Man Middo tz
Senior Member
- Sep 9, 2020
- 154
- 230
SIMULIZI: SABABU NI KIFO CHAKO BABA! (Kisa cha kweli cha kusisimua)
SEHEMU YA KWANZA (01)
MTUNZI: Man Middo Tz +255 655 969 973
Hakika kila kukicha shukrani kwa Muumba kwa kukufikisha siku nyingine ingawa huwezi kujua siku hiyo itakua ya furaha au huzuni. Basi nakumbuka ilikua siku ya tarehe 23 mwezi wa 3 mwaka wa 2009. Katika siku hii ninayoikumbuka katika maisha yangu yote, ilianza vizuri tu kama siku nyingine.
Masaa yalivyozidi kwenda moyo wangu ulikua ukinienda mbio sana. Sikujua kwanini lakini furaha ilianza kupotea kadri masaa yalivyozidi kwenda. Kila nilipomtazama baba, nuru usoni mwake ilipotea kabisa!! Nakumbuka siku hii tulikua likizo ndogo ya wiki hivyo watoto wote tulikua nyumbani, basi siku hii alikua akitutizama sana wanae.
Sikutishwa na kututazama sana kwasababu baba yangu mzee Nelson Magoma alikua akitupenda sana wanae. Lakini kilichonitisha ni pale nilipomuona baba yangu akitokwa na machozi wakati akitukazia jicho wanae. Pia akaanza kutoa nasaha
“Wanangu nawapenda sana, someni sana, someni kwa bidii mje kumsaidia mama yenu kwasababu huko mbeleni maisha yenu yatakua magumu”
Baba ananigeuzia jicho huku akionekana kujawa na uchungu dhidi yangu, moyo wangu ulizidi kunienda mbio ingawa niliamini baba yangu kwakua ni mtu wa imani. Pia ni mwalimu huenda nasaha zile anatoa kwa dhati ili wanae tujue ni kipi anakimaanisha. Jicho la baba kwangu sio tu kuwa lilikua la upendo wa dhat lakini pia lilionyesha uchungu ndani yake, akaniambia
“Nyamlya Soma sana mwanangu, unakili sana na una kila kitu kwasasa”
Sikujua anamaanisha nini lakini mimi nikamuitikia kwa kutikisa kichwa tu. Kitu kingine ni pale aliponiita jina la ukoo baadala ya jina langu la Anna Nelson Magoma au Hesha jina langu la utani.
Baba yangu alikua akinipenda sana. Alikua akionyesha mapenzi makubwa kwangu sio kwamba hakuwapenda wengine lakini kuna kitu kilimfanya baba anikubali sana nitakisema mbeleni.
Uuuh! Siku hiyo usiku baada ya chakula baba akatuita wanae wote tukakusanyika, wakati huo nikashukuru Mungu siku kama imepita salama kwakua yale matukio yaliyojaa uchungu yamepita. Basi baba baada ya kutuita akasema.
“Nimewaita hapa nataka leo tufanye maombi ya kifamilia, Anna naomba uongoze maombi sawa”
“Sawa baba” nikatikia.
Kusema ukweli pamoja na umri wangu wa miaka 11 Wakati huo lakini nilikua naweza kufanya maombi sana kuwazidi ndugu zangu wengine wakubwa. Basi nikaongoza maombi nikamaliza, baada ya kumaliza baba akasema
“Haya maombi ya leo ni muhimu sana naomba hata nikiwa sipo muwe mnaomba hivi, muwe mnakusanyika hivi kama familia, nawapenda sana wangu”
Nasaha ile ikanifanya nijawe na huzuni na moyo wangu uniende mbio, lakini pia hata nilipomtazama mama alionekana mwenye kutafakari yale maneno aliyotamka baba. Sikujali sana kwasababu usiku umefika tukaagana kisha nikaingia chumbani kwangu, dada zangu wakenda zao, hao walikua wakilala kwa bibi yangu na wazazi wakaingia chumbani kwao kulala wakiwa na mdogo wangu wa mwisho mwenye umri wa miaka mitano.
***
Daah! Nikikumbuka machozi yanitoka! Basi nilivyofika kitandani nikajilaza, muda huo wa saa nne usingizi haukukawia nikalala. Ilivyofikausiku nadhan ilikua kama saa 6:30 hivi nikiwa usingizini nilistuka nikasikia kishindo kwa mbali sana huko nje! Lakini maajabu usingizi ukanipitia tena. Kwa mazingira ya kijijin ni kawaida muda kama huo kuwa kwenye usingizi mzito. Lakini baada ya kama dakika 10 purukushani zikanishtua usingizini. Nilivyoamka nikwa bado na usingizi singizi nikasikia sauti za wanaume wakisema
“Mama toa hela…” Mwingine akasikika akisema
“Wee mwanamke tunataka hela tuondoke….au tuwaue watoto wote” Mara ikasikika nyingine kutoka nje ikisema
“Mpigeni kwanza ndio atatoa hela”
Muda huo nilikua nimekaa kitandani sielewi nini kinaendelea zaidi ya zile sauti, Mungu wangu!! Ghafla nikaskia panga kama sita au saba mfululizo kana kwamba mtu anakata miti vile Daah! Damu zikanienda mbio mwili ukatetemeka. Mama nae akaanza kulia kwa kupiga ukunga.
“OOOOH mama nakufaaa... Mama eeh!!”
“Ukiendelea kupiga kelele atafia hapa hapa na wanao wote, bora uwe kimya”
Kweli mama akatii, Sasa kile kitendo cha kumsikia mama analalamika kikanijaza uchungu na kuniuma mnoo, nikatoka kuelekea seblen.
Mawazo yangu niliamini baba ndio anampiga mama, sasa nilipofika sebleni nikakuta wanaume nazani wanafika 5 au 6 kila mmoja kafunga tochi kwenye paji la uso.
Sikuwatambua pia kutokana na kile kilio sikufuatilia ni akina nani. Sasa nilivyosimama mbele ya mmoja wao hakuniona alikua bize anapanga vitu vya baba kuweka kwenye briefcase kubwa ya baba! Alikua akiweka nguo za baba, saa ya ukutani, saa za mkononi, kioo na vingine vidogo dogo. Basi nilipovitambua vile vitu nikamuliza
“Kaka mbona mnapanga vitu harafu Mama anapigwa na baba kwani wamegombana nini? Na nyie mmetokea wapi”
Alivyosikia hivyo ndio akagundua kuwa nipo pale, mmoja akanifuata akanipiga na panga kwa bapa kama ananichapa, harafu akaniongoza hadi chumbani huku naugulia maumivu. Pamoja na maumivu lakini nilikua namuliza maswali ila hajibu, nikafika kitandani akasema
“Lala hapo harafu nikuone unatoka uone”
Nikatii akanifunika shuka akatoka, sasa hapo akili ndio ikarudi na kutambua kuwa hapa kuna hatari kubwa. Yale matukio yote ya mchana kutwa yakanza kujirudia, akili yangu ikanituma na kujua baba yupo kwenye hatari.
Kwa jinsi baba alivyokua ananipenda hata awe na hasira kiasi gani nikimsemesha tu lazima aniambie, mimi nilikua mdogo sana lakini nilikua kama mshauri wa familia. Sasa akili ikanituma nimfuate baba ila hofu nimeambiwa hakuna kutoka. Ghafla nikasikia kishindo kikali sana kama kuna mzigo unanguka kutokea chumbani kwa baba na mama.
Kitendo kile kikanikurupusha nikavaa ujasiri nikatoka, nia yangu nikamuone baba lakini ile kutoka tu nilikutana na kipigo kikali mno. Bonge la bao na mateke huku wakisema
“Wewe si umeambiwa ulale husikii, Toka apaa..!!”
Sasa aliponipiga kofi la uso likanipeperusha nikajikuta nakutana na utelezi nikakunguka, hapo chini nikagundua kilichoniangusha ni damu tena nzito ikitokea chumbani ambako baba yupo. Ile damu illikua imetapakaa hadi sebleni damu nyingi mnoo uuuh! Hapo nguvu zikaniishia nikamsikia mama akisema
“Anna mwanangu rudi chumbani ulale ili ubaki msaada kwa ndugu zako”
Sauti ile ikaninyong’onyesha sana, kupitia kauli hiyo ya mama nikagundua mmoja kati ya baba au mama atakufa! Kumbe wakati huo baba yupo kwenye hali mbaya sana…………ITAENDELEA.
JE UNAJUA KIPI KILIFUATIA? JE KWANINI MZEE NELSON ANAULIWA KIKATILI HIVYO? ANNA ATAVUMILIA?
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA ILI KUJUA KWANINI ANNA ANASEMA “SABABU NI KIFO CHAKO BABA” HATUJUI KIPI KIMETOKEA KWENYE MAISHA YAKE HADI IKAWA SABABU NI KIFO CHA BABA YAKE.NUKUU “Katika maisha wanasema HAKUNA KITAKACHO DUMU MILELE HIVYOHUTAKIWI KUJIPA MAWAZO MENGI KWASABABU HAIJALISHI UNA HALI MBAYA KIASI GANI IPO SIKU ITABADILIKA TU” Ni kweli hiyo kauli, lakini kwa baadhi ya watu ni tofauti kabisa kuna watu toka wanze kupatwa na matatizo katika maisha yao imekuamwendelezo tu tena muda mwingine yakawa yanazidi baadala ya kupungua. Tazama Anna anasema “Sababu ni kifo chako baba” akimaanisha sababu ni kifo cha baba yake ndio maana anakumbwa na matatizo makubwa.Kikubwa kama umzima wa afya mshukuru Mungu sana kwa kila jambo kuna watu wanatamani waishi maisha kama yako lakini haiwezekani.