyokuwa yamemkaa bambam mdomoni.

Ila yote hayo tulikuwa tumeyafukia kwenye kaburi la sahau, kwani kipindi naenda shule ngozi yake ilikuwa imeanza kuparara na kuwa na mabakamabaka sikwambii ya chui, huku mabega yakimwagika yakimwacha kikongwe.

Nillivuta pumzi ndefu tayari kukabiliana na lolote nitakalo liona ndani ya lile jeneza. Nilijua fika nilikuwa nakutana na fuvu la mama peke yake. Ila amini usiamini..................

Itaendelea

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app
 
Dah
giphy.gif
 
Sehemu ya 02

.... Nilijua fika nilikuwa nakutana na fuvu la mama peke yake. Ila amini usiamini ni mimi ndimi nlikuwa ndani ya jeneza na mimi ndimi nlikuwa naulialia mwili wangu mwenyewe.Niliruka kwa mshangao na kujibwaga chini nkitizama huku na kule na kuiona sura ya mamangu Bi hamza aliyekua akilia sana.Nilijikombakomba kutoka pale chini na kuelekea kwa mama ili nimtie faraja kuwa nlikuwa hai ila yote ilikuwa kazi bure.Uwepo wangu hukutambulika tena.Hakuna aliyeweza kuniskia achilia mbali kuniona nlitambua kuwa nlikuwa mfu hai kama si msukule.

Haikupita kitambo kidogo kabla mwili wangu kupumzishwa kwenye nyumba yake ya milele huku nkiachwa na maswali mengi yasiyokuwa na majibu.Nilikufaje? Nilifikaje nyuma ya mlango na kwa msaada wa nani? Yote hayo yalikuwa maswali ambayo sikuwa na majibu yake.

×××××

Jua lilikuwa limefika utosini na wale wote waliokuwa wamekuja kunisabahi katika safari yangu ya mwisho walikuwa wanatiririkwa jasho,sisemei njaa waliokuwa nayo na sio wao tu bali hata mimi.Kwa jua lile nililazimika kutafuta sehemu ya kivuli nipumzike nikisubiri chakula ambacho si muda mrefu kitagawiwa kama alivyotaarifu baba.Japo nlitambua fika sina uwezo wa kubeba chakula changu mwenyewe ilinibidi kupita katika sahani za watu na kujipigia matonge kutuliza njaa.Wakati nikielekea kwenye kivuli nilipata wazo la kupita katika vikundi vya watu ili nipate fununu juu ya kifo changu.Na yote nliyoyasikia yalinitia huzuni."Alikuwa akirudi kutoka shule wakapata ajali ndo mauti yakamkuta"Nilimsikia baba akimwambia rafiki yake.Sasa kama nlipata ajali nlifikaje nyuma ya mlango? Nikavuta taswira ya yale nliyokuwa nkiskia kuhusu watu kufanywa misukule.Je mimi pia nlikuwa nimefanywa msukule?Kama ni kweli nani alifanya hivyo?Sikutaka kuyajua yote hayo kwa muda huo nilitaka kujaza tumbo kwanza ............

itaendelea

Sent from my SM-J500F using JamiiForums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom