SteveMollel
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 8,803
- 25,442
UTANGULIZI
Kifo kina wivu sana, hutuondolea wale tunaowapenda. Hutuacha na majonzi na kumbukumbu za kuumiza, lakini pia hutubakizia jeraha kubwa ambalo hata likipona basi hutuachia alama ya kovu kwenye paji la uso. Kovu lisilofichika.
Ila ndivyo ilivyo asili, hatuwezi kupambana nayo. Kama tujuavyo, kwakuwa tumeumbwa basi ni lazima kufa. Mikono ya binadamu haina nguvu za kutosha kuzuia kifo labda kukikawiza tu. Na pindi wapendwa wetu wanapotuacha, hata tukiumizwa vipi, twasema ni mapenzi ya Mungu, basi nayo yatimizwe. Amempenda zaidi. Ndio. Sisi tulimpenda lakini Mungu wake aliyemuumba na kumleta miongoni mwetu amempenda zaidi.
Lakini je, ni kweli vifo vyote Mungu amependa? Wapendwa wetu wote waliotutoka, ilikuwa ni amri ya Mungu? Walifikia muda wao wa kuitwa? Na kama HAPANA, basi nao waenda wapi na ingali hawakuitwa?
Basi huko jirani na hata kule kwenye ulimwengu wa mbali tumekuwa tukisikia msemo wa 'DAMU YA MTU HAIENDI BURE' kumaanisha kwamba pale unapoimwaga basi itatafuta thamani yake kwanguvu. Haitakuacha ukaishi salama. Na maisha yako yatakuwa deni kulipia thamani ya damu hiyo ambayo haikuwa na makosa.
Kuna mifano kadhaa ya uhalisia ...
Mnamo mwaka 1999 huko China kwenye jiji la Hongkong, wahusika watatu wa genge la wahuni walimkamata dada mmoja aitwaye Fan Man-yee wakisema kuwa wanamdai dada huyo takribani dola alfu ishirini za kimarekani. Sasa kwakuwa dada Fan Man-yee hakuwa na pesa hiyo anayodaiwa, wakamtesa vibaya kwa mwezi mzima kabla dada huyo hajafa kutokana na majeraha makubwa aliyosababishiwa. Alipokufa, mabwana wale wakakatakata mwili wake, wakachemsha baadhi ya vipande vya mwili wake na kuvitupia vingine kwenye makopo ya taka.
Mmoja wa mabwana hao alikuwa na mpenzi wake wa miaka kumi na mitatu ambaye naye alishiriki kwenye mateso ya marehemu. Mpenzi huyo alikuwa akiitwa Ah Fong. Na iliripotiwa tangu mauaji ya Fan Man-yee yalipotokea, mwanamke huyo, Ah Fong, alidai kuona vitu asivyovifahamu vikimtesa na kumsumbua haswa. Mara kwa mara aliona taswira ya Fan Man-yee ikidai roho yake. Hakuishi amani. Na kwaajili ya kuokoa nafsi yake, akaamua kujisalimisha mwenyewe polisi aliposema yote waliyoyafanya yeye pamoja na genge la mpenzi wake.
Lakini Polisi hawakumwamini Ah Fong. Walipuuzia kwa kudhani ni matatizo tu ya vijana wachipukiao. Ila walipofanyia upelelezi kwenye eneo ambapo Fan Man-yee aliteswa, wakagundua kuna viungo vya binadamu. Lile genge likakamatwa na kesi kupelekwa mahakamani. Ah Fong akatoa ushahidi wote na kupelekea wahusika wa lile genge kuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Mbali na hilo, mnamo mwaka 1987, huko Marekani, bwana mmoja aitwaye Terry Childs alimchoma kisu msichana wa miaka kumi na saba aitwaye Lois Sigala mpaka kifo chake. Teery akashtakiwa na kuhukumiwa miaka 41 jela. wakati akiwa kifungoni, alikiri kufanya mauaji kadhaa. mmoja wa watu aliowaua alikuwa akiitwa Linda Ann Jozovich. Mnamo 1979 alimteka mwanamke huyo akampiga, akamkaba na kumchoma visu mara kadhaa, kisha akaficha mwili wake kwenye milima ya Santa Cruz, California. Ikachukua zaidi ya miaka kumi kugundua mabaki ya mwanamke huyo.
Terry alisema kuwa ilibidi akiri mauaji aliyoyafanya ili ajiweke huru dhidi ya 'roho' za watu aliowaua. Alisema alikuwa anawaona watu hao kwenye chumba chake cha jela, wakisimama na kumtazama. Akasema pia kuwa Linda Ann amekuwa akimfuata na kumghasi. Lakini alikuja kupotea baada ya yeye kutubu. Na kutubu kwake huko kukapeleka akaongezewa kifungo, cha maisha kabisa, asifae kupewa msamaha wowote ule.
Roho za watu walioonewa, haziendi mpaka zipate haki yake. Zitawanda na kuzurura kutafuta thamani yake iliyonyang'anywa mpaka kutimia kwake kisha ndipo ziende salama kwa amani. Zitagonga mlango ama kufungua dirisha. Zitafuata nyayo na kukutazama nyuma ya miti na mapazia ... mpaka pale zitakapokuwa huru.
Lakini je, vipi pale roho hiyo itakapoanza kulipiza kisasi kwa mji mzima kama kisasi kizazi kwa kizazi? Vipi pale roho hiyo inapodai thamani kubwa ambayo ni ngumu kuilipa?
***
Nitatuma simulizi hii hapa kutokana na ratiba yangu. Kwa wale watakaoihitaji, basi wanifuate whatsapp 0685 758 123 kwa ada ya shilingi alfu tatu tu.
Karibuni ...
ONYO: USISOME UKIWA UNATEMBEA BARABARANI.